1. Ujumbe Mfupi wa Simu ya Mkononi (SMS)
- Andika neno STIKA acha nafasi
- Andika Namba ya Stika i.e. STIKA 8091390
- Itume kwenda namba 15200
Utatozwa TSHS 100 kwa ujumbe. Baada ya muda utapokea ujumbe wenye taarifa za uhalali wa stika pamoja na bima ya chombo chako.
2. Tovuti ya https://mis.tira.go.tz
- Bofya Hakiki Stika ya Bima|Validate Motor Insurance Sticker, kisha ingiza namba ya stika na bofya Hakiki|Validate.
Kama taarifa zako sio sahihi wasiliana na kampuni iliyokukatia bima au toa taarifa Polisi kuhusiana na aliyekuuzia bima hiyo.
EPUKA BIMA BANDIA, KATA BIMA HALALI KWA USALAMA WA CHOMBO CHAKO NA ABIRIA