Shindano la ususi: Nani mkali wa kusuka nywele Dar? Jiandae!#SukaSuka ni jukwaa la Times FM ambalo linavumbua wakali wa kusuka Mtaa Kwa Mtaa kila wiki mara 3. Kwa miezi miwili tumekua tukiingia kitaani kusaka wakali ambao wanaweza kusuka mitindo yote kwa speed zaidi ya mwendo kasi. Washindi wanatapa zawadi papo hapo kutoka #DarlingHair kuwanao karibu ili kuwasaidia mbinu na njia za kijasiriamali waweze kufanikiwa katika fani yao ya ususi.

Bila msusi, dada zetu wasingeringa hapa mjini. Bila Msusi mabrothermen wasingedata kwa watoto wa hapa town! Piga saluti kwa wasusi wote.

Kama we ni msusi mkali uwe mwanamke, mwanaume tunakuja kitaani kwako soon kama kawa.

Jiandae kwa zawadi kibao na kutoboa katika ususi #SukaSuka2016 #SukaSukaNaTimesFM.