Katibu Mkuu OWM na Waziri wa Elimu wakagua shule zilizoathiriwa na tetemeko la ardhi Kagera

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (wa kwanza kushoto) akimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua wakati walipotembelea shule ya sekondari ya Nyakato kujionea athari za maafa ya tetemeko la ardhi Mkoani Kagera Septemba19, 2016
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua (wa kwanza kushoto) akizungumza wakati wa ziara yake alipotembelea shule zilizopata athari za maafa ya tetemeko la ardhi mkoani Kagera, wa kwanza kulia ni Waziri Joyce Ndalichako
Dkt. Hamisi Mwinyimvua (kulia) akiangalia jengo la ofisi ya walimu lililoathiriwa na maafa ya tetemeko la ardhi katika shule ya sekondari ya Mugeza Mkoani Kagera 
Baadhi ya majengo ya shule ya sekondari ya Ihungo yariyobomoka kutokana na athari za maafa ya tetemeko la ardhi Kagera. 
  • Picha zote: Ofisi ya Waziri Mkuu