Pia walitembelea Kituo cha Watoto Yatima Hamugembe chenye watoto 36 ambacho kipo chini ya mwangalizi Bi. Saada ambacho kimepata matatizo kwa Nyumba zake kuanguka chini na kuwapa na kuwafariji
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Aikael Mbowe akisalimiana na Bi. Saada mwangalizi wa Watoto Yatima
Wakiteta na Wanakijiji wa Kibeta sehemu Mama anayotokea Mbunge wa Bukoba Mjini Wilfred Muganyizi Lwakatare
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia akipata Ndizi kwenye Soko la Nyakanyasi wakati wa kuwatembelea Wahanga wa Tetemeko la Ardhi Bukoba leo.
Sehemu ya Majengo katika Shule hiyo kwa sasa baada ya kutokea Tetemeko
Tetemeko likiwa limeharibu sana sehemu kubwa ya Kanisa katika Shule hiyo ya Ihungo iliyopo kilometa 8 kutoka Bukoba Mjini
Taswira ya sasa Wanafunzi wa Shule ya Ihungo wakijipanga kuondoka Majumbani mwao baada ya Tetemeko la jumamosi kuwaathiri kiasi kikubwa na kushinikizwa kufunga shule hiyo kwa wiki mbili kupisha kuangaliwa upya kwa Shule hiyo kutokana na kuathiriwa na tetemeko.
Wakiwa Kanisani ndani, Kanisa lililojengwa miaka mingi iliyopita
Akiwa Kanisani hapo alipata muda akafahamu Viongozi mbalimbali katika picha waliopitia katika kanisa Hilo linalotimiza miaka 125 hivi karibuni lililozinduliwa mwaka 1892 likiwa ni kanisa la kwanza likifahamika Kashozi Parish.
Mh. Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia pia alitembelea Kanisa la Kashozi
Kanisa la Kashozi kwenye Taswira ambalo pia limepata shida kwenye Tetemeko la Ardhi lililotokea hivi karibuni siku ya Jumamosi sept. 10, 2016.