Loading...
Wednesday

Polisi yahusisha UKUTA na vifo vya askari polisi katika benki ya CRDBKamishna Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Nsato Marijan Mssanzya (CP), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu tukio la mauaji ya askari wanne katika Benki ya CRDB Tawi la Mbande yaliyotokea usiku wa kuamkia leo.
Na Dotto Mwaibale

KUFUATIA mauaji ya askari wanne yaliyotokea Kata ya Mbande Temeke kwa watu wanaodhaniwa ni majambazi kuvamia benki ya CRDB na kuwaua askari hao kwa kutumia silaha za moto jeshi la Polisi limetangaza kiama na kuwataka wahusika wote kujisalimisha.

Katika hatua nyingine jeshi la polisi limehusisha tukio hilo na Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (UKUTA) kufuatia matamko ya baadhi ya viongozi wa kisiasa ambao wamesikika katika majukwaa ya kisiasa wakihamasisha wafuasi wao wawashambulie askari wa Jeshi la Polisi.

Kauli hiyo imetolewa na Kamishna Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Nsato Marijan Mssanzya (CP), wakati akizungumza waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana ambapo pia alikiri kuwa mazoezi yanayofanywa na polisi yamelenga kukabiliana na Ukuta.

Akizungumza kwa hisia CP Mssanzya pia alipiga mikutano ya ndani yenye viashiria vya uchochezi na hata ikifanyika kwenye majukwaa watamshusha muhusika na kumfikisha kwenye mkono wa sheria.

Aidha CP Mssanzya aliwataja askari waliouawa katika tukio hilo wakati wakibadilishana lindo kuwa ni E.5761 CPL Yahya, F.4660 CPL Hatibu, G 9524 PC Tito na G 9996 PC Gastoni na raia wawili waliojeruhiwa aliowataja kuwa Ali Chiponda na Azizi Yahya wote wakiwa wakazi wa Mbande.

"Katika tukio hilo majambazi ambao idadi yao haikufahamika walifanikiwa kupora silaha mbilo aina ya MSG na lisasi 60 na hakuna pesa wala mali ya benki hiyo kuibiwa au kuharibiwa, ni dhahiri kuwa waharifu hao walikuwa na kusudio moja tu la kuwashambiulia askari polisi, " alisema.

Alisema katika hali ya kushangaza baada ya tukio hilo kuna baadhi ya watu waliandika mitandaoni kubeza na kukeji mazoezi ya kawaida ya jeshi la polisi na wengine waliandika ujembe wa kushabikia tukio hilo la kuuawa kwa askari polisi huku wengine wakidiriki kuandika ujumbe unaosema endapo watapigwa na polisi Srptemba1 mwaka huu basi viongozi wa jeshi hilo wawaondoe askari wanaoishi uraiani na kuwarudisha kambini.

Aliongeza kuwa jeshi la polisi limejipanga vema kukabiliana na matukio yote ya uvunjifu wa amani nchini.
  • Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062 na kushirikishwa kwetu. Imechapishwa hapa wavuti.com ilivyo (yaani "as is") hivyo ikiwa kuna makosa ya aina yoyote, tafadhali wasiliana na mwandishi. 


Mwigulu Nchemba"Usiku huu nimefika Mbande - Temeke,eneo lilipofanyika tukio baya la uhalifu wa kutumia silaha ambapo watu/majambazi zaidi ya saba wakiwa na silaha wamevamia eneo la Benki ya CRDB-Mbande na kuua askari 4 waliokuwa wakishuka kwenye gari tayari kwa kupokezana lindo. Pia wamejeruhi raia wa kawaida wawili,nimewajulia hali zao na wote wanaendelea vizuri.
Hatutaishia kulaani tu tukio hili na matukio mengine kama haya,natoa rai kwa wahusika kujisalimisha.Vilevile wananchi na raia wema tunaomba ushirikiano wenu katika vita hii ya kupambana na wahalifu hawa na wanaotuzunguka kwenye maeneo yetu."
KUFUATIA mauaji ya askari wanne yaliyotokea Kata ya Mbande Temeke kwa watu wanaodhaniwa ni majambazi kuvamia benki ya CRDB na kuwaua askari hao kwa kutumia silaha za moto jeshi la Polisi limetangaza kiama na kuwataka wahusika wote kujisalimisha.

Katika hatua nyingine jeshi la polisi limehusisha tukio hilo na kile kinachoitwa Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (UKUTA) kufuatia matamko ya baadhi ya viongozi wa kisiasa ambao wamesikika katika majukwaa ya kisiasa wakihamasisha wafuasi wao wawashambulie askari wa Jeshi la Polisi.

Kauli hiyo imetolewa na Kamishna Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini, Nsato Marijan Mssanzya (CP), wakati akizungumza waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana ambapo pia alikiri kuwa mazoezi yanayofanywa na polisi yamelenga kukabiliana na Ukuta.

Akizungumza kwa hisia CP Mssanzya pia amepiga marufuku mikutano ya ndani yenye viashiria vya uchochezi na hata ikifanyika kwenye majukwaa watamshusha muhusika na kumfikisha kwenye mkono wa sheria.

Amesema Jeshi hilo limebaini kwamba mikutano hiyo imekuwa ikitumika kuchochea wananchi na kuwahamasisha kuvunja sheria za nchi na kufanya mapambano na jeshi la polisi

“Kwa sababu hiyo basi,kwa hali ya kutumia mikutano ya ndani kuchochea watu kuvunja sheria na kupambana na askari, hivyo basi kuanzia sasa jeshi la polisi nchini linapiga marufuku mikutano yote ya ndani” amesema.

Aidha CP Mssanzya aliwataja askari waliouawa katika tukio hilo wakati wakibadilishana lindo kuwa ni E.5761 CPL Yahya, F.4660 CPL Hatibu, G 9524 PC Tito na G 9996 PC Gastoni na raia wawili waliojeruhiwa aliowataja kuwa Ali Chiponda na Azizi Yahya wote wakiwa wakazi wa Mbande.

“Katika tukio hilo majambazi ambao idadi yao haikufahamika walifanikiwa kupora silaha mbili aina ya MSG na lisasi 60 na hakuna pesa wala mali ya benki hiyo kuibiwa au kuharibiwa, ni dhahiri kuwa waharifu hao walikuwa na kusudio moja tu la kuwashambiulia askari polisi, ” alisema.

Alisema katika hali ya kushangaza baada ya tukio hilo kuna baadhi ya watu waliandika mitandaoni kubeza na kukeji mazoezi ya kawaida ya jeshi la polisi na wengine waliandika ujembe wa kushabikia tukio hilo la kuuawa kwa askari polisi huku wengine wakidiriki kuandika ujumbe unaosema endapo watapigwa na polisi Septemba1 mwaka huu basi viongozi wa jeshi hilo wawaondoe askari wanaoishi uraiani na kuwarudisha kambini.

Aliongeza kuwa jeshi la polisi limejipanga vyema kukabiliana na matukio yote ya uvunjifu wa amani nchini.

1 comments :

  1. Habari hizi zote hapa ukweli umejificha.inteligensi ya nchi ikiingiza mambo ya kisiasa kama hivi nchi imekwisha. Kusuka jambo, kuunganisha mambo hakutaleta amani wala suluhishi lolote nchini na linazidi kuleta uchochezi pia kutoka usalama yenyewe.. ni jambo tete. Wengi hawawezi kuliona.haya mambo yote ya umuta, serikali ingeepusha zamani sana. Lakini haiko kwenye utatuzi ipo kwenye tit kwa tat ambayo imekosa mwelemeo wa kutaka kuunganisha nchi hii. Haya yote yamesababishwa na serikali yenyewe kuwa ya kibabe, kutokufuata sheria za katiba. Watu wakiogopa kusema ukweli patakiwapo matomeo ni haya. Wazee wanazunguka kushindwa kwaambia viongozi mmekosea. Mnatafuta ushuruhishi bila kumwita na kumkalisha chini mhusika mkuu kubadili mwrnendo, na kauli chafu na zinazoleta mgawanyo kivyama. Raisi anaposimama jukwaani aweme maslahi ya watanzania wote kwanza na mbele zidi ya chama chake. Ameamua kutetea chama jukwaani kila siku na kuwaweka watanzania pembeni. Kwa nini asiambiwe ukweli. Anapokataza wapinzani waliochaguliwa kufuata utaratibu, akawLazimu wWe mabubu, na kujiruhusu yeye peke yake na wakuu wa mikoa, wilaya, akijua wote ni ccm, na kwa nini watanzania tusilione hili tatizo na wote tukalipinga hadharani na tukijua tuna uhuru huo? Na kwa nini tukae kimya tunapoona pisi wanaruhusiwa kutangaza vita kuua watu ambao wanahami asilimia miMoja juandamana. Na tupo radhi kutumia tofauti ki hama kubambimiza kesi siku hadi siku. Hawa polisi wameuawa na majambazi ambao wameshindwa muwazatiti wsmeelekeza nguvu zao zote kujiandaa kuwafyeka chdema tarehe mosi. Hawa majambazi ni werevu wanatumia weekness ya maono potofu na mufanya uhalifu wakijua serikali na polisi wataunganisha moja mwa moja na chadema. Tanzania inahitaji inteligensi mpya ya kisomi inayoendana na mabadiliko ya sasa kisiasa.ama la ndo hivyo mnswapa fursa mJambazi kufanya hili na maovu mengine sababu nguvu zote mmezoelekeza chadema na upinzani.. namwona Zitto kimya .yujo wapi sasa. Je anafurahia pia kuona chadema wanaburuzwa na chama chake je. Kafyata kimya au anaunga ccm. Ili aibuke kwa wengine kunyanyaswa.

    ReplyDelete

 
Toggle Footer
TOP