Yaliyosababisha ITV, Clouds Tv & Radio kupigwa faini na TCRA

Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania leo imevitoza faini ya jumla Sh19m vituo vya utangazaji, ITV, Clouds TV na Redio Clouds kwa kukiuka kanuni za utangazaji.

TCRA wanasema Clouds Media imepigwa faini hiyo kutokana na kosa la kushabikia mapenzi ya mbuzi na binadamu kwenye chombo chao cha habari na kupiga wimbo wa mwanamuziki Mwana FA ambao unapaswa kupigwa muda maalumu ambao wameagizwa.

ITV wamepigwa faini hiyo kutokana na kipindi kutoka bungeni kilichokuwa kinaoongozwa moja kwa moja, ambapo Mbunge wa Iringa Mjini alisikika akisema, "Naibu Spika amekuwa kama anavaa pampas, hataki kubanduka kwenye kiti kuongoza bunge".

TCRA imewakumbusha wadau wote kufuata sheria na maadili ya utangazaji ili kuepuka adhabu na ukiukwaji wa maadili.