NUMET yaipa serikali siku 21 kuhusu mafao ya kujitoa la sivyo...

CHAMA cha wafanyakazi wa sekta ya Nishati na Madini Tanzania (NUMET) kimetoa siku 21 kwa serikali kueleza muda wa kuanza kutolewa kwa fao la kujitoa kama ilivyokuwa zamani ikiwemo kurejeshwa kwa mswaada wa fao hilo bungeni.

Chama hicho pia kimeazimia kufanya maandamano nchi nzima Oktoba 17 mwaka huu endapo serikali itashindwa kutekeleza mambo hayo mawili kwa muda walioutoa ili iwe njia ya kuishinikiza kutekeleza kutatua madai yao .

Akizungumza na waandishi wa habari jana Katibu wa chama hicho Nicomedes Kajungu alisema baada ya maandamano endapo serikali itaamua kuziba masikio na kutokusikiliza kilio hicho,chama kitawataka waajiri waache kukata michango kwenye mishahara ya wafanyakazi hadi mgogoro huo utakapokuwa umemalizika.
“Serikali itambue kuwa wafanyakazi hawawezi kuweka pesa zao kwenye mifuko ya hiari kwani fedha hiyo wanayoweka haizai faida badala yake inapoteza thamani siku hadi siku hivyo tunahitaji fao hilo liendelee kutolewa kwa sababu waajiri wanachangia kiwango sawa ya kile wanachama wanachochangia ili kuondoa hasara inayosababishwa na kushuka kwa thamaniya shilingi”alisema Kajungu.
Kwa upande wake katibu wa chama hicho kanda ya ziwa Shigela Aloyce alieleza kuwa, serikali ilifanyie mzaha suala hilo kwani hicho ni kipato cha wafanyakazi na kwamba haiungi mkono hoja ya kuweka fedha ili uvune uzeeni kwani hauatkauwa na nguvu ya uzalishaji.
“Watoto wanahitaji kwenda shule na vijana kufikia ndoto zao iweje utueleze kuipata ela yetu mpaka uzeeni huoni kama tunaongeza kundi la utegemezi na kushindwa kufikia malengo thamni ya ela ni kidogo na nguvu ya uzalishaji huna tena”alieleza Shigela.
Ikumbukwe kuwa Serikali kupitia vikao vyake vya bunge kutaka kuondoa utaratibu wa fao la kujitoa kupitia mswaada wa sheria ya mifuko ya jamii uliotarajiwa kusomwa kwa mara ya kwanza kwenye bunge septemba 6 hadi 16 mwaka huu.
  • Imeandikwa na  ANNASTAZIA MAGINGA, Mwanza.