Mapitio ya magazetini, Jumatatu, Januari 4, 2015

Mwl. Mndeme: Kwa nini simu za mikononi ni tishio kwa jamii yetu?

SIMU ZA MIKONONI: SEHEMU YA II

Kwa nini simu za mikononi ni tishio kwa jamii yetu?

Katika makala hii na zitakazofuata, ninapotumia neno matumizi ya simu za mkononi, ninamaanisha mawasiliano ya kupiga na kupokea simu; utumaji na upokeaji wa ujumbe mfupi wa simu (SMS); matumizi ya mitandao ya kijamii kupitia simu; kucheza games kupitia simu; kutuma na kupokea barua pepe; na matumizi mengine ya intaneti kupitia simu.
https://1.bp.blogspot.com/--NMZ7DFagP0/Vom4Pb3kT0I/AAAAAAAABmI/uVqvpNxG-6M/s400/simu%2Bnyingi.jpg
Tangu kugunduliwa kwa teknolojia ya simu za mikononi, imekua na kuenea/kusambaa kwa haraka sana duniani kuliko teknolojia nyingine yoyote ile ambayo imewahi kugunduliwa katika historia ya mwanadamu. Kwa mfano: wakati ugunduzi wa runinga umetokea kama miaka 100 iliyopita, Tanzania bara tumeanza kutazama runinga kama miaka 25 tu iliyopita. Kulingana ya repoti ya mwisho wa mwaka 2014 ya Mamalaka ya Mawasiliano nchini (TCRA),Tanzania kuna wastani wa
runinga 1,000,000 pekee. Simu za mezani (landline au za TTCL) zimegunduliwa kwa mara ya kwanza na mskotishi Alexander Graham Bell mwaka 1876 lakini hadi mwezi wa tisa mwaka huu ni wateja (subscribers) takribani 304,000 pekee ndio wanamiliki simu hizi. Hali kadhalika, wakati ugunduzi wa internet umetokea miaka ya 1960, Tanzania tumeanza kutumia internet mwishoni mwa miaka 1990 tena kwa watu wachache sana. Hadi mwezi wa tisa mwaka 2015 ni takribani watu 1.9M pekee ndio wanamiliki (subscribers) huduma hii ikiwa ni pamoja na maofisi. Mashine za kufulia nguo (washing machines) zimeanza kutumika nchini Sweden mwanzoni mwa miaka ya 1950 lakini hadi sasa watanzania wanaotumia teknolojia hii kama kifaa cha nyumbani ni wa kutafuta na huenda kuna mikoa haina hata mashine moja. Usambazaji umeme umefanyika kwa mara ya kwanza nchini Uingereza mwaka 1881 lakini hadi leo miaka 135 baadaye, umeme ni huduma ya anasa Tanzania na umewafikia watu chini ya 40%.

Kinyume na hayo yote, teknolojia ya simu za mikononi imeanza kutumika rasmi mwishoni mwa miaka ya 1980 lakini haikuchukua miaka kumi ikawa imeshaingia nchini kupitia makampuni kama ya Traitel, Mobitel na mengine. Kutokana na taarifa za TCRA, hadi mwezi wa sita mwaka 2015 kuna watumiaji wa simu (yaani SIM cards zilizoko zinazotumika) milioni 35.6. Unaweza kuona ni kwa jinsi gani simu za mkononi zimekua sehemu ya maisha ya watanzania. Teknolojia hii imekuza na kuboresha mawasiliano na upatikanahi wa taarifa kwa kiasi kikubwa. Simu za mikononi kuweza kutumia internet imechagia zaidi ongezeko la matumizi yake na kubadilisha kabisa dhana nzima ya mawasiliano katika jamii.  

Tafiti nyingi za kisayansi zimefanyika kote duniani kuhusu matumizi ya simu. Hata hivyo, tafiti nyingi zilizofanyika katika mazingira ya nchi kama zetu (nchi za dunia ya tatu) kuhusu matumizi ya simu za mikononi, zimejikita katika kutazama faida zake na jinsi ya kuzitumia kukabiliana na changamoto mbalimbali kama vile kurahisisha mihalama ya fedha; mawasiliano na utoaji wa huduma za afya; ufanyaji biashara; na utafutaji wa masoko na bidhaa. Hali kadhalika, nyingi ya hizi tafiti zimejikita zaidi katika teknolojia yenyewe na inavyofanya kazi huku machache yakisemwa kuhusu uhusiano wa teknolojia ya simu za mikononi na maisha ya kila siku ya watu na tamaduni zao.


BOFYA HAPA kuendelea kusoma makala hii