Wanafunzi 172; Darasa chumba 1


Wanafunzi 172 wa Shule ya Msingi Mwinyi katika Manispaa ya Tabora hulazimika kutumia chumba kimoja cha darasa kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa.

Kwa mujibu wa Mkuu wa shule hiyo, Simon Toyi:
  • Shule ina wanafunzi 1721 
  • Vyumba vya madarasa 10 (upungufu wa vyumba 20 ikiwa ni wastani wa kila darasa kuwa na wanafunzi 45)
  • Upungufu wa matundu ya vyoo 37 (kwa sasa kuna matundu 10 na mahitaji yakiwa 47)
Toyi aliongeza kuwa hali hiyo inachangia kwa kiasi kikubwa kuzorotesha maendeleo ya elimu shuleni hapo.

via MTANZANIA