Jiunge "Jamii Active", jifunze, jadili kuhusu Mazoezi, Mazingira na Afya
Rais Magufuli akutana na viongozi mbalimbali Ikulu; CAG alinganisha pato la taifa la serikali: Tanzania vs KenyaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Juma Assad Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Profesa Mussa Juma Assad Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuberi Ally Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuberi Ally, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania MheshimiwaDkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Bw. Biswalo Eutropius Mganga Ikulu jijini Dar es Salaam.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi CCM Alhaji Abdallah Bulembo aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi CCM Alhaji Abdallah Bulembo Ikulu jijini Dar es Salaam.
  • Picha zote: IKULU

Waziri Lukuvi aagiza shamba la Kapunga lirejeshwe kwa wananchi


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi ameagiza ekari 1,870 za ardhi ya shamba la Kapunga wilayani Mbarali mkoani Mbeya kurejeshwa kwa wananchi kwa kugawiwa wanavijiji. Hatua hiyo inamaliza mgogoro wa miaka kumi uliokuwa kati ya wananchi hao na mwekezaji.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa ahadi ya rais Dk. John Pombe Magufuli ya kuchukua mashamba yasiyoendelezwa.

Kwa kipindi cha miaka kumi, wananchi hao walikuwa wakilalamika kukodishwa mashamba ya kulima mpunga na mwekezaji huyo kwa masharti magumu.

Mapitio ya magazeti leo Jumanne, Januari 5, 2015


Atakayekutoza damu, tuambie, tutamfukuza kazi - Agizo la Naibu Waziri:


Afisa Uendeshaji wa Ofisi za Mpango wa Taifa wa Damu Salama zilizopo jijini Dar es Salaam, Bw. Abdu Juma akitoa maelezo ya namna wanavyoendesha shughuli zao kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kingwangalla aliyefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi hizo, Januari 4, 2016. (Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Na Modewjiblog, Team.

Waziri Nchemba "awatimua" wakurugenzi wote NARCO na kuagiza wachukuliwe hatua kisheria

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi akiwasili kwenye mradi uliodumaa wa ujenzi wa machinjio ya kisasa wa ranchi ya Ruvu, Januari 4, 2016.Wakati Taifa na Mataifa yakiendelea kutoa pongezi zao kwa serikali ya Rais J. P. Magufuli kwa kasi yake ya uchapa kazi, Mawaziri wake pia wameendelea kuonesha namna walivyodhamiria kusimamia shughuli za maendeleo ya nchi yetu.

Jumatatu, Januari 4, 2016, Mhe. Mwigulu Nchemba mwenye dhamana ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi amefanya ziara ya siku moja kwenye ranchi ya Taifa ya Ruvu kukagua ujenzi wa majengo ya machinjio ya kisasa ulioanza mwaka 2010.

Katika hali ya kusikitisha na kulazimu kuchukua hatua za kinidhamu, Mwigulu Nchemba amekutana na ubadhilifu wa shilingi bilioni 5.7/= ambazo zilitolewa kwaajili ya ujenzi wa jengo hilo. Fedha hizo zilizokuwa zimelengwa kuwezesha ujenzi wa machinjio hayo ya kisasa hazijafanya kazi kama ilivyokusidiwa.

Waziri huyo wa Kilimo amekuta mradi huo umetelekezwa tangu mwaka 2010, sababu za kutelekezwa kwa mradi huo zikidaiwa kuwa ni kutofautiana kwa mkandarasi na bodi ya NARCO (Kampuni ya Usimamizi wa Ranchi za Taifa) hazikukubalika na Mhe. Mwigulu Nchemba ambaye baada ya kusikiliza kwa makini ufafanuzi wa kutoka kwa viongozi wa ranchi hiyo aliamua ifuatavyo.
  • Kwanza, Mwigulu Nchemba amewatimua wakurugenzi wote wa bodi ya NARCO yenye dhamana ya kusimamia ranchi za Taifa kwa kushinda kukamilisha ujenzi wa mradi huo.Mbali na kushindwa,bodi hiyo imeutelekeza mradi huo na hivi sasa inapendekeza kujengwa kwa mradi mwingine kama huo ndani ya eneo hilohilo la ranchi ya ruvu.
  • Pili, Mwigulu Nchemba amesitisha utumishi wa Mkurugenzi Mkuu wa ranchi za Taifa kwa kushindwa kuchukua hatua za kusimamia ujenzi wa mradi huo hadi kukamilika kwake.
  • Pia, Waziri huyo wa kilimo ameagiza kupitia vyombo vya sheria, wahusika wote walioshiriki ama kwa makusudi au kwa njia yoyote kuhujumu mradi huo usifanikiwe, wanachukuliwa hatua haraka iwezekanavyo.
  • Mwisho, Nchemba amewaagiza wataalamu wa wizara yake kuhakikisha ndani ya siku 7 wanampelekea ripoti ya thamani ya jengo lililokwisha kujengwa na fedha zinazotakiwa kumalizia ujenzi wa jengo hilo.
Sambamba na hatua hizo, Mwigulu ametoa rai kwa watumishi wote wa umma kuwa mstari wa mbele kusimamia kwa ufanisi na uzalendo miradi yote ya maendeleo ya nchi yetu, Mbali na hapo, serikali ya Rais Magufuli haitakuwa tayari kuona mali ya umma inachezewa na kuibiwa wakati kuna Watanzania wanaweza kusimamia mali hizo na kuziendeleza.

Sehemu ya jingo lililobaki kama gofu mara baada ya kutelekezwa na uongozi wa bodi ya ranchi za Taifa (NARCO)
Mwigulu Nchemba akishangaa namna mali hii ya umma ilivyotekelezwa.
Mwigulu akiwa na jopo la wataalam wakiendelea kutathimini hasara iliyojitokeza kutokana na ujenzi mbovu wa machinjio ya kisasa hapa Ruvu.
Mwigulu Nchemba akiwa na Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwani wakisikiliza kwa makini sababu zilizopekea jingo hilo kutelekezwa. Anayetoa maelezo wa mwisho kushoto ni msimamizi wa ranchi hiyo Ngd. Bwire.
Sehemu ya jingo ikiwa imetelekezwa bila kuendelezwa kiujenzi.
Hii ni sehemu ya ukuta wa jingo hilo ambao umekatika kutokana na kukaa muda mrefu bila kuendelezwa.
Mwigulu Nchemba akiendelea kupewa maelezo ya kina kuhusu ubadhilifu uliojitokeza kwenye ujenzi huu.
Mhe. Ridhiwani Kikwete, Mbunge wa Chalinze akitoa malalamiko yake kwa Waziri.Mwigulu Nchemba kuhusu kukosekana kwa mahusiano mazuri kati ya wamiliki wa ranchi na wananchi wanaozunguka ranchi ya Ruvu.
Kwa mbali hili ndio jengo la machinjio ya kisasa lililokuwa linajengwa na hatimaye kutelekezwa bila kuendelezwa tangu mwaka 2010.
Mhe.Mwigulu Nchemba akiteta jambo na viongozi wanaohusika na kulinda baadhi ya vifaa vilivyonunuliwa kwaajili ya ranchi hiyo ya kisasa.
Mhe.Mwigulu Nchemba akioneshwa baadhi ya Ng'ombe wanaopatikana kwenye ranchi hiyo.
Mwigulu Nchemba akiwa kazini kwenye shamba la Mifugo la Ruvu hii leo.

Mwigulu Nchemba akidadisi utunzaji wa maji ya Mifugo inayopatikana ndani ya ranchi ya Ruvu.

Picha/maelezo na Festo Sanga Jr

Serikali yainunulia Hospitali ya Taifa ya Muhimbili mashine ya CT-scan

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Hamis Kigwangala (katikati), akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mionzi cha Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk. Flora Lwakatare kuhusu mashine mpya ya CT-Scan alipofanya ziara katika hospitali hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Prof. Lawrence Mseru.
Na Magreth Kinabo –MAELEZO

Serikali imenunua mashine mpya ya CT-Scan yenye thamani ya takriban dola za Marekani milioni 1.7 yenye uwezo wa hali ya juu kwa ajili ya kutoa huduma za uchunguzi wa magonjwa mbalimbali katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH) iliyopo jijini Dar es Salaam.

Ununuzi wa mashine hiyo, umefanyika kufuatia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli aliyoifanya hivi karibuni ambapo aliutaka uongozi wa hospitali hiyo kuboresha huduma zake na kuhakikisha vifaa tiba na dawa vinapatikana ili kuhakikisha Watanzania wanapata huduma bora za afya.

Hayo yamegundulika leo baada ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kingwangala aliyoifanya leo katika hospitali hiyo, ambapo alitembea Idara ya Magonjwa ya Dharura,Idara ya Mionzi, sehemu mpya ya wagonjwa waliopo chini ya ungalizi maalum(ICU), ambayo inafanyiwa ukarabati na wodi mojawapo.

Naibu Waziri akitembelea katika Idara ya Mionzi ambapo alijionea mashine za MRI na CT –Scan zinavyofanyakazi.
Akizungumzia kuhusu mashine ya CT-Scan Mkuu wa Idara ya Mionzi, Dkt. Flora Lwakatare alisema mashine hiyo , iliyotengenezwa na kampuni ya Siemens mpya imefungwa siku mbili zilizopita na imeshaanza kufanya majaribio kwa wagonjwa 26 tangu ilipofungwa

Dkt. Flora aliongeza kwamba mashine hiyo iko moja tu nchini na katika nchi za Afrika Mashariki nchi nyingine iliyonunua mashine hiyo ni Kenya katika Hospitali ya Aghakhan.

“ Mashine hii inatoa huduma za hali ya juu kwa magonjwa ya moyo, ubongo tumbo kifua na inauwezo wa kupima kifua na tumbo kwa sekunde sita,” alisema.
Akizungumzia kuhusu mashine hiyo Naibu Waziri huyo, alisema imenunuliwa kwa fedha za Serikali wala sio mkopo.

“Tunatarajia kununua mashine hii katika hospitali ya Dodoma na Mwanza,” alisema Waziri Kingwangala.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa MNH, Profesa Laurence Maseru alisema mashine hiyo ina sahani 128 mara 2 ikilinganishwa na iliyokuwepo ambayo ilikuwa inatumia sahani sita.
Kwa upande wa mashine ya MRI ambayo tangu ilipofanyiwa matengenezo makubwa Novemba 26, mwaka jana hadi sasa imesha hudumia wagonjwa 560.

Dkt. Kingwangala alitembea katika Idara cha huduma za dharura na kuangalia jinsi huduma zinavyotolewa, ambapo alielezwa na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura Dkt. Juma Mfinaga alisema ambayo huhudumia wastani wa wagonjwa 300 hadi 400 kwa siku ambacho kinafanya kazi kwa kutumia mfumo maalum wa kompyuta bila kutumia karatasi.

Naibu Waziri huyo, mbali na kupongeza maboresho yaliyofanyika na huduma nzuri, alitoa maagizo kwa uongozi wa hospitali hiyo kuboresha huduma za zilinazotolewa hospitalini kuwa za kitaifa zaidi.
Alitolea mfano huduma kulipa kwa kuongeza vitanda na matumizi ya choo kimoja kila chumba ili kuweza kuvutia wateja.

“Sisi tunaweza kufanya biashara kwa kuboresha huduma za kulipa ili zimpendeze na kuvutia wateja. Na fedha zitakazopatikana zitatumika kununua dawa , vifaa tiba na kuwapatia wafanyakazi motisha, alisema.

Aliutaka uongozi huo pia kuhakikisha inawalipa wafanyakazi fedha za malipo ya ziada kwa wakati ifikapo tarehe 25 ya mwezi unaofuata,kutumia mfumo wa kompyuta sehemu zote, kupunguza msongamno wa wagonjwa na kuwa wabunifu.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Hamis Kigwangala akiangalia wodi mpya ya ICU wakati wa ziara yake katika Hospitali ya Taifa muhimbili. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Prof. Lawrence Mseru.


Mtaalam wa Mionzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbi, Medard Mallya akimuonesha mashine ya MRI.

Taarifa ya Serikali ya mwelekeo wa ugonjwa wa kipindupindu

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangalla akitoa tamko kwa umma, kuhusu mwenendo wa ugonjwa wa kipindupindu katika mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake jijini Dar es Salaam. Pichani chini kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu katika Wizara ya Afya (Kaimu Mkurugenzi), Michael John.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangalla ametoa tamko kwa umma, kuhusu mwenendo wa ugonjwa wa kipindupindu ulioanza tarehe 15 Agosti, 2015 katika mkoa wa Dar es Salaam na kusambaa kwa kasi katika Mikoa mingine 21 ya Tanzania Bara ambayo ni Pwani, Morogoro, Iringa, Kilimanjaro, Dodoma, Kigoma, Geita, Mara, Manyara, Arusha, Shinyanga, Tabora, Singida, Tanga, Lindi, Rukwa, Kagera, Katavi, Mbeya na Mwanza na Simiyu.

Tangu ugonjwa huu uanze, jumla ya watu 12,810 wameugua Kipindupindu, na kati yao jumla ya watu 202 wameshafariki kwa ugonjwa huu ambayo ni sawa na asilimia 1.6 ya waliougua. Katika kipindi cha wiki iliyoanza tarehe 28 Desemba 2015 hadi tarehe 3 Januari 2016, kumekuwa na jumla ya wagonjwa walioripotiwa 590 na vifo 6, ambayo ni asilimia 0.01 ya wagonjwa wote. Mkoa wa Mara (Musoma Mjini) ndio ulikuwa unaongoza kwa kasi ya maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu ukifuatiwa na Singida (Iramba), Morogoro (Morogoro Vijijini) na Manyara (Simanjiro).

Takwimu zinaonyesha kuwa licha ya kuwa na nafuu katika wiki ya nyuma, wiki hii kasi ya maambukizi inaonesha kupanda tena kwenye mikoa ya Mwanza na Arusha. Katika mkoa wa Arusha, maambukizi yamepanda kutoka wagonjwa wapya 60 hadi 111 kwa wiki. Katika mkoa wa Mwanza, kasi ya maambukizi imepanda kutoka wagonjwa wapya 45 hadi 66 kwa wiki.

Kasi ya maambukizi ya Kipindupindu katika wiki iliyopita imepungua kwa kiasi kikubwa katika mikoa ya Mbeya na Tanga. Aidha, mikoa ya Dar-es-Salaam na Lindi haijaripoti mgonjwa yeyote mpya wa Kipindupindu katika wiki iliyopita. Tunawapongeza kwa hatua hii kutokana na juhudi zinazofanywa na wadau ambao kwa pamoja, wameshirikiana kudhibiti ugonjwa huu kwa karibu zaidi.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, kwa kushirikiana na Sekta nyingine husika, wadau wa maendeleo na wadau wengine inaendelea kukabiliana na ugonjwa huu kwa njia mbalimbali. Kikosi kazi maalum chini ya uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu kinakamilisha mpango unaoshirikisha Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto , TAMISEMI, Wizara ya Maji na Umwagiliaji, DAWASCO, DAWASA, Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi pamoja na Sekretariat ya Mkoa wa Dar-es-Salaam, kwa ajili ya kuhakikisha kuwa mikakati ya kupambana na ugonjwa huu inakuwa jumuishi na ya haraka.

Bado Wizara inaendelea kusisitiza kuwa, ili kudhibiti ugonjwa na kuokoa vifo vinavyotokana na ugonjwa huu, wananchi wanasisitizwa kunywa maji yaliyo safi na salama, kuepuka kula chakula kilichoandaliwa katika mazingira yasiyo safi na salama, kunawa mikono kwa sabuni na maji safi yanayotiririka:- kabla na baada ya kula, baada ya kutoka chooni,Baada ya kumnawisha mtoto aliyejisaidia na baada ya kumhudumia mgonjwa

Aidha, ni muhimu kuhakikisha kuwa wananchi wanatumia vyoo wakati wote na kutokujisaidia ovyo katika vyanzo vya maji vya mito, mabwawa na ziwani. Wizara ilishapiga marufuku kuuza matunda yaliyokatwa na vyakula barabarani katika mazingira yasiyo safi na salama. Hivyo, Mamlaka za Mikoa na Halmashauri pamoja na watendaji ambao ni Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Maafisa Afya, ziendelee kutoa taarifa kuhusu utekelezaji wa jambo hili.

Wizara inapeleka tena timu za wataalm katika mikoa iliyoathirika zaidi na kipindupindu ambayo ni Simiyu, Mara, Morogoro, Manyara, Singida, Arusha na Mwanza. Timu hizi zitaungana na timu za mkoa wa wilaya kusaidia kudhibiti ugonjwa huu.

Hitimisho

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, inaendelea kukumbusha kuwa, mikoa ambayo bado haijaathirika ichukue hatua za tahadhari za kuzuia ili isipate mgonjwa yeyote wa Kipindupindu.

Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) hapa nchini, Dk Rufaro Chatora (kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano makao makuu ya wizara hiyo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangalla.Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Afya (walioketi) na waandishi wa habari katika mkutano huo.