Faida za matumizi ya karafuu katika kuutibu mwili


Karafuu ni zao linalotokana na mkarafuu, ingawa karafuu hazimo katika kundi la vyakula wala vinywaji lakini ni kiungo na dawa muhimu sana kwa maisha ya binadamu.

Mikarafuu ilianza kupandwa kwenye visiwa vya Shelisheli, Mauritius na sehemu nyinginezo katika karne ya 19. Miche ya mikarafuu ililetwa Zanzibar kutoka Indonesia, mashariki ya mbali mwaka 1818.

Mikarafuu inastawi zaidi Visiwani vya Unguja na Pemba ambapo katika miaka 30 iliyopiata Zanzibar ilikuwa inazalisha asilimia 80 ya karafuu zote zinazohitajika duniani ambapo uchumi wake ulitegemea sana zao la karafuu.

Karafuu zina matumizi mengi, ambapo hutumika kama kiungo katika vyakula na vinywaji, dawa kwa maradhi ya tumbo, meno na misuli vile vile hutumika katika kuleta harufu nzuri ya kinywa, mwili na mazingira ya nyumbani.

Pia karafuu zinatumika katika uzalishaji wa bidhaa nyengine ikiwemo sigara, mafuta ya karafuu ambayo hutumika kwa kuchulia misuli inayouma, kutengezea dawa za meno na perfume kwa ajili ya manukato.

Karafuu zinatumika sana kwenye mapishi ya vyakula mbali mbali ikiwemo nyama, biriani, pilau, mchuzi wa masalo na vyakula vikavu kama vile vileja, beskuti na donas na kwa ubande wa vinywaji karafuu hutumika katika chai na maziwa .

Kama vilivyo viungo vyengine karafuu nazo zina utamu, ladha na harufu nzuri ya kuvutia na kupendeza katika vyakula hivyo ambapo watu wengi hasa katika bara la Asia, Mashariki ya kati na ulaya hupenda sana kiugo cha karafuu katika vyakula vyao.

Karafuu inasaidia usagaji mzuri wa chakula tumboni na ni nzuri kwa matibabu ya maumivu ya tumbo, tumbo kujaa gesi na kiungulia. Hivyo karafuu ni miongoni mwa kiungo muhimu katika vyakula kutokana na vinasaba vya aina ya eugnol vilivyomo ndani ya karafuu.

Aidha karafuu hutumika katika utengenezaji wa mafuta (mafuta ya karafuu) ambapo mafuta hayo husafisha damu, tafiti zinaonyesha kuwa visanaba vilivyomo katika karafauu vinapunguza sumu katika damu. Vinasaba aina ya eugnol vilivyomo ndani ya karafuu vinasaidia mzunguko mzuri wa damu.

Kutokana na ukuaji wa viwanda duniani kumekuwa na mahitaji makubwa ya karafuu pamoja na kuongezeka kwa nchi zinazozalisha ambapo karafuu hutumika sana kwa utengenezeji wa sigara katika nchi za Ulaya, Asia na Marekani.

Sigara zinazotengenezewa karafuu kutoka Zanzibar zina thamani na ubora zaidi duniani kuliko sigara zinazotengezewa karafuu kutoka nchi nyengine kutokana na ubora wa karafuu za Zanzibar.

Pia karafuu hutumika katika viwanda kwa ajili ya kutengezea dawa za meno kwa ajili ya kutunza meno na kuondosha maumivu ya meno na ufidhi, kung’arisha meno na kuleta harufu nzuri ya kinywa, harufu iliyomo katika karafuu inasaidia kuondosha harufu mbaya mdomoni.

Kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa mwaka 2011katika Jarida la Asia Plant Science and Research toleo namba 1 (2) karafuu husadia kutibu vidonda vya mdomo na kuimarisha Afya ya fizi pamoja na kuzuia meno kuoza.

Aidha Mafuta ya karafuu yamekusanya vinasaba vya eugnol ambavyo vimekuwa vikitumiwa na Madaktari wa meno kwa miaka mingi kutibu matatizo ya meno na ufizi.

Karafuu inatumika katika urembo ambapo hutumika kusugulia mwili (scrub) kwakuchanganya unga wa karafuu kavu iliyosagwa na mafuta ya nazi na liwa ambapo husuguliwaa mwili mzima kuondoa uchafu.

Mbali na hayo pia karafuu hutengenezewa sabuni ambazo ni nzuri kwa kuondosha maradhi ya ngozi kama vile harara, vipele na chunusi na kuifanya ngozi iwe nyororo na yenye kuvutia. Sio hayo tu lakini pia karafuu hutumika kutengenezea mafuta mazuri kwa sababu karafuu ina harufuu ya kipekee inayovutia.

Hivyo karafuu na mafuta ya karafuu ni mazuri kwa ajili ya kutunza ngozi hasa kwa ngozi yenye mabaranga, mba na kuchakaa ambapo huifanya ngozi kuwa nzuri na yenye kung’ara.

Matumizi ya karafuu na mafuta ya karafuu kwa kawaida humfanya mtu kuwa mchangamfu kwa kuondoa uchofu kwa vile karafuu inaiweka akili katika hali nzuri na kufanya ubongo ufanye kazi vizuri. Pia husadia kuondoa matatizo ya kusinzia, kupoteza kumbukumbu na wasiwasi.

Mafuta ya karafuu husaidia kuondosha maumivu ya kichwa kwa kuchanganganywa na chumvi na kupakaa kwenye paji la uso hupoza maumivu. Pia huondosha matatizo katika mfumo wa upumuaji na kusafisha koo na hutibu kikohozi, mafua na pumu.

Mchanganyiko wa mafuta ya karafuu na mafuta ya ufuta (sesame oil) ni mazuri kwa kuondsha maumivu ya sikio.​​​
  • Makala hii imeandikwa na Zuhura Omar na Pili Khatib - MUM

Sheria ya marufuku ya kelele za ibada, muziki, ngoma za nusu uchi yaanzaBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limeanza kung’ata kwa kutumia kanuni ili kudhibiti uchafuzi wa mazingira kwa kelele na mitetemo.

Kwa sasa mtu akitaka kufanya sherehe mtaani, kupiga muziki kwa kelele, kuendesha ngoma za kukesha za nusu uchi (vigodoro) au ‘bai koko’ au kufanya ibada kwa kelele mitaani, atapaswa kulipa Sh milioni 10.

Pia, baa na kumbi za starehe za usiku zitakazopiga kelele, zitapaswa kulipa kiasi hicho.

Aidha, NEMC imesema pia kuwa wale watakaohusika na kelele za migodini za kutumia baruti, kupasua miamba zilizo zaidi ya matakwa ya sheria ya mazingira ya kelele na mitetemo, watapaswa kulipa Sh milioni tano ili kupata kibali.

NEMC imetaka watu kuheshimu kanuni za viwango vya kelele na mitetemo katika maeneo mbalimbali nchini. Imeonya kuwa watakaokiuka, hatua kali zitachukuliwa dhidi yao. Kanuni hizo zimeanza kutumika mwaka jana (2015).

Mkurugenzi Mtendaji wa NEMC, Bonaventure Baya alisema hayo Dar es Salaam jana. Alisisitiza kuwa uchafuzi wa mazingira, unaosababishwa na kelele na mitetemo, umekuwa ukifanyika bila kujali sheria za nchi na sasa watashughulikia suala hilo ipasavyo.

Alisema hivi sasa kanuni za kudhibiti suala hilo, zimekamilika na zimeanza kutumika kikamilifu. Mtu yeyote atakayekwenda kinyume cha kanuni na sheria, atachukuliwa hatua kali. Baya alitoa ufafanuzi kuwa yapo maeneo yenye kelele zaidi ya viwango vinavyoruhusiwa kisheria, ikiwamo maeneo ya migodini.

Alieleza kwamba kanuni zimeweka vigezo na tozo maalumu la kuanzia Sh milioni tano hadi Sh milioni 10, kulingana na eneo na aina ya kelele na mtetemo. Alisema mambo mengine ambayo kanuni zimeweka ni faini kwa kila kanuni itakayovunjwa na kusisitiza kuwa hatua hizo zitachukuliwa ipasavyo.

Kulingana na hatua hiyo ya NEMC, sasa mtu mwenye kutaka kufanya sherehe mtaani, itakayohuisha kelele zitakazosumbua jamii pamoja na majirani zake, ikiwamo muziki maarufu wa ‘kigodoro’, ibada za makanisani zinazozidi matakwa ya kisheria ya uanzishwaji wa makanisa hayo katika jamii, atapaswa kulipa Sh milioni 10 ndipo aruhusiwe kuendelea na shughuli yake.

Kwa mujibu wa NEMC, ruhusa hiyo inayo lipiwa, pia ina muda na viwango vyake, ambapo kila muda husika unapoisha, kelele zinapaswa kupunguzwa ama kuzimwa. Hii inahusisha pia baa na kumbi za starehe za usiku.

Baya aliitaka jamii kuepuka uchafuzi huo wa mazingira wa kelele na mitetemo, ambao watu wengi wamekuwa wakidhani si tatizo. Alitaka watu kuheshimu matakwa ya sheria na kanuni kwa nyakati za mchana na usiku.

“Tumekuwa tukipokea malalamiko kutoka kwa watu wengi, wakilalamikia usumbufu wa kelele na mitetemo kutoka kwa watu wanaoendesha shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii katika jamii,” alifafanua Baya.

Alitoa angalizo kwa wanaotumia vyombo vya muziki na sauti katika maeneo ya makazi, ambavyo vimeleta madhara kwa afya za watu. Alisema matumizi ya vipaza sauti na vyombo vya sauti kubwa, wanapaswa kuwa na kibali maalumu.

Alieleza kuwa kanuni za kelele na mitetemo, zimeweka vigezo na viwango vya sauti kwa ajili ya kudhibiti uchafuzi wa mazingira katika maeneo ya hospitali, makazi, migodini, kumbi za kijamii, kumbi za usiku za starehe, matangazo, baa na maeneo mengine.

Baya alisema baraza limepata changamoto kadhaa, ikiwamo uelewa mdogo wa jamii kuhusu kiwango cha sauti kinachotakiwa na kisichoruhusiwa na baadhi ya watu kwa makusudi huvunja sheria.

Kuhusu faini, alisema sheria ya mazingira imeweka wazi faini kwa wanaokiuka na kuchafua mazingira kwa kelele na mitetemo. Faini hiyo haiingiliani na tozo la Sh milioni tano hadi Sh milioni 10 lililoelezwa, ambapo mtu anapaswa kulipa si chini ya Sh milioni 50 na si zaidi ya Sh milioni 50 ama kifungo jela.

Kaimu Mkurugenzi wa Usimamizi wa Sheria za Mazingira wa NEMC, Ruth Lugwisha alisema tatizo la kelele na mitetemo, limekuwapo kwa muda mrefu. Alisema tangu kupitishwa kwa kanuni, tayari watu kadhaa wamewajibishwa.

Alisema miongoni mwa waliowajibishwa ni makanisa, kumbi za starehe na baa. Hata hivyo, hakuwa tayari kuwataja wahusika wala maeneo. Alisema uwajibishwaji huo ulihusisha faini, kufungiwa na onyo.

Jihadhari! Utapeli unaotumia Osifi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma


Marufuku Watumishi wa umma kutumia anuani za domain binafsi kwa mawasiliano ya kiserikali

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao Dkt. Bakari Jabiri akitoa ufafanuzi kwa Waziri Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki (kulia) kuhusu kituo cha ufuatiliaji mifumo ya mawasiliano Serikalini leo jijini Dar es Salaam. 
Na. Aron Msigwa –MAELEZO

Serikali imepiga marufuku matumizi ya barua pepe za kawaida kwa watumishi wa umma wanaotuma au kupokea taarifa za Serikali na kuwataka watumishi hao kuhakikisha kuwa wanatumia mfumo rasmi wa Mawasiliano ya Barua Pepe Serikalini (GMS) ulioanzishwa na Serikali kwa lengo la kuimarisha mawasiliano kwa njia ya Mtandao.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Angella Kairuki alipokuwa akizungumza na Watendaji na Watumishi wa Wakala ya Serikali Mtandao ( e Government Agency) wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji na ufanisi wa matumizi ya TEHAMA Serikalini.

“Sasa kuna watumishi 7000 wanaotumia anwani za Barua pepe za Serikali ,idadi hii ni ndogo lazima iongezeke, hatuwezi kuendelea kuruhusu utumaji wa taarifa za Serikali kwa kutumia Barua Pepe nje ya mfumo huu” Amesisitiza na kuongeza kuwa Serikali haijakataza matumizi ya barua pepe za kawaida kwenye mawasiliano binafsi.

Amesema kwa kutambua umuhimu wa uimarishaji wa mawasiliano ya TEHAMA Serikalini na kuongezeka kwa matumizi ya TEHAMA katika utumaji wa taarifa kupitia mitandao mbalimbali ipo haja ya kuweka msisitizo kwa watumishi wa umma kutumia Barua Pepe za Serikali.

Mhe. Kairuki amewataka watendaji wa Wakala hiyo kuhakikisha kuwa wanasimamia uratibu wa zoezi hilo ili kuhakikisha kuwa Wizara, Idara na Taasisi zote za umma zinaunganishwa na mfumo rasmi wa Serikali ili kuwa na mfumo mmoja wa Mawasiliano.

“Katika hili ninatoa siku 60 muhakikishe kuwa mnakamilisha kwa Taasisi zilizobaki ili kwa wale watakaopuuzia hatua zianze kuchukuliwa” Ameeleza Mhe. Angella.

Aidha, ametoa wito kwa watendaji wa Wakala hiyo kuweka mpango wa kuwawezesha na kuwajengea uwezo wa kitaaluma watumishi waliopo kazini kwa kujenga utaratibu wa kuwarithisha uzoefu watumishi ili kuendelea kuimarisha ufanisi na utendaji wa Wakala hiyo.

Mhe. Kairuki amewataka kuwa wabunifu katika kuanzisha mifumo mipya ya TEHAMA ili kuimarisha dhana ya Serikali mtandao ili kupunguza gharama hadi kufikia asilimia 5 ya fedha zinazotumika kuendeshea masuala mbalimbali ambayo yangefanywa kupitia matumizi ya TEHAMA.

Akizungumzia kuhusu ununuzi wa vifaa vya TEHAMA serikalini ameitaka Wakala hiyo kutoa ushauri ili kudhibiti mianya ya ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha katika kununulia vifaa hivyo kwa gharama kubwa wakati vinaweza kupatikana kwa bei ya kawaida.

“katika hili Serikali itachukua hatua kwa yeyote atakayebainika katika upotevu wa mapato muhakikise mnazisaidia Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali katika masuala ya ununuzi wa mifumo na vifaa vya TEHAMA ili mifumo inayonunuliwa iwe na manufaa kwa wananchi na thamani halisi ya fedha”

Amesema Serikali itaendelea kuboresha utoaji wa huduma kupitia mtandao ili wananchi waweze kupata huduma hizo mahali walipo kwa gharama nafuu na kutoa wito kwa watumishi wa Wakala ya Serikali mtandao (e-Gov) kuwa wabunifu katika kutengeneza programu mbalimbali na mifumo salama itakayowasaidia wananchi kupata huduma.

Aidha, katika hatua nyingine ameitaka e-Gov kuendelelea kujenga uwezo katika kudhibiti dharura na majanga mbalimbali yanayoweza kujitokeza katika matumizi ya TEHAMA na kuitaka Wakala hiyo iendelee kulifanyia kazi suala la kuwezesha mifumo ya Serikali kuzungumza kati ya taasisi moja hadi nyingine ili huduma zote ziweze kupatikana katika eneo moja na kuondoa urudufu wa mifumo iliyopo.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (e-Gov) Dkt. Jabiri Bakari akitoa taarifa ya utendaji wa Wakala hiyo amesema kuwa licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali toka kuanzishwa kwake Julai 11, 2012 imeendelea kupata ufanisi katika uimarishaji wa Serikali Mtandao.

Amesema kuwa Wakala hiyo inaendelea kuhakikisha kuwa huduma za Serikali zinawafikia wananchi kupitia mtandao mahali walipo na kuhakikisha kuwa inafanikisha lengo la huduma zote za Serikali kupatikana chini ya dirisha moja.

Aidha amesema kuwa Wakala ya Serikali Mtandao itaendelea kuhakikisha kuwa usimamizi wa viwango vya matumizi ya TEHAMA katika Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali vinazingatiwa.

Rais Magufuli amjulia hali Kadinali Pengo aliyelazwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakimjulia hali Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki la Dar es salaam katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo January 1, 2016. Kardinali Pengo alilazwa hospitalini hapo jana jioni kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.