Rais wa Chama cha Hemophilia Tanzania Richard Minja ashiriki WFH 2016 World Congress


TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA KIMATAIFA WA HEMOPHILIA2016, MAREKANI

Kongamano la Kimataifa kuhusu ugonjwa wa Hemophilia limemalizika Orlando, nchini Marekani Julai 24-28, 2016. 

Hemophilia ni ugomjwa wa damu wa kurithi ambapo damu inakosa uwezo wakuganda pale mshipa unapodhurika. Huwapata zaidi watoto wa kiume.

Kongamano hilo lilikutanisha zaidi ya wadau 6,000 kutoka takribani nchi 130 duniani chini ya World Federation of Hemophilia (WFH). Malengo makuu yalikuwa kuboresha tiba na maisha ya wagojwa.

Pamoja na mambo mengine, kongamano ni jukwaa la kutambua jitihada zinazofanyika duniani kote hususani utafiti wa kupata tiba na uangalizi bora kwa wagonjwa. Hutengeneza jukwaa na mtandao kwa wagonjwa, wazazi/jamaa, madaktari bingwa, wahudumu, watengeneza sera na watafiti wa dawa na kujenga mahusiano na baraza la kubadilishana uzoefu na utaalamu kwa washiriki toka sehemu mbalimbali duniani.

Moja ya mafanikio ni ugunduzi wa dawa (factors) zenye uwezo wa kufanya kazi mwilini kwa muda mrefu zaidi (longer half-life drugs) na hivyo maisha bora kwa wagonjwa. Pili ni upatikanaji wa misaada (donations) ya dawa kutoka makampuni yanayotengeneza dawa kwa nchi maskini. 

Ikumbukwe nchi hizi hazimudu kununua dawa kwa wagonjwa kutokana na bei yake kuwa kubwa. 

Tanzania imewakilishwa na Raisi wa Chama cha Hemophilia Tanzania Bw. Richard Minja.
Richard Minja at the Orlando, Florida summit