Wafanyabiashara Kariakoo wachangia walioathiriwa na tetemeko la ardhi Kagera


Mwenyekiti wa Jumuia ya Wafanyabiashara wa Kariakoo, akizungumza jijini Dar es Salaam, baada ya kupokea michango ya fedha na vifaa kutoka kwa wanachama wa jumuia hiyo kwa ajili ya walioathirika kwa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Jumla walichanga fedha na vifaa vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni 60.7.

Mwenyekiti wa wafanyabiashara Mtaa Muhonda, Kariakoo, akimkabidhi Mwenyekiti wa Jumuia ya Wafanyabiashara Kariakoo (JWK), Philimon Chonde, fedha taslimi mchango kutoka kwa wafanyabioashara hao kwa ajili ya walioathirika kwa tetemeko Kagera. Wa pili kushoto ni Katibu Mkuu wa JWK, Abdalah Mwinyi na Mweka Hazina wa jumuia hiyo, Silvanus Mande.

Katibu wa JWK, Mtaa wa Raha Square, Frank Nduta akikabidhi vitenge na bidhaa nyingine kwa Mwenyekiti wa JWK, Philimon Chonde

Wafanyabiashara wa Mtaa wa Mchikichi Kariakoo, wakitoa msaada wa misumari kwa ajili ya waathirika wa tetemeke, Kagera.


  • Picha zote: Richard Mwaikenda aka Kamanda wa Matukio blog