NW Kigwangalla ataka maelezo mezani kesho kuhusu upungufu wa chanjo


DKT. KIGWANGALLA ACHUKUA HATUA JUU YA UPUNGUFU WA CHANJO NCHINI

  • AAGIZA AKUTE MAELEZO MEZANI JUMATATU YA KESHO
  • ATAKA BAADHI YA MAAFISA WAJIPIME

Naibu Waziri wa Afya, Mhe. Dkt. Kigwangalla ameagiza yafuatayo akiwa ziara ya kikazi Mkoani Geita jana Agosti 20, 2016.

Amesema, "kuna maeneo chanjo zipo, na maeneo hazipo ama ndiyo wana dozi za mwisho. Hapa ni Geita, bohari ya chanjo ya Mkoa.

Hakuna #chanjo za OPV, Rotavirus, BCG na tetanus. Wangepaswa kuwa na stock ya miezi mitatu mbele. Kwenye ngazi ya Taifa wanapaswa kuwa Na chanjo za miezi Sita mbele ndiyo tuseme tuna 'availability'.

Naagiza nikute maelezo ya kina mezani kwangu Jumatatu, kuwa ni nani haswa amesababisha chanjo kupungua kwenye maeneo mengi nchini? 

Na mpaka sasa amechukuwa hatua gani za kuwajibika? Je, changamoto ipo hazina ama kwenye ofisi ya Mkurugenzi wa Huduma za kinga? Vyovyote vile, nataka utetezi uje ukiwa na vielelezo, kabla sijachukua hatua stahiki. 

Chanjo ni eneo pekee kwenye sekta ya Afya tulilofanikiwa Kwa zaidi ya 95%! 

Haikubaliki kurudisha nyuma mafanikio haya." 

#hapakazitu #siasanivitendo #baloziwawanawake #mzeewafield #dr_kigwangalla