Taarifa ya Polisi Dar: Kukamatwa silaha; Kuuawa majambazi; Sare za UKUTA


KUUAWA MAJAMBAZI HATARI 03 JIJINI DAR WAPATIKANA NA RISASI 300 ZA SMG NA MAGAZINE 10


KUKAMATWA KWA BASTOLA AINA YA BWOWNING NA RISASI 06

Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 22.08.2016 03:45 hrs huko maeneo ya Mabibo Loyola, kata ya Mabibo (W) Magomeni kikundi cha Ulinzi shirikishi wa eneo hilo wakiwa kazini waliona kundi la watu kati ya watu watatu hadi wanne wakiwa wanatembea.

Baada ya kuwaona waliwatilia shaka na kuwasimamisha iliwaweze kuwahoji. Hata hivyo katika mahojiano watuhumiwa wengine walifanikiwa kukimbia ambapo mtuhumiwa mmoja mwanaume asiyefahamika anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka (20 – 25) alikamatwa.

Baada ya mtu huyo kukamatwa alianza kuwatishia kuwa atawaua huku akitamka maneno ya kiislam akisema ”Taqbir” na “Allah Huaqbar “ ghafla mtu huyo aliingiza mkono mfukoni na kutoaa kitambaa cha kufuta jasho na kukitupa chini ambapo bomu lililipuka. Kuona hivyo ulinzi shirikishi walikimbia na mtu huyo kuanza kukimbia huku akiwa na begi mgongoni. Hata hivyo mmoja kati ya hao ulinzi shirikishi alimpiga mtuhumiwa huyo rungu kichwani eneo la kisogoni, pamoja na kupigwa rungu kichwani mtu huyo aliendelea kukimbia na alitupa begi chini na kuendelea kukimbia. Ulinzi shirikishi nao waliendelea kumkimbiza na kufanikiwa kumkamata ambapo wananchi walijitokeza na kumpiga hadi kufa kisha kumchoma moto. Askari polisi baada ya kupata taarifa hizo, walifika eneo la tukio ambapo ulifanyika upekuzi katika begi hilo na kukutwa magazine 10 za SMG zikiwa na jumla ya risasi 300.

Hadi sasa askari wapo eneo la tukio wakifanya upekuzi katika nyumba mbalimbali kuwatafuta watuhumiwa wengine ambao inasadikiwa bado wapo eneo hilo. Msako mkali unaendelea kuwatafuta watuhumiwa hao waliokimbia.

KUUAWA KWA MAJAMBAZI WAWILI KATIKA MAJIBIZANO YA ANA KWA ANA

Katika tukio lingine tarehe 21.08.2016, saa 21:30hrs usiku huko Tandika Mtaa wa Chiwanda nyumba no. 08 Mkoa wa Temeke, Kikosi Maalum cha Kupambana na Ujambazi wa kutumia silaha cha Polisi Kanda Maalum Dar Es Salaam kilifanikiwa kuwaua majambazi wawili katika majibizano ya risasi ya ana kwa ana.

Tukio hilo lilitokea katika maeneo hayo ambapo askari walipata taarifa kutoka kwa msiri kuwa kuna kundi la majambazi wanataka kuvamia nyumba hiyo.

Mara baada ya kupokea taarifa hizo Askari walifika eneo la nyumba hiyo kabla ya majambazi hao hawajaanza kupora ambao idadi yao walikuwa watano wakiwa na pikipiki mbili ambazo hazikusomeka namba.

Baada ya majambazi hayo kugundua kuwa wanafuatiliwa majambazi hayo walianza kuwafyatulia askari risasi ambazo hazikuleta madhara, ndipo askari walijibu mapigo na kufanikiwa kuwapiga risasi majambazi wawili wanaume umri kati ya miaka (25 – 30), ambao walifariki dunia papo hapo na wengine watatu walifanikiwa kutoroka.

Katika upekuzi mmoja wa majambazi hao alikutwa na bastola moja aina ya Browining ikiwa na risasi 06 namba zake zikiwa zimefutwa. Jitihada za kuwatafuta majambazi waliokimbia unafanyika na upelelezi unaendelea.


KUPATIKANA KWA SARE AINA YA FULANA ZENYE MANENO YA UCHOCHEZI ZIKIWA NA ALAMA YA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm mnamo tarehe 20/08/2016 majira ya saa 12:00 jioni lilipata taarifa toka kwa raia wema kuwa maeneo ya mtaa wa Ufipa Kinondoni kuna duka linauza flana rangi mbalimbali zenye maneno ya uchochezi yaliyoandikwa ‘’TUJIPANGE TUKATAE UDIKITETA UCHWARA’’ rangi nyeupe idadi yake 28, rangi nyekundu fulana 18 zenye maneno ‘UKUTA’ fulana 6 za Kakhi zenye maneno ‘’UKUTA’ Na fulana zingine rangi nyeusi 23 zenye maneno ’’UKUTA’’.

Aidha Polisi baada ya kupata taarifa hizo walifika eneo la tukio na kumkamata mtuhumiwa aitwaye YORAM SETHY MBYELLAH miaka 42, mfanyabiashara, mkazi wa Mburahati akiwa anauza fulana hizo dukani kwake. Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na baada ya upelelezi kukamilika atafikishwa mahakamani.

KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA KWA KOSA LA WIZI WA GARI

Mnamo tarehe 09.08.2016 saa 18:00hrs jioni huko Masasi Mjini kwenye gereji ya magari, Kikosi Maalum cha Kupambana na wizi wa Magari cha Polisi Kanda maalum cha Dar Es salaam kimefanikiwa kumkamata mtuhumiwa OMARY GILLIAD OMARY (35) kazi dereva kwa wizi wa gari. Mtuhumiwa alikamatwa kwa wizi wa gari No: T.612 AUJ aina ya Toyota Hiace mali ya mlalamikaji KAISARI MWALIMU YUSUFU (26) Mfanyabiashara mkazi wa Sinza.

Gari hilo iliyoibiwa tarehe 25.06.2016 likiwa limeegeshwa nyumbani kwa mlalamikaji maeneo ya Sinza ambapo mtuhumiwa alichukua gari hilo kwa nia ya kufanya kazi.

Baada ya mtuhumiwa kupewa gari hilo aliipeleka mafichoni Masasi Mjini mkoani Mtwara ambapo Kikosi cha Kupambana na Wizi wa Magari Cha Polisi Kanda Maalum ya Dar Es salaam kilifanya ufuatiliaji na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa pamoja na kielelezo gari. Mtuhumiwa anahojiwa na upelelezi utakapokamilika atapelekwa mahakamani kujibu shutma inayomkabili dhidi yake.

KINARA MWIZI WA VIFAA VYA MAGARI AKAMATWA AKIWA NA VIFAA MBALIMBALI VYA MAGARI

Kikosi maalum cha kupambana na wizi wa magari cha Polisi Kanda Maalum Dar Es Salaam kimefanikiwa kumkamata mtuhumiwa hatari anayejihusisha na wizi wa magari na viafaa vyake. Mtuhumiwa huyo alikamatwa tarehe 01/08/2016 majira ya saa 08:30 usiku, maeneo ya amani mtaa wa kongo askari wakiwa doria walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja aitwaye SALUMU S/O ISSA @HASSANI (43) Mkazi wa mbagala akiwa na (1).SIDE MIRROR 12 (2). SITE MIRROR 11(3) CAMP BAMPA 24 (3).PLATE SIDE MIRROR 44 (4) VITASA28 (5).SIDE LAMP 11 (6).INDICATOR 17 vifaa hivyo Vyote vikiwa ni mali za wizi akiwa ameviiba na baada ya kumhoji alikiri kuhusika na wizi huo. Mtuhumiwa huyo atapelekwa mahakamani wakati wowote upelelezi utakapokamilika.

TAARIFA YA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI KANDA MAALUM YA D’SALAAM KUANZIA TAREHE 21.08.2016 HADI TAREHE 22.08.2016.

Taarifa ya Kikosi cha Usalama barabarani Kanda Maalum ya D’salaam ya ukamataji wa makosa ya Usalama Barabarani kwa kipindi cha kuanzia tarehe 21.08.2016 hadi tarehe 22.08.2016 ni kama ifuatavyo:-
  1. Idadi ya magari yaliyokamatwa 5,346
  2. Idadi ya Pikipiki zilizokamatwa 216
  3. Daladala zilizokamatwa 1,121
  4. Magari mengine (binafsi na malori) 225
  5. Jumla ya Makosa yaliyokamatwa 20,562
Jumla ya fedha za Tozo zilizopatikana TSH 161,750,000/=

S.N.SIRRO – CP
KAMISHNA WA POLISI
KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM