Madereva wa magari 36 ya mizigo Tanzania - Burundi wasitisha huduma baada ya kupigwaMadereva wa Tanzania wanaoendesha magari ya mizigo kuingia nchini Burundi wamejikuta katika wakati mugumu baada ya kudai kunyanyaswa na askari wa Burundi kwa kuwatoza fedha zisizokuwa na stakabadhi, huku wale wasiotoa fedha wakifungiwa kwenye vyoo.

Mmoja wa madereva wa magari hayo Bw Maskini Juma amesema askari wa Burundi katika kituo cha forodha cha Kobero nchini humo walimfungia chooni kwa saa 18 wakitaka shilingi au faranga laki 4 kwa kosa la kukutwa akiongea na mwanamke ndani ya gari.


Aidha dreva mwingine aliyepigwa, Shaaban Juma amesema madereva wamekaa Kobero kwa mwezi mmoja na nusu wakitaka kupeleka chakula cha shirika la Caritas nchini Burundi lakini hawajaruhusiwa kuingia nchini humo kwa kukosa vibali.

Kiongozi wa Jeshi la polisi katika mkoa wa Muyinga, Kabul Jamali amesema changamoto za usalama na mazingira wanazolalamikia madereva wa Tanzania yatashughulikiwa kuimarisha mahusiano mwema baina ya Tanzania na Burundi.

Katika hatua hatua nyingine, viongozi wa usalama upande wa Kata ya Kabanga wilayani Ngara wamewahimiza madereva kusitisha mgomo wa kuendelea na safari na kuutaka uongozi wa Burundi kuondoa vikwazo ili amani iweze kupatikana.

  • HABARI/PICHA: Shaaban Ndyamukama - Ngara, Kagera.


Dereva juu na chini Shaaban Juma Mohamed yeye alikamatwa na askari polisi wa Burundi, baada ya kukamata kijana aliyekuwa akichana turubali la gari lake kuiba mfuko wa ngano na mapigano yakaanza baina ya kijana huyo na utingo wa gari lake, naye katika kuwaamua ndipo alishambuliwa na askari wa Burundi kwa kupigwa mgongoni na mguuni.


Baada ya majadiliano ya muda mrefu wa viongozi wa pande mbili za mpakani, Kamanda wa Jeshi la Polisi wa mkoa wa Muyinga nchini Burundi, Kabura Jamali (katikati pichani) anayesimamia askari wa Kobero, aliahidi kuchukua hatua na kuwasihi madereva kuendelea na safari zao hadi Bujumbura na mikoa mingine ya nchi hiyo.