wavuti.com itaadimika

Nashukuru kwa kila mmoja aliyetembelea blogu hii ilipoanzishwa ikiwa nukta77.com hadi sasa wavuti.com

Watembeleaji wa mara kwa mara wa blogu hii mmekuwa marafiki zangu kwa namna mbalimbali. Mnakumbuka vyema kwa jinsi nilivyojitahidi kuhakikisha habari za uhakika zinapatikana kwa wakati, mpaka hapo nilipojaaliwa kupata mtoto na kushindwa kumudu kuendelea kufanya hivyo, kutokana na ukweli kuwa kipaumbele kilibadilika.

Ni kwa sababu hiyo tena, ninalazimika kupunguza zaidi idadi ya kasi ya machapisho hapa kutokana na ajira yangu (ambayo ndiyo chanzo cha kipato kinachoniwezesha si tu kutimiza mahitaji muhimu ya familia, bali pia kuniwezesha kulipia na kuendesha blogu hii kwa 'hobby') kunihitaji zaidi. Sheria za kazi zimebadilika na siwezi kutumia muda wa kazi kufanya shughuli binafsi.

Hivyo basi, kutokana na maelezo hayo, natangaza rasmi kuwa wavuti.com haitakuwa "active" tena, machapisho yatakuwa adimu kwa kuwa nitaendelea tu kuweka taarifa muhimu pale tu ninapopata wasaa wa ziada nje na baada ya majukumu ya ajira na familia. 

Kwa taarifa hii, nakutakieni usomaji mwema wa blogu na tovuti nyingine za habari kwa ajili ya kujua yaliyojiri ndani ya Tanzania na hata nje ya mipaka ya nchi, pale suala linapohusu Tanzania au kugusa maisha ya Watanzania wanaoishi nje ya nchi.

Wasalaam,
Subi