Mzee Yusuf aomba watu na vituo vya redio na burudani visipige nyimbo tena zakeMfalme wa Muziki wa Miondoko ya Pwani (Taarabu) Afrika Mashariki na Kati, Mzee Yusuf leo ametangaza kuachana rasmi na muziki huo wa kidunia na kuamua kumrudia mwenyezi Mungu, imeripoti blogu ya Michuzi.

Mzee Yusuf ametangaza hivyo leo Ijumaa, Agosti 12, 2016 Muda mfupi baada ya kumaliza swala ya Ijumaa katika msikiti wa Ilala Bungoni (Masjid Taqwa) huku akibubujikwa na machozi mengi.

Mzee Yusuf ameomba waumini wamuombee msamaha kwa Allah kwa kipindi chote alichokuwa amemuasi na kadhalika amewaomba wanamuziki wengine ambao ni waislamu kuachana na muziki na kuzitumia fani zao walizonazo katika kutangaza na kumsifia bwana Mtume Muhammad (S.AW).

Aidha amewaomba watu wote wenye CD zake majumbani pamoja na vituo vya redio na televisheni kuacha kupiga nyimbo zake na wakikaidi wafahamu madhambi yote yatakuwa juu yao kwani yeye hivi sasa anafanya toba kwa Allah.