Mwandishi habari EATV makahakani kwa tuhuma za kumuua kwa kumchinja dada yake

Mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha East Africa (EATV), Richard Steven na kaka zake wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kwa tuhuma za kumchinja hadi kufa dada yao aliyetajwa kwa jina la Celina Bugaisa, limeandika gazeti la MTANZANIA.

Steven na kaka zake, Robert Bugaisa (49) na Godfrey Stephen (39), wanatuhumiwa kutenda kosa hilo Julai 26, mwaka huu katika Mtaa wa Wazo Hill, Dar es Salaam.

Akisoma shtaka hilo mbele ya Hakimu Anipha Mngwira, wakili wa upande wa Jamhuri, Doroth Massawe, alidai washtakiwa walitenda kosa hilo huku wakijua kuwa ni kinyume cha sheria.

Hakimu Anipha alisema mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza shtaka hilo hivyo kesi yao itatajwa tena Agosti 26, mwaka huu.