Waziri Ummy Mwalimu akizungumza mbele ya watumishi wa MO alipokwenda kusikiliza changamoto za watumishi hao leo |
Akizungumza na watumishi wa MOI Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amemtaka Dkt. Kiloloma kukaa na bodi ya taasisi hiyo ili kupata ufumbuzi wa matatizo ya watumishi wake ndani ya siku 14 ili wafanyakazi waweze kutoa huduma bora kwa watanzania.
“Naagiza Bodi ya MOI pamoja na Kaimu Mkurugenzi wake ili kupata ufumbuzi wa matatizo ya watumishi wake ndani ya siku 14 ili kuondoa malalamiko na kuleta ufanisi bora katika taasisi hii”alisisitiza Mhe. Ummy.Aidha Mhe. Ummy amesema kuwa amepokea changamoto zao na za taasisi hyo nakuhaidi kuzitatua ndani ya mwezi mmoja na kuwataka wasichoke kutoa huduma bora kwa watanzania ili kuokoa maisha yao na kupambana na umaskini.
Mbali na hayo Mhe. Ummy ameagiza watendaji wa Wizara yake kuleta mkakati wa kupambana na kupunguza ajali za barabarani hasa zitokanazo na bodaboda ndani ya siku 14 ili kuwapa nafuu madaktari na wauguzi wa MOI kuweza kuondoa mlundikano wa wagonjwa hospitalini hapo.
Kaimu Mkurugenizi wa MOI Dkt. Othman Kiloloma |
Aidha Dkt. Kiloloma ameongeza kuwa MOI imeweza kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 1.1 kwa mwezi kutoka kiasi cha shilingi milioni 400 kwa kipindi kilichopita.
Baadhi ya watumishi wa MOI wakimsikiliza kwa makini Waziri Mwalimu |
- Imenukuliwa kutoka kwenye blogu ya serikali