Mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwezi Agosti 2016

Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisi kwake Dar es Salaam leo mchana, kuhusu fahirisi za bei za taifa kwa mwezi Agosti, 2016. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Takwimu za Ajira na Bei, Ruth Minja.
Na Dotto Mwaibale

OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS), imesema Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipindi cha mwezi Agosti Umepungua kwa asilimia 4.9 kutoka asilimia 5.1 katika kipindi cha mwezi Julai 2016.

Hiyo inamanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa kwa mwaka ulioisha mwezi Agosti, 2016 imepunguwa ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwezi Julaai 2016.

Hayo yamebainishwa Jijini Dar es Salaam leo na Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa NBS, Ephraim Kwesigabo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema Nchi zote za Afrika Mashariki kasi ya mfumuko wa bei imepuguwa katika kipindi cha mwezi Agost mwaka huu.

Alisema baadhi ya nchi hizio ni Kenya Mfumuko wa bei umepunguwa kwa asilimia 6.26 kutoka asilimia 6.36 katika kipindi cha mwezi Julai na Uganda bei imepunguwa kwa asilimia 4.8 kutoka asilimia 5.1 kwa mei Julai Mwaka huu.

"Kupungua kwa mfumuko huo nhini kumesababishwa na kupungua kwa kasi ya bei ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula katika maeneo mbalimbali ya nchi," alisema Kwesigabo.

Alisema mwenendo wa bei za baadhi ya bidhaa z vyakula zilizoonesha kupungua ni pamoja na bei za Samaki kwa asilimia 701, Mafuta ya kupikia kwa asilimia 7.02 na mbogamboga kwa ailimia 6.9.

Pia bidhaa zisizo za vyakula zilionesha kupunga ni pamoja bei za Gesi kwa asilimia 22.8, Mafuta ya taa kwa asiimia 8.8, dezeli asilimia 9.8 na Petroli asilimia 15.8.

Aidha Fahilisi za bei ambacho hutumika kupima mabadiliko ya bei za huduma mbalimbali zimepungua kwa asilimia 103.28 kwa mwezi Agosti mwaka huu kutoka 103.50 katika kipindi cha mwez Agosti mwaka 2015.

Alisema kupungua kwa fahilisi za bei umechangiwa hasa na kupungua kwa baadhi ya bidhaa za vyakula ambazo ni nafaka kwa asilimia 0.6, Unga wa muhogo asilimia 2.1, dagaa kwa asilimia 3 na mbogamboga asilimia 2.6.

Hata hivyo alisema thamani ya shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma imefikia sh.96 na senti 83 katika mwezi Agosti mwaka huu kutoka desemba 2015 ilivyokuwa sh.96 na sent 62 kwa mwezi Julai mwaka huu.

Kwesigabo alisema mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi umepunguwa kutoka asilimia 7.6 kwa mwezi Julai hadi kufikia asilimia 7 kwa Agosti mwaka huu.

  • Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062Tanzania inflation slows to 4.9 pct yr/yr in August


DAR ES SALAAM, Sept 8 (Reuters) - Tanzanian inflation edged down in August after food and fuel prices rose more slowly, the statistics office said on Thursday.

The state-run National Bureau of Statistics said inflation fell to 4.9 percent year-on-year last month from 5.1 percent in July. Month on month, the headline inflation rate was 0.2 percent in August.

Food and fuel prices are key drivers of inflation in east Africa's second-biggest economy.

"This is the first time this year that the annual headline inflation rate has decreased below 5 percent, which is the government's mid-term target for the inflation rate," Ephraim Kwesigabo, a director at National Bureau of Statistics, told a news conference.

The inflation rate for food and non-alcoholic beverages decreased to 7.0 percent from 7.6 percent in July, he said.

Tanzania changed the formula for calculating its annual headline inflation rate in February by reducing the weight of food in the basket of goods it uses. (Reporting by Fumbuka Ng'wanakilala; Editing by George Obulutsa and Toby Chopra)