Baada ya taarifa ya jana, TRA yazungumza leo

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi TRA, Richard Kayombo, akizungumza na waandishi wa Habari Dar es Salaam leo
KATIKA harakati za kuhakikisha kuwa Mapato yote stahiki yanakusanywa ipasavyo na kwa Wakati, Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imejiwekea mikakati mbalimbali ya kuongeza wigo wa vyanzo vya Mapato pamoja na kukusanya Mapato kikamilifu.

Mikakati hiyo ni kama ifuatavyo;
  • Kulifanya eneo la Kariakoo kuwa Mkoa Maalumu wa Kodi kutokana na eneo hilo kuwa kitovu cha biashara hapa nchini na kuhakikisha kila mfanyabiashara anakuwa na Mashine ya Kielektroniki ya kodi (EFDs) na kuitumia ipasavyo.
  • Katika kutekeleza hilo Mawakala wote wa EFDs wamefungua ofisi ya pamoja katika jengo la Al-Falah Towers lililopo mtaa wa Msimbazi Kariakoo ili kurahisisha upatikanaji wa mashine hizo na kutatua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara katika matumizi ya mashine hizo.
Aidha Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi TRA Bw. Richard Kayombo ametoa wito kwa wananachi na wafanyabiashara kujitokeza kuhakiki taarifa zao za usajili wa TIN kabla ya Tarehe 15 Oktoba 2016 katika vituo vifuatavyo kwaajili ya zoezi hilo kwani muda hautaongezwa baada ya tarehe hiyo maana baada ya tarehe hiyo zoezi hili litahamia mikoa mingine.

Vituo hivyo vya uhakiki ni pamoja na:
  1. Mkoa wa Kodi Ilala: Jengo la Mariam Tower (Shaurimoyo) na 14Rays (Kariakoo-Gerezani)
  2. Mkoa wa Kodi Kinondoni: Jengo la LAPF (Kijitonyama) na Kibo Complex (Tegeta) na ofisi za TRA Kimara.
  3. Mkoa wa Kodi Temeke: Uwanja wa Taifa na Ofisi za TRA Mbagala- Zakiemu
  4. Wilaya ya Kigamboni: Ofisi za TRA Kigamboni
Pamoja na kuhakiki taarifa zao, wafanyabiashara wote ambao hawana TIN nchini wanaombwa kufika katika ofisi ya TRA iliyoko karibu nao ili kujisajili kuepuka kukumbwa na msako unaondelea hivi sasa nchi nzima pamoja na uhamasishaji.

Wakati huo huo Bw. Kayombo amewahimiza wamiliki wa vituo vya mafuta kutekeleza agizo la Serikali la kufunga mashine za EFDs kabla au ifikapo tarehe 30 Septemba 2016 kwani kinyume na hapo ukaguzi utaanza kufanyika kuanzia tarehe 1 Oktoba na hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wale wote watakaobainika kukiuka agizo hilo.

Katika kuhakikisha kwamba kodi ya ongezeko la thamani VAT inakusanyawa kwa Wakati Mamlaka inawakumbusha walipakodi wote waliosajiliwa na Kodi ya Ongezeko la Thamani - VAT kuwasilisha ritani ya kila mwezi kabla au tarehe 20 ya kila mwezi badala ya tarehe 27 iliyokuwepo kabla ya mwaka hu wa fedha.

Kwa upande wa walipa kodi zaa makadirio na kodi za makampuni (Corporation Tax) wanakumbushwa kulipa kodi zao mapema mwezi hu wa tisa badala ya kusubiri msongamano mwisho wa mwezi ambao unaweza kuwasababishia usumbufu.

Hivyo hivyo walipakodi wote wanaodaiwa madeni ya kodi za nyuma au malimbikizo wanakumbushwa kutembelea Mameneja wa mikoa, Wilaya na ofisi mbali mabli za TRA zinazowahudumia ili kujadiliana namna ya kulipa madeni hayo.

Kutokana na mikakti mizuri iliyowekwa na uiongozi wa TRA na serikali Mpaka sasa baadhi ya mikakati hiyo imeanza kuonyesha mafanikio na mwelekeo mzuri wa makusanyo ambapo kwa kipindi cha mwezi Agosti 2016 TRA imekusanya Trillioni 1.158 ikilinganishwa na lengo la Trillion 1.152 ambayo ni asilimia 100.57. ambapo Mwezi Agosti mwaka 2015 TRA ilikusanya billioni 923.

Wito wetu kwa wanahabari na wananchi kwa ujumla ni kuendelea kutuunga mkono kwa kuhimiza kutoa risiti pamoja na kudai risiti katika kila manunuzi pamoja na kutoa taarifa za dalili za ukwepaji wa kodi wa aina yoyote mahali popote nchini