Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu akagua vizuizi vya barabarani

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua akiweka sahihi katika kitabu cha wageni wakati wa ziara yake katika Vizuizi vya barabarani (Mizani) na Mipakani kwa lengo la kufanya Tathimini ya Utekelezaji wa mpango wa maboresho ya mazingira ya biashara na uwekezaji nchini Septemba 15, 2016.
Msimamizi wa Kituo cha Mamlaka ya Mapato TRA kilichopo Mkoani Pwani Bw. David Kisanga akitoa maelezo juu ya utendaji wa ofisi zao kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua wakati alipotembelea ofisi hizo Mkoa wa Pwani.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua akimsikiliza Msimamizi wa Kizuizi cha Vigwaza Mkoani Pwani Bw. Titus Michael wakati wa ziara yake kujionea hali halisi ya vituo hivyo kwaajili ya Maboresho ya mazingira ya biashara na Uwekezaji nchini.
Baadhi ya magari yakipima uzito wa mizigo katika Mizani ya Vigwaza mkoa wa Pwani, Septemba 15, 2016.
Picha zote: Ofisi ya Waziri Mkuu