Idara ya Mahakama yawafuta kazi maafisa wa mahakama 34 ijapokuwa walishinda kesi


Jaji mkuu Mheshimiwa Othman Chande amesema idara ya mahakama imewafuta kazi mahakimu na mafisa wa mahakama 34 kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo matumizi ya vifaa vya mahakama kwa manufaa binafsi, ukiukwaji wa sheria na maadili yanayoongoza shughuli za utoaji wa haki mahakamani.