Mambo 6 ambavyo watu hujutia sana umri unaposonga na uzeeni

Naamini wote tunajua tunazaliwa, tunakua na ipo siku tutakuja fikia uzeeni. Hivyo kila mtu kwa kujua hilo, hujitahidi sana kuishi maisha ambayo hatakuja kuyajutia kwa hapo baadae akifika uzeeni. Kwa kifupi, kila mtu anapenda uzee wake uwe mzuri ambao hauna lawama.
Hakuna ambaye anapenda aje achekwe na watoto au wajukuu zake eti kwa kutotimiza majukumu fulani. Kila mtu anapenda watoto au wajukuu zake wamsifie kwamba kweli babu enzi za ujana wako ulifanya makubwa. Hilo ndilo kila mtu analolitamani litokee katika uzee wake.

Lakini hata hivyo kwa wengi waliofikia uzeeni kile wanachokitamani kiwe, huwa hawakipata kwa sababu kadhaa. Hujikuta wakiishi maisha ya kujuta sana. Majuto hayo hutokana hasa na mambo ambayo waliyafanya wakiwa vijana na kupelekea pengine maisha yao kuwa magumu.

Sitaki uwe miongoni mwa watu ambao wakifika uzeeni uje ujute kwa kulia sana. Leo nanawa mikono kwa kukuonyesha vitu vya msingi ambavyo wengi huvijutia sana kila wanapofika uzeeni. Sasa basi, vitu hivyo ambavyo wengi huvijutia sana hasa wanapofikia uzeeni ni kama hivi vifuatavyo;-.

1. “Kwa nini nilipoteza muda sana?”


Kati ya jambo la wazi ambalo wengi waliofikia uzeeni wanalojutia ni kule kupoteza muda. Huwa ni watu wa mawazo sana kutokana na lawama ambazo wanazipata kutoka kwa jamii, watoto au wajukuu zao.

Mara nyingi lawama hizi huelekezwa ni kwa nini maisha yao yako hivyo. Maswali kama babu ulikuwa wapi wakati wnzako wanawekeza huulizwa sana. kwa hali kama hiyo suala la kupoteza muda hujutiwa sana na wengi wakiwa uzeeni.

Wengi hujuta sana kwa kupoteza muda wao.


2. “Kwa nini sikuwekeza mapema?”


Si kupoteza muda tu ambapo wengi wanapofikia uzeeni hujutia. Ila wakati mwingine wanajuta kwa nini hawakuwekeza mapema wakati wa ujana wao. Hujiuliza maswali mengi kwa nini hawakununua mashamba, hawakujenga nyumba, au kwanini hawakufanya uwekezaji wa maana?

Hayo yote huibuka mara baada ya kujiona wao wapo mikono mitupu na hawana nguvu tena. Kilio, sononeko na majuto yanakuwa makubwa sana, hali ambayo inaweza kupelekea kupata magonjwa yasiyotarajiwa kama shinikizo la damu.

3. “Kwa nini sikuishi kwa kufuata ndoto zangu?”


Hili pia huwa ni jambo linaloleta majuto hasa kwa wengi wanaopofikia uzeeni. Kitu ambacho hujiuliza kila wakati kwa nini waliishi maisha ya kutimiza ndoto za watu wengine, badala ya kukaa chini na kutimiza ndoto zao. Hapa huwaza sana je, kipindi hicho walikuwa wamerogwa.
Hapa walio fikia uzeeni hujiona wana hatia na makosa makubwa sana ambayo waliyafanya wakiwa ujanani. Ukweli wote huo wanakuja kuujua baada ya kugundua kumbe hakuna hata kitu cha maana walichokifanikisha duniani zaidi ya kufanikisha ndoto za wengine na kusahau za kwao.

4. “ Kwa nini sikuwasaidia wengi kutimiza ndoto zao?”


Pia hufika mahali wale waliofikia uzeeni hutambua kwamba upo umuhimu mkubwa sana wa kuisaidia jamii, hata kwa kidogo walichonacho. Lakini kila wakiangalia hakuna msaada wa maana walioutoa. Hapo sasa ndipo huanza kuumia na kuwaza mengi.

Kiuhalisia, huwa ni kipindi kigumu sana. Hapo ndipo unapoona wanajaribu kutoa angalau msaada lakini inakuwa inashindikana kwa sababu pengine hawakujiweka vizuri kiuchumi. Majuto ya kutokuwasaidia wengine huwaumiza sana pia.

5. “Kwa nini sikujituma sana? ”


Wapo wengine ambao hujita na kujilaumu kwa sababu ya kuona kwamba walitakiwa kujituma sana hadi kufanikiwa. Sasa wanaona hawajafanikiwa na wanajua wazi hilo ni kosa lao. Kila wakati wanapata shida na kujiuliza kwa nini hawakujituma sana ili kujenga maisha mazuri zaidi.
Ikiwa kweli una kiu kubwa ya kutaka uzee wako uonekana wa maana, basi unalazimika kujituma sana kwenye kila jambo unalolifanya. Ikiwa hutajituma na kuweka misingi imara wakati ukijana, sahau kuwana mafanikio uzeeni na zaidi utalamikiwa na kujutia uzee wako wako wote.

6. “ Kwa nini sikuishi na familia yangu kwa upendo?”


Haya ni majuto huwa yapo wale wazee ambao kila wakikumbuka waliishi na familia kwa migogoro mibgi sana. pi hali hiyo ilipelekea hata kutengana na kujikuta wakiziacha familia zao zikiteseka.
Sasa inapofika kipindi chha uzeeni hujikuta wakijuta na kujilaumu ni kwanini hayo yote yalitokea. Ni kwa nini hawakuweza kuaysuluhisha mapema na kusababisha mgogoro ambao unawasumbua hapo wakiwa uzeeni.

Kwa kawaida unapokuwa kuwa kijana unaweza ukafanya makosa mengi na ukayachukulia kawaida. Lakini inapofika uzeeni ndio unaanza kuelewa kwa nini ulikosea kufanya hivyo.

Maisha yako yapo mkononi mwako, kama bado una nguvu, jifunze kuwajibika ili baadae usije ukajuta kwenye maisha yako ya uzeeni. Ukiangalia kwa ufupi hayo ndio baadhi ya mambo ambayo wengi hujutia wakifikia uzeeni mwao.

Endelea kutembelea dirayamafanikio.blogspot.com kujifunza kila siku.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,

Ni wako rafiki,
Imani Ngwangwalu,
Simu; 0713 048035,
Email: [email protected]