Agizo la Rais Magufuli baada ya kutembelea Uhuru Publications na shangwe za wafanyakazi alipoondoka

Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akiwasalimia wananchi waliojitokeza katika Mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam, wakati akitoka Ofisini kwake, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, katika Mtaa huo, kwenda Ofisi za Kampuni ya Uhuru Publications Limited, Wachapishaji wa Magazeti ya Uhuru, Mzalendo na Burudani leo.


Wafanyakazi wa kampuni ya Uhuru Publications wameichongea bodi ya wakurugenzi wa kampuni hiyo kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli kuhusu uuzwaji kinyemela wa mtambo wao wa kuchapisha magazeti.

Hayo yamebainishwa leo na wafanyakazi hao baada ya Rais Magufuli kuwatembelea na kusikiliza matatizo yao na changamoto wanazokumbana nazo.
"Mmesema mtambo wenu umeuzwa kama chuma chakavu kwa Sh 6 milioni alafu na mnatumia Sh 52 milioni kuchapisha magazeti kwa mwezi, kwani mtambo wenu ulikuwa umeharibika sana kiasi kwamba ulishindikana kutengeneza mkaokoa kiasi hichi cha fedha," alisema Rais Magufuli.
Mtambo huo wa kuchapisha magazeti ulinunuliwa kwa Sh 200milioni kutoka Bulgaria na ulisitisha huduma ya kuchapisha magazeti hayo tangu 2012 ambapo kwa sasa kampuni hiyo inachapisha katika mtambo wa Jamana kwa Sh 52 milioni kwa mwezi.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akifuatana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipowasili katika Ofisi za Uhuru Publications Limited mtaa wa Lumumba, Da es Salaam, ambako baada ya kutembelea baadhi ya ofusi za kampuni hiyo alizungumza na wafanyakazi ambapo ameahidi kutatua kero zinazowakabili kwa muavuli wake wa uenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akifuatana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipowasili katika Ofisi za Uhuru Publications Limited mtaa wa Lumumba, Da es Salaam, ambako baada ya kutembelea baadhi ya ofusi za kampuni hiyo alizungumza na wafanyakazi ambapo ameahidi kutatua kero zinazowakabili kwa muavuli wake wa uenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akiwasilikiliza wafanyakazi wa UPL alipowasili katika ofisi hizo leo. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana

Mkuu wa Kitengo cha kompyuta, wa UPL, Moses Makambi akimpatia maelezo Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli, alipoingia chumba cha Usanifu wa kurasa

Mkuu wa Kitengo cha kompyuta, wa UPL, Moses Makambi akimpatia maelezo Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli, alipoingia chumba cha Usanifu wa kurasa

Mkuu wa Kitengo cha kompyuta, wa UPL, Moses Makambi akimpatia maelezo Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli, alipoingia chumba cha Usanifu wa kurasa, Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana

Kaimu Mharuri Mtendaji wa UPL. Ramadhani Mkoma akiongoza Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli kuingia katika chumba cha habari kuzungumza na wafanyakazi

Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli akiingia katika chumba cha Habari cha Uhuru Publications kuzungumza na wafanyakazi


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpatia maelezo ya utangulizi, Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli. Kushoto ni Kaimu Mhariri Mtendaji, wa UPL Ramadhani Mkoma

Wafanyakazi wakiwa ukumbini

Wafanyakazi wakifuatilia kwa makini mazungumzo yao na Rais Dk. Magufuli

Mwenyekiti wa CCM, Dk. John Magufuliu akiandika wakati Kaimu Mhariri Mtendaji wa UPL Ramadhani Mkoma akieleza changamoto zinazowakabili wafanyakazi katika utendaji kazi wao wa kila siku

Baadhi ya wafanyakazi wakishangilia baada ya Mwenyekiti wa CCM, Dk. John Magufuli kuahidi kushughulikia kero zao kwa nafasi yake ya Ueneyekiti wa CCMMwenyekiti wa CCM Rais Dk. Magufuli akimsikiliza Kaimu Mhasibu Mkuu wa UPL huku akinukuu dondoo muhimu

Mwenyekiti wa Chama Cha Wafayakazi wa UPL cha RAAWU, Moses Makambi akieleza changamoto kwa Dk. Magufuli
Ukumbi wakati wa mkutano wa wafanyakazi wa UPL na Mwenyekiti wa CCM, Dk. Magufuli

Katibu Mkuu wa CCM, akimfafanulia jambo Dk. Magufuli

Wafanyakazi wakiwa wametulia kufuatilia alichokuwa akisema, Dk Magufuli

Dk. Magufuli akitaka ufafanuzi wa jambo kutoka kwa Kaimu Mhariri Mtendaji wa UPL

Mfayakazi wa UPL Fred Majaliwa akieleza kero anazooma zinakwamisha utendaji wa kazi za UPL

Rhoda Kangero kutoka Idara ya Rasilimali watu, akieleza kero na changamoto

Wafanyakazi wa UPL wakimuombea dua Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli

Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akiondoka ofisi za UPL baada ya kuzungumza na wafanyakazi leo Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na watatu kushoto ni Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimshauri jambo, Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli nje ya Ofisi za UPL. Kulia ni Msemaji wa CCM, Christopher Ole Sendeka


Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akiwasalimia wananchi kabla ya kuondoka baada ya kuzungumza na wafanyakazi wa UPL

Wafanyakzi wa UPL wakimshangilia Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli wakati akiondoka

ZIFUATAZO NI SHAMRASHAMRA ZA WAFANYAKAZI WA UPL, BAADA YA UJIO WA DK. MAGUFULI KATIKA OFISI ZAO LEO

  • PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO