Ndugu wa wagonjwa kutoka mikoani walala nje ya hospitali Muhimbili

Zaidi ya ndugu wa wagonjwa 50 wanatoka katika mikoa mbalimbali nchini hulazimika kulala nje ya hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya uongozi wa hopitali hiyo kuwatimua eneo walilokuwa wakilala hapo awali, ambapo wamekuwa wakilala hapo baada ya wengi kukosa ndugu Dar es Salaam huku pia fedha za malazi kwao zikiwa ni tatizo.