Kumbe Tanzania akina baba nao wana likizo ya uzazi?

Kuna makala nimeisoma kwenye NPR, nikakutana na hiyo ramani yenye takwimu kama zinavyoonekana, na kama iko sahihi, ndiyo sababu yangu ya kuhamaki kwa swali nililouliza hapo juu kwa mshangao.

Nadhani wako wanaume wanaoitumia likizo hiyo ya uzazi kumsaidia mwenza pale anapohitaji, ila lazima nikiri kuwa katika ukuaji wangu, sikumbuki kusikia mwanaume amechukua likizo ya uzazi. Nawaza vile vile kuwa hata ikiwa zinachukuliwa, kutokana na mfumo wetu wa maisha na utamaduni, sitashangaa kuwa likizo hiyo kwa baadhi ya akina baba itakuwa ndiyo mapumziko yao binafsi kama siyo kushinda vijiweni na baa/vilabu vya pombe.

Aghalabu wapo watakaosema sivyo. Huenda watasema uzoefu wao. Basi, na mnikosoe kwa uthabiti na uthibiti wa kauli pasina tashwishi.