Kamanda Kova astaafu na kumkabidhi mikoba Kamishna Sirro na kusimulia asiyoyasahau


ALIYEKUWA Kamanda wa Polisi katika Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova amestaafu rasmi na kuagwa jana huku akikiri kuwa hatasahau joto la uchaguzi mkuu 2015 lililosababishwa zaidi na mchuano wa wafuasi wa wagombea urais John Magufuli wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Edward Lowassa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Akizungumza wakati wa kuagwa kwake na kisha kukabidhi majukumu kwa kamanda mpya wa kanda hiyo, Naibu Kamishna wa Polisi, Simon Sirro, Kova alisema uchaguzi huo uliofanyika Oktoba 25, 2015 ni miongoni mwa vipindi vitatu asivyotarajia kuvisahau katika maisha yake yote ya kulitumikia jeshi la polisi.

Alivitaja vipindi vingine asivyovisahau wakati akilitumikia jeshi la polisi katika Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuwa ni tukio la kuvamiwa kwa kituo cha polisi Stakishari lililoacha vifo kwa baadhi ya askari wake na pia ajali ya helikopta.

Akieleza zaidi kuhusiana na uchaguzi mkuu, Kova alisema uchaguzi huo ulimpa changamoto kubwa kutokana na wagombea hao kuungwa mkono na watu wengi kiasi cha kuhofia kutokea machafuko, hasa kutokana na kuwapo kwa mwamko mkubwa wa kisiasa miongoni mwa wafuasi wa wagombea.
Hata hivyo, Kova alisema anashukuru kuwa serikali iliwaunga mkono vya kutosha katika kulinda usalama na hivyo kufanikisha uchaguzi huo kwa ufanisi.

“Napenda kuishukuru serikali kwa ushirikiano mkubwa waliotupatia jeshi la polisi wakati wa uchaguzi kwa kutuongezea vifaa vya kazi kama magari ya kufanyia doria, silaha pamoja, kwani vilituwezesha kufanikiwa kulinda amani na utulivu wa hali ya juu,” alisema Kova.

Akisimulia safari yake ndani ya jeshi la polisi kwa ufupi, Kamanda Kova alisema kabla ya kuteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi wa Kandaa Maalumu ya Dar es Salaam, aliwahi kuwa katika idara ya upelelezi kwenye mikoa ya Arusha, Kigoma, Mwanza, Kinondoni (Magomeni) na baadaye kuwa Kamanda wa Polisi katika Mkoa wa Mbeya. 

“Nina utumishi wa miaka 40 ndani ya jeshi la polisi na nilikuja kuwa Mkuu wa Polisi wa Jiji la Dar es Salaam (RPC) nikitokea Mbeya mwaka 2008,” alisema.

MATUKIO 

Akielezea matukio ya ajali ya helikopta na uvamizi Stakishari, Kova alisema hayo hatayasahau kama ilivyokuwa kwa mikikimikiki ya uchaguzi mkuu 2015.

Alisema tukio la Stakishariu lililowapoteza askari wanne hatalisahahu kwani hapo kabla alizoea kukabiliana na vitendo vya ujambazi vinavyohusisha uporaji wa fedha na mali na siyo ugaidi wa kuiba silaha kwenye vituo vya polisi.

Hata hivyo, alisema anafarijika kuona kuwa kwa kushirikiana vya kutosha ndani ya jeshi lao Kanda maaalum ya Dar es Salaam aliyokuwa akiiongoza, walifanikiwa kuwakamata wahusika wote waliofanya tukio hilo. 

Alisema tukio jingine ni kuanguka kwa helikopta wakati wa kutembelea wananchi waliokumbwa na mafuriko mwaka 2014 jijini Dar es Salaam, akiwa pamoja na aliyekuwa Makamu wa Rais, Dk. Gharib Bilal, aliyekuwa Waziri wa Ujenzi ambaye sasa ni Rais wa Tanzania, John Magufuli na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik.

Simon Sirro
Simon Sirro
AMTAMBULISHA KAMANDA SIRRO 

Kamanda Kova alimtambulisha rasmi Naibu Kamishna wa Polisi Sirro, kuwa mrithi wa wadhifa wake.

Akiongea na waandishi wa habari juu ya hatua hiyo, Kova alisema kwake yeye, kukabidhi madaraka kwa Kamanda Sirro ni kitendo cha kihistoria kwani ilikuwa ni ishara ya kuhitimisha salama utumishi wake ndani ya jeshi hilo. 

“Ni siku ya kihistoria katika maisha yangu kutokana na tendo hili. Lakini naahidi kuendelea kutoa ushirikiano wa kila namna kwa Kamishna Sirro,” alisema

AKABIDHI VYETI

Katika hatua nyingine, Kova alikabidhi vyeti kwa maofisa 110 wa jeshi la polisi kutokana na utendaji wao katika hafla ya kumuaga.

Alitumia fursa hiyo kufanya ukaguzi wa baadhi ya vitu vilivyokamatwa na jeshi la polisi yakiwamo meno ya tembo, gari mbili, moja likiwa aina ya Toyota Ford liliibwa nchini Afrika Kusini na Toyota Toyota GX210 ambayo yote yalikamatwa eneo la Buguruni Jijini Dar es Salaam.

Kova alimtaka mrithi wake, Kamanda Sirro kufuata nyayo za uongozi wake kwa kuendeleza amani na utulivu katika jiji la dare s Salaam kwa kuhakikisha idadi ya matukio inaendelea kuwa ndogo zaidi.

Kwa upande wake Kamanda Sirro alimsifu Kamanda Kova kwa kazi yake nzuri aliyofanya kwa muda wote alipokuwa wakifanya kazi pamoja na kusema kuwa alikuwa kama mwalimu kwa kila afisa wa jeshi hilo kwa muda mrefu wa utumishi wake.

Alisema kuwa amefanya kazi kama kaimu wake wa kanda hiyo kwa miaka miwili, na kwa muda wote huo kanda hiyo ilikuwa shwari bila kuwepo na wimbi la machafuko.

“Nimefanya naye kazi vizuri kwa miaka isiyozidi miwili na amekuwa mwalimu kwangu na siyo kiongozi tu… ninachoweza kumuahidi ni kuwa nitaendeleza jitihada za kulinda usalama wa raia na mali zao,” alisema.

Da' Chemi ataja kilichosibu Ommy Dimpoz kufungwa jela Marekani

Mwimbaji maarufu wa Bongo Flava, Ommy Dimpoz (28) alifungwa jela Marekani katika ziara yake ya hivi karibuni. Alifungwa jela huko Minnesota.
Si kweli kuwa alikutwa na madawa ya kulevya. Ommy hakuwa na Visa ya kumruhusu kufanya kazi Marekani. Alitakiwa kuwa na O-1 Visa ambayo wanapewa wasanii. Wale wafadhili wake walifanya makosa katika kumwombea Visa hasa kama walijua atafanya show kubwa kinachotangazwa sehemu nyingi na kiingilio kikibuwa. Uncle Sam (Serikali ya USA) anataka hela yake (kodi)
Mimi kama Msanii ninaelewa process ya kuomba Visa ya Usanii. Zinatolewa kiasi fulani kila mwaka na nyingi zinaenda kwa wasanii kutoka Canada, Ulaya, na nchi za Marekani ya Kusini (South America). Chache sana zinaenda kwa wasanii kutoka Afrika. Navyoona kulikuwa na njama za kumwonea Ommy hapa USA. Nani aliwaambia hao polisi kuwa hana Visa ya Usanii.
Pole sana Ommy Dimpoz.
Imenukuliwa kutoka kwenye blogu ya Chemi Che-Mponda

[video] "?Facts" "Figures" za chaguzi alizozitoa Lowassa alipomnadi Lema


Alichosema Haji Manara (Simba) kuhusu kauli ya Jerry Muro (Yanga)


Aeleza sababu za Waislam kuwatakia heri Waktristo


[video] Aibu michezoni: Marefa, Wachezaji "walivyopopopana" kiwanjani Mwanza


Bajeti ya uchaguzi iko tayari [video] Makamu II wa Rais Zanzibar ajibu maswaliMakamo wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema bajeti ya uchaguzi wa marudio imeshatengwa na wanachosubiri ni Mwenyekiti wa Tume ya  Uhaguzi Zanzibar (ZEC) atangaze tarehe hiyo ya kufanya uchaguzi.

Amesema bajeti hiyo haitatofautiana na ile iliyotumika katika uchaguzi wa Novemba 2015 iliyofikia karibu ya shilingi bilioni saba.

Amekanusha kauli kuwa uchaguzi huo hautafanyika kwa vile matokeo yanayolazimisha kutangazwa na CUF yameshafutwa kwa mujibu wa sheria kutokana na kasoro kadhaa zilizojitokeza.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Miaka 52 ya Mapinduzi, Balozi Seif amesema mazungumzo yanayoendelea ni ya kuhakiksha amani inaimarika Zanzibar na si suala la uchaguzi uliofutwa.

Akizungumzia kuhusu maadhimisho ya miaka 52 sherehe za Mapinduzi Balozi Seif amewabeza wanaosusuia sherehe hizo kwa madia kuwa Rais Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein kuwa si halali ni upotoshwaji mkubwa.

Amefahamisha kuwa rais huyo yupo kihalali na hata mawaziri wake wote na watamaliza ukomo wao atakapoapishwa rais mwingine kama ilivyoanishwa katika kifungu cha 28 (1) a cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 na si kama inavyeleezewa kuwa ukomo wake umeisha tangu tarehe 2 Novemba.

Kwa mujibu wa Balozi Seif, maadhimsiho ya sherehe hizo yanatarajiwa kuanza kesho kwa shughuli za usafi na ufunguzi wa miardi ya maendeleo 24 na kufikia kilele chake Januari 12 katika uwanja wa Aman.

Mawasiliano ya SUMATRA kwa ajili ya kupendekeza nauli za mabasi ya DART

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti, Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kwa vyombo vya habari kwenda kwa wananchi inawaalika wadau wote wa usafiri kupendekeza viwango vya nauli za mabasi yatakayotoa huduma ya usafiri wa haraka Jijini Dar es Salaam.

Mamlaka hiyo  pia inapokea maoni ya wananchi kupitia:
  • Kuchangia maoni kwenye mkutano utakaofanyika Januari 5, 2016 katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam kuanzia saa 3 na nusu asubuhi
  • Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA, S.L.P 3093, Dar es Salaam.
  • Barua pepe: [email protected] 
  • Maoni ya maandisi yatapokelewa kwenye ofisi ya Mkuregenzi Mkuu iliyopo Jengo la Mawasiliano House (Makutano ya barabara ya Ali Hassani Mwinyi na Nkumo), kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 9 alasiri. 
Mwisho wa kupokelewa maoni ni Januari 13 mwaka huu.

Mamlaka hiyo imepokea maombi ya nauli kutoka kampuni ya UDA-RT inayolenga kutoa huduma ya mpito ya usafirishaji jijini Dar es Salaam katika kutekeleza awamu ya kwanza ya mradi wa DART. Maombi yaliyowasilishwa na kampuni hiyo ni safari kwenye njia za pembeni (feeder route) shilingi 700, safari kwenye njia kuu (trunk route) shilingi 1,200 na njia zote mbili ni 1,400 ambapo wanafunzi watalipa nusu nauli anayotoa mtu mzima.

Job: Chief of Party, Tanzania Youth Entrepreneurship Project

Organization: Winrock International
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 31 Jan 2016

Job: Director of Finance & Administration, Tanzania Youth Entrepreneurship Project

Organization: Winrock International
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 31 Jan 2016

Job: M&E Specialist, Tanzania Youth Entrepreneurship Project

Organization: Winrock International
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 31 Jan 2016

Job: Youth Employment and Livelihoods Specialist, Tanzania Youth Entrepreneurship Project

Organization: Winrock International
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 31 Jan 2016

Usalama wa Taifa wamfuta kazi aliyekuwa mlinzi wa Nyerere, Lowassa


  • Ni ofisa usalama mwandamizi aliyepigana Vita ya Uganda
  • Alikuwa ‘bodyguard’ wa Nyerere aliyemfia mikononi
ALIYEKUWA mlinzi wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ofisa usalama mwandamizi, Aloyce Tendewa, amefukuzwa kazi.

Taarifa zilizolifikia MTANZANIA Jumamosi kutoka vyanzo vyake vya uhakika vilivyo serikalini, zimedai kuwa Tendewa amefukuzwa kazi na mwajiri wake ambaye ni Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) kwa kosa la kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kikazi.

Mbali na taarifa hizo, imeelezwa pia kuwa sababu nyingine ya kufukuzwa kwake kazi kwa mwanausalama huyo ambayo hata hivyo haijathibitishwa na vyanzo vya uhakika vya gazeti hili, ni madai ya kutoa taarifa za kubadilishiwa kituo chake cha kazi cha awali.

Inadaiwa kuwa Tendewa baada ya kuvuliwa jukumu la kumlinda Lowassa alibaki na kinyongo moyoni kwa sababu hakuridhika na hatua hiyo hivyo alivujisha taarifa hizo kwa vyombo vya habari jambo lililoelezwa kuwa ni kinyume na maadili ya kazi yake.

Kwa mujibu wa vyanzo vya gazeti hili, Tendewa alipewa barua ya kuachishwa kazi juzi jioni baada ya kuvuja kwa uhamisho wake kwenye vyombo vya habari.
“Alikuwa bado anataka kuendelea kumlinda mzee (Lowassa), lakini kuna vitu alishindwa kuvitekeleza kwa ufasaha kwa hiyo kitendo cha kuondolewa kilimuudhi akaamua kupeleka taarifa gazetini jambo ambalo ni kinyume na taratibu zao za kazi za kiusalama,” 
alidokeza mmoja wa maofisa aliyezungumza na gazeti hili.

Kwa upande mwingine taarifa zinaeleza kuwa mpango wa kutimuliwa kwa Tendewa uliandaliwa kwa muda wa miezi kadhaa na barua ya kufukuzwa iliandikwa baada tu ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka jana.

Kwamba, pamoja na sababu nyingine Tendewa anadaiwa kushindwa kuwasiliana inavyotakikana na viongozi wake kuhusu majukumu yake ya kiulinzi wakati akiwa mlinzi wa Lowassa.

Taarifa zinadai, kushindwa huko kwa Tendewa kuliwafanya viongozi wake kufikia uamuzi wa kumfukuza kazi na kwamba barua yake iliandikwa mapema Desemba mwaka jana, lakini hakukabidhiwa hadi hivi karibuni alipovujisha siri za kuhamishwa kwake kituo cha kazi.

Mmoja wa watoa habari wa gazeti hili aliyeko serikalini ameeleza kuwa Tendewa aliundiwa kamati ya kumchunguza kuhusu kushindwa kutekeleza majukumu sawasawa ambayo ilifanya kazi kwa muda wa wiki mbili na kuwasilisha ripoti yake makao makuu.

Hata hivyo, alisema bado kuna utata kuhusu mtu aliyesaini barua ya kufukuzwa kazi kwa Tendewa ambaye kwa wadhifa wake ilipaswa kusainiwa na Mkurugenzi Mkuu lakini badala yake imesainiwa na ofisa wa cheo cha chini.

Jitihada za kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Taifa, Othmani Rashid, hazikuweza kuzaa matunda hadi tunakwenda mitamboni na hata Mkuu wa Kikosi cha Usalama wa Viongozi, Ben Mashiba naye hakuweza kupatikana.

Tendewa amefukuzwa kazi akiwa amebakiza mwaka mmoja kustaafu utumishi wake katika Idara ya Usalama wa Taifa.

Rekodi zilizoonwa na gazeti hili za utendaji kazi wa Tendewa zinaonyesha kuwa baada tu ya kuajiriwa na TIS, alipelekwa katika kikosi cha walinzi wa hayati Mwalimu Julius Nyerere na kutokana na uhodari wake aliaminiwa na Mwalimu.

Aidha, rekodi hizo zinaonyesha kuwa Tendewa ni miongoni mwa wana usalama wachache waliopigana vita ya kumng’oa aliyekuwa Rais wa Uganda, Fashisti Iddi Amini Dada mwaka 1978 na 1979 na akiwa vitani alitekwa na kwenda kuzuiliwa nchini Sudan.

Historia hiyo inaonyesha kuwa Tendewa aliokoka kuuawa kwa risasi akiwa mateka muda mfupi baada ya kurejeshwa nchini kutoka Sudan siku chache baada ya Rais Yoweri Museveni kushika madaraka ambapo mmoja wa walinzi wanawake wa rais alimuona na kumtambua kuwa alikuwa mmoja wa wapiganaji hodari wa Tanzania na si muasi kama ilivyokuwa ikidhaniwa hivyo alirudishwa Tanzania.

Baada ya kurejeshwa nyumbani alipewa jukumu la kuwa mlinzi wa Mwalimu Nyerere na hata alipong’atuka madarakani aliendelea na kazi hiyo hadi Mwalimu alipofariki dunia katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas London nchini Uingereza.

"Ambaye hakubaliani na hilo asimame pembeni tu ili waliobaki waendelee” Rais Magufuli

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence S.Milanzi akila kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaapisha Makatibu Wakuu na Naibu wakatibu wakuu iliyofanyika katika Ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam.

  • Video ya tukio zima la kuapishwa ipo mwishoni mwa taarifa hiii

RAIS John Magufuli amewataka makatibu na manaibu makatibu wakuu walioapishwa jana kukubali ahadi ya uadilifu wa viongozi na asiyetaka akae pembeni.

Muhimbili ‘informer’ patient refuses to leave MOI


The patient, Chacha Makenge, is currently putting up in Ward Number 18 of the Muhimbili Orthopaedic Institute (MOI), and according to the Acting Director, Dr Samwel Swai, he had been discharged since December 10.

According to him, after realising that Makenge was not able to pay for his fare back home in Mugumu, Serengeti District in Mara Region, prompting the hospital to pay his fare but he disappeared without notifying anybody at the facility.

According to MOI Public Relations Officer, Mr Patrick Mvungi, the hospital paid 33,000/- for Makenge’s fare while another 57,000/- was set aside as his pocket money. But he reportedly disappeared before taking his ticket and the money.

“He came back on December 17 and since then he has stayed in the ward and our efforts to convince him to leave the hospital has hit a brick wall,’’ he said. The acting MOI chief said the hospital was now contemplating calling specialists from the MNH Psychiatric Department to examine the state of his mind to see if he is mentally challenged.

Makenge has been at the hospital for three months and according to Dr Swai, his treatment had cost the facility more than 300,000/- . But he insisted that he had fully recovered and that he had no any other problems that needed treatment from MOI.

On November 9, Dr Magufuli made an impromptu visit to MNH and ordered that Makenge, who had stayed in the hospital for two months, be taken for an immediate CT-Scan. Makenge had from his hospital bed; briefed Dr Magufuli on what was transpiring at the hospital, including the quality of services and failure of crucial equipment at the facility.

The ‘Daily News’ visited Makenge but he declined any comment regarding his decision to stay on. He did not utter a word despite efforts to convince him to talk.

The Nurse in-Charge of the ward, Ms Lidarose Rutaguza, said Makenge had at one point left his bed and went on to sleep on the floor without stating why he had opted to do so.

“There are times when he would decide to disappear from the hospital and go out for the whole day and come back in the evening without saying what he has been doing out there,’’ she added.
  • via The Daily News

Viwango vya ufaulu mitihani havijabadilika - Taarifa ya Wizara


Basi latumbukia mto Lukosi na kuua, kujeruhiWATU watatu wamekufa baada ya basi la abiria lenye namba za usajili T 922 BUW aina ya Yutong mali ya kampuni ya AL- Hushoom, kutumbukia kwenye mto Lukosi eneo la Msosa, Iyovi, Wilayani Kilosa, mkoa wa Morogoro baada ya kugonga kingo za daraja na kuparamia miti miwili

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo alisema leo kuwa ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa nane mchana, wakati basi hilo likitokea jijini Dar es Salaam kwenda mkoani Mbeya.

Miongoni mwa waliokufa ni dereva wa basi hilo. Wapo majeruhi 16, kati yao 14 walilazwa katika Kituo cha Afya cha Mtandika kilichopo eneo la wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa na wengine sita walisafirishwa hadi hospitaali ya mkoa wa Iringa na kulazwa huko.Taarifa: Mafuriko Kilosa hadi Gulwe yasababisha TRL isimamishe huduma

KAMPUNI YA RELI TANZANIA (TRL)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI (PRESS RELEASE)

Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania TRL umetangaza kusitisha kwa muda kuanzia jana Januari 01, 2016, huduma zake baada ya eneo la reli ya kati ya Kilosa mkoani Morogoro na Gulwe mkoani Dodoma tuta la reli kukumbwa na Mafuriko.

Kwa mujibu wa taarifa za kifundi eneo lililoathiriwa na mafuriko ni kubwa hivyo Wahandisi na Mafundi wa TRL wako eneo la mafuriko kutathmini ukubwa wa kazi yenyewe.

Kutokana na uamuzi huo treni ya abiria kutoka bara ilibidi safari yake ikatizwe ilipofika Dodoma na tayari utaratibu unaandaliwa wa kupata mabasi 17 kuwasafirisaha hadi Dar es Salaam abiria 1,119. wa treni hiyo.

Hali kadhalika kwa vile tarahe ya kuanza tena huduma bado haijaujulikana, safari zote kuanzia jana Januari 01, 2016, kwenda bara zimefutwa na abiria husika wametakiwa kufika katika vituo vya reli walikokata tiketi ili warejeshewe fedha zao na kupata fursa ya kutafuta usafiri mbadala. 

Aidha imesisitizwa kuwa Uongozi kwa wakati muafaka itatoa taarifa kamili kuhusu lini huduma za TRL kwenda bara zitaanza tena.

Wito unatolewa kwa kila mwananchi atakayepata taarifa hii muhimu amwaarifu mwenzake.

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa niaba ya  
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Mhandisi Elias Mshana.
Dar es Salaam,
Januari 02, 2016

mwisho

Makatibu Wakuu na Manaibu wapewa semina elekezi ya siku moja


Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akizungumza na Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu wakati akifungua Semina Elekezi kwa Makatibu hao Ikulu jijini Dar es SalaamBaadhi ya Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika Semina elekezi ya siku moja Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Kitabu: Dokta John Magufuli - Safari ya Urais, Mafanikio na Changamoto


Heri ya mwaka mpya. Nina furaha kuwafahamisha kuwa kitabu kipya, "Dokta John Pombe Magufuli: Safari ya Urais, Mafaniko na Changamoto katika Urais wake" sasa kinapatikana. Kitabu hiki ni mfululizo wa vitabu kadhaa ninavyotarajia kuvichapisha mwaka huu 2016.

Wakati kitabu hiki kikiingia sokoni, kitabu kingine kuhusu taaluluma ya Usalama wa Taifa kipo katika hatua za mwisho, na matarajio ni kukiingiza sokoni mwishoni mwa mwezi huu.

Kitabu hiki cha Dokta Magufuli kina sura sita. Katika utangulizi, kitabu kinazungumzia mazingira ya uchaguzi mkuu uliopita, msisitizo ukiwa kwenye hali ya nchi ilivyokuwa kabla ya uchaguzi huo.

Kadhalika, utangulizi huo unaelezea mabadiliko ya ghalfa ya kisiasa, hususan ndani ya CCM, yaliyojitokeza kufuatia jina la mwanasiasa aliyekuwa maarufu kuliko wote wakati huo, Edward Lowassa, kukatwa na chama hicho tawala wakati wa mchakato wa kupata mgombea wake wa kiti cha urais.

Sura ya kwanza inamtambulisha Dokta Magufuli, kwa kuangalia historia fupi ya maisha yake. Sura ya pili inaeleza mchakato aliopitia Dkt Magufuli hadi kuibuka mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM. Sura hii inachambua kwa undani ushindani miongoni mwa makada zaidi ya 40 waliochukua fomu kuwania urais kupitia chama hicho.

Sura ya tatu inaelezea fursa alizokuwa Dokta Magufuli na CCM kwa ujumla katika kipindi cha kampeni na uchaguzi mzima kwa ujumla. Sura hii inachambua uimara wa mwanasiasa huyo sambamba na turufu za kawaida za CCM katika kila uchaguzi. Kwa uapnde mwingine sura hiyo yaangalia pia mapungufu yaliyopelekea urahisi kwa Dokta Magufuli kumshinda mpinzani wake mkuu Lowassa, sambamba na mapungufu ya UKAWA yaliyoiwezesha CCM kushinda.

Sura ya nne inajadili changamoto na vikwazo kwa Dokta Magufuli na CCM kwa ujumla wakati wa kampeni. Kadhalika, sura hii inazungumzia jinsi Lowassa na UKAWA walivyoshindwa kutumia changamoto hizo za wapinzani wao.

Sura ya tano inajadili urais wa Dokta Magufuli tangu aingie Ikulu, wakati sura ya mwisho inajadili changamoto zinazoukabili urais wake na kutoa mapendekezo.

Nimejitahidi kadri nilivyoweza kuandika kitabu hicho kama mtu niliyeufuatilia uchaguzi huo kwa karibu. Natambua kuna wanaoweza kuwa na hofu kuwa 'niliisapoti CCM na Dokta Magufuli wakati wa kampeni, na kutoiunga mkono UKAWA na Lowassa.' Naomba kuwatoa hofu kwani kitabu hiki ni si cha kiitikadi bali kwa ajili ya Watanzania wote bila kujali tofauti zao za kiitikadi.

UTAKIPATAJE?

Bei ya kitabu sasa ni Shilingi 4,000 tu. Ili kukipata, nunua kwa M-PESA namba 0744-313-200 jina JOHN ZABLON MPEFO au TIGO-PESA namba 0652-112-071 jina CHRISTINE JOHN MANONGI

KARIBUNI SANA

[video] Kivutio cha Irente View Point - Lushoto, TangaHapa ndipo kileleni na mwonekano wa Irente
Watu wengi wamekuwa na utaratibu wa kukalili kuwa wanapoambiwa kwenda kufanya utalii basi mawazo yanahamia katika hifadhi za taifa au Fukwe za Bahari, wakati kuna utalii wa kupanda milima,utalii wa uwindaji utalii wa picha, utalii wa kiutamaduni,Utalii wa Ikolojia,utalii wa fukwe,Michezo ya kwenye maji, utalii wa mali kale,utalii wa mikutano,utalii wa matibabu,utalii wa mashambani na utalii wa jiji.

Irente View Point inapatikana katika kijiji cha Irente kilichopo wilayani lushoto mkoani Tanga, eneo hili liligunduliwa na wazee wa kale ambao walikuwa wakifika hapo kwa ajili ya kuomba na kufanya matambiko na wengine walikuwa wakifika katika eneo hilo kwaajili ya kufanya ibada hasa wakati wa sikukuu za Christmas

Eneo hili lina urefu wa Mita 1500 kutoka usawa wa Bahari , ukiwa juu unaweza kuona maeneo mbalimbali vizuri bila usumbufu wowote, pia watalii wengi wamekuwa wakifika eneo hilo kutokana na hali ya hewa kuwa nzuri, kuona Mandhari nzuri hasa wakati wa asubuhi na jioni.

Jinsi ya kufikia ikiwa unatokea upande wowote, fika hadi Mombo, panda daladala Tsh 3,000 mpaka Lushoto mjini baada ya hapo unaweza panda Boda boda Tsh 3,000 au ukachukua Tax Tsh 10,000 , kiingilio ni Tsh 2,000.

Hii ni Miamba mikubwa iliyopo Irente na moja ya kivutio kikubwa katika eneo hili kwa upande kwa Kushoto.Eneo hili wakazi wa Irente wanaliita Pango ambapo watu wengi wanapenda kupigia pichaHii ni njia ya kuelekea Pangoni
Ukiwa Juu ndani ya Pango utaona hivi

Mmoja wa walinzi akiandika akiwakatia risiti wageni mbalimbali waliotembelea eneo hilo.


Mmoja wa wandishi wa Blogs za Mikoa Fredy Tony akiwa amefika kujionea eneo hilo.

(Imeandaliwa na Fredy A. Njeje 0765056399)