U.S.A. pledges $407 million aid to Tanzania

REUTERS, Mon Aug 1, 2016 -- The United States pledged $407 million aid to Tanzania on Monday, months after cancelling a similar payment due to an election that it said had violated the country's commitment to democracy.

The U.S. Millennium Challenge Corporation (MCC) canceled a $473 million aid package in March after elections in the Zanzibar archipelago that it said were not free and fair. It said at the time that other aid commitments would not be affected.

Haji Semboja, an economics professor at the University of Dar es Salaam, told Reuters the new assistance implied that Washington was satisfied with ongoing government reforms.

"Although the MCC initiative and this new funding are two separate programmes, this new aid commitment is a sign that Tanzania is heading in the right direction," he said.

The U.S. embassy said the $407 would be disbursed this year to support the areas of health, agriculture, natural resource management, education, energy and democratic governance.

It is part of a five-year aid deal signed between the U.S. Agency for International Development (USAID) and Tanzania on Monday and constitutes half of the U.S. government's expenditure on development in Tanzania, the U.S. embassy said.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Leo tarehe 1 Agosti 2016, Bi Sharon Cromer Mkurugenzi Mkazi akiwakilisha Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) na Dk. Servacius Likwelile, akiiwakilisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamesaini mkataba wa miaka mitano wa msaada wa USAID kwa Tanzania (five-year strategic assistance agreement). Kwa kupitia mkataba huu, Marekani, kwa uratibu kamili wa Serikali ya Tanzania, inalenga kuisaidia Tanzania kufikia azma yake ya mageuzi ya kiuchumi na kijamii na kuwa nchi yenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. Chini ya mkataba huu, mwaka huu, Serikali ya Marekani kupitia USAID inatarajia kuwekeza nchini Tanzania Dola za Kimarekani milioni 407 katika sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na sekta za afya, kilimo, usimamizi wa maliasili, nishati na utawala wa kidemokrasia. Uwekezaji huu wa Dola za Kimarekani milioni 407 ni nusu ya bajeti ya mwaka ambayo Serikali ya Marekani hutumia kwa maendeleo na miradi mingine ya pamoja nchini Tanzania ambayo baadhi hutekelezwa na Serikali ya Tanzania na mingine hutekelezwa na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayofanya kazi nchini Tanzania.

Kwa taarifa zaidi kuhusu mkataba huu, tafadhali wasiliana kwa barua pepe na Japhet Sanga ([email protected]), Afisa Habari Mwandamizi wa Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam au Bw. Benny Mwaipaja, ([email protected]), Kaimu Afisa Habari Mkuu wa Serikali – Wizara ya Fedha, Dar es salaam.