BAA CPA Review Classes at Mzumbe University Dar Es Salaam Campus College

                    

         
MZUMBE UNIVERSITY

       (CHUO KIKUU MZUMBE)

         DAR ES SALAAM CAMPUS COLLEGE

Tel:         + 255 22 2152586 GENERAL                                                                               Plot No.941/2
Cell:         + 255  (0)689 455 588                                                                                             Upanga Olympio Street
Fax:        + 255 22 2152584                                                                                                    P. O. Box  20266  
Email:     [email protected]                                                                                                DAR  ES  SALAAM

Website: http://www.mzumbe.ac.tz                                                                                     TANZANIA

                                                              
9th December 2015

NBAA CPA Review Classes at Mzumbe University Dar Es Salaam Campus College

Mzumbe University Dar Es Salaam College Campus (MUDCC) will conduct NBAA CPA Review classes from January 2016. Classes will start on 10th January 2016. The registration for Review starts 5th December 2015.

Venue: Mzumbe University Dar Es Salaam College Campus Upanga (High quality, fully air-conditioned classes, library with all essential readings).They will be conducted both in weekdays (From Monday to Friday ) and Weekends(Saturday and Sunday)

The Review classes are for   Intermediate and Final Levels.

Courses
BI Financial Management
B2 Financial Accounting
B3 Auditing Principles and Practice.
B4 Public Finance and Taxation I                                     INTERMEDIATE LEVEL
B5 Performance Management
B6 Management, Governance and Ethics   

C1 Corporate Reporting
C2 Auditing and Assurance Services
C3 Business and Corporate Finance                                   FINAL LEVEL
C4 Public Finance and Taxation

N.B: Come and Notice the difference towards your dreams in accounting profession career. Get all the subjects under one roof!

Experts: The following are key resources personnel and their qualifications.

Prof. H. P. Ngowi ……..PhD,
Prof. G. Nyamsogoro……PhD, CPA (T)
Mr. Peace Lumelezi……. .CPA (T). Msc A& F, ADA, Diploma in IFRS
Mr. Lusekelo Kasongwa  …. CPA (T) MBA, BAF, PhD (on progress)
Ms.  Mwanjaa Lyezia ……., CPA (T), CISA, Msc. Accounting & Finance, B. Com (Accounting)
Mr.Angelus Mamba……, CPA (T), ADA Msc..Investment and Finance (On Progress)
Mr. Victorius Kamuntu……, CPA (T), ADA, Msc.AEB (On progress)
Mr. Yona Nathan Bulangwahe… CPA (T), B. Com (Accounting)

Cost: 150,000 Tshs per Subject for more than two Subjects.
        : 200,000 Tshs per Subject for Single Subject

Payment: All payments should be made through: Mzumbe University Receiving Account Number 01J1043012201, CRDB.

Registration and contact persons
i)              Professor Honest Prosper Ngowi, +255 754 653 740; [email protected]

ii)             Mary Mwakatika; +255 754437354; [email protected]

"Mimi ndiye Rais na nisiposema mimi nitawatuma wasaidizi wangu kuwaeleza" - Dk Shein

STATE HOUSE ZANZIBAR

OFFICE OF THE PRESS SECRETARY

PRESS RELEASE

Zanzibar 06 Januari, 2016

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema yeye bado ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar na kutoa changamoto kwa wasioiamini Katiba hiyo kupeleka shauri hilo Mahkama Kuu ya Zanzibar ambayo ndiyo pekee yenye uwezo wa kutafsiri Katiba.

Amebainisha kuwa yeye anaongoza nchi kwa mujibu wa Katiba na Sheria na kwamba kama si uwezo huo aliopewa Kikatiba hana sababu ya kuendelea kukaa madarakani pamoja na serikali anayoingoza.

“Tuko madarakani na uongozi wote wa serikali… yupo Makamu wa Kwanza wa Rais, Makamu wa Pili wa Rais na mawaziri” alisisitiza Dk. Shein na kuongeza kuwa hao wanaodai kujiondoa serikalini huo ni uamuzi wao wenyewe.

Alibainisha kuwa yeye na serikali anayoingoza kuendelea kuwepo madarakani “si uamuzi wake” na wala yeye hana “ubavu” wa kujiweka madarakani bali ni Katiba ambayo inajieleza wazi.

Dk. Shein ametoa kauli hiyo leo kwa nyakati tofauti wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba katika siku yake ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu kisiwani humu kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi.

Aliwaambia wananchi hao kuwa yako mengi yanayosemwa lakini hawapaswi kuyasikiliza kwa kuwa kama ni serikali yeye ndiye Rais hivyo wanapaswa kumuamini anachowaeleza.

“Ya mjini yapo yasikilizeni lakini kwa Serikali mimi ndiye Rais na nisiposema mimi nitawatuma wasaidizi wangu kuwaeleza” Dk. Shein alibaisha na kuongeza kuwa ya vyama kila mtu ana chama chake.

Alifafanua kuwa kama ni suala la Chama cha Mapinduzi (CCM) yeye ndiye Makamu Mwenyekiti Zanzibar na kama kuna la kuwaeleza wana CCM na wananchi atawaeleza yeye na viongozi wenzake wa chama hicho pamoja na taarifa za vikao vya chama vyake.

Dk. Shein aliwaeleza wananchi hao kuwa ushindani wa kisiasa si ugomvi bali ni utaratibu wa kupeana changamoto katika uongozi ambao lengo ni kuwaletea wananchi maendeleo.
“tusikejeli maendeleo yetu, tuthamini chetu na ushindani wetu wa kisiasa usirejeshe nyuma maendeleo yetu” Dk. Shein alitahadharisha.

Dk. Shein aliruejea wito wake wa kuwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo yameanza tarehe 3 Januari na yanatarajiwa kufikia kilele tarehe 12 Januari, 2016 katika kiwanja cha Amaan.

Aliwakumbusha wananchi hao kuwa Mapinduzi ya Zanzibar ambayo yaliyomfanya Rais wa kwanza wa Zanzibar Mzee Abeid Amani Karume kutangaza Jamhuri ya Zanzibar, ndiyo yaliyowakomboa wanyonge wa Visiwa vya Zanzibar kwa kuondosha aina zote za ubaguzi na kuwapa mamlaka ya kujiamulia mambo yao.

Dk. Shein aliwaeleza wananchi wa Pemba kuwa meli mpya iliyonunuliwa na Serikali MV Mapinduzi II ambayo ilizinduliwa hivi karibuni, itawasili kisiwani humo tarehe 10 Janauri na siku itakayofuata itawachukua baadhi ya wananchi kwenda Unguja kushiriki maaadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi.

Alisisitiza kuwa serikali itawalipia gharama za usafiri wa kwenda na kurudi Unguja wale wote watakaoteuliwa kuwemo kwenye safari hiyo kufuatana na utaratibu utakaowekwa kama alivyokuwa ameahidi wakati meli hiyo ilipokuwa inatengenezwa nchini Korea ya Kusini.

Katika ziara hiyo Mheshimiwa Rais amefuatana na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo mawaziri, makatibu wakuu na wabunge.

Postal Address: 2422 Tel.+255 776 613 015, Fax: 024 2231822
E-mail: [email protected] & [email protected]

Askari mwingine Mwanza aua

ASKARI wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, PC Joel Francis (41) mwenye namba F.4965 anadaiwa kumpiga Donald Magalata (30) kwa fimbo na kumsababishia kifo.

Tukio hilo limetokea ikiwa ni wiki moja imepita,baada ya askari mwingine mkoani hapa Dau Elisha mwenye namba H 852 PC wa kituo cha Nyamagana kumuua askari mwenzake PC Petro Matiko wenye namba H 5950 kwa risasi na baadaye kujipiga risasi kichwani na kufariki dunia papo hapo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Justus Kamugisha alisema tukio hilo lilitokea Januari mosi, mwaka huu saa moja asubuhi katika kambi ya Polisi Mabatini.

Alisema siku hiyo, PC Francis alikwenda nyumbani kwake na kumkuta marehemu ambaye alikuwa rafiki yake wa karibu akiwa amelala.

Alisema baada ya askari huyo kuingia ndani kwake, aligundua pochi yake ya kutunzia fedha, kadi mbili za benki na kitambulisho cha kazi vyote vilikuwa havionekani ndipo alipoanza kuhoji.

“Marehemu alikuwa rafiki yake PC Francis, alikuwa akimsaidia kazi mbalimbali za nyumbani, ingawa marehemu alikuwa akifanya kazi ya ulinzi hotel ya Mwanza iliyopo katikati ya jiji.

“Sasa mzozo huo, ulisababisha PC Francis kumfunga pingu miguuni marehemu na kuanza kumpiga ovyo sehemu mbalimbali za mwili kwa kutumia fimbo kitendo kilichosababisha kupiga kelele kuomba msaada.

“Kelele za kuomba msaada ziliwafanya majirani zake pale kambini wafike na kumkuta akiwa na hali mbaya na kumchukua hadi Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa ajili matibabu,”alisema.

Alisema kutokana na kipigo alichopata, marehemu alifariki Januari 2, mwaka huu wakati akipatiwa matibabu.

Alisema tayari jeshi hilo, linamshikilia Pc Francis kwa mahojiano juu ya tukio hilo na atachukuliwa hatua za kisheria kwa mujibu wa taratibu wa kijeshi.

Kamanda Kamugisha, alisema anashangazwa na tukio hilo kufanywa na askari ambaye anapaswa kusimamia sheria na haki za binadamu, huku akisisitiza kitendo hicho kisichukuliwa kama maadili na maagizo ya jeshi la polisi, bali ni tabia ya mtu mmoja.

Mitego ya wavuvi yadhuru propeller ya MV Serengeti na kuikwamisha ziwa Victoria kwa saa 6


ABIRIA 269 waliokuwa wakisafiri kutoka Mwanza kuelekea wilayani Bukoba, wamenusurika kufa baada ya meli ya Mv Serengeti waliokuwa wakisafiria kupata hitilafu ya injini katika ziwa Victoria.

Meli ya Mv Serengeti ambayo muda sio mrefu ilitoka katika matengenezo, katikati ya mwaka jana ilipata hitilafu kama hiyo ikiwa ziwa Victoria na abiria kitendo ambacho kinaelezwa kuwapa wasiwasi watumiaji wa chombo hicho.

Meli hiyo iliyokuwa na abiria 269, tani 64 za mizigo pamoja na gari ndogo, ilipata hitilafu kwenye mfumo wa shafti na majembe ya upande wa kulia (Starboard side) ambayo ambayo yalisababisha meli hiyo kuchelewa kutia nanga katika Bandari ya Bukoba.

Akizungumza leo na waandishi wa habari mjini hapa, Kaimu Meneja wa Kampuni ya Usafirishaji Majini, Kapteni Winton Mwassa, amesema meli hiyo iliondoka juzi kutoka Mwanza saa 12 : 40 jioni na kutia nanga jana saa 6: o5 mchana na kwamba ilipata hitalafu majira ya saa 6:20 usiku.

Amesema kuwa mpaka sasa chanzo cha meli hiyo kuchelewa kutia nanga bado hakijafahamika na kwamba walipata taarifa kutoka kwa Nahodha wa Meli hiyo, Bembele Ng’wita kwamba mfumo wa shafti na majembe ya kulia ya upande wa kulia yamepata hitilafu.

“Kwa mjibu wa taarifa ni kwamba saa 6:20 usiku mfumo huo ulipata hitilafu iliyopelekea injini kuwa nzito na kusababisha meli kutetemeka na joto la injini kupanda na kupelekea injini hiyo kuzimwa kwa usalama zaidi,” amesema Mwassa.

Hata hivyo amesema baada ya hali hiyo meli iliiendelea na safari yake kwa kutumia injini moja na kwamba imewasili salama katika Bandari ya Bukoba saa 6: 05, abiria wote na mali zao wapo salama.

Amesema baada ya kupata taarifa hizo, kampuni imemtuma mpiga mbizi (Diver) kwa usafiri wa ndege ili akakague mfumo huo na kuweza kubaini tatizo na chanzo cha kusababisha hitilafu hiyo na kwamba kwa mjibu wa Nahodha huenda meli ilinasa katika nyavu za wavuvi.

Mwassa aliwataka watanzania kutokuwa na wasiwasi na usafiri huo na kuwataka kuondoa zana potofu kwamba watumishi wa meli hiyo wanauhujumu usafiri meli zinazomilikiwa na Serikali kitendo ambacho alikikana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Justus Kamugisha, alipotafutwa kuzungumzia tukio hilo hakupatikana ofisini kwake na kwamba yupo nje ya ofisi.

Si mlisema Mbunge wenu sijasoma....


Rais Magufuli azungumza Ikulu na Rais mstaafu Kikwete

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais Mstaafu wa Awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu Jijini Dar es salaam.

Katika Mazungumzo hayo Rais Mstaafu Kikwete amemtakia Rais Magufuli heri ya Mwaka mpya na kumpongeza kwa uongozi mzuri.

Rais Kikwete pia amesema anaunga mkono juhudi mbalimbali zinazofanywa na Rais Magufuli ikiwemo ukusanyaji wa mapato ya serikali.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
06 Januari, 2016.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam.


Tamko la JUMAZA na Taasisi za Kiislam kuhusu hali ya kisiasa Zanzibar

Katibu Mtendaji wa JUMAZA, Sheikh Muhiddin Zubeir Muhiddin na Mwenyekiti wa Taasisi za Kiislamu Zanzibar, Sheikh Ali Abdallah Shamte

TAMKO LA JUMUIYA YA MAIMAMU ZANZIBAR (JUMAZA) KWA KUSHIRIKIANA NA TAASISI ZA KIISLAM ZANZIBAR KWA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU MGOGORO WA KISIASA ZANZIBAR TAREHE 6-1-2016 KATIKA UKUMBI WA UMOJA WA WALEMAVU


Awali tunamshukuru Mwenyezi Mungu aliyetuwezesha kukutana katika hafla hii hali ya kuwa ni wazima; sala na salamu zimfikie Mtume wetu Mtukufu Muhammad (S.A.W), jamaa zake, maswahaba zake na wote wanaowafuata kwa wema hadi Siku ya Malipo.

Ndugu waandishi wa habari, tunawashukuru sana kwa kuitikia wito wetu wa kuhudhuria katika mkutano huu muhimu wenye lengo la kutafuta maslahi na mustakbali mwema wa nchi yetu.

Sisi Viongozi wa Dini ya Kiislamu Zanzibar tunawashukuru sana Wazanzibari wote kwa kuendelea kudumisha amani na utulivu katika nchi yetu pamoja na kukabiliwa na mtafaruku mkubwa wa kisiasa ambao haujawahi kushuhudiwa katika historia ya Zanzibar uliotokana na hatua ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salim Jecha kuufuta Uchaguzi wote uliofanyika tarehe 25 Octoba, 2015 na matokeo yake katika tangazo lake la tarehe 28-10-2015.

Kitendo hicho cha kuufuta Uchaguzi huo, kimepelekea nchi yetu kuingia katika mgogoro mkubwa wa kikatiba na kisiasa. Wananchi wa kawaida ambao ndio wapiga kura wanaathirika kisaikolojia kwa kushindwa kujua khatima ya kura walizozipiga. Kwa upande mwengine kumekuwa na ongezeko la ugumu wa maisha visiwani Zanzibar unaotokana na mfumuko wa bei kwa bidhaa muhimu na mzunguuko wa pesa kuwa mdogo kutokana na baadhi ya Wafanya biashara kuwa na khofu ya kuendelea na shughuli za uzalishaji kwa khofu ya kutokea vurugu.

Ndugu waandishi wa habari, sisi tukiwa viongozi wa jamii tumeshughulishwa sana na mtafaruku huu wa kisiasa unaotukabili ambapo hadi sasa tumechukua hatua zifuatazo kusaidia kufikia ufumbuzi:-
Tuliwaandikia barua za nasaha viongozi wote wakuu wa kisiasa wanaoshiriki katika mazungumzo ya kutafuta ufumbuzi wa mkwamo huu wa kisiasa.
 1. Tuliwaandikia barua Mabalozi wa nchi sita waliopo Tanzania kuomba wasaidie katika kuutafutia ufumbuzi mgogoro huu katika kuhakikisha kuwa demokrasia inachukua mkondo wake. Mabalozi wahusika ni kutoka nchi za Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Norway na Sweeden.
 2. Tulimwandikia barua Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kumkumbusha dhima yake ya kuingilia kati mgogoro huu ili kupatikana ufumbuzi wa haraka.
 3. Kupitia khutuba za Ijumaa katika misikiti mbali tumekuwa tukiwanasihi wananchi wawe na subra ili watoe fursa kwa viongozi wa kisiasa kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huu kwa njia za amani.
Ndugu waandishi wa habari, Wananchi wa Zanzibar tulipata matumaini tulipoona kuwa viongozi wakuu wa kisiasa wanakutana kuzungumzia hali ya kisiasa nchini, tuliamini kuwa katika vikao hivyo Viongozi hawa wenye kuheshimika wakitawaliwa na busara, hekima, uadilifu na wakiweka mbele maslahi ya taifa badala ya vyama vyao basi muda si mrefu tungepata ufumbuzi wa mgogoro huu. Bahati mbaya tunaambiwa ni vikao 8 sasa vimeshafanyika tokea kikao cha mwanzo cha tarehe 9 Novemba, 2015 hakuonekani kuwa matumanini yale wananchi waliyoyajenga kwao kuwa yatatimia. Tunasema hivi kwa sababu kwanza vinaendeshwa kwa usiri mkubwa mno na hadi leo hakuna taarifa yoyote iliyotolewa kwa umma. Hali hii inawafanya wananchi kutoelewa kinachoendelea na hivyo kuishi maisha ya wasi wasi na kukosa utulivu hata wa kufanya shughuli zao za kimaisha. Kasoro nyengine ni kuwa vikao hivi vimechukua muda mrefu sana na hivyo kuibua maswali mengi na shaka kwa wananchi. Pia tabia iliyojitokeza ya baadhi ya wajumbe wanaoshiriki mazungumzo hayo kutoa kauli zinazoshabikia msimamo wa upande mmoja kunawatoa imani wananchi juu ya kuwepo kwa nia njema katika mazungumzo hayo na kwamba mazungumzo hayo yanaweza kuivusha nchi yetu katika mkwamo huu wa kisiasa unaohatarisha usalama wa nchi yetu.

Kutokana hali hii sisi Viongozi wa Dini ya Kiislam Zanzibar tunatamka kwamba:-
 1. JUMAZA na Taasisi za Kiislam Zanzibar zinawataka Viongozi wakuu wa kisiasa wanaoshiriki katika mazungumzo kuwajibika kwa kuweka mbele maslahi mapana ya nchi, kuhitimisha mazungumzo yao haraka iwezekanavyo na kutoa maamuzi rasmi ikiwa ni muongozo wa kutukwamua hapa tulipo kwa njia ya amani na salama. Tunawatanabahisha kuwa jamii yetu kwa sasa ni mfano wa bomu linaloweza kuripuka wakati wowote ule.
 2. Ukimya na uvumilivu wa Wazanzibari uliopo kamwe usichukuliwe kuwa wao ni Malaika bali ni binaadamu kama walivyo wengine ambao wanaweza kufikia hatua ya kushindwa na uvumilivu na kutoa maamuzi magumu yanayoweza kutufikisha pahala pabaya na kuigharimu sana nchi yetu. Hatuombi jambo hili kutokea lakini likitokea viongozi wakuu wa kisiasa watabeba dhima mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Hivyo basi, tunawaomba Viongozi wakuu wa kisiasa wanaoshiriki katika mazungumzo ya kutafuta ufumbuzi, ni wakati muwafaka sasa watoke hadharani na watoe taarifa kwa umma juu ya hatua iliyofikiwa na ikiwezekana lini mazungumzo hayo yatakamilika na Wazanzibari watarajie nini kutokana na mazungumzo hayo.
 3. Sisi Viongozi wa Dini ya Kiislam Zanzibar, tunapinga kwa nguvu zetu zote kauli za uchochezi zinazoendelea kutolewa na wanasisa ambazo zinazidi kujenga khofu, hamasa na chuki miongoni mwa wananchi. Aidha, tunasikitika kuona kuwa kauli hizo zinatolewa bila ya kujali mazungumzo yanayoendelea ya viongozi wakuu ya kutafuta ufumbuzi.
 4. Sisi Viongozi wa Dini ya Kiislam Zanzibar, kwa heshima kubwa tunamuomba sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dk. John Pombe Magufuli ambaye ameonesha dalili njema za uadilifu na uwajibikaji mkubwa achukue hatua za wazi na za haraka katika kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huu kabla nchi yetu haijatumbukia pahala pabaya. Aidha, tunamuomba kusimamia kwa udhati na ujasiri kuona haki inachukua mkondo wake na maamuzi ya Wazanzibari walio wengi yanaheshimiwa.
 5. Katika Uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba, 2015 JUMAZA ilikuwa na waangalizi katika majimbo yote ya Unguja na Pemba, kasoro zilizoripotiwa katika Uchaguzi huu ni kasoro ndogo ndogo mno na kwa hakika ni afadhali kuliko chaguzi zote zilizopita huko nyuma tokea kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vyangi. JUMAZA inashangazwa sana na hatua ya kufuta Uchaguzi huu iliyochukuliwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jecha Salim Jecha. JUMAZA inauliza kwanini wakati tulipokuwa na kasoro kubwa zaidi katika chaguzi za mwaka 1995, 2000, 2005 na 2010 Uchaguzi haukufutwa na kutakiwa kurejewa tena iwe Uchaguzi wa mwaka 2015 tu? Na jee kama uchaguzi utakaorejewa nao ukawa na kasoro zitakazolalamikiwa, utafutwa tena? Tutafanya chaguzi ngapi kwa mtindo huu?
 6. Taasisi za Kiislam Zanzibar zinawaomba Waislamu wote kuendeleza dua ili kuitakia mema nchi yetu na kumkabidhi Mwenyezi Mungu kwa wale wote wanaokusudia shari. Aidha, zinawaomba Maimamu na Makhatibu kukemea kauli zinazohatarisha amani na mshikamano wa jamii.
 7. JUMAZA na Taasisi za Kiislam Zanzibar zina khofu kubwa juu ya kurejewa kwa Uchaguzi, uzoefu unaonesha kuwa nchi zilizorejea uchaguzi katika Bara la Afrika kama vile Nigeria, Zimbwabwe, Malawi na kwengineko hatimaye zilitumbikia katika machafuko makubwa. Kama hilo halitoshi Zanzibar tuna historia mbaya ya kurejea Uchaguzi. Wengi tunakumbuka katika historia ya Zanzibar kile kinachoitwa ‘vita au machafuko ya Juni ‘. Uchaguzi wa Januari mwaka 1961 ulilazimika kurejewa mwezi wa Juni 1961, ambapo ulipelekea machafuko makubwa ikiwemo vifo vya watu 68, maelfu kujeruhiwa, nyumba kuvunjwa na kuchomwa moto. Kwa historia hii JUMAZA na Taasisi za Kiislam Zanzibar hazioni kuwa ni busara kurejewa kwa Uchaguzi uliofanyika kwa ufanisi na kukamilika. Penye nia njema na utashi wa kisiasa basi njia ya uadilifu iliyo wazi ya kutukwamua hapa tulipo ni kwa Viongozi wakuu wa kisiasa kufikia ufumbuzi na makubaliano haraka iwezekanavyo.
Mola wetu Mtukufu tunakuomba kwa rehma zako utuwezeshe kufikia ufumbuzi unaofaa juu ya tatizo linalotukabili na uziunganishe nyoyo za Wazanzibari kuwa pamoja, kupendana na kuweka mbele maslahi ya nchi yao. Amiin.

AHSANTENI

………………………………..

MUHIDDIN Z. MUHIDDIN
KATIBU MTENDAJI
JUMUIYA YA MAIMAMU ZANZIBAR

WM Majaliwa amuagiza Mganga Mkuu kuondoa duka lake na kuchukulia hatua Madaktari watoa mimba

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsalimia Josephine John ambaye amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma kwa matibabu. Alikuwa katika ziara ya mkoa huo Januari5, 2016.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaonya Madaktari vinara wa Hospitali ya Rufaa ya Songea ambao wanasifika kwa kufanya biashara ya kutoa mimba wanawake na wanafunzi kuacha tabia mara moja, la sivyo atawafukuza kazi na kuwafunga jela.

Waziri Mkuu alitoa onyo hilo jana wakati alipotembelea Hospitali hiyo na kuzungumza na watumishi kwa lengo la kuwasisitiza kutoa huduma bora kwa wagonjwa,ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 3 mkoani Ruvuma.

Alisema Hospitali ya mkoa huo inasifika kwa kutoa mimba wanawake na kuwalaza wagonjwa wao wodi namba 5, kitendo ambacho serikali haikuruhusu wala haikubaliani nacho.

"Naomba mkuu wa mkoa fanya ziara ya kushtukiza katika wodi namba 5 utakuta wanawake wametolewa mimba, wakiwemo wanafunzi na kisha madaktati hao wanatumia wodi zetu kuwalaza wagonjwa wao waliowatoa mimba.Ni marufuku na nitawachukulia hatua kwani majina ya madaktari hao ninayo," alisisitiza majaliwa.

Waziri Mkuu Majaliwa alimuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa huo, Dk. Daniel Malekela na Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo Dk. Phils Nyimbi kuwafuatilia madaktari wanaojihusisha na vitendo hivyo na kutoa taarifa ili wachukuliwe hatua kali.

Pia, alimuagiza mganga mkuu Dkt Daniel Malekela kuondoa duka lake lililo jirani na hospitali hiyo ili kuondoa hisia kwamba dawa zinaibiwa na kupelekwa kwenye maduka ya watumishi.


Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na Madaktari na Wauguzi wa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma baada ya kuitembelea akiwa katika ziara ya mkoa huo Januari 5, 2016.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo, Thabiti Mwabungu na kulia ni Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na bibi Antonia Moyo ambaye alikuwa akipata matibabu katika chumba maalum cha waze katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma wakati alipoitembelea hositali hiyo akiwa katika ziara ya mkoa huo Januari 5, 2016. Kulia ni Mkuu wa Mkoa huo Thabiti Mwabungu.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,akimsalimia mtoto Flora Mapunda (1) ambaye amelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Ruvuma ambayo Waziri Mkuu aliitembelea na kuzungumza na watumishi akiwa ktika ziara ya mkoa huo Januari 5, 2016.

Malumbano kuhusu misamaha ya kodi: TRA yatoa ufafanuzi wa TRA

TAARIFA KWA UMMA

Kumekuwa na upotoshwaji kuhusu zoezi la ufuatiliaji wa matumizi ya misamaha ya kodi inayosimamiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa wafanyabiashara, wawekezaji, Taasisi za Dini na Taasisi zisizo za kiserikali kwa maelezo kwamba TRA inazilenga baadhi ya Taasisi.

Sheria ya Mamlaka ya Mapato Tanzania inaipa Mamlaka ya kusimamia, kukagua na kuhakiki mapato ya Serikali pamoja na kuzuia ukwepaji wa kodi wa aina yoyote ile ikiwemo matumizi mabaya ya misamaha ya kodi inayotolewa kwa mujibu wa Sheria.

Kifungu cha 5 (3) cha Sheria ya TRA kinatoa mamlaka kwa TRA kufanya jambo lolote lenye tija na manufaa katika kufanikisha utekelezaji wa majukumu yake kisheria.

Kwa vile misamaha ya kodi inatolewa kwa mujibu wa Sheria zinazosimamiwa na TRA, ni wajibu wa Mamlaka kuhakiki kama bidhaa au huduma zilizosamehewa zinatumiwa na watu au Taasisi zinazostahiki misamaha hiyo au kwa miradi iliyokusudiwa.

Hivi karibuni kumekuwepo na taarifa za upotoshaji kwamba TRA imeilenga Taasisi moja ya kidini kwa kuiandikia barua ya kuomba vielelezo na ufafanuzi juu ya misamaha ya magari iliyopewa awali na kuonekana kana kwamba ni utaratibu mpya wa utoaji wa misamaha.

Tungependa kufafanua kwamba TRA haibagui wala kulenga Taasisi yoyote bali inatekeleza wajibu wake wa kufuatilia misamaha iliyotolewa

Katika kipindi cha Mwezi Oktoba hadi Desemba 2015 TRA iliwaandikia walipakodi 65 kupata vielelezo juu ya matumizi ya misamaha ya kodi walioipata na katika hao zimo Taasisi za kidini 39.

Ukaguzi huu huisadia TRA kupata taarifa muhimu ili kuishauri Serikali namna bora ya kutoa misamaha kwa ajili ya kuleta tija na ufanisi uliokusudiwa ikiwemo kurahisisha upatikanaji wa huduma muhimu za jamii na kupunguza umaskini. Aidha taarifa za misamaha ya kodi zinaisadia TRA kubaini matumizi bora ya misamaha pamoja na mianya ya upotevu wa mapato kupitia misamaha hiyo ili TRA ichukue hatua zinazostahili pale inapobainika kuwa kuna ukwepaji na kuziba mianya hiyo.

Zoezi hili ni endelevu hivyo tunaziomba Taasisi zote za kidini na mashirika yote yanayonufaika na misamaha ya kodi kuchukulia zoezi la ukaguzi wa misamaha hiyo kuwa ni utekelezaji wa sheria na wahusika wote ushirikiano kwa TRA pale wanapohitajika ili zoezi hilo lifanyike kwa ufasaha na kwa manufaa kwa wote.

“Pamoja Tunajenga Taifa Letu
A. J. Kidata
KAIMU KAMISHNA MKUU.

Sasa unaweza kuhakiki na kuboresha taarifa za umiliki wa ardhi kwa kutumia simu

Msemaji wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi Mboza Luandiko akionyesha kwa waandishi wa habari namba inayotumika katika kuhakiki taarifa za umiliki wa viwanja na mashamba kwa kutumia simu ya mkononi kushoto ni Kamishna Msaidizi Kanda ya Dar es salaam Bw. Mathew Nhonge.
Serikali imeanza kutumia mfumo wa simu za mkononi kuwawezesha wamiliki wa ardhi kuhakiki na kuboresha taarifa zao za ardhi kote nchini.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Msemaji wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi Mboza Luandiko wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliolenga kutambulisha huduma hiyo mpya kwa wananchi.
“Mfumo huu unamwezesha mmiliki wa ardhi kuhakiki na kuboresha taarifa zake za ardhi kwa kutumia simu yake ya mkononi kwa kuandika neno Ardhi kwenda namba 15774” 
alisisitiza Luandiko. Akifafanua, amesema kuwa wakati mwananchi anatuma ujumbe huo anatakiwa awea na nyaraka zake za umiliki wa ardhi au barua ya toleo kwa wale ambao bado hawajapata hati.

Akizungumzia faida za mfumo huo Luandiko amebaini sha kuwa utasaidia kulinda milki za wateja na kuondoa kabisa tatizo la matapeli.

Faida nyingine ni kuongeza uwazi katika kugawa ardhi na hivyo kupunguza migogoro ya ardhi ambapo hati milki zitatolewa kwa wingi zaidi kwa kuwa mfumo huo ni rafiki katika utoaji wa huduma.

Aidha mfumo huu utarahisisha Mawasiliano kati ya mmiliki wa ardhi na Wizara hali itakayoongeza tija katika upatikanaji wa huduma kwa kuwa zinaweza kupatikana kwa njia ya simu ya mkononi ikilinganishwa na hapo awali ambapo mwananchi alitakiwa kufika katika Ofisi za Wizara ili kupata huduma husika.

Huduma ya mfumo wa uhakiki wa taarifa za umiliki wa viwanja na mashamba imeanza katika mkoa wa Dar es salaam na baada ya hapo tathmini itafanyika kabla ya kuanza kutumika katika Mikoa yote.
 • Taarifa ya Frank Mvungi

WM Majaliwa awasimamisha kazi viongozi wa Chama Kikuu Cha Ushirika Ruvuma

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha kusindika tumbaku cha mkoani Ruvuma na kuwasimamisha kazi viongozi wa Chama Kikuu Cha Ushirika cha SONAMCU.

Akizungumza jana jioni (Jumanne, Januari 5, 2016), katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu Ndogo ya Songea, wakati alipokutana na wakulima wa zao la tumbaku wa Wilaya ya Namtumbo, Wananchama wa Vyama Vya Ushirika vya Mkoa wa Ruvuma, viongozi wa Mkoa pamoja na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Edwin Ngonyani ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini, Waziri Mkuu amesema, Serikali ina dhamira ya kufufua kiwanda cha kusindika tumbaku cha SONAMCU, na lengo la kutembelea kiwanda hicho ni katika utekelezaji wa agizo la Rais John Pombe Magufuli la kufufua viwanda nchini.

Waziri Mkuu Majaliwa, ametembelea maeneno mbalimbali ya kiwanda hicho na kukagua mitambo iliyokua ikitumika kusindika tumbaku, kabla kiwanda hicho kuzimwa miaka kadhaa iliyopita baada ya kukosa malighafi za kuendelea na uzalishaji.

Pia, amemtaka Afisa Biashara kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Bibi. Stela Lugongo kuandaa na kuwasilisha kwake mkakati wa kufufua kiwanda hicho cha kusindika tumbaku, na baadae kuwasimamisha kazi viongozi wote wa Chama Kikuu cha Ushirika cha SONAMCU waliohusika na tuhuma hizo na kutaka wafikishwe Mahakamani.

“Serikali imeazimia kufufua viwanda, hasa vile ambavyo havina wawekezaji vimebaki vyenyewe, Tunahitaji kujua namna ya kuvifufua”. Alisema Waziri Mkuu huku akishangiliwa.

Waziri Mkuu Majaliwa pia, amesikiliza na kujibu kero mbalimbali za wakulima wa tumbaku wa Mkoa huo, ambao walilalamikia mfumo wa Vyama vya Ushirika na namna ambavyo vyama hivi vimekua vikiwaibia fedha zao hadi kushindwa kuendelea kulima zao la tumbaku na kukosa masoko ya mazao yao.

Aidha, Waziri Mkuu amewasihi wakulima kuwa watulivu na kusubiri maamuzi ya Mahakama baada ya kuwa viongozi wa Chama cha Ushirika SONAMCU ambao wamehusika na wizi wa fedha za wakulima kiashi cha Shilingi milioni 800 kwa kipindi cha mwaka 2011 hadi 2014 tayari wamefikishwa Mahakamani na uchunguzi unaendelea. Pia, amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu kukutana na wakulima hao ili kupatia ufumbuzi matatizo yao.

Aidha, ametoa wito kwa wakulima kuendelea kulima zao la tumbaku kwa kuwa linaongeza pato la mtu mmoja mmoja, linasaidia kuchangia pato la Mkoa na kukua kwa uchumi wa nchi. Amewashauri wakulima kuunda na kuviendesha Vyama Vya Ushirika kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizopo.

Waziri Mkuu amemaliza ziara yake mkoani Ruvuma, atafanya majumuisho ya ziara hiyo leo, kabla ya kuagana na viongozi wa Chama na Serikali na kurejea jijini Dar es Salaam.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P 3021,
11410 DAR ES SALAAM
JUMMATANO, JANUARI 6, 2016.

Waziri Nchemba avunja bodi ya vyama vya wakulima wa tumbaku IringaWAZIRI wa Kilimo, Mifugo na Uvivu, Mwigulu Nchemba amewanusuru wanachama wa vyama vya ushirika wa kilimo cha tumbaku wilayani Iringa kutapeliwa na baadhi ya viongozi wao, matrekta tisa yaliyokopeshwa kwa vyama hivyo kupitia mkopo uliotolewa na benki ya CRDB, miaka minne iliyopita.

Ameamuru viongozi hao tisa kutoka chama cha ushirika Mfyome, Magubike, Kiwemu, Kitai, Mhanga na Kampuni ya umoja wa Wakulima wa Tumbaku Iringa (ITCOJE Ltd) wakabadhi ofisi zao mara bada ya kuondoka Iringa jana.

Pamoja na kuwataka viongozi hao waachie ngazi na taratibu za kujaza nafasi zao zifanywe haraka iwezekanavyo, Waziri Nchemba amemuagiza Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini, Dk Audax Lutabazibwa kuifuta bodi ya ITCOJE na kuhakikisha taratibu za kuunda bodi mpya zinafanywa haraka iwezekanavyo.

Mbali na kumiliki gari la kisasa aina ya Toyota Land Cruiser VX bodi hiyo pia inamiliki roli aina ya Scania linalofanya kazi ya kusambaza kuni na pembejeo kwa wanachama wa vyama hivyo

Nchemba alikuwepo mjini Iringa juzi kwa mwaliko wa wakulima wa Tumbaku wa wilaya ya Iringa ambao pamoja na mambo mengi yanayohusu changamoto za kilimo na biashara ya tumbaku nchini, walimueleza jinsi baadhi ya viongozi wao wanavyotumia madaraka yao kujineemesha kinyemela kupitia mgongo wa vyama hivyo.Kati ya watuhumiwa hao tisa yupo Mwenyekiti wa ITCOJE, Msafiri Pamagila na Afisa Ushirika wa Wilaya ya Iringa, Emanuel Samile ambaye waziri huyo ametaka achunguzwe kama alizingatia taratibu za kazi na sheria zinazounda vyama hivyo wakati naye akinufaika na moja ya matrekta hayo.

Kabla ya kutoa maamuzi hayo, Nchemba alitumia takribani saa 4 kuwasikiliza walalamikaji (wanachama wa vyama hivyo) na walalamikiwa (viongozi watuhumiwa) na kujiridhisha kwamba viongozi hao walitumia madaraka yao kufanya udanganyifu uliolenga kuwahalalishia umiliki wa matrekata hayo ambayo mkopo wake ulilipwa na wanachama wa vyama hivyo.

Akitumbua majipu, Nchemba aliyembatana na Lutabazibwa na Mkurugenzi wa Bodi ya Tumbaku Tanzania, Wilfred Mushi katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa siasa ni kilimo baina yake na wakulima wao alisema:

“Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa na vyombo vyenu nitamke hapa hapa kwamba matrekta hayo ni mali ya vyama vya msingi, kwa kuwa yalikopeshwa kupitia vyama hivyo na yamelipwa na wanachama wenyewe kupitia vyama vyao vyao vya msingi kama ambavyo ushahidi kutoka CRDB unaonesha.

Mkurugenzi wa CRDB Iringa, Kisa Samwel alikiri katika kikao hicho kuvikopesha vyama hivyo mkopo uliotumika kununua matrekta hayo kwa kupitia mwavuli wao wa ITCOJE na wala mikopo hiyo haikuwa kwa ajili ya viongozi wanaotajwa.

“Nikuhakikishie mheshimiwa waziri, benki yetu ilikopesha vyama na mikataba inaonesha hivyo; haya madai ya mikopo hiyo kugeukwa ya viongozi fulani hatuyafahamu na hayatuhusu. Kwetu sisi wakopaji ambao ni vyama ndio waliolipa mikopo hiyo na mpaka sasa nyaraka zinaonesha hivyo,” alisema.

Alisema mikopo ya matrekata hayo ilikwishalipwa na vyama hivyo lakini yameendelea kutumika kama dhamana katika benki hiyo baada ya vyama hivyo kuyatumia kukopa fedha kwa ajili ya msimu wa kilimo wa 2015/2016 unaonendelea.

Awali mmoja wa wanachama wa vyama hivyo, Ombeni Mvella alimwambia waziri kwamba inashangaza matrekata hayo ambayo mkopo wake ulilipwa na vyama hivyo, kumilikishwa kwa watu wachache kiunjaunja.

“Mheshimiwa waziri tunanyanyaswa na viongozi wa ITCOJE, tulidhani ni watetezi wa wakulima, sasa wameguka kuwa wanyanyasaji wa vyama vya msingi,’. Matrekata yalikopeshwa na vyama lakini yemeguka kuwa mali ya viongozi wachache,” alisema.

Katika utetezi wao, watuhumiwa hao walisema waliteuliwa na wanachama wa vyama hivyo kuwa wasimamizi wa matrekta hayo kwa makubaliano kwamba watayamiliki moja kwa moja baada ya mikopo yake kwisha; jambo lililomshangaza waziri na viongozi wengine waliokuwepo.

“Yaani kwa kuwa msimamizi tu basi mali husika inageuka kuwa yako. Kwahiyo na mimi nikisimamia wizara hii itakuwa sahihi kweli baada ya miaka mitano nipewe rachi moja au kingine chochote ambacho ni mali ya umma?” aliuliza kwa mshangao.

Akijitetea, Mwenyekiti wa ITCOJE alisema; “katika makubaliano yaliyotuwezesha kunufaika na matrekata haya hata sisi tulikuwa tukilipa fedha zetu. Mimi binafsi nililipa Sh Milioni 7 ili kupata trekta hilo ambalo pia nimekuwa nikilitumia kwa gharama zangu kulima mashamba ya wanachama wa vyama vya msingi.”

Naye Afisa Ushirika wa wilaya ya Iringa, Samile alijitetea akisema alipata trekta analomiki kwa kuwa yeye ni mmoja wa wanachama wa vyama hivyo vya ushirika mwenye mashamba makubwa.

“Nikiri kwamba trekta langu nimelipata kwa kupitia mkataba wa kulisimamia kama ilivyo kwa wengine. Sijatoa hata senti tano katika mkopo wake na niseme wazi kwamba matrekta hayo yalikopeshwa kwa vyama vya msingi, sisi sio wakopaji wala walipaji; sisi tumepewa baada ya kuyasimamia,” alisema huku akitetemeka.

Akionesha kukasirika kwa kupotezewa muda na viongozi hao, Nchemba alisema nimekuja Iringa kwa umuhimu wa jambo hili huku nikijua kwamba kesho natakiwa kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri Dar es Salaam.

Alisema atafanya kosa kubwa kama atahalalisha utapeli uliofanywa na viongozi hao wachache ambao ushahidi wa benki na wanachama unaonesha hawajatoa hata senti tano toka mifukoni mwao kulipa madeni yake na hivyo akaagiza hatua hizo zichukuliwa haraka iwezekanavyo.

Alisema inashangaza kuona baadhi yao wanatoa utetezi eti walitoa fedha zao za mifukoni kulipia sehemu ya mikopo ya matrekta hayo wakati maelezo na ushahidi wa kibenki unaonesha wanachama kwa kupitia vyama vyao ndio waliolipwa, tena kwa vyama hivyo kukatwa moja kwa moja fedha hizo kwenye akaunti zao.

“RC, DC na viongozi wote nataka navyoondoka tu Iringa, wale viongozi wote waliofanya utapeli huo wakabidhi ofisi kwa wanachama wao; nataka bodi ya ITCOJE ifutiliwe mbali na taratibu za kupata viongozi wa kuziba nafasi hizo ufanywe haraka kwa usimamizi wenu na hakikisheni zinaundwa timu za kusimamia matrekta hayo” alisema.

Vazi la Taifa: Mapendekezo ya michoro itakayotumikaVitambaa vya Kanga vilivyopendekezwa kwa ajili ya kutumika kama Vazi la Taifa.


Vitambaa aina ya Vitenge vilivyopendekezwa kwa ajili yaVazi la Taifa

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

CAG aanza kukagua na kubana waajiri ili waliokopa HESLB walipe

OFISI ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) imeanza kukagua taasisi za umma kuhusu utekelezaji wa matakwa ya sheria inayowataka kuwatambua waajiriwa walionufaika na mikopo ya elimu ya juu na kuwasilisha makato kwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. George Nyatega, sheria iliyoanzisha HESLB inazitaka taasisi zote za umma kuijulisha Bodi kwa maandishi kuhusu waajiriwa wapya katika taasisi hizo ndani ya siku 28 na Bodi kuthibitisha kama waajiriwa hao ni wanufaika wa mikopo au hapana.

“Baada ya kuajiriwa mtu huyo ambaye amepata elimu yake ya chuo kikuu au taasisi yoyote ya elimu ya juu nadni au nje ya nchi kuanzia mwaka 1994 hadi sasa, mwajiri anapaswa kuitaarifu Bodi kwa maandishi ndani ya kipindi cha siku 28 tangu ajira hiyo,” inasomeka sehemu ya taarifa ya hiyo iliyochapishwa na vyombo mbalimbali vya habari jana ikiwemo tovuti ya HESLB.

Taarifa hiyo, ambayo pia inapatikana katika tovuti ya HESLB, inaongeza kuwa baada ya Bodi kupokea taarifa kutoka kwa waajiri hao na kuthibitisha kuwa waajiriwa ni wanufaika wa mikopo, mwajiri atapaswa kuijulisha Bodi na kuanza kukata sehemu ya mshahara wa mwajiriwa ndani ya siku 30 na kuwasilisha makato hayo kwa Bodi ndani ya siku 15 kabla ya kila mwisho wa mwezi.

Kwa msingi huo, HESLB kupitia tangazo hilo, HESLB imewajulisha waajiri kuwa CAG amejumuisha matakwa hayo ya kisheria katika kazi zake za ukaguzi katika taasisi za umma kwa lengo la kuongeza kasi ya ukusanyaji mikopo iliyoiva.

“Ni imani ya HESLB kuwa waajiri katika utumishi wa umma watatoa ushirikiano kwa ofisi ya CAG ili kuondokana na matatizo ya kisheria,” amesema Bw. Nyatega katika taarifa yake.

HESLB ilianzishwa mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai 2005 ili, pamoja na mambo mengine, kutoa mikopo ya elimu ya juu kwa Tanzania wahitaji na kukusanya mikopo iliyoiva kutoka kwa wanufaika wa mikopo hiyo tangu mwaka 1994.

WM Majaliwa: Serikali hijaridhia pendekezo la UDART la nauli za mabasi ya DART

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali haijaridhia viwango vipya vya nauli ya mabasi yaendayo kasi vilivyopendekezwa na waendeshaji wa huduma ya mabasi yaendayo kasi Dar es Salaam (UDART).

Akizungumza leo na waandishi wa habari, mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akitokea mkoani Ruvuma kwa ziara ya siku 3, Waziri Mkuu amesema Serikali haijaridhia mapendekezo ya nauli ya kutoka Mbezi hadi Kimara shilingi 700, Mbezi hadi Kariakoo shilingi 1200, na nauli ya kutoka Mbezi hadi Mwenge shilingi 1400 na wanafunzi watatozwa nusu ya viwango hivyo vya nauli.

Waziri Mkuu amesema gharama hizi ni kubwa mno kwa wananchi, “Serikali iliwekeza katika mradi huu ili kusaidia watumishi na wananchi ambao hawana vipato vikubwa” alisema Majaliwa.

Aidha, ameagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na wadau wakutane kupanga upya viwango hivyo na kama watashindwa basi Serikali itaendesha mradi huo.

Tarehe 25, Novemba 2015, Waziri Mkuu alimuagiza aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya TAMISEMI na waendeshaji wa mradi wa mabasi yaendayo kasi Dar es salaam (UDART) kupitia misuada yote na kurekebisha miundombinu ili mradi huo wa mabasi uanze kufanya kazi ifikapo tarehe 10, Januari 2016, imebainika kwamba UDART hawakuandaa mpango wa biashara wala kuanisha gharama za uendeshaji.*******************

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA WAZIRI MKUU

TAARIFA KWA UMMA


KAULI YA SERIKALI KUHUSU MAPENDEKEZO YA NAULI ZA MABASI YAENDAYO HARAKA (DART)


Tarehe 25 Novemba 2015 niliwaagiza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Wakala wa Barabara na Uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wapitie masuala yote ya kisheria yanayohusu Mradi na kuhakikisha kuwa miundombinu inakamilika ili Mradi uanze kutoa huduma tarehe 10 Januari 2016.

Baada ya kupitia mikataba na nyaraka mbalimbali imebainika kwamba:

a) Hakuna Mpango wa Biashara ulioandaliwa na Mwekezaji yaani Kampuni ya UDART iliyopewa jukumu la kutoa huduma za mpito (ISP);

b) Gharama za uwekezaji (ununuzi wa magari, vifaa vya kutozea nauli na gharama nyingine) haziko bayana.

Pamoja na kuwepo kwa kasoro hizi kubwa tarehe 05 Januari 2016 Mwekezaji aliwasilisha kwa Mamlaka ya Kudhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) ombi la nauli za Mabasi Yaendayo Haraka kama ifuatavyo:

i). Mbezi-Kimara 700/= (Mwanafunzi nusu ya nauli)

ii). Mbezi-Kivukoni 1,200/= (Mwanafunzi nusu ya nauli)

iii). Mbezi-Kimara-Ubungo-Mwenge 1,400/= (Mwanafunzi nusu ya nauli).

Kigezo kikubwa cha kupanga nauli pamoja na mambo mengine ni gharama za uwekezaji (capital costs) na gharama za uendeshaji (operational costs). Hivyo kwa kukosekana gharama halisi za Uwekezaji ni dhahiri kuwa viwango hivyo vya nauli vinavyopendekezwa havina uhalisi.

Tafsiri ya viwango hivi vya nauli kwa mtumishi mwenye kima cha chini cha mshahara cha 260,000/= kwa mwezi na amabaye ana mke na watoto wawili wanaosoma atatumia zaidi ya robo tatu (75%) ya mshahara wake kwa kulipa nauli.

Serikali haikubaliani na mapendekezo hayo ya nauli kwa sababu gharama za uwekezaji za Mwekezaji huyo hazifahamiki na hakuna Mpango wa Biashara unaoeleza mtiririko wa biashara ya Mabasi Yaendayo Haraka.

Kwa kuwa viwango hivyo vya nauli vilivyopendekezwa havikutokana na misingi halisi ya gharama za uwekezaji na uendeshaji na kwa vile watumiaji wa huduma za mabasi hayo wameonesha kutomudu viwango hivyo vya nauli, Serikali hairidhishwi na viwango hivyo kwa kuwa havina uhalisia.

Imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu

Wizara yakanusha habari ya TANESCO iliyochapishwa na The Citizen

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 

WIZARA YA NISHATI NA MADINI 

TAARIFA KWA UMMA 

Tunakanusha taarifa iliyochapishwa na gazeti la The Citizen la Januari 5, 2016 katika ukurasa wake wa 12 yenye kichwa cha habari: ‘Umma kununua asilimia 49 ya hisa za Tanesco’. Mwandishi na Mhariri wamejiandikia taarifa hiyo kwa sababu wanazozijua wao. 

Sehemu ya taarifa inasema: Serikali ya Tanzania ina mpango wa kuuza hisa ya Shirika la Umeme Tanzania kwa umma... 

Pia, sehemu nyingine inasema: Waziri wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo aliliambia gazeti la East African kuwa Serikali itatoa asilimia 49 ya hisa za Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wakati huo Serikali ikibaki na hisa zingine... 

Tungependa wananchi kwa ujumla waelewe kwamba taarifa hiyo si sahihi na inapotosha umma. Taarifa sahihi kama ifuatavyo: 
 • Kwanza, Waziri Sospeter Muhongo hajafanya mahojiano yoyote na mwandishi wa gazeti hilo la The East African wala gazeti la The Citizen. 
 • Pili, Serikali haina mpango wa kuuza hisa za TANESCO kwa umma. 
Mkakati uliopo wa Mageuzi ya kuboresha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ujulikanao kama Electricity Supply Industry Reform Strategy and Roadmap (ESI-RSR) 2014 – 2025 ni kama ifuatavyo: 

MAELEZO YA MKAKATI NA MWELEKEO WA KUREKEBISHA SEKTA NDOGO YA UMEME (ESI-RSR) 

Mwezi Juni 2014, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilipitisha na kuchapisha mkakati wa mageuzi wa Electricity Supply Industry Reform Strategy and Roadmap (ESI-RSR) 2014 – 2025. Lengo la msingi wa mkakati huo ni kuboresha mazingira ya uwekezaji wa sekta binafsi katika nyanja za uzalishaji na usambazaji, na kuongeza uunganishaji wa umeme katika ngazi zote. 

Utekelezaji wa mpango huo ambao unatarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka kumi na moja (11) umegawanyika katika vipindi vikuu vitatu ambavyo ni muda mfupi, wa kati na muda mrefu. 
 • Mkakati wa muda mfupi ni kutenganisha shughuli za Uzalishaji ili zifanywe na Kampuni Tanzu ya TANESCO. Umiliki wa uzalishaji, usafirishaji na usambazaji chini ya awamu hii itaendelea kuwa chini ya Serikali, kama mbia moja. 
 • Mkakati wa muda wa kati unahusu kutenganisha sehemu ya usambazaji kutoka kwenye usafirishaji. Katika Awamu hii, Kampuni za uzalishaji, usafirishaji na usambazaji zitaendelea kuwa chini ya umiliki wa Serikali. 
 • Mkakati wa muda mrefu utahusisha Ofisi za Kanda kujihusisha na usambazaji wa huduma za umeme ambazo pia zitagawanywa kulingana na uwezo wa kujiendesha. Katika kipindi hicho cha muda mrefu, kampuni binafsi za usambazaji umeme zitaendelea kushiriki katika shughuli za uzalishaji na usambazaji umeme kwa ajili ya kuchochea ushindani na ufanisi kwenye soko. 
Tunawahimiza wadau wote kusoma mkakati wa mageuzi ujulikanao kama Electricity Supply Industry Reform Strategy and Roadmap (ESI-RSR) 2014 – 2025 ambao unapatikana mitandaoni Aidha, tunawakumbusha Waandishi wa Habari na Wahariri ambao hawazingatii maadili ya taaluma yao kuandika taarifa sahihi ili kuepusha upotoshaji kwa umma. 

Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano Serikalini 6 Juni, 2015

TRA yavuka lengo la makusanyo kwa mwezi

Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka Tanzania (TRA) (Katikati) Alphayo Kidata akizungumza na waandishi wa Habari wakati akitoa taarifa za ukusanyaji wa mapato wa kila mwezi. 
Jumla ya shilingi trilioni 1.4 imekusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika kipindi cha mwezi Desemba mwaka uliopita wa 2015.

Kiasi hicho ni sawa na ongezeko la wastani wa shilingi bilioni 490 kwa mwezi ukulinganisha na wastani wa makusanyo ya kuanzia Julai hadi Novemba ambapo, TRA ilikuwa imekusanya wastani wa shilingi bilioni 900 kwa mwezi.

Takwimu hizo zimetolewa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Kamishna Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliolenga kutoa taarifa kwa umma juu ya ukusanyaji wa kodi nchini.

Ameongeza kuwa katika kipindi cha kuanzia Julai mwaka jana hadi kufikia Desemba mwaka huo TRA ilikuwa imekusanya wastani wa shilingi trilioni 6.4 ambayo ilikuwa ni sawa na asilimia 95.5 ya lengo la kukusanya trilioni 6.5 katika kipindi hicho.

Kaimu Kamishna huyo ametaja sababu za kuongeza kwa makusanyo ya kodi kuwa ni pamoja na kuziba mianya ya upotevu wa mapato na kuweka mifumo mizuri ya ufuatiliaji ili kumrahisishia mlipa kodi kulipa kodi anayostahili bila usumbufu.

Kidata amesema kuwa katika kutekeleza azma ya Serikali ya Awamu ya tano ya kuongeza mapato Mamlaka hiyo itasimamia kwa ukaribu ukusanyaji wa mapato na kuwabana wote wenye nia ya kukwepa na hatimaye kuwafikisha katika vyombo vya sheria watakaobainika wamekwepa kodi.

Katika hatua nyingine Kaimu Kamishina Mkuu wa TRA huyo amesema jumla ya shillingi billioni 11.8 zimekusanywa kutoka kwa wafanyabiashara walioondosha makasha katika Bandari Kavu kinyume na taratibu za forodha.

Amesema kuwa makusanyo hayo yanajumuisha shilingi bilioni 5.3 kuoka kwa Kampuni na wafanyabiashara 19 ambao wamemaliza kulipa kodi za makasha yao na wengine 19 ambao wamelipa sehemu ya kodi ya makasha yao.

Taarifa ya
Raymond Mushumbusi - MAELEZO
Dar es Salaam
6.1.2016

***************

PIKIPIKI ZA USAFIRI ZAONGEZEWA MUDA WA KUJISAJILI

Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) imesema imeongeza muda kwa usajili wa vyombo vya usafiri vya pikipiki za magurudumu mawili na matatu mpaka Februari Mosi mwaka 2016.

Hayo yamesemwa leo na Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Alphayo Kidata alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari katika kikao chake cha kutoa taarifa kwa umma juu ya ukusanyaji wa kodi, Kaimu Kamishna Mkuu amesema wameamua kuongeza muda wa zoezi la usajili wa pikipiki ili kuiwapa nafasi wale ambao bado hawajasajili. “ Natoa wito kwa wamiliki wa vyombo vya pikipiki kusajili vyombo vyao mapema ili wasipatwe na adha itakayojitokeza baada ya muda uliotolewa kumalizika ” Alisema Kaimu Kamishna Kidata.

Ameongeza kuwa zoezi hilo lilikumbwa na changamoto kadhaa zilizowalazimu kuongeza muda mara mbili, ambazo ni umbali wa vituo vya usajili na makazi ya wamiliki wa pikipiki hasa mikoani,pamoja na upotevu wa nyaraka za kununulia pikipiki.

Aidha Kaimu Kamishna Alphayo Kidata ameomba wananchi kufungua ukurasa mpya wa ushirikiano na Mamlaka ili kutimiza azimio la Serikali ya Awamu ya Tano ya kulijenga taifa kwa kufanya kazi na hasa kulipa kodi stahiki zinazoleta mapato yanayowezesha maendeleo katika taifa letu.

Zoezi la usajili wa pikipiki lilianzishwa kwa lengo la kurahisisha ukusanyaji wa mapato kutoka katika vyombo hivyo, zoezi hili lilipangwa kukamilika tangu Desemba 31 2015 lakini ikaonekana wengi hawakusajili pikipiki zao hivyo basi Mamlaka imetoa mwezi mmoja mpaka Februari Mosi 2016 kwa wenye pikipiki kusajili.

Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) imesema itaendelea kupambana na wale wote watakaogundulika kwa wizi wa kazi za sanaa.

Agizo hilo limetolewa na Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Alphayo Kidata alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari na kueleza kuwa wapo katika operesheni ya kukamata wezi wa kazi za sanaa.

"Ipo kamati ambayo inajumuisha wadau kama Bodi ya Filamu, Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na COSOTA ikishirikiana na Jeshi la Polisi katika kupambana na wizi wa kazi za wasanii unaokidhiri siku hadi siku' alisema Kaimu Kamishna Kidata.

Serikali ipo makini kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania katika kukusanya mapato hasa kuongeza maeneo ya kukusanya mapato ikiwemo eneo la kazi za sanaa hivyo Serikali haitakubali kuona inakosa mapato hayo na yoyote anayejua mtu au kikundi cha watu kinachofanya wizi wa kazi za sanaa atoe taarifa ofisi za TRA.

***************

Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka Tanzania (TRA) (Katikati) Alphayo Kidata akisisitiza jambo wakati alipofanya mazungumzo na waandishi wa habari kuhusu taarifa za ukusanyaji wa mapato wa kila mwezi Kushoto ni Kaimu Kamishna wa Forodha Jocktan Kyamuhanga na kulia ni Kaimu Kamishna wa Kodi za Ndani Yusufu Salum.

Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) imesema itaendelea kupambana na wale wote watakaogundulika kwa wizi wa kazi za sanaa.

Agizo hilo limetolewa na Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Alphayo Kidata alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari na kueleza kuwa wapo katika operesheni ya kukamata wezi wa kazi za sanaa .

"Ipo kamati ambayo inajumuisha wadau kama Bodi ya Filamu, Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na COSOTA ikishirikiana na Jeshi la Polisi katika kupambana na wizi wa kazi za wasanii unaokidhiri siku hadi siku' `Alisema Kaimu Kamishna Kidata.

Serikali ipo makini kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania katika kukusanya mapato hasa kuongeza maeneo ya kukusanya mapato ikiwemo eneo la kazi za sanaa hivyo Serikali haitakubali kuona inakosa mapato hayo na yoyote anayejua mtu au kikundi cha watu kinachofanya wizi wa kazi za sanaa atoe taarifa ofisi za TRA.

Job: Chief of Party - Youth Entrepreneurship Program, Tanzania

Organization: Catholic Relief Services
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 05 Feb 2016

Job: Program Manager II - Employment Skills Specialist

Organization: Catholic Relief Services
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 05 Feb 2016

Job: Program Manager II - Entrepreneurial Skills Development Specialist

Organization: Catholic Relief Services
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 05 Feb 2016

Job: Program Manager II - Youth Life Skills Specialist

Organization: Catholic Relief Services
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 05 Feb 2016

Job: Program Manager II - Monitoring, Evaluation, Learning and Accountability (MEAL)

Organization: Catholic Relief Services
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 05 Feb 2016

Job opportunity at the BBC: Multimedia Broadcast Journalist, Dira TV

Job Introduction

BBC Africa is a multimedia operation with an extremely varied output focusing on African and Global audiences. This position focuses on African TV Broadcasts in Kiswahili, it is a daily news and current affairs programme for our Kiswahili speaking audiences in East Africa.

Role Responsibility

This role requires a strong understanding of the constraints of generating original TV material from Africa and preferably proven experience in delivering powerful stories for TV. You will be expected to research, present, write, edit and adapt stories or programme material. Finding contributors, interviewees and other sources of material will be a large part of your role. You’ll be writing and creating original material for all Multimedia output. You’ll also be performing live on audio or video with or without a script. You will be responsible for thinking through and around editorial problems. The position will expect you to conduct interviews either in the studio or on location. You’ll be liaising closely with other team members, along with reporters and stringers.

The Ideal Candidate

You’ll have complete comprehension of written and spoken English, coupled with the ability to communicate effectively. You will need a full command and up to date knowledge of Kiswahili (first or equivalent language).
This role requires you to have an excellent broadcasting voice, with strong presentation skills and be able to perform at the microphone with flair. Preferably you will bring a track record of producing stories and programmes for TV. You’ll have substantial, recent and relevant full-time experience as a journalist. You’ll be able to write scripts for a variety of audiences and forms of media. This position requires you to have a wide current knowledge of Eastern Africa. You will be experienced with reporting, in the field, on African political, economic, sport and social issues. You’ll be able to demonstrate a good range of contacts for interview purposes

The salary will be up to £40,000pa (including all allowances).

The application deadline is midnight on Tuesday 12th January 2016

To apply please click the button below or visit https://careershub.bbc.co.uk and search for reference number - BBC/TP/471010/13481.

Package Description

Job Title: Multimedia Broadcast Journalist, Dira TV
Location: London
Contract: 2 x permanent vacancies
Hours: 5 x 8 hour days 
Grade: 7D
Salary: maximum of £40,000pa (including all allowances).
Application deadline:  midnight on Tuesday 12th January 2016

Open to Job Share

About the Company

We don’t focus simply on what we do – we also care how we do it. Our values and the way we behave are very important to us. Please make sure you’ve read about our values and behaviours in the document attached below. You’ll be asked questions relating to them as part of your application for this role.