Chozi la Mama aliyetapeliwa! Waziri Lukuvi aelezea maagizo ya kuzuia utapeli wa ardhi hasa vijijiniSimanzi, uchungu na maumivu ya 'bomoa bomoa'


Ujenzi wa barabara ya Kurasini (interchange)Picha via WhatsApp

New Zealand Development Scholarships for students from Africa, Asia, Latin America, Caribbean

New Zealand Development Scholarships (NZDS) give candidates from selected developing countries an opportunity to gain knowledge and skills through study in specific subject areas which will assist in the development of their home country. Awardees are required to return to their home country for at least two years after the completion of their scholarship to apply these new skills and knowledge in government, civil society or private business organisations.

NZDS are funded by the New Zealand Aid Programme, the New Zealand Government’s overseas aid and development programme. They are managed by the New Zealand Ministry of Foreign Affairs and Trade (MFAT).

NZDS are for postgraduate study in New Zealand and are available to candidates from specific Latin American and African countries, some Chinese provinces, and from Nepal, Timor-Leste and Mongolia. NZDS are also available for undergraduate study to candidates from Timor Leste.

Eligible countries
RegionEligible countries
African Commonwealth countries (CLICK HERE for instructions)Botswana, Cameroon, Ghana, Kenya, Lesotho, Malawi, Mauritius, Mozambique, Namibia, Nigeria, Rwanda, Seychelles, Sierra Leone, South Africa, Swaziland, Tanzania, Uganda, Zambia
Africa - non-Commonwealth countries (CLICK HERE for instructions)Algeria, Angola, Dijbouti, Ethiopia, Egypt, Gambia, Senegal, Tunisia, Zimbabwe 
 AsiaMongolia,  Nepal,  Timor-Leste
 Latin America (CLICK HERE for instructions)Argentina, Bolivia, Brazil, Chile, Colombia, Costa Rica, Cuba, Euador, El Salvador, Guatemala, Honduras, Nicaragua, Mexico, Panama, Paraguay, Uruguay, Venezuela
Caribbean Commonnwealth countries (CLICK HERE for instructions)Antigua & Barbuda, Bahamas, Belize, Dominca, Grenada, Guyana, Jamaica, St Lucia, St Vincent & the Grenadines,
Caribbean non-Commonnwealth countries (CLICK HERE for instructions)Dominican Republic, Haiti, Suriname

Kinondoni na Ilala zapata mameya na manaibu

Boniface JacobPichani juu ni diwani wa Kata ya Ubungo, Boniface Jacob akishangilia mara baada ya kushinda kwa nafasi ya Umeya wa Kinondoni kwa kupata kura 38, mapema leo Januari 16.2016, dhidi ya mpinzani wake, Benjamini Sitta aliyepata kura 20, dhidi ya kura zote zilizopigwa 58 katika Manispaa hiyo ya Kinondoni.

Uchaguzi huo uliokuwa wa huru na haki kwa pande zote, kura zilizipigwa kwa uwazi kwa pande zote.

Kura za Unaibu Meya nafasi hiyo ilienda kwa mgombea wa CUF ambaye ni Jumanne Amiri Bunju ambaye yeye alipata kura 38 wakati mpinzani wake kutoka CCM Diwani Manyama akiambulia kura 27 huku kura moja ikiharibika.


Pichani chini ni shughuli ilivyokuwa katika kuwachagua Meya na Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala. Shughuli hiyo ilifanyika leo katika ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es Salaam.


Matokeo ya Meya na Naibu Meya yakujumlishwa na baadhi ya wajumbe wa Meya, Naibu Meya wakiwa na Mwanasheria wao leo mara baada ya kumaliza kugika kura katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya viongozi wakiwa kwenye ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es Salaam.
Isaya Mgurumi
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mgurumi akitangaza matokeo ya Umeya na Unaibu Meya katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.

Wananchi wakishangilia ushindi wa Meya na Naibu Meya mara baada ya kutangazwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mgurumi jijini Dar es Salaam leo.

Charles Kwiyeko
Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kwiyeko akizungumza na madiwa wa Manispaa ya Ilala leo mara bada ya ushindi

Omary Salum
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Salum Kumbilamoto akiwashukuru madiwani waliompigia kura leo mara ya kuibuka kidedea katika uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Karimjee leo jijini Dar es Salaam.

Maendeleo ya ujenzi wa daraja la KigamboniImeelezwa kuwa daraja hili lililoanza kujengwa mwaka 2012 kwa Ushirikiano wa Mfuko wa NSSF na Kampuni za China, linatarajiwa kukamilika ujenzi wake mwaka huu. Daraja lina urefu wa mlalo wa kadirio la kilomita 2 likiunganisha Kurasini na Kigamboni.Inauzwa: Black Mazda Atenza version 6


On sale 

Mazda Atenza version 6
Year of manufacture 2005
Engine capacity 2260 cc, petrol

Interested parties call 0689 484 444


[video] Waziri Nchemba awasweka selo Mawakala, Watendaji waliokiuka agizo la serikaliChangamoto zilizoanza kujitokeza kwenye "Elimu Bure"

WAKATI serikali ikisisitiza kauli ya elimu bure, wanafunzi wapatao 602 wa shule ya Msingi Magamba, iliyopo Jimbo la Songwe, wilaya ya Chunya mkoani hapa wanalazimika kukaa chini. Kalulunga blog imebaini.

Hali hiyo imebainika wakati wa ziara ya mwanadishi wa habari hii,
inayoendelea mkoani Mbeya kuona utekelezaji wa kauli ya Rais JohnMagufuli kuhusu elimu bure

Shule hiyo ina wanafunzi 700, ambapo idadi ya madawati ni 98, ambayo yanakaliwa na wanafunzi wa darasa la saba na darasa la sita.

Kutokana na hali hiyo, baadhi ya wanafunzi wamebuni mbinu mpya yakukalia matofali huku baadhi yao wakilazimika kutoka na vigoda
majumbani mwa wazazi wao na kwenda navyo shuleni kwa ajili ya kukali kisha mchana hurudi navyo.

Ofisa mtendaji wa Kijiji hicho, Sabina Shitundu, alikiri kuwepo kwa adha hiyo ambayo alisema ni changamoto kubwa kwasababu pia ili kutatua tatizo hilo inawawia vigumu kwa madai kwamba suala la kuchangia madawati limeingiwa na siasa.

“Ni kweli tuna upungufu mkubwa wa madawati kutokana na wingi wa wanafunzi na wazazi tulipoitisha mkuytano wa kijiji ili wachangia angalau shilingi 2,500 kwa mwaka lakini waligoma” alisema Ofisa huyo.

Alipoulizwa nini hatima ya upatikanaji wa madawati hayo 602, alieleza kwamba, kutokana na wananchi kugomea zoezi la kuchangia madawati katika shule hiyo, wamewataka wazazi wa watoto wanaosoma katika shule hiyo, kuwa kila mzazi achangia kiasi cha shilingi 20,000, ambazo wazazi wawili watalazimika kununua dawati moja lenye thamani ya Tsh. 40,000.

Mbunge wa jimbo hilo, Philipo Mulugo, alipotafutwa kwa njia ya simu ili kutaka kufahamu kama anajua tatizo la wananchi wake, simu haikuweza kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi kupitia simu yake ya kiganjani hakuweza kujibu, ambapo taarifa zaidi kutoka kwa baadhi ya watu wake wa karibu zilisema alikuwa kwenye ziara na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, eneo la Saza Mine, ambako kuna mgogoro kati ya wananchi na wawekezaji.

Wakati huo huo, upungufu wa walimu katika baadhi ya shule wilayani Chunya limeendelea kuwa tatizo sugu, huku suala la upataji mimba kwa wanafunzi nalo likitajwa.

Katika shule ya Msingi Kasasya kata ya Mtanila, yenye wanafunzi zaidi ya 500, ina walimu wanne tu, huku shule ya Msingi Kalangali yenye wanafunzi 300 nayo ina walimu wanne ambapo mmoja wapo ni mzee na anasumbiliwa na maradhi hiyo ikifika saa sita analazimika kuondoka shuleni, huku shule zilizopo mjini, shule moja ina walimu zaidi ya 20.

Wakati huo huo, kuna “majipu” yanaendelea kuchunguzwa kama yameiva, kuhusiana na malalamiko ya walimu kuhusu fedha za uhamisho na likizo ambazo baadhi inaonyesha kuwa zilifanyika malipo lakini wahusika hawajapata.

Afisa elimu wa mkoa wa Mbeya, Charles Mwakalila, ambaye kabla hajapata nafasi hiyo alikuwa afisa elimu wa wilaya hiyo, alipoendewa ofisini kwake kwa ajili ya mahojiano, alimfukuza Mwandishi wa habari ambapo alimwamuru Katibu wake Muhtasi amwelekeze Mwandishi kuenda katika chumba cha wasaidizi wake namba 12 wanaoshughulikia masuala ya uhamisho wa wanafunzi!
  • Taarifa ya NA GORDON KALULUNGA, MBEYA via blog

Taarifa ya mabadiliko ya muundo wa Kamati za Bunge

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MABADILIKO YA MUUNDO WA KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE

____________________

Kamati ya Kanuni ya Bunge iliyoundwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai hivi karibuni, leo imekutana Jijini Dar es Salaam na Kuridhia mapendekezo ya mabadiliko katika muundo wa kamati za Bunge yaliyowasilishwa na Mhe. Spika ili kuendana na mabadiliko ya Muundo wa Wizara katika Serikali ya awamu ya Tano.

Mabadiliko hayo ambayo yamefanywa chini ya kanuni ya 155 (3) ya kanuni za Kudumu za Bunge yamezingatia madaraka aliyonayo Spika kufanya marekebisho kwenye nyongeza za kanuni kwa kushauriana na kamati hiyo.

Akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo Mh. Ndugai ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati hiyo amesema amelazimika kufanya mabadiliko katika muundo wa kamati ili kuendana na mabadiliko ya Wizara na kwa kuzingatia kuwa muundo wa kamati umetajwa kwenye nyongeza ya nane.

Katika muundo huo Kamati mbili mpya zimeundwa ambazo ni kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo na kamati ya kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma.

Akifafanua kuhusu maamuzi ya Kikao hicho, katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah amesema kikao hicho kimekuwa na mafanikio makubwa na kuridhia mapendekezo ya Mhe. Spika kama yalivyowasilishwa.

Aidha Dkt. Kashililah aliongeza na kusema kuwa Kamati nyingine zimefanyiwa mabadiliko kwenye majina na nyingine mbili kuunganishwa na kufanya kamati mpya za Bunge kuwa kama ifuatavyo:
Kamati zilizounganishwa ni:

·        Kamati ya Huduma na maendeleo ya Jamii - imeunganishwa kutoka iliyokuwa Kamati ya Maendeleo ya Jamii na kamati ya Huduma za Jamii
·        Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama –imeunganishwa kutoka iliyokuwa Kamati ya Ulinzi na Usalama na kamati ya mambo ya Nje.
Kamati zilizofanyiwa Marekebisho madogo kwenye majina ni:
·        Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira (awali ilikuwa Kamati ya Viwanda na Biashara)
·        Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii (awali ilikuwa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira)
·        Kamati ya Utawala na Serikali za Mitaa (awali ilikuwa Kamati ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa)

Kamati zilizobakia kama ilivyokuwa awali ni pamoja na:
·        Kamati ya Uongozi,
·        Kamati ya Kanuni za Bunge,
·        Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge,
·        Kamati ya Katiba na Sheria
·        Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji,
·        Kamati ya Miundombinu
·        Kamati ya Nishati na Madini.
·        Kamati ya bajeti
·        Kamati ya Masuala ya Ukimwi
·        Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na
·        Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC)
Wabunge wote wanatakiwa kuwasili Dodoma tarehe 20 Januari, 2016 tayari kwa kuanza Vikao vya Kamati kabla ya Mkutano wa Bunge unaotarajiwa kuanza tarehe 26 Januari, 2016.

Imetolewa na,

Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano.
Ofisi ya Bunge,
S.L.P 9133,
DAR ES SALAAM

15 Januari, 2016.

Taarifa: Maeneo yatakayoathirika kwa kuzimwa mtambo wa maji wa Ruvu Juu

Shirika la Maji Safi na Majitaka Dar-es-salaam (DAWASCO), Linasikitika kuwatangazia wakazi wa jiji la Dar-es-salaam na Mji wa Kibaha mkoan pwani kuwa Mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Juu utazimwa kwa wastani wa Saa 36 kwa siku za Jumatatu 18/01/2016 na Jumanne 19/01/2016.

Mtambo wa Ruvu Juu utazimwa ili kuruhusu Mkandarasi Kumalizia kazi za Ujenzi kwa kuunganisha Pampu za Mtambo mpya Mtoni. Zoezi hili linaashiria kukamilika kwa upanuzi wa Mtambo wa Maji wa Ruvu juu. Shirika linakusudia kuzalisha maji mapya toka Mtambo wa Ruvu Juu kuanzia tarehe 28 Februali 2016 na Kuondoa kabisa tatizo la maji kwa maeneo yanayohudumiwa na Mtambo wa Ruvu Juu

Kuzimwa Kwa mtambo wa Ruvu Juu kutapelekea maeneo yafuatayo katika Jiji kukosa Maji:

MLANDIZI, KIBAHA, KIBAMBA, MBEZI, KIMARA, UBUNGO, KIBANGU, MAKUBURI PAMOJA NA ENEO LOTE LA TABATA.

WANANCHI MNASHAURIWA KUHIFADHI MAJI NA KUYATUMIA KWA MATUMIZI YA LAZIMA.

Wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 022-2194800 au 0800110064 (BURE)
DAWASCO INAWAOMBA RADHI WANANCHI KWA USUMBUFU UTAKAOJITOKEZA.

IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
DAWASCO-MAKAO MAKUU

Mkurugenzi TCAA asimamishwa kazi; Mhasibu Mkuu, Meneja Manunuzi wahamishwaSerikali kupitia Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mabarawa imemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Charles Chacha na kutaka kuhamishwa mara moja kwa Mhasibu Mkuu Alhaji Said Mteule na Meneja manunuzi wa taasisi hiyo, Said Kaswela kwa kushindwa kusimamia ukusanyaji wa mapato ya taasisi.

Mbarawa alitoa agizo hilo jana akiwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango pamoja na watendaji wa TCAA katika ziara aliyoizungumzia kuwa ni ya kuangalia uendeshaji na ukusanyaji wa mapato unavyofanyika katika taasisi hiyo.

Pamoja na maamuzi hayo, serikali imeona pia ifanye uchunguzi kuhusu ununuzi wa mtambo wa kufuatilia vyombo angani unaojulikana kama Automatic Data Surveillance-Broadcast (ADS-B) na mtambo wa kukusanya taarifa za usafiri wa anga (AMHS), ambayo imegharimu kiasi cha Euro milioni 1.5/=.

Mitambo hiyo ilitakiwa kuanza kufanya kazi tangu Novemba mwaka jana, lakini mpaka sasa haijaanza kufanya kazi.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mpango alisema kikubwa kinachopiganiwa na serikali ni kukusanya mapato yote ya kodi na yasiyo ya kodi na katika mamlaka hiyo, kuna vyanzo vinavyoweza kuiingizia serikali fedha nyingi.

Kikwete azungumza na Perriello kuhusu hali ya Burundi

Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete akiwa na Mjumbe Maalum wa Marekani katika Ukanda wa Maziwa Makuu, Thomas Perriello, baada ya mazungumzo yao kuhusu hali ya Burundi, yaliyofanyika jana, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam. (Picha na Bashir Nkoromo).

Taarifa ya kusitishwa leseni za vituo 27 vya redio na runinga

Mkurugenzi Mkuu wa Malaka ya Mawasiliano Tanzania, TCRA, Dr. Ally Y. Simba

update

Mnamo tarehe 15 Januari 2016 Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilitoa taarifa kwa umma kuhusu kufungia Watoa Huduma za Maudhui ya Utangazaji (Redio na Televisheni) 27 waliokuwa wanadaiwa ada na tozo mbalimbali zinazotokana na leseni zao. Aidha,tarehe 18 Januari 2016 ilichapichwa taarifa ya makampuni ambayo yatafungiwa kwa muda ikiwa watashindwa kulipa ada na tozo hizo katika magazeti mbalimbali. Nia ilikuwa kuwakumbusha kwa mara ya mwisho utekelezaji wa wajibu wao kwa mujibu wa sheria na masharti ya leseni.

Baada ya taarifa hizo katika magazeti Mamlaka ilipokea maombi kutoka katika vituo vingi vikiomba kutokufungiwa vituo vyao na kwamba waruhusiwe kufanya malipo siku hiyo ya tarehe 18 Januari 2016 na kuwasilisha stakabadhi katika ofisi za TCRA kuthibitisha kuwa malipo yamekamilika. Mamlaka ilikubali maombi hayo na hadi kufikia mwisho wa saa za kazi tarehe 18 Januari 2016, redio 12 kati ya 20 na kituo kimoja kati ya vituo vya television 6 vimelipa ada na tozo zote au kubakiza kiasi kidogo cha deni ambalo walikuwa wanadaiwa na hivyo kuviruhusu kuendelea kutoa huduma ya utangazaji kama kawaida. Kwa wale ambo hawajamaliza malipo yote Mamlaka inaingia nao mkataba maalumu wa lini bakaa la deni litalipwa, na kwamba wasipofanya hivyo kwa muda uliokubalika hatua nyingine za kisheria zitachukuliwa.

Hadi kufikia tarehe 19 Januari 2016 ni vituo 13 ambavyo havijaweza kulipa deni wanalodaiwa na wala hawajawasiliana na Mamlaka. Hivyo basi Mamlaka imeendelea na utekelezaji wa sheria wa kusitisha utoaji wa huduma za utangazaji kwa vituo vya redio na television vilivyoorozeshwa hapa chini, hadi hapo watakapotekeleza wajibu wao wa kulipa ada na tozo wanazodaiwa. Hii inamaanisha ya kuwa vituo hivi vitafunguliwa pindi watakapolipa ada na tozo husika. Ikiwa watashindwa kufanya hivyo kwa muda wa miezi mitatu kuanzia tarehe 19 Januari 2016 hatua zaidi za kisheria kwa mujibu wa Kifungu 22(a) cha Sheria ya EPOCA ya Mwaka 2010 zitachukuliwa dhidi yao ikiwa ni pamoja na kufuta leseni zao za kutoa huduma ya utangazaji.

Vituo vilivyofungiwa ni;

1. Breeze FM ya Tanga
2. Country FM Radio ya Iringa
3. Generation FM Radio ya Mbeya
4. Hot FM Radio ya Mbeya
5. Impact FM ya Dodoma
6. Kifimbo FM Radio ya Dodoma
7. Rock FM Radio ya Mbeya
8. Iringa Municipal TV
9. Sumbawanga Municipal TV
10. Tanga City TV
11. Mbeya City Municipal TV

Mamlaka inapenda kuwakumbusha makampuni yote yaliyopewa leseni ya kutoa huduma za utangazaji wa redio na televisheni na huduma zingine zote zinazosimamiwa na Mamlaka kuhakikisha kwamba wanatimiza wajibu wao wa kisheria na masharti ya leseni ili kuondoa usumbufu usio wa lazima kwao na kwa watumiaji.

Inawezekana ikiwa kila mtu atatimiza wajibu wake.

IMETOLEWA NA

Dr. Ally Y. Simba
MKURUGENZI MKUU
20 Januari, 2016

-----------------

KUSITISHWA (KUSIMAMISHWA) KWA LESENI ZA WATOA HUDUMA ZA MAUDHUI YA UTANGAZAJI KWA KUSHINDWA KULIPIA ADA ZA LESENI 


Mnamo tarehe 15 Julai 2015 Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilitoa taarifa kwa umma kuhusu Watoa Huduma za Maudhui ya Utangazaji (Redio na Televisheni) 40 waliokuwa wanadaiwa ada mbalimbali zinazotokana na leseni zao. Aidha, tarehe 28 Septemba 2015 Mamlaka iliwapa watoa huduma hao nafasi ya mwisho ya kulipa ada wanazodaiwa ifikapo 31 Desemba 2015. Hadi tarehe 4 Januari, 2016 ni watoa huduma 11 tu kati ya 40 wamelipa ada hizo kama walivyotakiwa kufanya.

Kuendelea kwa watoa huduma kutokulipa ada za leseni ni ukiukwaji mkubwa wa masharti ya leseni chini yakifungu cha 21(g) cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (The Electronic and Postal Communications Act- EPOCA) Sura 306 ya Sheria za Tanzania. Kifungu 22(a) cha Sheria ya EPOCA, pamoja na mambo mengine kinaipa nguvu Mamlaka kusimamisha au kufuta leseni iwapo itathibitishwa kwamba mwenye leseni amekiuka kwa kiwango kikubwa masharti ya leseni kama yalivyoainishwa kwenye kifungu 21 na inapothibitishwa kwamba hakuchukua hatua kurekebisha ukiukwaji huo ndani ya siku 30 tangu apewe/apate notisi/taarifa ya ukiukwaji huo.

Kufuatia kushindwa kwa watoa huduma walioorodheshwa hapa chini kulipa ada zao za leseni, Mamlaka ya Mawasilianio Tanzania imesimamisha leseni zao na kuzitaka redio na televisheni ambazo majina yao yanaonekana hapa chini kusitisha mara moja utoaji wa huduma za utangazaji kwa miezi mitatu kuanzia tarehe 18 Januari 2016.

1. BREEZE FM
2. COUNTRY FM RADIO
3. EBONY FM RADIO
4. GENERATION FM RADIO
5. HOT FM RADIO
6. IMPACT FM
7. IRINGA MUNICIPAL TV
8. KIFIMBO FM RADIO
9. KILI FM RADIO
10. KISS FM RADIO
11. KITULO FM RADIO
12. MBEYA CITY MUNICIPAL TV
13. MUSA TELEVISION NETWORK
14. PRIDE FM RADIO
15. RADIO 5
16. RADIO FREE AFRICA
17. RADIO HURUMA
18. RADIO SENGEREMA
19. RADIO UHURU
20. ROCK FM RADIO
21. SIBUKA FM RADIO
22. STANDARD FM RADIO
23. STAR TELEVISION
24. SUMBAWANGA MUNICIPAL TV
25. TANGA CITY TV
26. TOP RADIO FM LIMITED
27. ULANGA FM RADIO

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inapenda kuwakumbusha wenye leseni wote kuhakikisha kwamba wanafuata Sheria na masharti ya leseni zao ikiwa ni pamoja na kulipa ada za leseni kwa Mamlaka kwa wakati.

IMETOLEWA NA

………………………………………….
Dr. Ally Y. Simba
MKURUGENZI MKUU

Januari, 2016

Taarifa ya kufutwa kazi Katibu Tawala mkoa wa Mwanza


Taarifa ya Kamishna kwa viongozi wa umma kuhusu Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS, SEKRETARIETI YA MAADILI YA
VIONGOZI WA UMMA

TAARIFA KWA UMMA

Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma inawafahamisha Viongozi wa Umma wanaowajibika na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya Mwaka 1995 kwamba tarehe ya mwisho wa urejeshaji wa Fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni ilikuwa ni tarehe 31 Desemba, 2015.

Hadi kufikia Disemba 31,2015 jumla ya Viongozi 11,428 tu wamerejesha matamko yao kwa Kamishna wa Maadili na Viongozi 3709 hawajatimiza wajibu huo wa kisheria na hivyo kukiuka Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya Mwaka 1995 yanayowataka viongozi kurejesha fomu hizo katika muda uliowekwa kwa mujibu wa sheria na hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mbele ya Baraza la Maadili, iwapo sababu za kuridhisha juu ya ukiukwaji huo wa sheria hazitatolewa kwa Kamishna wa Maadili.

Serikali pia imeanzisha utaratibu wa kutia saini Fomu ya Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wote na Watumishi wote wa Umma ambao wako katika mihimili mitatu (3) inayounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yaani Serikali, Bunge na Mahakama.

Viongozi wote wanaowajibika na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya Mwaka 1995 wanatakiwa kutia saini Tamko la Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma na kurejesha kwa Kamishna wa Maadili kabla ya tarehe ya mwisho ambayo ni tarehe 28 Februari, 2016. Wakuu wa Wizara, Taasisi na Idara au sehemu husika wahakikishe Viongozi waliopo sehemu zao wanatia saini katika tamko hilo.

Kwa kuzingatia Misingi ya Maadili iliyoainishwa katika Ibara ya 132 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya mwaka 1995 Viongozi wa Umma wanapaswa kuzingatia viwango vya juu vya Maadili, uzingatiaji wa maadili utakuza utu, uwazi, uadilifu, uwajibikaji, maendeleo ya nchi na kuimarisha imani ya wananchi kuhusu dhana ya Utawala Bora kwa ujumla.

Jaji (Mst.) Salome S. Kaganda
KAMISHNA WA MAADILI