Mwanafunzi aliyefia 'guest house' alibakwa na kunyongwa

Mganga Mkuu Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, Dk Aubery Mushi amesema kifo cha mwanafunzi aliyekutwa nyumba ya kulala wageni Septemba 29, kimetokana na kubakwa na baadaye kunyongwa.

Akizungumza na gazeti hili jana, Dk Mushi alisema uchunguzi umebaini kuwa kabla ya kunyongwa, mwanafunzi huyo aliyekuwa akisoma kidato cha nne Sekondari ya Katente, Zainab Salum (18), aliingiliwa kimwili na watu wawili, mmoja akitumia kondomu na mwingine hakutumia.

Alisema uchunguzi unaonyesha mtu mmoja alimshika miguu na mwingine kumnyonga shingo kwa kutumia mikono baada ya kumbaka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo alisema wanamshikilia mwalimu mmoja wa sekondari, anayedaiwa kuwa na uhusiano wa mapenzi na mwanafunzi huyo.