Mbele na nyuma ya kurasa za magazeti ya Tanzania leo Jumatano, Januari 13, 2015


FULL SPEECH of the USA President, Barack Obama, Final State of the Union Address - 1/12/2016


Barack Obama, 44th President of the United Stats of America
Barack Obama, 44th President of the United States of America (photo via Medium, January 12, 2016)

Mr. Speaker, Mr. Vice President, Members of Congress, my fellow Americans:

Mo Ibrahim Foundation - GDAI - MSc Scholarships

The Centre of African Studies offers 3 MSc scholarships to African residents as part of the Governance for Development in Africa Initiative funded by the Mo Ibrahim Foundation.


In order to be considered for funding, applicants must first secure a place for the MSc by applying directly to the SOAS admissions office.
Once the place is secured, the applicants can apply for the scholarship. Candidates will be assessed on academic merit by a panel consisting of SOAS academic members. The assessment of your application will be based on the information in your scholarship application. Selectors will be looking at the following:
  • academic achievement and evidence of critical analytical capabilities;
  • references;
  • supporting statement;
  • evidence of interest in and knowledge of linkages between governance and development
Please note that CAS reserves the right not to award scholarships and will only award them where there are applicants judged to meet sufficiently high academic standards and with demonstrable interests in fields relevant to the objectives of the GDAI.
Deadline to apply: 30 April 2016

Downloads

AzamTv video: Kumbukumbu zilizozikwa - Mapinduzi ya Zanzibar

Taarifa ya habari ChannelTEN, Jumanne, 11.01.2016


Call: Knowledge for Tomorrow - Cooperative Research Projects in Sub-Saharan Africa

This funding initiative aims at extending and strengthening research in the regions of Sub-Saharan Africa.

Objective

The funding initiative is open to all disciplines and aims at the development and sustainable reinforcement of research in Sub-Saharan Africa. Research projects, developed and carried out by African scholars and scientists in close cooperation with their German partners, shall provide junior researchers in Africa with an opportunity to enhance their skills and academic qualifications. Special emphasis is put on the development, reinforcement, and extension of academic networks inside Africa beyond existing language barriers.

Scope of Funding

The following call aims at post-docs starting academic careers in Africa. Funding can only be approved for research projects carried out in cooperation with a partner academic institution in Germany, and for Junior and Senior Fellowships with a 36-month duration.
Open Calls
Call for Pre-Proposals for Postdoctoral Fellowships on Livelihood Management, Reforms and Processes of Structural Change. Deadline for application is April 6, 2016. Details of conditions and the application procedure can be found under Information for Applicants 81k (pdf). Applications must be filed electronically via the application portal.
Workshops, Symposia and Summer Schools in Africa
Applications will only be accepted for processing after previous consultation with the respective contact person.

Background

The funding initiative was introduced in 2003. By way of preparation, the Foundation organized a number of events during which the pertinent parameters were discussed. This applied especially to the researchers on the African side.

From time to time, the Volkswagen Foundation organizes thematic workshops in order to aid the identification of promising areas of future-oriented research and the development of innovative lines of research in a spirit of partner-like cooperation. These meetings are used to discuss the current status of research, identify research issues, and to explore and develop possibilities for cooperation with other researchers and research institutions inside sub-Saharan Africa. Attendance at these workshops is by invitation only. Details of how to apply are posted on the Foundation’s homepage.

Information on previously held thematic workshops.

Serikali kugawanya kwa uwiano madaktari na mabingwa nchini

Mheshimiwa Ummy Mwalimu akizungumza na Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Peramiho, Dk Venance Mushi, alipotembelea hospitali hiyo asubuhi ya leo
SERIKALI imesema itapanga mgawanyo maalumu ili mikoa yote iweze kunufaika na huduma za Madaktari na Madaktari bingwa na kutatua kero za wananchi wanazopata za kufunga safari ndefu kuhangaikia huduma za wataalamu hao.

Aidha itaendelea kushughulikia suala la kuboresha mazingira ya kazi kwa Madaktari na watumishi wa Sekta ya Afya kwa ujumla ikiwa ni pamoja na maslahi yao ili kuwafanya wahamasike kufanya kazi hapa nyumbani badala ya kwenda kufuata maslahi makubwa nje ya nchi.

Kauli hiyo ya serikali imetolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa huduma za madaktari bingwa mkoani Ruvuma jana

Alisema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Daktari John Magufuli, imedhamiria kukabiliana na upungufu wa Madaktari kwa kuanzisha utaratibu maalumu wa mgawanyo huku ikiongeza idadi ya wahitimu wa fani hiyo katika vyuo mbali mbali vya Udaktari hapa nchini.

“Kama mtakumbuka hivi sasa kuna mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Muhimbili unaoendelea katika eneo la Mlongazila, vilevile kuna ujenzi wa Hospitali ya kisasa unaoendelea katika Chuo Chuo Kikuu cha Dodoma, kote huko kunatarajiwa kutoa Madaktari wa kutosha ili kuziba pengo la Madaktari na Madaktari Bingwa lililopo hivi sasa.” Alisema waziri ummy.

Alisema mipango hiyo iliyoanza katika Awamu ya Nne itaendelezwa kwa kasi zaidi ili taifa lifikie lengo la kuwa na Madaktari Bingwa karibu zaidi na wananchi wengi kwani imeonekana kuwa kuna mlundikano mkubwa wa Madaktari na Madaktari Bingwa sehemu za mijini kama vile katika mikoa ya Dar es Salaam, Kilimanjaro, Mwanza na Arusha.

Katika uzinduzi huo ambapo pia alikabidhi hospitali ya rufaa Songea dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya Shilingi milioni tano, pamoja na mashuka mia tatu, Waziri Ummy aliuagiza Mfuko wa taifa wa Bima ya Afya, kuongeza kasi ya kusajili wanachama wapya ili kuwapunguzia wananchi adha ya gharama za matibabu.

Aliwataka viongozi mbalimbali kusaidia jitihada hizo ili kuhakikisha kwamba wananchi Tanzania wanapata huduma za afya wanapozihitaji na kwa gharama nafuu kwa kuwa katika mfuko wa NHIF.
Aidha alisema serikali itafanyia kazi uwasilishaji wa muswada wa Sheria ambayo itamtaka kila mwananchi awe mwanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

“Ni matumaini yangu kuwa utekelezaji wa Sheria hii utasaidia kuboresha huduma za matibabu na kuondoa changamoto ya ufinyu wa rasilimali kwa ajili ya kuendeshea huduma za afya kwa wananchi wa Tanzania” alisisistiza waziri Ummy.

Akizungumzia uboreshaji wa huduma za matibabu zinazotolewa kwa wananchi hususan katika maeneo ya vijijini kupitia Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) unaosimamiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya alisema amfurahishwa na Kazi ya kuboresha miundo mbinu na kuongeza makundi mbalimbali ambapo hadi Desemba 2015 jumla ya wanufaika 6,677,241 walijiunga katika Halmashauri 144 nchini, hii ni asilimia 15.3 ya Watanzania wote.

Hata hivyo alisema Mkoa wa Ruvuma una changamoto kubwa ya halmahsauri zake kuwa na idadi ndogo ya wanufaika waliojiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF). Hadi kufikia tarehe 31 Disemba 2015 idadi ya wanufaika ilikuwa ni 188,136 kati ya walengwa 1,376,891 ambayo ni sawa na asilimia 14 ya lengo la uandikishaji kimkoa.

Alizihimiza Mamlaka za Halmashauri zote nchini, kuhakikishe zinatumia vyanzo mbalimbali vya mapato vinatokana na uchangiaji wa huduma za matibabu kutumia fedha hizo kuboresha huduma ikiwemo dawa, vitendanishi na vifaa tiba.

Awali katika hotuba yake ya utambulisho Kaimu Mkurugenzi wa NHIF, Michael Mhando aliomba uongoziwa Mkoa na Halmashauri zote, ziandae programu maalum ya uhamasishaji wananchi kwa lengo la kurudisha hadhi ya mkoa wa Ruvuma kwenye CHF ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga ndio iliyokuwa ya kupigiwa Mfano ndani na nje ya nchi.

Aidha alisema Mpango wa huduma za madaktari bingwa mkoa wa Ruvuma unatekelezwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watotokwa kuwatumia Madaktari Bingwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, MOI na Hospitali za Rufaa za Kanda.

Alisema mpango huo umeshatekelezwa katika mikoa kumi na tatu hadi sasa.

Alisema kabla ya kutekeleza mpango huu hapa mkoani Ruvuma, waliwatuma Madaktari wao ambao walishirikiana na Madaktari mkoani Ruvuma kubaini mahitaji halisi ya wananchi katika huduma hizo za Madaktari bingwa na kukubaliana kuwa wanahitaji zaidi huduma za Madaktari bingwa katika maeneo ya magonjwa ya masikio, pua na koo, mfumo wa njia ya mkojo, magonjwa ya watoto, magonjwa ya ndani na moyo, pamoja na bingwa wa dawa za usingizi na wagonjwa mahututi.
mwisho

Baadhi ya wanachama wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), wakiwa sehemu ya mapokezi, tayari kwa kupata huduma
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu ametembelea jengo la zahanati ya Mpingi, wilaya ya Songea Vijijini na kuzungumza na wanakijiji wa eneo hilo.

Ziara hiyo ni moja kati ya kazi anazozifanya mkoani hapa kwa lengo la kuzungumza na wananchi, watoa huduma na watumishi wa sekta ya afya ili kuboresha huduma za matibabu na kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli mbalimbali za afya ikiwemo uchangiaji katika mfuko wa Bima ya Afya.

Baada ya kufika kijijini hapo na kuona jitihada zilizofanywa na na wananchi katika kujenga zahanati ya kijiji, Waziri Ummy aliwaahidi wananchi hao mabati na misumari ili kuunga mkono ujenzi wa zahanati hiyo.


Mheshimwa Ummy Mwalimu akisaini kitabu cha wagenii kijijini Mpingi


Baadhi ya wananchi wa Mpingi waliohudhuria kumlaki Waziri Ummy Mwalimu alipotembelea majengo ya zahanati yaoWaziri Ummy Mwalimu akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Benson Mpesya, kutembelea majengo ya zahanati ya Kijiji cha Mpingi


Mzee Mohamed Mussa, mkazi wa kijiji cha Mpingi akimshukuru Waziri Ummy Mwalimu kwa kutembelea kijiji chao na kutoa msaada wa bati na misumari ya kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji

Hotuba aliyoitoa Dk Shein katika maadhimisho ya miaka 52 ya SMZ

HUTUBA YA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI, MHE. DK. ALI MOHAMED SHEIN, KATIKA MAADHIMISHO YA SHEREHE ZA MIAKA 52 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR, AMAAN STADIUM 

TAREHE 12 JANUARI, 2016

Nakala ya maandishi ya Hotuba ya Maalim Seif aliyoitoa Jumatatu, Januari 11, 2016

Internet World Growth: The Digital Divide

The following table shows the world Internet growth between Dec 2000 and Nov 2015 in the following World Geographic Regions.
World Regions
Internet
Dec 2000
Internet
Nov 2015
Growth %
2000-2015
ASIA
114,304,000
1,622,084,293
1,319.1 %
EUROPE
105,096,093
604,147,280
474.9 %
EUROPEAN UNION
94,593,400
402,937,674
326.0 %
AFRICA
4,514,400
330,965,359
7,231.3 %
NORTH AMERICA
108,096,800
313,867,363
190.4 %
SOUTH AMERICA
14,292,100
249,291,302
1,644.3 %
MIDDLE EAST
3,284,800
123,172,132
3,649.8 %
CENTRAL AMERICA
3,217,400
77,876,335
2,320.5 %
OCEANIA / AUSTRALIA
7,620,480
27,200,530
256.9 %
THE CARIBBEAN
559,419
17,656,562
3,056.2 %
WORLD TOTAL
360,985,492
3,366,261,156
832.5 %
Note: Internet Users in millions of persons. Copyright © 2016,

From the above table, several facts become evident about the Internet's current situation and growth in the world: the region with the highest number of users is Asia, with a 40.2% penetration rate, and high digital divide.

The region with the highest growth rate is Africa, however, it still has a very low Internet penetration rate of 28.6%, indicating a high digital divide.

The region with the highest Internet penetration rate is North America, 87.9%, indicating a very low digital divide.

Enrique de Argaez, CEO
Miniwatts Marketing Group
www.internetworldstats.com

Taarifa ya Simba SC ya 'kutimua' makocha wake

Simba sports club
Dar es salaam
12-1-2016

Taarifa kwa vyombo vya habari

Kwa masikitiko makubwa klabu ya Simba inawaarifu umma kupitia vyombo vya habari.uamuzi wake wa kuvunja mikataba yake na makocha wake.kocha mkuu Dylan Kerr na kocha wake wa makipa Iddi Salim.

Ktk uamuzi wake uliofanywa mchana huu na kikao cha kamati ya utendaji.ambapo makocha hao waliitwa.klabu ya Simba na walimu hao kwa pamoja wamekubaliana kuvunja mikataba ya ajira zao kwa faida ya pande zote mbili.

Kwa sasa kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja atakuwa na timu.huku mchakato wa kumpata kocha mkuu ukiendelea..

Mwisho uongozi unawashkuru walimu hao kwa huduma waliyoitoa katika kipindi chote cha uwepo wao klabuni.

Imetolewa na Haji S.Manara
Mkuu wa mawasiliano wa klabu ya Simba.
Simba nguvu moja

Sunderland AFC helping lead the way at Tanzanian sports park

A ground-breaking sports park in Tanzania is continuing to make strides in the community of Dar es Salaam as youth programmes prove a huge hit.

The JMK Youth Park, a multi-sport facility developed by Symbion Power and Sunderland AFC, officially opened to the Tanzanian public in October last year, and in less than six months is leading the way in two major initiatives to help some of the most vulnerable people in Dar es Salaam.

The ‘Street Kid’ and ‘Beach League’ entitled programmes are offering youngsters across Dar es Salaam access to world-class sports coaching programmes, organised leagues, education, equipment and most of all, a first-class facility to utilise.

Over the course of the past month, the ‘Street Kid’ programme has been running, aimed at engaging those young people who are not in formal education and are living in deprivation.

While at the Park, these youngsters not only have the chance to play sport, they are also being educated about health risks such as HIV, malaria and the perils of drug abuse, through the park's partnership with Grassroot Soccer.

Furthermore, those who show up without adequate footwear to play, receive football boots or trainers to play in, that were donated to the youth park by Barclays Premier League club and partner, Sunderland AFC, along with football shirts and other sportswear.

As part of its involvement Sunderland AFC provide the technical and practical support to the development of the park, which has seen thousands of youngsters already benefit from a joined up approach combining sport, education and community engagement, harnessing the knowledge and expertise of Sunderland AFC and its own successful academy.

The ‘Beach League’ was inspired by Symbion Power owner Paul Hinks who would see impoverished children play barefoot and football-less on the beaches of Dar es Salaam. Now these children have been given access to the brand-new 3rd generation artificial pitch which is at the centre of the JMK Youth Park.

The league is run for under-16 players and every Sunday all eight team's from the city's beaches play fixtures. The league has proven so successful that its expansion is now a priority for the league founders, Elieneza Nsanagnzelu and Frank Lusawa, who also run the ‘Street Kid’ programme.

Ray Power, Technical Director at the Park, said: "These two programmes are particularly heart-warming and it is fantastic to see them in full flow. Frank and Elly were tasked with going to the streets and beaches to invite participants to our programmes only a month ago and we already now have 200 of these youngsters coming to the park every week.

“I really believe that these two young coaches will be the most famous people on the streets of Dar in the coming months, thanks to the fantastic results they are achieving"

For information about either the Street Kid or The Beach League, please contact [email protected] or [email protected], or call the booking office on 0222183491.

For more information about Sunderland AFC in Africa please visit www.safc.com/the-club/safc-global and for further developments related to the park, please follow @jmkpark on Twitter and Instagram.

-ends-

Issued by Sunderland Association Football Club

Maamuzi ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa ligi ya soka

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi umeipa Polisi Dodoma ushindi wa pointi tatu na mabao matatu baada ya Mji Mkuu FC kumchezesha mchezaji Peter Ngowi aliyekuwa na kadi tatu za njano kwenye mechi yao ya Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes iliyochezwa Desemba 26, 2015 mjini Dodoma.

Uamuzi huo umefanywa kwa kuzingatia Kanuni ya 37(4) na 14(37) ya Ligi Daraja la Kwanza. Mji Mkuu FC ilikuwa imeshinda mabao 2-1 katika mechi hiyo iliyofanyika kwenye Uwanja wa Mgambo mjini Mpwapwa.

Kamishna wa mechi ya Ligi ya Daraja la Kwanza ya StarTimes kati ya Polisi Tabora na Panone FC ya Moshi, Shabani Funyenge amesimamishwa kutokana na ripoti yake ya mechi hiyo iliyochezwa Januari 2 mwaka huu kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora kuwa na upungufu.

Klabu ya Friends Rangers ya Dar es Salaam imepigwa faini ya sh. 200,000 (laki mbili) kutokana na washabiki wa timu yake kutoa kashfa na lugha za matusi wakati wa mechi ya Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes dhidi ya Kiluvya United iliyofanyika Novemba 8, 2015 kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Kaume jijini Dar es Salaam.

Pia imetakiwa kulipa kibendera cha kona (corner flag) pamoja ubao wa matangazo wa geti la kuingilia ndani kwenye Uwanja wa Karume ambavyo vilivunjwa na washabiki wa timu hiyo mara baada ya mechi hiyo.

Mtunza vifaa wa timu ya Kimondo, Emily Nehemia, Meneja wa timu ya Polisi Tabora, Idd Kibwana, Kiongozi wa Panone FC, Said watafikishwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutokana na kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu kwenye mechi za Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes.

Mji Mkuu FC imepigwa faini ya sh. 100,000 (laki moja) kwa kutohudhuria kikao cha awali cha maandalizi ya mechi (pre match meeting) katika mchezo kati yao na Polisi Dar es Salaam uliochezwa Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani. Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Kwanza.

Klabu za Polisi Tabora na Panone FC kila moja imepigwa faini ya sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa mujibu wa Kanuni ya 14(48) kugombania kuingia uwanjani kupitia mlango wa VIP badala ya ule wa kawaida kwenye mechi yao ya Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes iliyochezwa Januari 2, 2016 kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.

Wachezaji Ally Mwanyiro wa Rhino Rangers na Hamisi Shaban wa Lipuli wamepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kila mmoja na kufungiwa mechi tatu kwa kosa la kupiga wachezaji wa timu pinzani wakati wa mechi zao za Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes kinyume na Kanuni ya 37(3) ya Ligi hiyo.

Pia Polisi Mara imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) baada ya mshabiki wao kuingia uwanjani na kumvamia mwamuzi kwa madai maamuzi yake hayakuwa sahihi wakati wa mechi yao ya Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes dhidi ya Mbao FC iliyofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.

Bango lililoangaziwa katika maadhimisho ya 52 ya Mapinduzi SMZ


TAARIFA KWA UMMA

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesikitishwa sana na ujumbe wenye maudhui ya ubaguzi ulioandikwa kwenye moja ya Bango lililobebwa na mmoja wa wananchi waliojitokeza katika maadhimisho ya Sherehe za Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaomba radhi kwa ujumbe huo, kinapinga na kinakemea kabisa fikra, hisia na mitazamo yoyote yenye maudhui ya kibaguzi.

Ujumbe huo sio tu kuwa una maudhui ya kibaguzi bali pia unaenda kinyume kabisa na falsafa na Shabaha ya waasisi wa Mapinduzi hayo Matukufu ya mwaka 1964 na unapingana na misingi na itikadi ya CCM inayohimiza Umoja na Mshikamano wa Kitaifa.

Daniel Chongolo
Mkuu wa Mawasiliano na Umma CCM.
11/01/2016


CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

CCM WAMEDHIHIRISHA FIKRA ZA KIKABURU


Katika hali isiyokuwa ya kawaida ambayo kwa namna yoyote haiwezi isingeachwa imee katika fikra za watu achilia mbali kuachiwa itembezwe hadharani, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia katika mojawapo ya mabango yaliyobebwa na wanachama wake kuiadhimisha Sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar, imedhihirisha kuwa inakumbatia fikra hatari za kikaburu.

Kupitia bango hilo ambalo kwa namna lilivyotengenezwa na lilivyobebwa ni vigumu kuamini kuwa liliibuka ghafla kama vile kitambaa cha mfukoni, mwanachama wa CCM akiwa amesindikizwa na wenzake, waliopita mlangoni mwa Uwanja wa Amani bila kuzuiliwa, kukemewa wala kubugudhiwa, ujumbe hatari wa kibaguzi umeandikwa 'MACHOTARA HIZBU ZANZIBAR NI NCHI YA WAAFRIKA'. Hizi ni fikra za kikaburu. Ni ishara ya mbegu za kibaguzi zilizokomaa na sasa zinachipua.

Kwa wafuatiliaji wa masuala ya kisiasa nchini na kipekee katika muktadha huu, siasa za Zanzibar wataelewa kuwa kauli iliyotolewa katika bango hilo, si ya bahati mbaya. Ni matokeo ya siasa za chuki zinazopaliliwa, kusimamiwa, kuratibiwa na hata kunyamaziwa na uongozi wa juu kabisa wa CCM.

Tutatoa mfano. Moja ya maskani maarufu za masuala ya kisiasa Visiwani Zanzibar inayomilikiwa na CCM iitwayo Kisonge imekuwa na kawaida ya kuandika lugha hatari zinazoashiria ubaguzi ulio wazi kabisa ulio na maudhui sawa sawa na huu uliotolewa leo kwenye Sikukuu ya Mapinduzi.

Mojawapo ya kauli ambazo ziliandikwa katika ubao ulioko katika maskani hiyo hivi karibuni wakati wa joto la Uchaguzi Mkuu uliopita, iliandikwa hivi "Katiba ni ya Unguja na nyinyi Wapemba mwende mkatengeze yenu Pemba."

Lugha hiyo na nyingine za namna hiyo kama ilivyotokea leo, zimekuwa zikitolewa mbele ya viongozi wa CCM au wanaziona lakini kwa sababu wanazozijua wao, pengine zinawasaidia katika kufikia malengo ya siasa hatarishi zinazokiuka misingi yote ya demokrasia, zimekuwa zikifumbiwa macho na kuzidi kumea vichwani mwa wanachama wao na kuleta mpasuko wa ubaguzi wa itikadi za kisiasa, rangi, kanda, kabila na hata dini, si Zanzibar pekee bali nchi nzima.

Kilichotokea leo Zanzibar, ni mwendelezo usiokuwa wa bahati mbaya bali maelekezo ya kimkakati ya kueneza propaganda za chuki miongoni mwa Watanzania ambayo ndiyo imebakia kuwa silaha pekee ya kuibeba CCM ikiwa ni dalili ya wazi ya chama kilichofilisika sera, kuacha misingi yake, kuishiwa ushawishi wa hoja na kukosa uhalali wa kisiasa hivyo kujihalalisha kwa ubaguzi kama huo.

Ni mwendelezo wa kauli za viongozi wakuu wa chama hicho ambazo hutolewa hadharani kwenye majukwaa ya siasa, wakiwabagua wanachama, wapenzi, wafuasi wa vyama vingine kuwa ni wa dini fulani, kanda fulani au kabila fulani. Wakijua kabisa hakuna kikundi chochote cha kisiasa chenye sifa hizo kwa sababu ni kinyume cha sheria na misingi ya taifa letu.

Ni mwendelezo wa kauli iliyowahi kutolewa na viongozi wa chama hicho dhidi ya viongozi wenzao na wala viongozi wakuu wa CCM hawakuthubutu hata kukaripia, tena yakiwa maazimio rasmi ya kikao kwamba "Rais wa Tanzania hawezi kutoka Kaskazini".

Kauli hiyo iliyotolewa baada ya kikao ilikuwa kauli ya kikaburu sawa sawa kabisa na ile iliyotolewa leo huko Zanzibar.

Mwalimu Nyerere, Baba wa Taifa aliwahi kusema ukaburu si rangi, ni fikra.

CHADEMA tunalaani na kupinga kwa nguvu zote mipango, mikakati, tabia na chembechembe za ubaguzi wa aina yoyote, ukiwemo huu wa kisiasa ambao sasa unaanza kusakafiwa kwa ubaguzi wa rangi kwa sababu tunaamini wanaobeba agenda hii hawataishia hapo bali watazidi kutugawa Watanzania pia kwa ubaguzi wa ukanda, ukabila na udini kama ambavyo wamekuwa wakijaribu kuchochea.

CHADEMA kwa kusimamia misingi yake na kuzingatia kikamilifu misingi ya taifa letu hasa haki, uadilifu, utu, umoja na uzalendo, haiko tayari kuona taifa likifikishwa huko na kuhatarisha maisha ya jamii nzima ya Watanzania kwa sababu ya maslahi ya kikundi cha watu wachache.

Tunamkumbusha Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Ernest Mangu kuwa kauli za namna hii ambazo zimekuwa zikipaliliwa na viongozi wa CCM na wengine wakitumia nafasi za kiserikali kuchochea ubaguzi ambao ni hatari kwa amani ya nchi na usalama wa raia na mali zao, ni ushahidi wa wazi kwa ajili ya hatua za kisheria badala ya jeshi hilo kujikita katika kubambikia wanachama, wafuasi na wapenzi wa vyama vya upinzani, hususan UKAWA tuhuma na kesi zisizokuwa msingi wowote kwa maslahi tu ya kisiasa kuisaidia CCM.

Wakati tukimtaka Rais John Magufuli kutimiza kwa vitendo kauli yake ya kwamba Serikali yake haitawabagua watu kwa misingi ya kisiasa (huku Waziri Mkuu wake akitoa maagizo kinyume kabisa na kauli hiyo) tunakitaka CCM, kupitia kwa Mwenyekiti wake, Jakaya Kikwete kama hakiko nyuma ya agenda hizo za kibaguzi na fikra hizo za kikaburu, kichukue hatua za haraka mara moja kuwawajibisha viongozi wake waliosimamia na kuachia jambo lililotokea leo huko Zanzibar.


Imetolewa leo Jumanne, Januari 12, 2016 na;

Tumaini Makene

Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Habari
CHADEMA
  • Chanzo cha taarifa: WhatsApp

Maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi ya Serikali Zanzibar


Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akisalimiana na Rais Mstaafu wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo katika killele cha sherehe za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kutimia miaka 52, zilizofanyika katika uwanja wa Amaan mjini Unguja, ambapo mgeni rasmi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein [Picha na Ikulu.]

WM Majaliwa awajulia hali WM mstaafu Sumaye na Balozi Kibelloh


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Waziri Mkuu, Mstaafu Frederick Sumaye ambaye amelazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu Januari 12, 2016.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (wapili kushoto) wakizungumza na Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye ambaye amelazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu, Januari 12, 2016. Kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu mstaafu Mama Esther Sumaye.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Balozi Hassan Kibelloh ambaye amelazwa katik hospitali ya taifa y Muhimbili kwa matibabu, Januari 12, 2016.

Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu