NW apata ajali

Gari la Naibu Waziri - TAMISEMI likionekana baada ya kugongwa katika ajali hiyo.
Naibu Waziri - TAMISEMI, Selemani Jafo amepata ajali eneo la Katela katika Kata ya Kiwira, Wilaya ya Rungwe Mbeya  baada ya gari dogo aina ta Corolla liliyokuwa likotokea Mbeya kwenda Rungwe kugongana na gari alilokuwa amepakia NW Jafo alipokuwa akitokea Tukuyu kikazi.

Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Mariam Mtunguja amesema gari la NW lilikuwa na watu watatu ndani ambao ni NW Jafo, Katibu wa NW na dereva ambao wote walitoka bila kuonekana na majeraha katila ajali hiyo na kupelekwa Hospitali ya Mkoa wa Mbeya ambapo walifanya uchunguzi wa ndani ya miili kabla ya kupewa ruhusa kuondoka, na daktari aliyewachunguza.

NW Jafo aliendelea na safari yake kuelekea mjini Dodoma ili kuwahi vikao vya Bunge
Gari lililigonga gari la Naibu Waziri likiwa limetupwa korongoni.
Askari wa usalama barabaran wilaya Rungwe, Mbeya wakipima ajali ilivyotokea.
  • via Mbeya yetu