Well, this much about roaches, I didn't know!

The Verge has a column where staffers post highly subjective reviews of animals. This Sunday they talk about the cockroach. Here are some interesting points...
The cockroach 
  • has lived on this Earth for more than 300 million years. It is the ultimate survivor. When a 6-mile-wide asteroid plummeted to Earth 65 million years ago, wiping out the dinosaurs and nearly all life on this world, the roach remained standing. Ice ages and continent shifts mean nothing to the cockroach. It has seen it all — and it will see what is to come.
  • can last for up to 40 days without water and a month and a half without food. 
  • can hold its breath for up to 40 minutes. 
  • can survive for up to 30 minutes submerged underwater. 
  • can handle up to 10 times more radiation than humans can withstand.
  • can live for a week or longer without its head. That's because only part of its brain resides in the head, while the rest is spread throughout the underside of its body. 
  • can go on breathing through small holes in its body like some sort of cyborg sponge. If that's not impressive enough, the severed head itself can also continue moving, waving its antennae around for hours once it has been detached. 
  • can withstand temperatures of -188 degrees Fahrenheit by creating their own antifreeze, which lowers the point at which their blood freezes — preventing ice crystals from forming in the coldblooded critter’s insides. 
  • can eat plants, garbage, the foods we eat; it even feasts on our skin cells and fecal matter. 
You can read the whole article here.

Za kuchaji za mwana ama za mshua?


Job: Health Management Information Systems Advisor

Organization: International Center for AIDS Care and Treatment Programs
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 26 Feb 2016

Job: Health Systems Strengthening Advisor

Organization: International Center for AIDS Care and Treatment Programs
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 26 Feb 2016

Job: Senior Global Fund Grant Advisor to the National TB Program-Tanzania

Organization: International Union Against Tuberculosis and Lung Disease
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 11 Feb 2016

Acha ushabiki maandazi


Rungwe apinga upekee wa mazungumzo ya CUF na CCM kuhusu uchaguzi Zanzibar

Aliyekuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya CHAUMMA, Hashim Rungwe amesema kuwa chama chake hakikubaliani na mazungumzo yeyote ya kutafuta suluhu ya Uchaguzi Mkuu Visiwani Zanzibar baina ya mgombea urais kupitia CUF, Maalim Seif Sharrif Hammad na Dk Ali Mohamed Shein wa CCM.

Pamoja na kutokubaliana na azma ya kurudiwa kwa uchaguzi visiwani humo, Rungwe amesema mazungumzo hayo hayakubaliki kwasababu hayajashirikisha wagombea kutoka vyama vingine.

Katika uchaguzi huo uliofutwa, CHAUMMA kilimsimamisha mgombea urais, Mohammed Masoud ambaye pia amepinga vikali Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha kufuta uchaguzi huo na kuitaka tume hiyo kutumia uwezo wake kuzitatua changamoto na kasoro zilizojitokeza kabla ya kufikia hatua hiyo.

Rungwe pia amekemea na kulaani vitendo vya kibaguzi vilivyooneshwa katika sherehe za Mapinduzi Zanzibar siku ya tarehe 12, Januari.

Taarifa ya serikali ya hatua zilizochukuliwa dhidi ya Stanbic Bank (T) Ltd

Waziri Dkt Philip Mpango (katikati) akitoa tamko kwa waandishi wa habari (hawamo pichani) jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Servicius Likwelile na kushoto kwake ni Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Bw. Lila Mkila.

HATUA AMBAZO ZIMECHUKULIWA DHIDI YA STANBIC BANK TANZANIA LIMITED KUHUSU USHIRIKI WAKE KUWEZESHA MKOPO WA SERIKALI WA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 600 


Utangulizi

Mwezi Julai 2013, Benki Kuu ya Tanzania kupitia ufuatiliaji wa kawaida wa shughuli za mabenki iligundua matatizo yaliyohusiana na hasara itokanayo na mikopo na pia kuacha na kuondolewa kazini kwa viongozi waandamizi wa Stanbic Bank Tanzania Limited (Stanbic) katika muda mfupi. Kutokana na hilo, Benki Kuu iliamua kufanya ukaguzi wa kulenga (Targeted Examination) katika benki hiyo. Ukaguzi huo ni kwa mujibu wa mamlaka iliyopewa Benki Kuu chini ya Kifungu 47 cha Sheria ya Benki Kuu ya mwaka 2006 na Kifungu 31 cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006.

Matokeo ya Ukaguzi wa Benki Kuu

Katika ukaguzi huo, wakaguzi wa Benki Kuu, pamoja na mambo mengine walibaini miamala ya kutia shaka iliyohusu malipo kwa kampuni ya kitanzania ya Enterprise Growth Market Advisors (EGMA). Kampuni ya EGMA ilihusika katika uwezeshaji wa upatikanaji wa Mkopo kwa Serikali ya Tanzania ambapo Standard Bank Plc (ambayo kwa sasa inajulikana kama ICBC Standard Bank) na Stanbic Bank Tanzania Limited kwa pamoja walikuwa “Mwezeshaji Mkuu” (Lead Arranger). Malipo hayo kwa kampuni ya EGMA yalikuwa yamefanyika kinyume na taratibu za kibenki na yalihusisha uongozi wa benki ya Stanbic. Jumla ya malipo yalikuwa ni kiasi cha dola za kimarekani milioni 6, na zililipwa katika akaunti ya EGMA na kutolewa kwa muda mfupi kwa njia ya fedha taslimu (cash) ambayo ni nje ya taratibu za kibenki.

Taarifa ya ukaguzi huo iliwasilishwa kwa benki ya Stanbic kwa mujibu wa taratibu, na Benki Kuu iliiagiza Bodi ya Wakurugenzi ya benki hiyo kuchukua hatua stahiki za kurekebisha kasoro zilizoonekana. Aidha, benki ya Stanbic iliagizwa kutoa taarifa kwa Kitengo cha Financial Intelligence Unit (FIU) kilichopo Wizara ya Fedha na Mipango kuhusiana na miamala hiyo yenye mashaka katika akaunti ya EGMA kama Sheria ya Kuzuia Utakatishaji wa Fedha Haramu ya mwaka 2006 (The Anti-Money Laundering Act, 2006) inavyoelekeza. Benki ya Stanbic ilitekeleza maagizo na kutoa taarifa FIU kuhusu miamala inayotiliwa shaka.

Mnamo 29 Septemba 2015, Benki Kuu ilipokea barua toka Idara ya Serikali ya Uingereza inayohusika na Upelelezi wa Makosa ya Kugushi na Rushwa (Serious Fraud Office - SFO) ikiiomba Benki Kuu ruhusa ya kutumia ripoti yake ya ukaguzi kama ushahidi katika kesi dhidi ya Standard Bank Plc ambayo ilikuwa ni mshirika wa Stanbic Bank Tanzania Limited katika kuwezesha mkopo wa dola za kimarekani milioni 600 kwa Serikali na kwamba ripoti hiyo ingekuwa wazi kwa umma. Benki Kuu iliijibu SFO kuwa kwa mujibu wa Sheria ripoti za Benki Kuu zinatolewa tu kwa benki au taasisi ya fedha inayohusika, hata hivyo, Benki Kuu haikuwa na pingamizi kwa SFO kutumia taarifa za ripoti hiyo kwa kuzingatia chanzo cha ripoti hiyo.

Hatimaye, Standard Bank Plc ilikubali makosa na ilitozwa faini ya jumla ya dola za kimarekani milioni 32.20, ambapo kiasi cha dola za kimarekani milioni 7 zinalipwa kwa Serikali ya Tanzania (dola za kimarekani milioni 6 zilikuwa ni fidia na dola za kimarekani milioni 1 ni riba).

Kwa kuzingatia mapungufu ya kufanya miamala iliyohusisha EGMA na pia kutokuweka taratibu madhubuti za udhibiti wa ndani, na kwa kuzingatia Kifungu 67 cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, Benki Kuu imeiandikia benki ya Stanbic barua ya kusudio la kuitoza faini ya shilingi bilioni 3. Sheria inaitaka benki ya Stanbic kutoa utetezi katika kipindi cha siku ishirini (20) ambacho kitaisha tarehe 30 Januari 2016. Endapo Benki Kuu haitaridhika na utetezi, benki ya Stanbic italazimika kulipa faini hiyo.

Hitimisho

Benki Kuu imechukua hatua hizo kama onyo kwa benki ya Stanbic na ili iweze kuwa makini katika kuhakikisha kuwa shughuli zake zinaendeshwa kwa mujibu wa taratibu za kibenki na kuzingatia Sheria.

Aidha, hatua hii ni onyo kwa mabenki na taasisi za fedha zisijihusishe na makosa ya aina hii ambayo ni kinyume cha taratibu za kibenki na ni uvunjaji wa Sheria za nchi. Hatua kali zitaendelea kuchukuliwa kwa benki au taasisi ya fedha yoyote itakayobainika kwenda kinyume na taratibu za kibenki na Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006.

...................................................................................................Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Philip Mpango (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawamo pichani)jijini Dar es Salaam, kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali dhidi ya Benki ya Stanbic Tanzania kutokana na ushiriki wake katika kuwezesha mkopo wa Serikali wa Dola za Kimarekani Milioni 600 na Kulia kwake ni Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania(BOT) Bw. Lila Mkila.

Maelezo ya hatua ya serikali kulifuta gazeti la MAWIO