Kuhusu ujumbe wa "Mtanzania aliyekatwa shingo" ughaibuni

Leo nimepokea picha na audio yenye maelezo yanayosimulia mkasa uliompata binti anayeonekana pichani, akiwa anahudumiwa kitabibu, ikisema kuwa ni Mtanzania aliyefanyiwa ukatili na kuchinjwa shingoni (picha inaonesha) na hivyo mwenye kutoa maelezo anataka picha hiyo isambazwe ili iwafikie ndugu na jamaa wa binti huyo.

Nimesambaza audio ile kwa watu na makundi kadhaa, ila picha niliiacha na kuwaomba wenye kuhitaji kuiona wanifahamishe niwatumie binafsi kwa kuwa si uungwa na na inaweza kumwogofya mtizamaji asiyeweza kustahimili kuona tukio kama hilo.

Ni matumaini yangu kuwa ujumbe huu utafikia wahusika wenye mamlaka na uwezo wa kufuatilia suala hili.

Nashukuru ndugu Kayu kwa ujumbe wako ambao ulikutana nami wakati najiandaa kuweka taarifa hiii.

Hivi karibuni mitandaoni imeenea video ya dada yetu wa kitanzania anaesemekana kachinjwa Oman.
Mitandaoni tumeona na kusoma mengi ambayo yanatulazimu kuwa waangalifu katika maelezo yetu kuhusu tukio lolote .Hapa simaanishi kuwa tukio halikutokea. La hasha.Wala sitoingia ktk details za vipi na wapi lilitokea.Kazi hii ni ya WAZIRI WETU WA MAMBO YA NJE apatiwe maelezo ya kina toka vyombo husika naye ATUJULISHE WATANZANIA TUJUE UKWELI WA TUKIO HILI LA KINYAMA AMBALO LIMETUUMA WENGI.Kuna dada yetu mwingine alivuliwa nguo India kwa kosa ambalo wala hakulifanya.

Tunaelewa umuhimu wa mawasiliano ya kidiplomasia lakini TUTAKAA KIMYA HADI LINI?THAMANI YA RAIA WETU HAINA TOFAUTI YOYOTE NA WA NCHI ZILIZOENDELEA.

Kila mmoja ana wajibu wa kuhakikisha Waziri wetu inamfikia taarifa ya dada yetu.(Nahisi atakuwa kashaiona ila si vibaya kumuongezea) Ama nini atachoamua Waziri,hilo lipo nje wa uwezo wetu.Ila kwa uzalendo aliokwisha tuonesha,hatuna shaka atalifuatilia kwa kina suala hili hadi tamati.

Cha kusikitisha katika tukio hili ni kuwa mbali ya kuenezwa picha, hatuoni comments nyingi za wanamitandao kama vile wafanyavyo pindi Barcelona ikicheza na Real!!! Moja ya vipimo vya mwamko wa jamii yoyote ni jinsi watu wa jamii hiyo wanavyoreact kwenye matukio ya kijamii na hasa yale ya ghafla.

KAYU LIGOPORA
[email protected]
Athens Greece

N.B (Kama kuna mtu ana simu ya Waziri pls amforwadie msg hii)