Anauliza Fungo: Unafanyaje usiku mnene barabarani unakutana na hii

UPDATE, 25 Septemba 2016: Nimekutana na maelezo kwenye blogu ya Cuthbert Kajuna, yanayoambatanana na picha niliyopachika hapo nini siku kadhaa zilizopita..
..Kuna Vijana wa maeneo ya Mapinga Kerege Bagamoyo - Pwani wanaigiza uvaaji wa nguo kana kwamba ni JINI.... na kichwani huwa wanafunga vitochi vikali mfano wa macho hivyo ukikutana nacho usiku hasa utumiapo Bajaji au Pikipiki. Pia wanasimama pembeni ya barabara na kujifanya kama wanakusimamisha, madereva wa pikipiki au bajaj hata wanaopita na MISIBA nawanapoona hivyo huacha vyombo na kukimbia kwa kiwewe hapo hao vibaka huiba wanachotaka kuchukua na kutokomea gizana...Hii imetokea mda si mrefu maeneo ya Bunju karibu na darajani... kuja jamaa kachukuliwa Bajaji. Hivyo tunatoa tahadhari kwa Mtu Yeyote atakayekutana na hali hii usisimame.