Mwanamichezo mahiri adhihirisha hasira dhidi ubaguzi wakati ulipoimbwa wimbo wa Taifa


Ubaguzi wa rangi ya ngozi umeendelea kuwakera na kuwaudhi hata wasiobaguliwa, kutokana na athari wanazoziona kwa jamaa na marafiki zao.

Ni hivi majuzi tu mitando ya kijamii na vyombo vya habari vililipuka kwa gumzo mara mbili

Mara ya kwanza ilikuwa ni baada ya Mmarekani aliyeliletea taifa lake sifa kwenye michezo ya Olimpiki, Gabby Douglas kuandamwa kwa maneno ya kashifa, kejeli, dharau na kuudhi kwa kutokuweka mkono kifuani kama ishara ya kuheshimu na kulipenda taifa lake wakati wimbo huo ukiimbwa mjini Rio de Janeiro, nchini Brazil mwaka huu.

Mara ya pili ilikuwa baada ya Mmarekani mwingine, Ryan Lochte aliyeshiriki Olimpiki izo hizo, kudanganya kuwa alishambuliwa na kuporwa katika moja ya vituo vya kuuzia mafuta nchini humo, kabla ya kugeuka na kukana kisha kuomba samahani baada ya watu kupaza sauti zao kuwa hili ni kosa kubwa lakini limepewa kisogo kutokana na rangi ya ngozi na jinsi ya mtu. 

Colin Kaepernick
Jana Ijumaa, mmoja wa wanamichezo maarufu wa mpira unaopendwa nchini Marekani "National Footbal League", Colin Kaepernick alidhihirisha hasira yake kwa kutokusimama kuonesha ishara ya heshima wakati wimbo wa taifa la nchi yake ulipokuwa ukiimbwa. Alipoulizwa sababu ya kutokufanya hivyo alisema:
"I am not going to stand up to show pride in a flag for a country that oppresses Black people and people of color," Kaepernick told NFL.com "To me, this is bigger than football and it would be selfish on my part to look the other way. There are bodies in the street and people getting paid leave and getting away with murder."
[...]
"This is not something that I am going to run by anybody," he said. "I am not looking for approval. I have to stand up for people that are oppressed. ... If they take football away, my endorsements from me, I know that I stood up for what is right."
Unaweza kusoma habari nzima: SBNation.com