Waziri Ndalichako aagiza kuondolewa mfumo wa GPA na kurudishwa Divisheni


WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, amefuta mfumo wa uwekaji matokeo wa ‘Grade Point Average (GPA) ulioanza kutumiwa na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) mwaka 2014.

Mfumo huo uliofuta mfumo uliokuwapo wa Divisheni, ulianza kutumika kwa kidato cha nne na sita na vyuo vya ualimu.

Inaelezwa kuwa mfumo huo ulianzishwa kujaribu kupandisha ufaulu baada ya kuonekana wanafunzi wengi walishindwa mitihani ya kidato cha nne, hasa mwaka 2013.

Mfumo huo ulilalamikiwa na wadau wa elimu waliodai kuwa ulikuwa unashusha kiwango cha elimu na kuwachanganya wanafunzi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dodoma jana, Profesa Ndalichako, ambaye aliwahi kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), alisema baraza hilo limeshindwa kueleza sababu za kutumia mfumo huo badala yake limeishia kutoa utaratibu uliotumika tu.

“Kwa mamlaka niliyonayo chini ya kifungu cha 20 cha Sheria ya Baraza la Mitihani Tanzania, sura ya 107, naliagiza Baraza kufanya mapitio ya mfumo unaotumika sasa wa wastani wa alama (GPA) kwa lengo la kurudi kwenye mfumo wa awali wa Divisheni.

“Viwango vya ufaulu vizingatie azma ya nchi kuelekea kwenye uchumi wa kati na Tanzania ya viwanda,” alisema Profesa Ndalichako.

Kuhusu mtihani wa pili (Paper two), aliitaka NECTA kuufuta kwa watahiniwa wa kujitegemea.

Mtihani huo ulianzishwa kama alama ya maendeleo wakati ni mtihani wa mwisho.“Wizara haiwezi kufikia azma ya kusimamia ubora wa elimu katika ngazi zote bila kuhakikisha viwango vya ufaulu vinawezesha kutoa wataalamu wenye stadi na maarifa badala ya kuwa na wahitimu wengi wenye vyeti lakini hawakidhi mahitaji ya soko la ajira,” alisema Profesa Ndalichako.

Januari 7 mwaka huu, Waziri Ndalichako alitembelea Necta na kuitaka itoe ufafanuzi wa kuacha kutumia mfumo wa divisheni na kutumia GPA.

Pia aliitaka itoe maelezo ya kuanzishwa kwa mtihani wa pili kwa watahiniwa wa kujitegemea.

Hata hivyo alisema jana kuwa maelezo yaliyotolewa yalikuwa yamejikita katika kueleza utaratibu badala ya sababu za kuutumia mfumo huo.

“Taarifa imebainisha kuwa uanzishwaji wa mfumo wa GPA ulitokana na maoni ya wadau bila kuwataja wadau husika na kueleza sababu walizotoa.

“Taarifa ya utafiti uliofanywea na Wizara ya Elimu haijataja idadi ya wadau waliojaza madodoso na wala haionyeshi mikutano ya kupata maoni ya wadau ilihusisha watu gani, ilifanyika wapi na lini,” alisema Profesa Ndalichako.

Kuhusu sababu kuwa NECTA ilipata maelekezo kutoka wa Wizara ya Elimu mwaka 2014, Profesa Ndalichako, alisema uchambuzi unaonyesha kuwa wizara ilikuwa imeelekeza baraza la mitihani liandae mfumo huo na kuuwasilisha kwa Kamishna wa Elimu upate kibali cha Serikali kabla ya kuanza kutumika.

“Hata hivyo, jambo hilo halikufanyika na badala yake Baraza hilo likaanza kutumia mfumo huo mwaka 2014. Nyaraka zilizowasilishwa hazionyeshi kama mapendekezo ya mfumo huo yaliwasilishwa kwa Kamishna wa Elimu,” alisema.

Alisema Baraza lilieleza faida ya kutumia GPA kuwa ni kueleweka kwake kwa urahisi na wadau jambo ambalo linapingana na maoni ya wadau yanayojitokeza kwenye vyombo vya habari, huku likishindwa kueleza udhaifu wa mfumo wa Divisheni.

“NECTA wameeleza kuwa mfumo wa GPA umerahisisha udahili wa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu (Collective Admission System- CAS) jambo ambalo si sahihi.

“Mfumo wa CAS ulianza kutumika Aprili 2010 wakati mfumo wa GPA ulianza kutumika mwaka 2014. Isitoshe huzingatia masomo mawili ya fani anayotarajia kusoma mwanafunzi siyo ufaulu wa jumla,” alisema.

Waziri alisema mfumo wa GPA ulikuwa bado kwenye majaribio hivyo haukupaswa kutumika kufanyia majaribio kwenye maisha ya watu.

Kuhusu sababu ya kuongeza mtihani wa pili kwa watahiniwa wa kujitegemea kama mbadala wa upimaji endelevu, alisema maelezo ya NECTA kuwa mtihani huo ni mbadala wa upimaji endelevu hayatekelezeki.

“Kitaalamu ‘paper two’ haiwezi kuwa alama ya maendeleo ya kila siku kwa kuwa inafanyika sambamba na mitihani mingine ya mwisho,” alisema Profesa Ndalichako.

Kwa sababu hiyo, Profesa Ndalichako, alisema kitendo cha baraza hilo kuingiza mfumo huo wa GPA katika marekebisho ya kanuni zake yaliyosainiwa na Waziri Oktoba 28 mwaka jana na kuchapishwa Novemba 6 mwaka jana kwenye gazeti la Serikali, ni kuonyesha kuwa mfumo huo ulianza kutumika bila kukamilika matakwa ya sheria.

“Mfumo wa GPA ulianza kutumika mwaka mmoja kabla haujaingizwa kwenye kanuni za mitihani,” alisema.

Akizungumzia hasara ya mfumo huo, Waziri Ndalichako alisema baadhi ya watahiniwa waliofaulu mitihani wanaonyesha kiwango kidogo cha maarifa kuliko kiwango cha ufaulu.

Alisema kuwapo daraja E kwenye alama za ufaulu wakati haihesabiki katika upangaji wa GPA kunawafanya watahiniwa waliopata E zote kwenye mitihani kujiona wako bora kuliko wenye D mbili na F zote, ambaye anahesabika kuwa amefaulu mtihani.

“Uwepo wa pointi za mfiko kwenye madaraja ya ufaulu kwa ngazi mbalimbali za elimu kunaleta mkanganyiko kwani inakuwa vigumu kueleza tafsiri ya madaraja hayo. Kwa mfano ‘Distinction’ ya kidato cha nne inaanza pointi 3.6 wakati ya ualimu inaanzia pointi 4.4,” alisema Waziri Ndalichako.

Pamoja na hatua hiyo aliyochukua, Profesa Ndalichako alisema bado Serikali haijaamua kuwachukualia hatua viongozi wa NECTA.

TAMONGSCO WAPONGEZA

Wakati huohuo, Chama cha Wamiliki wa Vyuo na Shule binafsi Tanzania (TAMONGSCO) kimepongeza hatua ya Profesa Ndalichako kufuta mfumo huo na kurejesha ule wa zamani wa Divisheni.

Katibu Mkuu wa Shrikisho hilo, Benjamin Nkonya aliliambia MTANZANIA jana kwamba mfumo wa GPA ulishusha madaraja ya ufaulu na kusaidia kusindikiza wanafunzi wengi zaidi kushindwa mitihani.

“Mfumo wa GPA ulikuwa mpango wa siasa, serikali iliona haijawekeza katika shule zake kwa kuweka maabara bora, kulipa vizuri walimu, kuweka mazingira mazuri hivyo kuchangia wanafunzi kufeli.

“Hivyo waliona wawadanganye wazazi kwa kuwaletea mfumo wasioujua huku wakitukwepa kutushirikisha wadau tukiwamo sisi.

“TAMONGSCO tunampongeza sana Waziri, Ndalichako na tunamshauri aweke mifumo endelevu ya kuzuia udhaifu wa aina hiyo kuingizwa katika sekta ya elimu katika siku za baadaye,” alisema Nkonya.
 • via Mtanzania

Salam za rambirambi za Rais Magufuli kwa msiba wa Asha Bakari Makame
Katuni: Taswira inayovutwa kuhusu kitakachotokea Bungeni...


Wanasiasa, Mawaziri walivyoifanya elimu kuwa kama "kinyozi na kichwa cha mang'aa"

Tamko la Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, kuhoji mabadiliko ya mfumo wa kupanga madaraja ya ufaulu kutoka ule wa madaraja kwenda GPA, umezua minong’ono kutoka kwa wadau wa elimu.

Akizungumza na watendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) hivi karibuni, Profesa Ndalichako alitoa siku saba kwa uongozi kumpa sababu za mabadiliko hayo, huku akisema mfumo huo mpya umekuwa ukilalalamikiwa na watu wengi hasa wanafunzi na wazazi.

Tusingependa kuchukua upande wala kutoa uamuzi kwa kuwa hili ni suala la kitaalamu zaidi, isipokuwa tuna wasiwasi na mustakabali wa sekta ya elimu. Ni ukweli usio na chembe yoyote ya shaka kuwa kama kuna eneo ambalo wanasiasa wamekuwa wakilichezea, hili la sekta ya elimu linaongoza.

Kwa miaka mingi sasa, sekta hii imekuwa ikivurugwa na wanasiasa hasa mawaziri. Ukweli ni kuwa kila anayechaguliwa kuongoza wizara ya elimu huja na mambo yake, kitendo kinachosababisha tuamini pengine wizara hii pamoja na unyeti wake, imekosa dira na dhima thabiti.

Wengi kwa mfano, tunakumbuka namna sekta ya elimu ilivyovurugwa kwa kiasi kikubwa miaka ya mwishoni mwa utawala wa Serikali ya Awamu ya Tatu.

Aliyekuwa Waziri wa Elimu na Utamaduni, Joseph Mungai alifikia hatua ya kuunganisha masomo ya Fizikia na Kemia na kuwa somo moja.

Hakuishia hapo, Waziri huyo akaagiza kufutwa kwa michepuo ya biashara, kilimo na ufundi kwa hoja kuwa wanafunzi walikuwa wakisoma masomo hayo mapema kabla ya kupata elimu ya msingi kwa kiwango cha kutosha.

Mara tu baada ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne kuingia madarakani, aliyekuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Magreth Sitta akaweka kando mipango ya Mungai na kurudisha tena mitalaa iliyofutwa.

Ndiyo maana haishangazi kuona leo Profesa Ndalichako akihoji matumizi ya mfumo wa GPA uliopewa baraka zote na mtangulizi wake, Dk Shukuru Kawambwa. Na kwa uzoefu wa mambo ulivyo katika wizara hii, uko uwezekano mkubwa kuwa mfumo mpya wa GPA hauna siku nyingi za kuishi kabla ya kuwekwa kando na uongozi mpya wa wizara.

Tunaamini kuna tatizo katika uendeshaji wa wizara hii muhimu kwa Taifa, kwani ukiondoa ‘vurugu’ za mawaziri, vyombo vinavyosimamia elimu navyo havijasalimika licha ya kuwa na watendaji wenye weledi mkubwa wa elimu. Vyombo hivi vimekuwa vikifanya madudu, hatua inayotupa wasiwasi kuhusu umakini wa watendaji wake.

Kwa mfano, mabadiliko ya mara kwa mara ya mitalaa inayosimamiwa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), upitishwaji wa vitabu visivyo na sifa uliofanywa na iliyokuwa Kamati ya Ithibati ya Vifaa vya Elimu (EMAC), ni miongoni mwa mambo yanayooyesha kuwapo kwa udhaifu mkubwa katika usimamizi wa sekta ya elimu nchini.

Tunawakumbusha watendaji wenye dhamana ya kusimamia elimu na Serikali kwa jumla kuipa sekta ya elimu nafasi yake inayostahiki katika maendeleo ya nchi. Itoshe sasa sekta ya elimu kuwa uwanja wa majaribio wa mifumo inayobuniwa na kudumu kwa muda mfupi.

Hatuwezi kuendelea hasa katika dunia ya sasa ya ushindani wa kielimu kama hatutokuwa na mipango madhubuti na endelevu ambayo kila anayepewa nafasi ya kusimamia elimu, atajivunia kuisimamia kwa nguvu zote.

Wenye mahoteli wazungumzia "ukame" ulioletwa na agizo la Rais MagufuliHatua ya serikali ya awamu ya tano ya kubana matumizi kwa kuzuia wizara, taasisi na mashirika ya umma kukutana katika hoteli kwa shughuli mbalimbali za kikazi, imeanza kuleta athari chungu huku baadhi ya wamiliki wa hoteli wakisema wameathirika kimapato na sasa wako mbioni kupunguza wafanyakazi.

Kadhalika, baadhi ya wasomi wamesema licha ya dhamira nzuri ya serikali katika kuhakikisha inabana matumizi ili fedha zitakazopatikana zielekezwe katika miradi ya maendeleo, bado kuna haja ya kuangalia kwa umakini athari zake. Pia wameonya kuwa sekta ya hoteli ikiyumba itaathiri wajasiriamali wengi na sekta binafsi kwa ujumla.

Baada ya kuapishwa na kuingia madarakani Novemba 5, mwaka jana, Rais Dk. John Magufuli ilitangaza hatua kadhaa za kubana matumizi yasiyo ya lazima ili kuipa nguvu ya kuwatumikia wananchi.

Miongoni mwa hatua zilizochukuliwa ni ni kupiga marufuku vikao vya kazi vya taasisi na mashirika ya umma kufanyika hotelini, kufanyika kwa hafla za kupongezana, kuadhimisha wiki mbalimbali zikiwamo za maji na Siku ya Ukimwi, warsha, semina, makongamano, mikutano na mafunzo.

Zingine ambazo sasa zinaelezwa kuathiri baadhi ya wajasiriamali na sekta binafsi ni pamoja na kufutwa kwa sherehe mbalimbali ikiwamo ya Uhuru, maadhimisho ya kitaifa na kimataifa yaliyokuwa yakiwalazimu wageni mbalimbali kutoka nje ya nchi kutua Tanzania au kusafiri kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili, umebaini kuwa tangu kutolewa kwa agizo la serikali kuzuia hafla, vikao na shughuli za serikali kwenye kumbi za hoteli, karibu hoteli zote hazijapata mikutano wala shughuli yoyote kutoka kweye taasisi za umma, mashirika wala wizara.

CHAMA CHA WENYE HOTELI

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wamiliki wa Hoteli Tanzania (HAT), Latifa Sykes, alisema sekta ya hoteli ni moja ya maeneo yanayoajiri watu wengi kwa sababu ya kuangalia wageni na kushughulikia matukio mbalimbali, ikiwamo mikutano.

“Kitu kitakachotokea na ambacho kwa sasa kinatokea ni kwamba hoteli za mjini ambazo zilikuwa zikipokea mikutano mingi, sasa zitapunguza wafanyakazi,” alisema.

Alisema mbali na kupunguzwa kwa watu na pato la hoteli hizo kupungua, kutaathiri pia serikali kwa sababu ilikuwa ikipata kodi mbalimbali ikiwa ni pamoja na ile ya ongezeko la thamani (VAT).

“Lazima tuwe makini na tujue kila hatua ina matokeo yake. Kwenye hii ya kupunguza mikutano, matokeo yake ni kupungua kwa mapato yaliyokuwa yalipwe serikalini na hakuna tena sababu ya kuwa na wafanyakazi wengi.

“Tunamuunga mkono Rais kwenye kubana matumizi mabaya ya serikali lakini ni vyema akaangalia hatua za utekelezaji zisiathiri uchumi na biashara zinazosaidia ukusanyaji wa kodi,” alisema.

HALI HALISI

Ofisa Mauzo wa hoteli ya Hyatt Regency (zamani Kilimanjaro Kempinsk), Godlove Mlaki, aliiambia Nipashe kuwa agizo la Rais Magufuli halijawaathiri sana kwa sababu hawategemei mikutano pekee ya serikali na taasisi zake kwa kuwa hoteli yao ni ya hadhi ya kimataifa.

Alisema athari ya moja kwa moja waliyopata kutokana na uamuzi wa serikali ni kukosa wateja ambao kwa kawaida huwapata wakati wa maadhimisho ya siku ya Uhuru, Desemba 9 ya kila mwaka.

Wakati wa sherehe za kitaifa, ikiwamo Uhuru, wageni mbalimbali ambao hualikwa kutoka nje ya nchi wakiwamo na marais na wafanyabishara, hufika kwa wingi nchini na kusaidia kuingiza fedha za kigeni kutokana na kulala kwenye hoteli na huduma zingine wanazohitaji katika siku zote wanazokuwapo nchini.

Mlaki alisema kutofanyika kwa sherehe za Uhuru kuliwakosesha fedha nyingi kwa sababu awali hoteli yao ilikuwa ikipokea wageni kutoka nje waliokuwa wakialikwa kuhudhuria sherehe hizo.

Alisema hoteli hiyo yenye kumbi 10 za mikutano, wateja wake wakubwa walikuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, na wastani wa mikutano waliyokuwa wakifanya kwa mwezi ilikuwa ikifikia 19.

Alisema kuna wakati walikuwa wakipata mikutano ya siku mbili hadi sita mfululizo kutoka serikalini.

“Toka mwaka jana Desemba hadi Januari hatujapata (kuandaa) mikutano yoyote kutoka serikalini,” alisema Mlaki.

Mmoja wa wafanyakazi wa hoteli hiyo, alisema mbali na wateja wananaotaka kumbi za mikutano, hata baadhi ya maaofisa wa serikali waliokuwa wakifika hapo ili kupata kifungua kinywa na chakula cha mchana, siku hizi hawapo tena.

Akifafanua juu ya ugeni wa marais waliokuwa wakifika kuhudhuria shehere za kitaifa, alisema: “Wakija marais wawili tu kwa mfano, ukiweka na walinzi wao, utakuta umeshafanya biashara ya zaidi ya vyumba 30, hapo hujaweka chakula na vinywaji. Kwa hiyo ile ni biashara kubwa sana kwetu,” alisema.

Katika hoteli ya Bahari Beach, Meneja anayehusika na kukodisha kumbi, Robert Vitus, alisema wameathirika kwa kiasi kikubwa kwa kuwa tangu kutolewa agizo la kuzuiwa kwa vikao na mikutano hotelini, hawajawahi kupata wateja kutoka serikalini.

Alisema hivi sasa wateja wanaowapata zaidi ni wale wanaotoka katika taasisi na kampuni binafsi pekee.

"Kwa ujumla, siku zote wateja wetu wakuu ni wale wanaotoka katika taasisi binafsi na wengine kutoka nje ya nchi. Watu wa serikalini kwa kiasi fulani walikuwa wateja wetu, japo si kama ilivyo kwa hawa wengine. Hivi sasa, hata hao asilimia ndogo ya wateja kutoka serikalini hatuwapati tena," aliongeza.

Meneja Masoko wa Hoteli ya Blue Pearl iliyoko Ubungo, Abdul Sheikh, alisema kutokana na serikali kuacha kufanya mikutano kwenye hoteli yao, baadhi ya wafanyakazi wamekosa kazi za kufanya.

“Yaani hakuna kabisa biashara siku hizi kulinganisha na ilivyokuwa awali ambapo kumbi zote zilikuwa zinajaa. Sasa hivi ni kama ulivyotukuta, hakuna kazi, kuanzia asubuhi hadi jioni, ni hivi hivi tu tunakaa” alisema Sheikh.

WASOMI WANENA 

Mtafiti wa Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Haji Semboja, alisema ingawa hoteli kadhaa zitakuwa zimeingia katika msukosuko wa kiuchumi, bado kuna haja kwa serikali kuangalia ushirikiano mkubwa wa maendeleo baina ya sekta binafsi na ya umma katika kukuza pato la nchi.

Alisema kadri anavyoona, agizo la Rais Magufuli, moja kwa moja halikulenga kusitisha mikutano mikubwa yenye idadi ya watu zaidi ya 200 hadi 500, bali ile midogo ambayo haikuwa na ulazima wa kufanyika katika kumbi za hoteli kwa lengo la kuokoa rasilimali fedha ambayo inaweza kufanya jambo mbadala.

“Kuyumba kiuchumi kwa hoteli hizo huenda kumechangiwa na uelewa mdogo wa tabia za Waswahili, ambao wanajumuisha kila kitu na kusababisha hofu iliyochangia kuyumba kiuchumi kwa sekta binafsi ambayo ni miongoni mwa mihimili muhimu ya serikali hasa katika uchangiaji wa uchumi wa ndani,” alisema.

Mkurugenzi wa Sera wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI), Hussein Kamote, alisema katika nchi yoyote serikali ni muhimili wa kwanza wa ununuzi wa bidhaa na huduma, hivyo inavyobana sana matumizi yake itasababisha kuathirika kwa sekta mbalimbali na kusababisha uchumi mkuu kushindwa kukua.

“Kubana bajeti ni jambo la kawaida, ila ibane na kuachia ili kutoa ushirikiano mzuri kwa sababu inaweza kusababisha madhara kwa sekta iliyodhamiria kuibana. Tunajua inaweza kubana na fedha zile zikatumika katika sekta nyingine kama elimu au afya,” alisema Kamote.

Alisema ni vigumu hoteli nyingi kumudu kujiendesha bila kupata mteja muhimu ambaye ni serikali, hasa kwa sababu serikali imeanza kwenye eneo linalogusa sekta ya utalii ambayo ni kitovu kikubwa cha uchumi.

Alisema huenda ajira nyingi kwa wafanyakazi wa hoteli zikapungua huku wengi wasijue la kufanya na kujikuta wakiangukia katika kundi la wazururaji au shughuli haramu kama za utapeli.

IKULU YAFUNGUKA

Kaimu Mkurugenzi, Kurugenzi ya Mawasiliano Ofisi ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, alisema kuyumba kiuchumi kwa hoteli nchini kutokana na agizo la Rais Magufuli si kazi ya serikali na wala agizo hilo haliwezi kubadilishwa.

Alisema Rais Magufuli alitoa agizo hilo kwa dhumuni la kupunguza matumizi yasiyo ya lazima kwa serikali na kuwataka Watanzania wote wapenda maendeleo wamuunge mkono katika suala hilo.

“Wizara zilikuwa zinatumia pesa nyingi sana kukodi kumbi kwa saa kadhaa wakati kuna kumbi katika wizara zao. Sasa kuyumba kiuchumi au kukosa wateja katika hoteli hiyo si kazi ya Ikulu,” alisema Msigwa.

Alisema hoteli zinapaswa kuwa wabunifu wa kupata fedha zaidi na si kutegemea wizara au taasisi kwenda kufanya mikutano katika hoteli zao.

Taarifa: Maswi ateuliwa Katibu Twala - Manyara; Makamishna: Mkuu Uhamiaji na Utawala Fedha wasimamishwaRais Magufuli aonesha uwezo wake katika fani ya ushoni


Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akionesha umahiri wake wa kutumia cherahani na kushona nguo za wafanyakazi wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kuvifahamu vitengo mbalimbali vya Ikulu jijini Dar es Salaam Januari 20, 2016


Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiendelea kushona kwa ustadi


Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akimalizia moja ya nguo za wafanyakazi wa Ikulu.

Picha: Ikulu

Tamko la Jukwaa la Wahariri kuhusu kufutwa kwa gazeti la MAWIO


Statement by Palestine Information Centre (Tanzania) regarding graffiti on Jerusalem church


مركز المعلومات الفلسطيني- تنزانيا
Palestine Information Centre (Tanzania)
Kituo cha Habari cha Palestina (Tanzania)
Press Release
 19 January 2016
------------------------------------------------------------------------------------------
Israeli settlers scrawl hate graffiti on Jerusalem church 

The Ambassador of the State of Palestine in Dar es Salaam condemns the latest vandalism act of spraying racist graffiti on the walls of the Dormition Monastery in occupied East Jerusalem carried out by extremist Israeli settlers last Sunday 17 January 2016 

H.E. Mr. Hazem Shabat, blamed the graffiti vandalism on the ongoing incitement campaigns carried out by Israeli settler leaders, in which they blatantly called for attack against places of worship and slaughtering Christians. 

The Ambassador also considered the recent attacks as a clear statement by Israeli settlers in response to the agreement between the Holy See and the State of Palestine that came into full force on Saturday 2 January, 2016. 

“The new attacks targeting Christian Churches represent an additional chapter in the long record of Israeli crimes and violations against the entire Palestinian people indiscriminately” he added. 

The attack comes only three weeks after a similar attack that was conducted by settlers against the Salesian Monastery in Beit Jamal. 

The Benedictine abbey is a popular site for pilgrims and tourists. It has been damaged several times in recent years. 

This latest act of vandalism took place against Christians in Jerusalem, as the racist graffiti was sprayed in the Hebrew language on the walls and doors of the monastery. 

The latest graffiti contained not only shameful insults against Jesus, but also called for slaughtering Christians and sending them to hell. 

This position was echoed by Wadie Abu Nassar, a senior advisor to the Catholic Church who said the doors of the Dormition Abbey church were vandalized with threats scrawled in Hebrew that read: "Kill the Christians, the enemy of Israel" and "The revenge is coming very soon," as well as "Send Christians to hell.”

Dormition Abbey dates back to the 5th century, and is thought to be the place where the Virgin Mary died. The abbey is owned by the German Benedictine Order and is considered to be one of the three earliest churches built in Jerusalem. 

Ambassador Shabat noted that this was one of the numerous attacks against the church in the occupied Palestine. In February 2015, for example, Jewish Settlers set fire to a religious school affiliated with Jerusalem's Greek Orthodox Church, which they sprayed with anti-Christian graffiti. 

This was denounced by the Patriarch of the Holy City of Jerusalem and all Palestine, Theophilos III, condemning what he called "repeated" attacks on Christian and Muslim places of worship in the Palestinian territories by extremist Jewish settlers. 

"The targeting of churches and mosques is caused by pervasive racism and hatred," he said. 

The latest incident is thus not the first Israeli attack against Dormition Abbey. Other many similar incidents have previously taken place against Christian sites, including churches, monasteries, and cemeteries. These incidents coincided with calls made by Jewish settler organizations to expel Christians from Jerusalem and to burn churches. The criminal acts by settlers take place under the slogan "price tag," a term used by Israeli extremists to mark nationalist-motivated hate crimes. 

Israeli settlers have carried out at least 221 attacks on Palestinians and their property in occupied East Jerusalem and the West Bank in 2015, according to the UN Office for the Coordination of Humanitarian Affairs. 

_____________________________________________________________________________

Contact us:  P.O Box 20307, 612 UN Road – Upanga West, Dar es Salaam Tel: 2152813, 2150643 Fax: 2153257 Email: [email protected]Website: www.pal-tz.org

Kauli ya Serikali kuhusu taarifa potofu zinazosambazwa kupitia mitandao ya kijamiiKaimu Mkurugenzi wa idara ya Habari MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa akitoa ufafanuzi juu ya taarifa za uzushi unaosambazwa katika mitandao ya Kijamii ya ndani na nje ya nchi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimwa Dkt. John Pombe Magufuli amefukuza wageni kutoka nje waliokuwa wanafanya biashara hapa nchini kwa kuwa Serikali yake haitataki wageni wafanye bishara zao nchini ambapo ukweli ni kwamba Serikali haijafukuza wageni wanaofanya biashara zao nchini na haina mpango wa kufanya hivyo kwa wageni wanaoishi nchini kwa vibali vilivyotolewa kisheria na Serikali.kushoto ni Naibu Kamishna na Msemaji wa Idara ya Uhamiaji Bw. Abbas Irovya na mwisho kushoto ni Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani Isaac Nantanga,Kulia ni Naibu Kamishna wa Idara hiyo Bw.Wilson Bambaganya.

Naibu Kamishna na Msemaji wa Idara ya Uhamiaji Bw. Abbas Irovya akitoa wito kwa Watanzania kuwafichua wale wote wanaoingia na kuishi nchini kinyume cha sheria ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwa mujibu wa Sheria na kanuni na kusisitiza kuwa Ofisi yake itaendelea kufanya oparesheni ya kuwakamata watu hao, kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa idara ya Habari MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa na Mwisho Naibu Kamishna wa Idara hiyo Bw.Wilson Bambaganya.

Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano Idara ya Habari Maelezo kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji ukilenga kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa za upotoshaji zinasozambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Serikali imewafukuza wafanyabiashara wakigeni wanaofanya kazi zao hapa nchini ,taarifa hizo si za kweli na zinalenga kuichafua Serikali ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.Picha na Frank Mvungi-Maelezo

Waraka wa Tiba Asilia wa mambo 5 wanayoafiki, 6 wasiyoafiki na 7 yatekelezwe

TAMKO LA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA (SHIVYATIATA) KUHUSU MAELEZO YA WAZIRI WA AFYA ALIYOYATOA TAREHE 15/01/2016, JUU YA TIBA ASILI NATIBA MBADALA.


Ndugu waandishi wa Habari na ndugu wananchi, shirikisho la vyama vya Tiba Asili Tanzania (shivyatiata) ni chombo kinachosimamia vyama vyote vya Tiba Asili hapa Nchini pamoja na Waganga wote wa Tiba Asili na pia ndiyo msemaji wao kwa Serikali, Mashirika ya Kitaifa na Kimataifa na kuhakikisha chombo hiki kinasimamia na kulinda maslahi yote ya Waganga wa Tiba Asili hapa nchini

Hivyo basi ,kutokana na maelezo yaliyotolewa na Waziri mwenye dhamana na mambo ya Afya mnamo hiyo tarehe 15/01/2016 shirikisho kwa kutambua dhamana tuliyonayo mbele ya Umma wa Waganga tunapenda kuwasilisha tamko letu kwenu nyinyi waandishi wa Habari na wanchi kwa ujumla ili muweze kuelewa yanayoendelea katika Tiba Asili hapa nchini.

Ndugu waandishi wa Habari, kwanza mtakumbuka kuwa mnamo tarehe 14/12/2015 Naibu waziri wa Afya maendeleo ya Jamii, jinsia, wazee na watoto Mhe. Dkt HAMISI KIGWANGALA (MB) alifanya ziara katika kituo cha Tiba Mbadala cha Tabibu anayejulikana kwa jina la Dr MWAKA. Baada ya ziara hiyo mengi yalizungumzwa na hata tamko la Wizara lililotolewa terehe 24/12/2015 lililohusu Tiba Asili na Tiba Mbadala kwa upande mmoja nalo lilichangia kuwepo kwa malumbano ya hapa na pale kutoka kwa watoa huduma wa Tiba Asili na Tiba Mbadala, na wengine wakafikia hatua ya kupinga agizo hilo na kuitisha mgomo.

Ndugu waandishi wa Habari tunapenda mfahamu kuwa Wizara ya Afya katika kufikia kutoa tamko hilo la tarehe 24/12/2015 hawakushirikisha chombo chenye dhamana ya waganga ambacho ni shirikisho hili la vyama vya Tiba Asili Tanzania, Lakini kwa kutambua dhamana tuliyonayo kwa waganga wote wa Tiba Asili na kwa kutambua kuwa popote panapokuwa na mgogoro basi njia sahihi ni kukaa mezani kujadiliana ili hatimaye amani ipatikane.

Hivyo sisi Shirikisho tuliomba kikao na Mh. Waziri wa Afya ambacho kilifanyika tarehe 28/12/2015 na ambacho kilionesha nuru ya kufikia maelewano, Na kwa kuwa siku hiyo tarehe 28/12/2015 Waziri wa Afya Mhe. UMMY MWALIMU alitamka mbele ya vyombo vya habari kuwa yupo tayari kukaa kujadiliana na yeyote Yule ambaye amekwazwa na agizo la Wizara.

Hivyo sisi shirikisho tuliweza kukaa na wadau wa Tiba Asili na Tiba Mbadala ambao kimsingi ndiyo haswa walikwazika na agizo hilo la Wizara na hatimaye tarehe 31/12/2015 tulifanya kikao cha pamoja kati ya wadau hao, shirikisho, na Wizara ya Afya tukiongozwa na Uenyekiti wa Mhe. UMMY MWALIMU (MB) ambaye ndiye waziri mwenye dhamana na mambo ya Afya .

Ndugu waandishi wa Habari napenda ifahamike kuwa kikao hicho cha tarehe 31/12/2015 tulikubaliana kuwa wale wote wanaopeleka matangazo yao na vipindi kwenye Baraza kwa ajili ya kuhakikiwa basi Baraza liwaruhusu kuendelea na program yao hiyo na uhakiki wa Baraza usizidi siku tatu (3) kwa ujumla makubaliano yote ilikuwa ni utekelezaji wa sheria namba 23 ya Tiba Asili na Tiba Mbadala ya mwaka 2002 na kanuni zake na pia sheria nyinginezo za nchi na pia utekelezaji huu uwe wa pande zote, na mwisho Mhe Waziri alituhaidi kuwa tamko lingine la Serikali litatolewa tukiwa wote.

Lakini katika hali ya kushitua na kushangaza Mhe Waziri wa Afya ametoa tamko bila ya kutushirikisha sisi wadau wengine kama tulIvyokubaliana .

Hivyo tunaamini Waziri asingefanya hivyo kukiuka makubaliano isipokuwa ni kushauriwa vibaya na vyombo vya chini yake ambavyo vinadhammana ya kumshauri juu ya Tiba na tunaamini hivyo kwa kuwa viongozi wenye dhamana ya kumshauri walio chini yake wao ni wanataaluma ya Udaktari wa kisasA, Hivyo wameshindwa kumshauri Waziri vizuri kwa sababu wanapigania maslahi ya Taaluma yaona hawapo tayari kutoa ushirikiano wa dhati kwa Tiba Asili, lakini tunamuomba Mhe. Waziri kwa kuwa yeye ni mwanasheria basi aimome sheria namba 23 vizuri ili aweze kujiridhisha.

Tunaamini kuwa viongozi hao walio chini yake wangetumia nafasi na dhamana waliyo nayo kumshauri Mhe Waziri vizuri juu ya Tiba Asili bila kuweka mbele maslahi ya Taaluma yao, basi yote haya yasingetokea .

Ndugu waandishi wa Habari, Tiba Asili imekuwepo hapa nchini kwa mika mingi kabla ya kuja tiba ya Kisasa ambayo kwa kadri siku zinavyozidi nayo inazidi kupoteza umaarufu wake na kuiacha Tiba Asili ikizidi kuchukua nafasi kubwa katika nchi yetu, Hivyo kitendo cha Tiba Asili na Sasa Tiba Mbadala kuzidi kuchukua nafasi kubwa kwa wananchi ambayo hivi sasa ni asilimia 70% mijini na asilimia 80% vijijini wanatumia Tiba Asili kitendo hicho kinawakera hao wanaoitwa madaktari wa kisasa na ndiyo maana maneno yamekuwa mengi kwa upande huu waTiba Asili na Tiba mbadala na kufikia hata hatua ya kutukejeri eti kwa nini tunavaa mavazi meupe wakati wa kutoa tiba?, kwa nini tunaitwa Madaktari kama wao? Na wengine hufikia kusema eti sisi waganga wa Tiba Asili na Tiba mbadala unaongoza kusababisha Vifo vya Wagonjwa kitu ambacho siyo kweli hata kidogo kwani Tiba Asili imeokoa na inazidi kuokoa maisha ya watu wengi mijini na vijijini, mfano mdogo katika Tiba Asili yapo magonjwa mengi yasiyoambukiza tunayatibu na pia tunaunga mifupa na waliovunjika hurejea katika hali yao ya kawaida ndani ya wiki mbili hadi mwezi mmoja kitu ambacho kwa Tiba ya Kisasa imekuwa ndoto kwao,

Lakini vilevile Tiba hiyo ya Kisasa ndiyo inaongoza kwa vifo vya watu wengi mijini na vijijini na ushaidi wa hilo ni uwepo wa mochwari karibu kila hospitali kwa ajili ya kuhifadhia maiti zitokanazo na watu waliokuwa ni wagonjwa na wakitibiwa katika Hospitali hizo na hao Madaktari bingwa wa Kisasa.

Ndugu waandishi wa Habari na ndugu wananchi, shirikisho la vyama vya Tiba Asili Tanzania tunapinga vikali matamshi yote yanayotolewa yakiwa yanalenga kuidhalilisha Tiba yetu ya Asili ambayo imekuwepo hapa nchini kwa miaka mingi na kwa sasa tunaiboresha na kuiendeleza ili iwe ya kisasa zaidi.

Hatupo tayari kuona watoa huduma wa Tiba Asili wananyanyaswa na kudhalilishwa ndani ya nchi yao, Hii ni nchi yetu sote.

Hivyo hakuna mwenye haki ya kujiona kuwa yeye na kundi lake ndiyo bora na wengine siyo bora, yeye ndiyo anahaki ya kuzungumzia mwili wa mtu na wengine hawana haki hiyo, yeye ndiyo ana haki ya kuvaa koti jeupe wakati wa kutoa Tiba na wengine haki yao ni kuvaa kaniki.

Kama kuna watu wapo tayari kuona hayo yanaendelea kutendeka sisi tunasema hatuko tayari na muda wote hatutokuwa tayari.

Hivyo katika hili tamko lililotolewa tarehe 15/01/2016 na Mhe Waziri wa Afya tunabainisha mambo gani tunayaunga mkono na mambo gani hatuyaungi mkono

MAMBO TUNAYOYAUNGA MKONO
 1. Tunaunga mkono Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala kuongezwa watumishi wa kutosha lakini wawe na moyo wa kuipenda Tiba Asili na Tiba mbadala
 2. Tunaunga mkono kuwepo mpango mkakati kwa muda mrefu kuwezesha kufanikisha uboreshaji wa Huduma wa Tiba Asili na Tiba mbadala lakini mpango huo uwe wa vitendo zaidi.
 3. Tunaunga mkono watoa huduma wote, vituo vyote vya kutolea huduma, dawa na vifaa tiba vinasajiliwa .
 4. Tunaunga mkono mwongozo wa mafunzo kwa watoa huduma wote nchini kuhusu namna ya kuweka kumbukumbu za wagonjwa , kutoa rufaa kwa wagonjwa (lakini rufaa hizo ziwe kwa pande zote siyo waganga tu kupeleka wagonjwa mahospitalini na mahospitali nayo yalete wagonjwa wao kwa waganga wa Tiba Asili na Tiba Mbadala)
 5. Pia tunaunga mkono kuwepo kwa mawasiliano kati ya Wizara Afya na Wizara zinazohusika na mambo ya Habari, OFISI YA RAIS Tamisemi, na Taasisi za utafiti
MAMBO AMBAYO HATUYAUNGI MKONO
 1. Hatuungi mkono kuondolewa kanuni inayoruhusu matangazo kwa idhini ya Baraza isipokuwa tunataka sheria iachwe kama ilivyo juu ya utoaji wa matangazo .
 2. Hatuungi mkono kuongezwa adhabu kwa sababu hata iliyopo haijawahi kutumika kwa wakosaji 
 3. Hatuungi mkono kuweka ukomo wa usajili mijini na vijiji kwa sababu tangu usajili uzinduliwe ni miaka mitano sasa na waganga waliosajiliwa hawazidi elfu kumi na moja (11,000), Hivyo siyo kazi rahisi kusajili waganga elfu sitini na nne(64,000) kwa muda wa miezi mitatu na sita, ikiwa wapo watu wamejaza fomu za Baraza tangu mwaka 2011 na walilipia Ada za usajili Banki lakini hadi leo hawajapata vyeti, kwa hiyo hata hatua ya kuwazuia wasitoe huduma hilo haliwezekani.
 4. Hatuungi mkono kuzuia kuuza dawa au kugawa dawa eti hadi iwe imesajiliwa na Baraza, kupimwa na maabara ya mkemia mkuu wa serikali na kupewa kibali na TFDA hilo halikubaliki kwa sababu tunaamini kuwa TFDA ni mmoja ya wanaosababisha migogoro ya Waganga ikiwemo kutoa vibali vya waganga kutangaza katika Radio na Televisheni na hali hawaruhusiwi kutoa vibali hivyo lakini Wizara ya Afya wameshindwa kuikemea TFDA, Tunataka utaratibu wa kupima dawa, kusajili katika Baraza uende sambamba na uuzaji na ugawaji wa dawa hizo kwa wagonjwa .
 5. Hatuungi mkono agizo la kusajili vifaa tiba TFDA kwani agizo hilo siyo la kisayansi na halitekelezeki kwa mazingira yaliyopo hapa nchini ambayo hivi sasa wapo watu wengi wananunua na kutumia vifaa tiba kwa ajili ya kujiangalia Afya zao kwa hiyo siyo kazi rahisi kwa mtu binafsi kwenda kusajili mashine ya Glukosi TFDA tunataka waachwe wavitumie kwa kuwa wao ndiyo wanavitumia na kuviamini.
 6. Hatuungi mkono kuzuia matangazo ya aina yoyote yanayohusu Tiba Asili kwa sababu sheria inaelezea utaratibu wa kutangaza , na pia tunaomba ifahamike kuwa matangazo yanayohusu Tiba Asili hayamuthiri mwananchi yeyote ikilinganishwa matangazo ya sigara na vilevi vingine lakini Wizara ya Afya ipo kimya juu ya matangazo hayo na kuacha watu wengi wakiangamia kwa kutumia vitu hivyo. Kama hoja ni Tiba isitangazwe kwa Dunia ya sasa haiwezekani watu ni wengi na vifaa vya kutangazia vipo, zamani watu walikuwa wachache na hakukuwa na vifaa vya kutangazia, isitoshe hata Ibada zinatangazwa kwanza ndiyo utaona watu wanajaa makanisani na misikitini kwa hiyo kusema Tiba isitangazwe haikubaliki hata kidogojambo la msingi ni kuboresha utaratibu iliopo unaohusu matangazo na siyo kuuondoa .
Uganga wa Tiba Asili na Tiba Mbadala siyo jambo la kuhujumu uchumi wala madawa ya Tiba Asili si madawa ya kulevya . Na pia kuwazuia watoa huduma kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari na mikutano ya hadhara kuhusu Tiba Asili na Tiba Mbadala nalo halikubaliki hata kidogo, Huo ni uvunjifu wa katiba na ni kinyume cha haki za Binadamu na pia itakuwa ni kuingilia Taaluma ya Mtu, isipokuwa zuio liwe kwa mtu ambaye si Mganga.

Hivyo basi kutokana na hayo tuliyoyaeleza tunaamini kuwa sisi waganga wa Tiba Asili na Tiba Mbadala tunahujumiwa na tunaamini kabisa wapo watu hawaitakii mema tiba yetu hii, hivyo tunataka mambo yafuatayo yatekelezwe:-
 1. Viongozi wote wenye dhamana ya kumshauri Waziri juu ya Tiba kwa kuwa wameshindwa kumshauri vema na wameegeme kupendelea Taaluma yaoTunaomba mamlaka ya juu iingilie swala hili ili haki itendeke
 2. Tiba Asili iundiwe Wizara yake kwa sababu madaktari wa kisasa sisi tunawapenda lakini wao hawatupendi wanaona Wizara ya Afya ni ya kwao peke yao.
 3. Ili tuwe na Imani na Wizara ya Afya tunataka tuwe na Mganga mkuu wetu wa Tiba Asili na Tiba Mbadala wa serikali kuliko kuwa na hawa wa kawaida ambao kazi yao kubwa ni kupendelea Taaluma zao.
 4. Kuanzia sasa Waganga wote wasajiliwe na shirikisho kwa kuwa ndiyo linaweza kuwatambua na kuwafuatilia kwa karibu utoaji wao wa huduma na Baraza libaki na kazi ya kuthibitisha vyeti vyao tu.
 5. Tunataka heshima ya Tiba Asili ienziwe na siyo kudharauliwa.
 6. Tunataka waziri mwenye dhamana na Afya awaeleze Watanzania ni watu wangapi wanakufa kwa siku katika hospitali za serikali na za Binafsi ambazo zina hao wanaoitwa Madaktari bingwa.
 7. Mamlaka ya juu ya Wizara ya Afya kwa maana ya Ofisi ya Waziri mkuu tunaomba iingilie kati swala hili, ikae na sisi wadau wa Tiba Asili ili ukweli ujulikane na muafaka upatikane tunaamini katika majadiliano, na tunaimani na Serikali yetu inayoongozwa na Mhe.Rais Dkt. JOHN POMBE MAGUFULI.
Ahsanteni sana kwa kunisikiliza

ABDULRAHMAN M. LUTENGA
Mwenyekiti wa Taifa wa Shirikisho la vyama vya Tiba Asili Tanzania
Tarehe 16/01/2016

Tanzania's Gov statement on dress code: President has not issued any ban on miniskirts


PRESS RELEASE

NO BAN ON MINISKIRTS BY PRESIDENT MAGUFULI

The Ministry of Foreign Affairs, East African, Regional and International Cooperation of the United Republic of Tanzania has noticed, with serious concern and disapproval, a grossly distorted report in the Kenyan Standard newspaper, purporting that H.E. President John Pombe Magufuli has banned the wearing of miniskirts in Tanzania.

Unfortunately, the false report, appearing in the daily newspaper's 'MondayBlues' gossip page on 18th January 2016, was taken for factual and circulated widely by other outlets and the social media in Kenya and beyond.The ministry deplores the casual manner in which the Standard handled the hearsay report and the reckless, totally unwarranted attribution of the imaginary 'ban' to the Tanzania Head of State.

While it appreciates the enthusiastic, positive reviews of H.E. President Magufuli's performance in the Kenyan and international media, the Ministry of Foreign Affairs takes strong exception at irresponsible distortions and misreporting, such as the one on miniskirts.

There is no doubt that H.E. President Magufuli and his government are strong proponents of decent dressing, but the ministry wishes to put the record straight that the President has not issued any ban on miniskirts for any reason.

The ministry understands that as a mainstream newspaper, the Standard is obliged to observe the highest standards of journalism, central of which is respect for facts and accurate reporting.

The ministry trusts that the distortion in question was inadvertent, not a malicious attempt to undermine the new administration in Tanzania, and that the Standard will show good faith by at least retracting the wrong information fed to its readers.

-Ends-

Issued by:
Government Communication Unit,
Ministry of Foreign Affairs, East African, Regional and International Cooperation.

Dar es salaam, January 20, 2016

UN SG appoints advocates to build widespread support for SDGs

UNITED NATIONS INFORMATION CENTRE – DAR ES SALAAM

UN Secretary-General appoints advocates to build widespread support for the Sustainable Development Goals


New York, 19 January – UN Secretary-General Ban Ki-moon announced today the appointment of a group of eminent persons to assist in the campaign to achieve the Sustainable Development Goals (SDGs) that world leaders unanimously adopted last September.

With a mandate to support the Secretary-General in his efforts to generate momentum and commitment to achieve the SDGs by 2030, the newly named SDG Advocates will add powerful voices to spur action on the visionary and transformational sustainable development agenda. The 17 SDGs aim to end poverty, fight inequalities and tackle climate change, while leaving no one behind.

“The 17 Sustainable Development Goals are our shared vision of humanity and a social contract between the world's leaders and the people,” said UN Secretary-General Ban Ki-moon. “They are a to-do list for people and planet, and a blueprint for success.”

The SDG Advocates will have the task of promoting the universal sustainable development agenda, raising awareness of the integrated nature of the SDGs, and fostering the engagement of new stakeholders in the implementation of the SDGs.

The diverse group of Advocates will engage with partners from civil society, academia, parliaments, and the private sector to develop new and ground-breaking ideas and ways to promote SDG implementation. The group includes Heads of State and Government, business and political leaders and prominent academia, as well as artists who have shown outstanding leadership in their field.

Ghanaian President John Dramani Mahama and Norwegian Prime Minister Erna Solberg will co-chair the group of SDG Advocates. The other Advocates include:
 • Her Majesty Queen Mathilde of Belgium
 • Her Royal Highness Crown Princess Victoria of Sweden
 • Her Highness Sheikha Moza bint Nasser, Co-Founder Qatar Foundation
 • Mr. Richard Curtis, Screenwriter, Producer and Film Director
 • Ambassador Dho Young-Shim, Chairperson, United Nations World Tourism Organization’s Sustainable Tourism for Eliminating Poverty Foundation 
 • Ms. Leymah Gbowee, Director, Gbowee Peace Foundation
 • Mr. Jack Ma, Founder and Executive Chairman, Alibaba Group
 • Mrs. Graça Machel, President, Foundation for Community Development
 • Mr. Leo Messi, World Renowned Footballer, UNICEF Goodwill Ambassador 
 • Ms. Alaa Murabit, Founder, The Voice of Libyan Women 
 • Mr. Paul Polman, Chief Executive Officer, Unilever
 • Professor Jeffrey Sachs, Director, Earth Institute at Colombia University
 • Ms. Shakira Mebarak, Artist, Advocate and Founder, Pies Descalzos Foundation, 
 • UNICEF Goodwill Ambassador
 • Mr. Forest Whitaker, Founder and CEO, Whitaker Peace & Development Initiative, UNESCO Special Envoy for Peace and Reconciliation
 • Professor Muhammad Yunus, Founder, Grameen Bank

HakiElimu yatoa waraka kuhusu changamoto ya Sera ya Elimu na Mafunzo (2014)

Dk. Bashiru Ali (kushoto), kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), akizungumza na wadau wa elimu na wanahabari wakati wa uzinduzi wa Waraka wa Hakielimu juu ya sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 uliofanyika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Profesa Willy Komba kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)
Na Dotto Mwaibale

MKURUGEZI Mtendaji wa Haki ya Elimu, John Kalage amesema ubora wa Elimu umekuwa ni changamoto ya muda mrefu na sasa ni muda muafaka kwa Serikali kuandaa mikakati itakayowezesha elimu katika ngazi zote.

Akizungumza Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa Waraka wa HakiElimu juu ya sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 uliofanyika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, Kalage alisema njia pekee za kufanikisha suala hilo ni kuwa na shule bora za umma ambazo zinahudumia wanafuzi wengi kuwa na walimu bora na wenye hamasa ya kufundisha kuwa na mifumo ya kufuatilia na kutathimini kiwango cha elimu katika ngazi zote na mifumo bora ya usimamizi wa shule.

"Napenda kuipongeza Serikali kwa juhudi za kuhakikisha sera ya elimu na mafuzo ya 2014 inapatikana, hii ni baada ya kuwepo kilio cha mda mrefu kwa umma na wadau wa elimu kudai kufanyiwa marekebisho kwa sera za elimu za zamani ambazo zilishapitishwa na wakati ni hivyo kushindwa kukabiliana na changamoto mpya za elimu," alisema.

Mkurugezi huyo alitolea ufafanuzi suala la kuboresha elimu alisema malengo ya sera yanatarajia kuhakikisha kuwa elimu inayotolewa nchini inakuwa bora na ya viwango vya ushindi.

Alisema katika uchambuzi wameonesha tafiti nyingi zinakubali kuwa elimu inayotolewa iwe yenye ubora kwani nimuhimu taifa lijitahidi kuboresha mazingira ya ufundishaji na kuwekeza katika ubora wa walimu ambao ndio msingi wa elimu yenyewe.

Kalage alisema ni muhimu Tanzania ifanye tathmini na kuweka bayana msimamo wake kuhusu lugha itakayo tumika kuelimisha jamii na kizazi kijacho.

"Hakielimu inaona kuwa njia pekee ya kutatua suala hili ni kuchagua lugha ambayo itaendana na uwekezaji ili kuwe natija katika ufundishaji na ujifunzaji wa wanafunzi ili wapate maarifa na ujuzi unaostahili na kuweza kushindana katika masoko ya ajira kimataifa," alisema Kalage.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugezi wa Sera na Mipango Chonya Caristus, alisema Serikali imekamilisha mikakati yote ya sera hiyo na wanachosubiri ni maboresho ya mwisho.


Wadau wa elimu wakiwa kwenye uzinduzi huo.


Mdau wa elimu Mtemi Zombwe akichangia mada katika mkutano huo. Kutoka kushoto ni Ofisa- Sera na Utafiti wa Hakielimu, Boniventura Godfrey na Dk.Geofrey Katabaro kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.Dk.Geofrey Katabaro kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (kulia), akichangia jambo katika uzinduzi huo.Watoa mada katika uzinduzi huo wakiwa meza kuu.Profesa Willy Komba kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), akichangia jambo katika uzinduzi huo.Mwenyekiti wa Bodi ya HakiElimu, Profesa Seleman Sumra (kulia), akizungumza na wanahabari.Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, John Kalage (kulia), akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa waraka huo.Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Elimu, Chonya Caristus (kushoto), akitoa ufafanuzi jinsi Serikali ilivyoandaa sera ya elimu.

 • Imeandaliwa na mtandao wa www.habarizajamii.com - simu namba 0712-727062

Taarifa ya Ofisi ya Bunge ya Jumatano, 20.02.2016 kwa Wabunge
Ofisi ya Bunge inapenda kuwafahamisha Waheshimiwa Wabunge na Wananchi kwa ujumla kuwa, uteuzi wa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge utafanyika kesho Alhamisi tarehe 21 Januari, 2016, na kufuatiwa na Uchaguzi wa Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa Kamati husika pamoja na Kamati kupatiwa maelezo juu ya Wajibu, kazi na Mipaka ya kazi ya Kamati na kupokea na kujadili Mpango kazi wa Kamati unaoishia Juni, 2016.

Kwa kuzingatia Kanuni ya 111 ya Kanuni za kudumu za Bunge, Toleo la Aprili, 2013 siku ya Ijumaa tarehe 22 hadi Jumamosi tarehe 23 Januari kutakuwa na Mkutano wa Wabunge wote ambao pamoja na mambo mengine utakuwa na lengo la kuwafahamisha Wabunge kuhusu Kanuni za Kudumu za Bunge na Uendeshaji wa Bunge, Nadharia ya mgawanyo wa Madaraka katika Mihimili ya Dola, Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge na Mambo Mengine ya Kiserikali.

Aidha, Kikao cha kwanza cha Kamati ya Uongozi ambacho wajumbe wake ni Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge chini ya Uenyekiti wa Mhe. Spika, kinatarajiwa kufanyika Siku ya Jumapili tarehe 24 Januari, 2016, ambapo Jumatatu tarehe 25 Januari, 2016 itakuwa ni siku mahususi kwa Wabunge kupata maelezo kuhusu Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano unaokusudiwa kutekelezwa katika Jamhuri ya Muungano.

Ratiba ya Shughuli za Mkutano wa pili wa Bunge unaotarajiwa kuanza Jumanne tarehe 26 Januari, 2016 itatolewa baadae.

Imetolewa na,
Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano.
Ofisi ya Bunge,
S.L.P 9133,
DAR ES SALAAM
20 Januari, 2016.