Moto waunguza mashamba na makazi Kimbiji

Tukio la uzuni na majonzi la kuunguzwa makazi na mazao limewapata wakazi na wamiliki wa maeneo ya ardhi katika Kata ya Kimbiji mtaa wa Ngobanya wilaya Kigamboni, mkoa wa Dar-es-salam siku ya tarehe 1 Oktoba 2016 baada ya watu wasio julikana kuchoma moto
uliosababisha kuungua kwa mazao na miti pamoja na makazi kule Kimbiji-Ngobanya, wilaya Kigamboni.

Mojawapo ya mashamba yalioungua lilikuwa na miti aina ya mitiki 140 na nyumba
ndogo ambayo ni makazi.

Moto huo ulizuka mchana wakati wenyewe waliustukia tu na hhuenda
umesababishwa na watu wenye vitendo vya kuchoma moto maneo.

Taarifa za moto huo zililipotiwa kwa viongozi wa kata hiyo ya Kimbiji akiwemo Mwenyekiti wa serikali za mtaa wa Ngobanya bwana Ismail Mahemb.

Kwa taarifa zaidi, simu 0713846688