Wawakilishi wa Tanzania wazungumzia kongamano la YALI 2016, Washington DC


Stanley Magesa (mjasiriamali) akifafanua jambo ndani ya studio kuhusu YALI 2016
Wawakilishi wa Tanzania YALI 2016 walipata fursa ya kutembelea katika studio mbalimbali na kuhojiwa hao ni baadhi ya Watanzania wanaowakilisha kwenye mkutano wa Mandela Washington Fellowship - Young African Leaders Initiative (YALI) 2016 waliomaliza mkutano wao hapa Washington DC Walikuwa wakarimu sana kujiunga nasi Studio na kuzungumza nasi kuhusu mambo mbalimbali.
Karibu uwasikilize


Heri Emmanuel (kati kutoka Mwanza) akieleza jambo huku Tusekile Mwakalundwa ( Mhadhiri na Mwanasheria kutoka Arusha) akisikiliza kwa makini. Kulia ni Mubelwa Bandio wa Kwanza Production na Vijimambo Radio

Baadhi ya wawakilishi wa YALI 2016 kutoka Tanzania, wajasiriamali Stanyey Magesa (Mwanza), Simon Malugu (Morogoro) na Lusajo Mwaisaka (Dar) wakiwa kwenye mahojiano Kilimanjaro Studio.

Mshiriki wa YALI 2016 Heri Emmanuel (Mwanza) kulia akaifafanua jambo huku akisikilizwa na mshiriki mwenzake ambaye pia ni Mhadhiri na Mwanasheria Tusekile Mwakalundwa (Arusha) na mjasiriamali na Lusajo Mwaisaka (kutoka Dar)