Loading...
Friday

Taarifa ya JWTZ kuhusu habari iliyochapishwa gazetini Tanzania Daima


Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limesikitishwa na taarifa iliyotolewa na gazeti la Tanzania Daima toleo Nambari 4290 la tarehe 01 Septemba 2016, ikihusisha shughuli za Jeshi hilo zinazoendelea katika maadhimisho ya miaka 52 ya kuzaliwa kwake na shughuli za kisiasa.
Tunapenda kuwataarifu wananchi kwamba kazi ya Jeshi ni kulinda na kutetea maslahi ya Taifa na mipaka ya nchi, aidha, Jeshi letu linafanya kazi kwa kufuata mila, desturi, nidhamu, kanuni na sheria za Kijeshi kwa weledi wa hali ya juu, hivyo lisihusishwe na propaganda zozote za kisiasa kwani Jeshi letu ni lenye maadili ya kitaasisi ya hali ya juu. 

Jeshi ni taasisi ya dola wala si taasisi ya kiitikadi, kwa maana uhusiano wake na wanasiasa ni wakati linapotetea na kulinda maslahi ya wananchi. Inaombwa kuwa makini katika utoaji wa maelezo au malalamiko, iachwe mara moja vyama vya siasa kuingilia ratiba za Kijeshi. 

Ikumbukwe kwamba tarehe 25 Julai kila mwaka ni siku ya kuwakumbuka Mashujaa wetu waliolitumikia Taifa hili kwa umakini na nguvu zote kwa kuleta mafanikio tunayoyaona, na hii ilipitishwa mwaka 1979 wakati Majeshi yetu yanarudi kutoka Uganda baada ya ushindi wa vita vya Kagera. 

Sherehe ya mapokezi hayo yalifanyika mji wa Bunazi Wilaya ya Misenye wakati huo Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera ilipoanzishwa kuwa tarehe hiyo iwe siku ya Mashujaa na kupitishwa Kisheria, ikabaki siku ya tarehe 01 Septemba kuwa ni siku ya kuanzishwa kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, hivyo jana tulikuwa tunasherekea siku ya kuzaliwa JWTZ. Ieleweke hivyo na iachwe mara moja kuchanganya shughuli za Kijeshi na mambo ya Kisiasa, viongozi wa kisiasa wekeni kumbukumbu zenu vizuri. 

Jeshi linasisitiza wanasiasa ni vizuri wakasoma vema historia ya nchi wanayotaka kuiongoza na wanayoongoza ili kuepusha upotoshaji, lugha na maneno yanayotolewa na viongozi wa kisiasa wenye matakwa binafsi kuhusisha shughuli za Jeshi na siasa zao yanatia ukakasi na kiungulia, awe makini kuongea vitu ambavyo haelewi na kutokuwa makini zaidi aelewe madhara yanayoweza kutokea kutokana na upotoshaji.

Jeshi letu linafanya shughuli zake ki weredi.

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0784-477638

1 comments :

  1. Ikiwa mnafumbia macho ukweli hamtaitendea haki nchi. Kunatofauti ya kusema ukweli ili kuboresha ulibzi na kudanganya unapotokea udhaifu. Najua kazi ya jeshi, ujasiri wake na uzito wa mazi ya jeshi na umaarufu wake. Lakini unapotokea udhaifu wowote lazima ukweli utumike. Kwani jeshi ni chombo maalum.mnapotetea ambapo hamhitaji kutetea pia nanyi mnagonganisha watu.mila binadamu hufanya makosa na inabidi aambiwe ukweli.uongozi unapofunika ukweli wa mambo pia haufanyi haki.ingawa kunamigongano kisiasa lakini kutumia jeshi kwa maslahi ya chama fharama zake ni kubwa mno kwa wananchi. Uongozi dhaifu tu, utafumbia macho makosa ya jeshi inapobidi ukweli utumike.kunamadhara makubwa kutoa sifa pasipo stahili. Nikama unalituma jeshi kufanya jambo kinyume cha sheria kwa baadhi ya watu kutokana na tofauti za itikadi. Mmeshuhudia mara nyingi polisi mutuhumu watu wasio na makosa. Na kama uongozi unaruhusu hii badala ya kuhakikisha kuwa kazi ya polisi ni kulinda na kuwa wakweli mnakichafua chombo hiki. Ilitokea wakati wa Mwongosi ingawa ilitokea hadharani serikali ilitetea. Matukio ya awamu iliyopita watu wa polisi na usalama walihusika katika utekaji. Haya ni matumizi mabovu ya jeshi. Kjeshi linapopiga watu, badala ya kuwalinda. Na juzi tumeambiwa baadhi ya majambazi ni polisi na wanajeshi wastaafu.sasa mnapotetea kauli ambazo ni kweli mnaipeleka nchi kubaya. Ni kama waziri mstaafu alipotoa amri piga, au raisi anapotoa kauli vunja, unajenga uhasama na kuruhusu matumizi mabaya ya chombo hiki. Sasa utatofautishaje kati ya polisi mzuri na polisi anayeammini akiwa kazini jambo la kwanza ni kumpiga raia.hii haileti picha. Polisi anaenda mafunzo makali ya kimwili na kiintelijesia ili aweze kufanya kazi zake na kabla ya kuhamaki afikiri ni njia gani atumie na si kukurupuka.sasa mnaandika hoja kwa kuwaplease viongozi badala ya kuhakikisha uhuru na weledi wa kazi kwa polisi na wanajeshi wote. Hatupo vitani, tupo uraiani. Nimesoma magazeti ya Zanzibari na kusikiliza hoja za Wazanzibari baada ya raisi Magufuli kwenda inasikitisha. Wananchi wakaao huko wanamaelezo na masikitiko makubwa yanayowathiri kila siku. Wanayaona, yanawagusa, lakini inasikitisha kuona uongozi wa juu toka bara ambao huishi huko na kukabiliwa na maisha magumu na ukweli wa mambo kwenda na kuwaambia wasulubiwe. Viongozi wajuu. Sasa kama wananchi bado hamuwajali, muwasimiliza, mukaa nao kama binadamu na kujadili na kusikiliza vilio vyao, badala yake unalazimisha mambo toka juu kama enzi za ukoloni hii tumefikia hatari isiyoepukana na madhara mnayapika viongozi na kuchochea moto mkali.mlisema ya Zanzibar sio yenu, lakini mmeenda muwaambia kuwa sisi, au mimi ndiye baada ya miezi kumi kupita na kuona mnatenda haki, ee hii ndiyo inayoigawa nchi hii. Utawala haujali, hautaki kuona ukweli, ni piga ya Pinda imerudi.Mungu tia utashi kwa binadamu dhaifu I waone mapungufu yao badala ya kuuficha.
    Tanzania ya amani imepotea.kuna mambo makubwa yanajipika chinichini hata mitutu na mabomu wala ndege za vitisho havitaleta usalama.

    ReplyDelete

 
Toggle Footer
TOP