Askofu Mtanzania afukuzwa kazi akiwa Marekani


Zaidi ya wachungaji hamsini wa kanisa la Anglikana Tanzania dayosisi ya Victoria Nyanza (DVN) wametangaza kumfukuza kazi ya uaskofu, askofu Boniface Kwangu wa dayosisi hiyo kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na ubadhirifu wa fedha pamoja na mali za kanisa hilo.

Tamko hilo la Wachungaji 53 wa dayosisi hiyo limesomwa mbele ya waumini wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Nicholas wakati wa ibada ya Jumapili na Mchungaji Andrew Kashilimu, ambaye pia ni mwenyekiti wa nyumba ya wahudumu.

Kufukuzwa kazi ya uaskofu kwa askofu Kwangu aliyehudumu katika dayosisi hiyo kwa miaka minane, kuanzia mwaka 2008 hadi kufikia leo, kunafanya jumla ya maaskofu waliowahi kufukuzwa na kanisa hilo kuwa wawili, akiwemo mtangulizi wake marehemu John Changaye ambaye alifukuzwa uaskofu mwaka 2007 kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha na mali za kanisa.

Askofu Kwangu amevuliwa wadhifa huo akiwa nchini Marekani ambako amekaa kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Kanisa la Anglikana Tanzania dayosisi ya Victoria Nyanza (DVN) lina jumla ya wachungaji sitini na zaidi ya waumini laki sita katika makanisa yake.

Hello - Diamond Platnumz new 2016 audio


Historia fupi za Salim Ahmed Salim na marehemu Mzee Badawi na mapinduzi SMZ

Salim Ahmed Salim na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, 1964
Mara baada ya kuundwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hapo mwaka 1964, Mambo ya Nje ni moja ya mambo yaliyokubalianwa kuwa yawe ya Muungano, hivyo nafasi kama za Ubalozi katika Nchi mbalimbali Washirika na Taasisi za Kimataifa ilibidi zigawanywe kati ya Watanganyika na Wazanzibari ili dhana ya Utanzania ipate kuonekana dhahiri.

Ni katika wakati husika ndipo Rais Julius Nyerere, Kama Mkuu wa Nchi na mtu mwenye Mamlaka ya Uteuzi wa Mabalaozi alipoomba majina ya wale ambao walionekana kuwa na sifa za kuteuliwa kuwa Mabalozi kutoka Zanzibar kwa Rais Abeid Amani Karume.

Miongoni mwa majina yaliyoletwa na Sheikh Karume kwa Mwalimu Nyerere ni jina la Kijana mdogo wa miaka 22 Salim Ahmed Salim, jambo ambalo lilimfanya Mwalimu Nyerere amuulize maa ya pili Rais Karume juu ya umri wa Kijana huyo, majibu aliyopewa ni kuwa huyo ni Kijana wa Zanzibar mwenye vigezo na uwezo, apewe nafasi.

Bila hiyana, Mwalimu Nyerere akamteua Kijana huyo Salim Ahmed Salim kuwa Balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Uarabu ya Misri, nafasi ambayo aliitumikia kwa muda wa Mwaka mmoja kati ya Mwaka 1964 na 1965 kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania Nchini India.

Unaweza kudhani kuwa Salim Ahmed Salim alipewa nafasi husika kwa upendeleo, au kwa kuwa Chama chake cha Ummah Party kilikuwa na mahusiano ya karibu na Chama cha ASP cha Karume.

Uwezo wa Dkt Salim Ahmed Salim katika kuieneza Diplomasia ya Tanzania kwa muda wa miaka 50 ya Muungano wetu unaonyesha dhana ya upendeleo isivyo na mashiko, lakini hata uzoefu na Ukindakindaki wake wakati akiteuliwa kushika nafasi hiyo pamoja na kuwa alikuwa na umri mdogo vinaonyesha kuwa aliistahili nafasi hiyo.

Salim hakuwa mgeni wa Siasa za Zanzibar, alichipukia katika Zanzibar Nationalist Party, ZNP chini ya ulezi wa Komredi mahiri, Profesa Abdulrahman Mohammed Babu na bega kwa bega naye alishiriki katika kukiasisi chama cha kwanza chenye kufuata Mrengo wa Kijamaa katika Afrika, Ummah Party, Chama ambacho kilishirikiana na ASP katika kutekeleza Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 yaliyomuingiza madarakani Karume.

Ni chama hiki, Ummah Party ndicho kilichotoa wanamapinduzi Majemedari kama Komredi Ali Sultan Issa, Kanali Ali Mahfoudh, Komredi Sharifu Ahmed Badawyi Qullatein na wengineo ambao walikuwa chachu ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kijana mdogo Salim Ahmed Salim alishirikiana na kulelewa na wote hao, jambo lililompa uzoefu, uwezo na mafunzo. Mpaka leo rekodi zinamuonyesha Dkt Salim A Salim aliyezaliwa Januari 23, 1942 kuwa ndiye Mtanzania mwenye umri mdogo zaidi kuteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nje ya Nchi.

Pichani ni kijana wa miaka 17 wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, Ndugu Salim Ahmed Salim wa ZNP akiwa pamoja na Rais wa TANU, Ndugu Julius Kambarage Nyerere. Picha husika inaonyesha uzoefu na ushiriki wa kijana huyu katika Siasa za Ukombozi tangu akiwa na umri mdogo tu.

TUJIKUMBUSHE NYEPESI NYEPESI KATIKA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUTOKA KALAMU YA DR. HARITH GHASSANY


Assalam Alaykum,

Inna Lillah wa Inna Ilayhi Raajiun - Mzee Ahmed Badawi Qullatein ametutangulia kunako haki.

Mara yangu ya kwanza kuonana na marehemu Mzee Badawi ilikuwa pale alipokuja Zanzibar kwa matembezi kutoka Dar es Salaam. Nilikwenda kuonana nae nyumbani kwake Malindi na ilikuwa tarehe 26 Julai 2005.

Ilibidi nimsubiri kidogo kwa sababu alikuwa anasoma Qur'an nyakati za asubuhi. Tulizungumza kiasi na alinikaribisha nikipata wasaa nende nikaonane nae kwake Dar es Salaam lakini sikujaaliwa.

Nilionana nae tena mara pili alipokuja Uroa na Bwana Ali Mohamed Yahya ambaye alikuwa ana tabia ya kumtembelea marehemu baba yangu. Nakumbuka vizuri marehemu Mzee Badawi kuniambia kuwa suluhisho la matatizo ya Waislam ni kuanzishwa kwa Dola ya Kiislam, na si jengine.

Tumebahatika wakati wa maombolezi ya kifo cha almarhum Mzee Badawi kupata maelezo ya mchango wake wa kisiasa kama ni kipande cha sehemu ya mwanzo wa maisha yake ya ujanani. Sheikh Salim Msoma ametueleza kuwa marehemu alifariki Makka wakati alipokwenda kufanya Hijja.

Ingelipendeza zaidi kama Salim Msoma angetueleza pia mabadiliko ya nafsi na ya kimtazamo ya marehemu Sayyid Ahmed Badawi alietokana na ukoo wa Masharifu, akawa mmoja wa waasisi wa "Marxist Umma Party of Zanzibar", na akafika kuipata bahati ya kufariki Makka wakati akiweko huko kwa ajili ya kufanya Hijja.

Salim Msoma ana uhuru wake lakini hakumtendea haki marehemu Mzee Badawi ambaye pia inasemekana aliomba "Tawbat Nasuha" kabla ya kufariki kwake dunia ambayo ndio kilele cha kujuta na kuomba maghfira kutoka kwa Muumba. Hilo ni jambo binafsi baina ya muumbwa na Muumba wake lakini linatuambia kitu sisi waja wake kuhusu hali ya marehemu Mzee Badawi kabla ya kurudi kwa Mola wetu sote. Wa Allahu Yaalam!

Sasa nakuja pale Salum Msoma alioitumia nafasi ya maombolezi ya kifo cha marehemu Mzee Badawi kutoa dukuduku lake juu ya kitabu cha Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru! Bado jini mkali wa historia anaendelea kuwasumbua baadhi ya Makomred na ndio maana hata marehemu Mzee Badawi aliefariki Makka akiwa na umri wa miaka 80 wanaona bora wamrudishe nyuma alipokuwa kijana mbichi kwenye umri wa miaka 30.

Hakuna kitu kilichowaudhi baadhi ya Makomred kama pale marehemu Mzee Aboud “Mmasai” aliposema na alivonukuliwa akisema 
“Tukaingia ndani, Migombani huku, buibui la Sauda akavaa Babu, sasa tunamwambia “wewe tukitoka uringeringe kidogo.” Dereva wa gari alikuwa Ali Saidi, taxi-driver, tulimchukuwa, kwa sababu yeye huyu alikuwa ni memba wa mapinduzi. Alikuwa ni mwenzetu. Tukampita asikari, akaingia ndani ya gari ile, tukatoka tukenda Kizingo. Kizingo Babake Fuko, mzazi, alikuwa na ngarawa na mwanawe mdogo Huseni, ndo akapakiwa Babu kupelekwa…kateremkia Mlingotini. Akateremshwa pale, sie tukarudi huku.”
Kabla ya Salim Msoma, yuko Komred mwengine (jina nalihifadhi) ambaye tuliwasiliana mwaka jana na alinipa uoni wake juu ya kitabu cha Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru! kwa kusema “Ninachotaka kusisitiza hapa, bila ya kuigeuza barua hii pepe na kuwa insha, ni kwamba zipo hizo tofauti kati ya wenye kukumbuka” na akatoa mfano:
“Tofauti nyingine ya makumbusho niliyoiona ni katika maelezo ya jinsi Babu alivyokimbizwa kutoka Unguja. Nijuavyo mimi hakuvalishwa buibui wala mke wa Marhemu Saleh Saadallah hajakuwako kwa Babu wakati wa yeye Babu kukimbizwa kama alivyohadithia Aboud Mmasai. Waliokuwapo hapo walikuwa Saadallah, Twala, Ashura aliyekuwa mkewe Babu...”
Mwaka jana nilibahatika kupokea mualiko jijini Washington DC ambao wageni rasmi walikuwa ni Bibi Ashura na mumewe. Nikajiambia kuwa hii itakuwa fursa ya kuusikiliza upande wa pili wa shilingi na kujua kama maelezo ya kutoroshwa marehemu Abdulrahman Babu ya marehemu Mzee Aboud “Mmasai” yalikuwa sahihi au yanahitajia marekebisho. Bi Ashura hakutaka kuingia katika mazungumzo haya na mie nikayawacha.

Maelezo ya Salim Msoma yanapingana na yale ya marehemu Mzee Aboud “Mmasai” juu ya mahala alipotoroshwa Babu kupelekwa Dar es Salaam kwa msaada wa kina marehemu Saleh Saadalla na Abdulaziz Twala. Mzee Aboud anasema ilikuwa ni Kizingo, Salum Msoma anasema ilikuwa Fumba.
Sijui kwanini Salum Msoma akangojea mpaka Mzee Badawi akafariki dunia ndio hii leo akaamua kutuletea kumbukumbu muhimu kama hii. Jambo la kutia tamaa ni Msoma anasema kuwa mtu alioiendesha gari iliomchukua Babu na Badawi Fumba yuhai na anaishi Dar es Salaam.

Sasa lilobaki ni kumuomba Bwana Msoma atuletee, hadharani au hata kwa pembeni, jina na maelezo ya dereva aliyempeleka marehemu Babu Fumba ili tuyahakiki maneno yake na yale ya marehemu mzee Aboud “Mmasai” tuweze kuiweka rekodi sawa katika toleo lijalo la kitabu cha Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru!

Muhimu katika maneno ya Bwana Msoma ni kukiri kwake kuwa marehemu Mzee Badawi alipewa taarifa ya mapinduzi na waandalizi wa mapinduzi ambao walikuwa kina marehemu Abdalla Kassim Hanga, Saleh Saadalla, na Abdulaziz Twala. Ameongeza kuwa Umma Party waliarifiwa kwanza hata kabla kuarifiwa marehemu Mzee Karume na viongozi wengine wa chama cha Afro-Shirazi.
Mungu amlaze mahala pema marehemu Mzee Ahmed Badawi Qullatein – Amin.

Taarifa nzima ya habari ChannelTEN, Jumapili 10.01.2016


Ally Saleh amzungumzia Mbwana Samata tokea amwone kiwanjani; "Amechelewa!"

[video] Operesheni ya kukamata wahamiaji haramu na kukagua vibali vya kazi vya wageni