Job: Capacity Development and Communications Specialist

Organization: International Potato Center
Country: Kenya, United Republic of Tanzania
Closing date: 01 Apr 2016

Job: Marketing Consultant, Population Services Intl., Tanzania

Organization: Population Services Intl.
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 19 Feb 2016

Job: M&E Advisor, Social and Behavior Change Communications (SBCC) Project, Tanzania

Organization: Population Services Intl.
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 19 Feb 2016

Job: Deputy Chief of Party, SBCC Project, Tanzania

Organization: Population Services Intl.
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 19 Feb 2016

Job: Senior Evaluation Consultant for Final Programme Evaluation of Women’s Economic Empowerment for Justice Project in Tanzania

Organization: Kilimanjaro Women Information Exchange and Consultancy Organization
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 31 Jan 2016

Job: Finance Manager - Tanzania

Organization: Land O'Lakes International Development
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 21 Feb 2016

Job: Chief of Party - Tanzania

Organization: Land O'Lakes International Development
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 21 Feb 2016

Call for Experts - Land O'Lakes International Development, Tanzania

Organization: Land O'Lakes International Development
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 21 Feb 2016

Job: Monitoring and Evaluation Manager - Tanzania

Organization: Land O'Lakes International Development
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 21 Feb 2016

Job: Zanzibar Restoration Expert

Organization: ACRA - Cooperazione Rurale in Africa e America Latina
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 05 Feb 2016

Job: General Logistics Delegate

Organization: International Federation of Red Cross And Red Crescent Societies
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 29 Jan 2016

Job: Project Fellow

Organization: World Federalist Movement-Institute for Global Policy
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 26 Jan 2016

Resolve complicated negotiations with this simple negotiation tactic "Indaba" technique

December 2015...

Negotiations are difficult by nature. Managing negotiations between 195 countries in order to arrive at a legally binding agreement, on the other hand, is nearly impossible. This was the problem that United Nations officials faced over two weeks at this month’s climate-change summit in Paris. To solve it, they brought in a unique management strategy.

The trick to getting through an over-complicated negotiation comes from the Zulu and Xhosa people of southern Africa. It’s called an “indaba” (pronounced IN-DAR-BAH), and is used to simplify discussions between many parties.

An indaba is designed to allow every party to voice its opinion, but still arrive at a consensus quickly. It works because opinions and arguments can only be aired in a particular way:

Instead of repeating stated positions, each party is encouraged to speak personally and state their “red lines,” which are thresholds that they don’t want to cross. But while telling others their hard limits, they are also asked to provide solutions to find a common ground.

When on Thursday (Dec. 10) things got particularly tricky in Paris, indabas were held in private rooms at all hours of the day. Different delegations rotated officials so that everyone could get some sleep.

It seems to have worked. “Including everyone and allowing often hostile countries to speak in earshot of observers, [one indaba] achieved a remarkable breakthrough within 30 minutes,” according to the Guardian. The agreement was presented today, and in a historic first all 195 countries adopted it without any objections.

Indabas were first introduced in climate negotiation talks in Durban in 2011. In the last minutes of the meeting, negotiators reached a deadlock. To prevent talks from collapsing, the South African presidency asked representatives from the main countries to form a standing circle and speak directly to each other.

The technique clearly impressed many. “It is a very effective way to streamline negotiations and bridge differences. It has the advantage of being participatory yet fair,” one West African diplomat told the Guardian. “It should be used much more when no way through a problem can be found.”

Mapendekezo ya miaka 10 iliyopita ya timu ya Prof. Chachage kuhusu Zanzibar


Profesa Chachage na watafiti wenzake waliwahi kuichambua 'Hali ya Kisiasa na Kijamii Tanzania na Uwezekano wa Kupatikana Amani ya kweli Zanzibar' mwaka 2006. Baada ya kuirejea historia ya mapinduzi na matokeo yake ya baadaye, walizungumzia suala hili linalosaidia kuelewa kwa nini sakata la Chama Cha Wananchi (CUF) na CCM linatokana na tafsiri kinzani kuhusu Mapinduzi.

Ahadi za kihistoria ambazo timu ya utafiti ya Chachage imeziainisha kwa hitimisho lifuatalo zinaweza kutusaidia kuelewa kwa kina kwa nini mfumo mzima wa SMZ inabidi ubadilike ili kutoa fursa kwa Wazanzibari wote kuwa na fursa sawa ya kuongoza dola bila misingi ya nafasi yao ama ya wazazi wao katika (historia ya) mapinduzi bali msingi mkuu wa uzalendo wao kwa Zanzibar kisiasa, kiuchumi na kijamii:
"Hakuna ubishi kwamba hatua zilizochukuliwa na serikali ya Zanzibar zilikuwa kwa maslahi ya Wazanzibari wote. Hata hivyo itakuwa makosa kukataa ukweli kwamba kulikuwa na matatizo ambayo ndiyo msingi wa kile kinachoitwa leo migogoro ndani ya jamii ya Wazanzibar.... Hali halisi ya Zanzibar inatupa picha tofauti kwani usawa na haki ambavyo vilikuwa vimelengwa na Mapinduzi ya Zanzbar bado ni ndoto. Tunapaswa kukubali kwamba Mapinduzi hayakukamilika au kuna mambo ambayo hayakufuatiliwa na yakapotosha nia nzuri ya mapinduzi ya kujenga jamii sawa na huru. Hali ya sasa ya kiuchumi na kisiasa nchini Zanzibar ni ushahidi tosha kwamba uhuru na usawa haupo na hicho ndicho kiini kikuu cha matatizo yanayoikabili Zanzibar sasa hivi."
Endapo tutakubaliana na pendekezo lifuatalo walilolitoa Chachage na timu yake miaka kumi iliyopita tutainusuru Zanzibar na kadhia isiyoisha ya kuwagawa Wazanzibari 'kwa mujibu wa mapinduzi':
"Katika kushughulikia suala na tafsiri ya Mapinduzi kusiwe na ulazima wa kuwalazimisha wale walioathirika vibaya na Mapinduzi au ambao hawakuunga mkono Mapinduzi kwamba ni maadui wa Mapinduzi na hivyo kuonekana kwamba wanakosa uzalendo na utaifa. Anayekubali Mapinduzi akubali na anayeyakataa ayakatae kwa sababu zake mwenyewe. Kama ilivyokuwa watu hawalazimishwi katika kuabudu na hili suala la kutukuza au kubeza Mapinduzi libakie katika uhuru wa mtu binafsi [Kwa mfano si busara kumlazimisha mtu aliyeuliwa baba yake asiyekuwa na hatia au aliyteswa wakati wa Mapinduzi na baadaye abadilike ayatambue Mapinduzi na kuyatukuza. Kufanya hivyo ni kuwalazimisha watu wawe wanafiki kusema kile wasichokiamini.]"

"Kuundwe Tume ya Ukweli na Upatanishi (Truth and Reconcilliation Commission) kama ile ya Afrika Kusini ili watu waondoleane kinyongo kwa yale yaliyopita nyuma na waanze ukurusa mpya wa ushirikiano na upendo katika jamii. Katika muundo wake, Mwenyekiti na Katibu wa Tume wasiwe wanachama wa Chama chochote, Wawe ni watu wenye sifa za kitaalamu, wenye wasta na uadilifu wanaokubalika na pande zote zinazopingana katika jamii."


Kwenye Chinese Night Party - Waziri Kitwanga asema: Operesheni kamata wageni, kamwe haitagusa wenye vibali halali


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akizungumza na raia wa China wanaoishi nchini, katika sherehe yao ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake, Waziri Kitwanga alisema Tanzania inatambua ushirikiano mzuri wa miaka mingi uliopo kati yake na China, hivyo raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi nchini, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni, kamwe haitagusa wenye vibali halali.


Kaimu Balozi wa China nchini, Zhang Biao akizungumza katika sherehe ya raia wa China wanaoishi nchini ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es Salaam, kabla ya kumkaribisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (hayupo pichani) kuja kuzungumza na mamia ya wachina hao waliohudhuria sherehe hiyo. Katika hotuba yake, Waziri Kitwanga alisema Tanzania inatambua ushirikiano mzuri, wa miaka mingi uliopo kati yake na China, hivyo raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi Tanzania, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni nchini, kamwe haitagusa wenye vibali halali.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick akimpongeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto), kwa kutoa hotuba nzuri iliyowafafanulia wachina waishio nchini kuwa Serikali ya Tanzania inawajali na inatambua umuhimu wa ushirikiano wao uliodumu kwa kipindi cha miaka mingi, hivyo raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi Tanzania, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni nchini, kamwe haitagusa wenye vibali halali. Wachina waishio nchini jana walifanya sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip na kuhudhuriwa na mamia ya wachina hao. Kulia ni Kaimu Balozi wa China nchini, Zhang Biao.


Raia wa China wanaoishi nchini wakishindana kula Tunda aina ya Tikiti wakati wa Sherehe yao ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es Salaam. Katika Sherehe hiyo ambayo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (hayupo pichani) alikuwa mgeni rasmi ilihudhuria na mamia ya raia hao wa China. Hata hivyo, Waziri Kitwanga alisema raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi Tanzania, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni nchini, kamwe haitagusa wenye vibali halali.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akiwapongeza raia wa China walioshinda mchezo wa bahati nasibu walioucheza katika sherehe yao ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es Salaam. Waziri Kitwanga katika hotuba yake alisema nchi yake inatambua ushirikiano mzuri wa miaka mingi uliopo kati yake na China, hivyo raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi nchini, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni, kamwe haitagusa wenye vibali halali.


Kikundi cha Karate kinachoongozwa na raia wa China wanaoishi nchini kikitoa burudani katika sherehe yao ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (hayupo pichani) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo, katika hotuba yake alisema nchi yake inatambua ushirikiano mzuri wa miaka mingi uliopo kati yake na China, hivyo raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi nchini, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni, kamwe haitagusa wenye vibali halali.


Sehemu ya raia wa China wanaoishi nchini, wakimsikiliza kwa makini, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba yake kwa Wachina hao katika sherehe yao ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es Salaam jana. Waziri Kitwanga katika hotuba yake alisema nchi yake inatambua ushirikiano mzuri wa miaka mingi uliopo kati yake na China, hivyo raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi nchini, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni, kamwe haitagusa wenye vibali halali. 

Kipanya na Mawaziri vs katazo la safari...Mtajua lugha za makabila yote!


Rais Magufuli atunuku Kamisheni kwa wahitimu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli


Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Majeshi Nchini Jenerali Davis Mwamunyange wakati alipowasili katika chuo cha Maafisa wa Kijeshi Monduli Mkoani Arusha kwa ajili ya kuwatunuku Kamisheni Maafisa wapya wa Jeshi kwa cheo cha Luteni Usu, anayetazama katikati ni Mkuu wa Chuo hicho Meja Jenerali Paulo Peter Massao.

Agizo la Waziri wa Afya alipokagua eneo maarufu kwa nyama choma Dodoma "Mnadani"

Waziri Ummy Mwalimu akizungumza na wafanyabiashara wa eneo la Msalato, Dodoma akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya hiyo, Dkt. Jasmine Tiisekwa (mwenye skafu shingoni) pamoja na Afisa Afya Mkuu wa Manispaa ya Dodoma Bw. Alek Barakena (mwenye suti nyeusi).

Na Rabi Hume, Modewjiblog

Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu ametembelea eneo la Msalato lililopo mkoani Dodoma sehemu ambayo inatumika kufanyia mnada wa nyama choma ikiwa ni moja ya ziara zake kufatilia hali ya ugonjwa wa kipindupindu katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Baada ya kutembelea mnada huo, Mhe. Ummy aliwataka wananchi wa eneo hilo kutambua kuwa bado ugonjwa wa kipindupindu upo na unaendelea kusambaa maeneo mbalimbali ya nchi hivyo ni wajibu wao kama wananchi kuweka mazingira yao katika hali ya usafi ili kutokomeza uonjwa huo.

Aidha ili kuzidi kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu, Waziri Ummy ameagiza kuendelea kutekelezwa kwa agizo la Mkuu wa Wilaya hiyo, Dkt. Jasmine Tiisekwa ambaye aliagiza kusimamishwa kwa shughuli za kuuza nyama nyoma katika eneo hilo la Msalato mpaka uongozi wa wilaya hiyo utakapojiridhisha kuwa ugonjwa wa kipindupindu umetoweka mkoani Dodoma.

“Kipindupindu kimesambaa sehemu nyingi nchini ikiwepo hapa Dodoma na hivyo naagiza katazo la Mkuu wa Wilaya, Dkt Jasmine Tiisekwa liendelee kuwepo hadi ugonjwa wa kipindupindu uishe Dodoma na niwajibu wa kila mwananchi kuhakikisha kipindupindu kinakwisha,” alisema Waziri Mhe. Ummy.

Pamoja na hayo pia Waziri huyo wa Afya ameutaka uongozi wa Manispaa ya Dodoma kufanya kikao cha pamoja na wafanyabiashara hao wa nyama choma ili kuona ni jinsi gani wanaweza kuendelea na biashara zao huku wakizingatia kanuni za usafi wa afya na mazingira bila kusababisha kuzidi kusambaa kwa kipindupindu.


Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akifafanua jambo kwa wafanyabiashara wa eneo hilo.


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akitoa maagizo ya wafanyabiashara hao kusitisha shughuli zao mara moja katika eneo hilo la Msalato mpaka uongozi wa wilaya hiyo utakapojiridhisha kuwa ugonjwa wa kipindupindu umetoweka mkoani Dodoma.


Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili kushoto), Mkuu wa Wilaya hiyo, Dkt. Jasmine Tiisekwa (wa tatu kulia) na Afisa Afya Mkuu wa Manispaa ya Dodoma Bw. Alek Barakena (kushoto) wakisikiliza hoja kutoka kwa mmoja wa wafanyabiashara wa eneo hilo (hayupo pichani).


Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akisikiliza hoja kutoka kwa mmoja wa wafanyabiashara wa eneo la Msalato lililopo mkoani Dodoma sehemu ambayo inatumika kufanyia mnada wa nyama choma ambaye jina lake halikupatikana alipofanya ziara ya katika eneo hilo.

TRA, Polisi yachunguza 'mzigo' ulioingizwa na StarTimes uliopo TBC

Polisi na maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wanachunguza mzigo ulioingizwa nchini na kampuni ya StarTimes na kuhifadhiwa kwenye ofisi zake zilizo ndani ya uzio wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Mikocheni, Dar es Salaam.

Polisi pia inachunguza kama bidhaa zinazoingizwa na kampuni hiyo ni zile zinazotumika kwenye biashara ya ving’amuzi au kwa ajili ya shughuli nyingine, kwa mujibu wa ofisa mawasiliano wa TRA.

StarTimes ni kampuni ya China inayofanya biashara ya kuuza ving’amuzi kwa ajili ya vituo mbalimbali vya televisheni, hasa vya TBC.

Habari ambazo gazeti hili imezipata kutoka vyanzo mbalimbali, zinaeleza kuwa mzigo huo unaosadikiwa pia kuwa na simu za mkononi na vifaa vya pikipiki, uliingizwa juzi na kuhifadhiwa kwenye ofisi za StarTimes.

Habari hizo zinasema kuwa baada ya TRA kuutilia shaka mzigo huo, ilituma maofisa wake ambao walikesha usiku wa kuamkia jana kuufanyia upekuzi ili kujua kama unalingana na bidhaa zilizoko kwenye nyaraka walizotumia kuuingiza nchini.

Gazeti hili lilifika ofisi za kampuni hiyo jana saa 3.30 asubuhi kupata ufafanuzi juu ya taarifa hizo, lakini hakuna aliyekuwa tayari kuzungumza lolote, kwa madai kuwa mmoja wa waandishi hao wa habari alipiga picha jengo la kampuni hiyo bila ya ruhusa.

Mmoja wa walinzi wa kampuni hiyo, alikanusha taarifa za kukamatwa kwa mizigo ya kampuni hiyo, akisema “hakuna kontena wala mzigo ulioingizwa hapa, na kama kontena zingekuwepo si mngeziona”.

Juhudi za kuzungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya StarTimes, Clement Mshana ziligonga mwamba baada ya askari aliyejitambulisha kwa jina la Isack Mwakyembe kusema ameagizwa na viongozi wa juu kutoruhusu mwandishi wa habari kutoka chombo chochote zaidi ya TBC kuingia.

“Nimepewa maagizo asubuhi ya leo kwamba humu ndani asiingie mwandishi na mimi nafuata utaratibu huo,” alisema.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo alisema kulikuwa na utata katika upangaji wa mizigo wa simu za mkononi zilizoletwa na Startimes.

“Watu wetu wako hapo StarTimes kuhakiki na kujiridhisha juu ya taarifa hizo. Tutawajulisha baadaye.” Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema apigiwe simu baada ya saa mbili kwa kuwa alikuwa kwenye kikao. Hata hivyo, alipotafutwa baadaye, hakupatikana.

Membe azungumzia Zanzibar: Kuna mambo makubwa yanayoendelea, lakini hawataki tu kutuambia


Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amepinga uamuzi wa kufutwa kwa matokeo yote ya uchaguzi visiwani Zanzibar akisema dunia inashangaa, na akaitaka CCM na Serikali isiwaachie watu wawili tu kutafuta njia za kutatua mgogoro huo.

Membe anakuwa mwanasiasa wa kwanza mwandamizi kutoka chama tawala kuonyesha waziwazi kutoridhishwa na uamuzi wa kufuta uchaguzi huo wa Rais wa Zanzibar, wawakilishi na madiwani ambao ulifanyika sambamba na uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, wabunge na madiwani wa Bara na Visiwani.

“Kinachoishangaza dunia si kuahirisha uchaguzi, bali ni kufuta matokeo ya majimbo yote,” alisema mwanadiplomasia huyo katika mahojiano maalumu na waandishi wa gazeti hili mapema wiki hii.

Uchaguzi wa viongozi wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25 sambamba na Uchaguzi Mkuu, ulifutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), Jecha Salim Jecha Oktoba 28 kwa maelezo kuwa sheria na taratibu zilikiukwa na akaahidi kuitisha uchaguzi mwingine baada ya siku 90 zinazomalizika wiki ijayo.

Chama kikuu cha upinzani visiwani, CUF, ambacho kilimsimamisha Maalim Seif Sharif Hamad kugombea urais, kinapinga uamuzi huo kikisema si mwenyekiti wa tume wala ZEC wenye mamlaka ya kufuta matokeo na kutaka mshindi atangazwe ili chama hicho kwa kushirikiana na CCM vikutane kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).

Katika kujaribu kutatua mgogoro huo, Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein na Maalim Seif wameshafanya vikao tisa Ikulu Zanzibar pamoja na marais wa zamani wa visiwa hivyo, Dk Amani Karume, Dk Salmin Amour na Ali Hassan Mwinyi, bila ya mafanikio na tayari katibu huyo mkuu wa CUF ameshatangaza kujitoa kwenye mazungumzo hayo.

Akizungumza kuhusu mgogoro wa kisiasa visiwani, Membe alisema inashangaza kuona uchaguzi ulifutwa kwenye majimbo yote, badala ya yale yaliyokuwa na matatizo.

“Kilichotokea Zanzibar kimeihuzunisha dunia,” alisema mbunge huyo wa zamani wa Mtama mkoani Lindi. “Watanzania waelewe, kilichoishitua dunia ni kule kufuta matokeo kwa ujumla wake. Yaani majimbo yote hakuna hata moja lililofanya vizuri? Hapa ndipo tunapata kigugumizi. Sasa tunakwenda wapi, tunafanya kitu gani?

“Ilitakiwa kuwe na ubaguzi; majimbo mawili, matatu, manne, matano, haya hayajafanya vizuri ndiyo uchaguzi urudiwe. Kaubaguzi kale kangewekwa, hiyo ingefanana na sura ya dunia ya haki.”

Waziri huyo mstaafu aliyehudumu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa miaka tisa, pia haridhishwi na jinsi mgogoro huo wa kisiasa unavyotafutiwa ufumbuzi kutokana na kuwahusisha zaidi Dk Shein na Maalim Seif.

“Kama kuna mwanasiasa anadhani tatizo la Zanzibar litamalizwa na sehemu moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pekee, anafanya makosa makubwa,” alisema Membe.

“Umoja wetu na Zanzibar ni umoja wa kusaidiana wakati wa raha na matatizo. Hili ni tatizo ambalo linaweza kuhatarisha si tu usalama wa Zanzibar, bali pia Muungano wetu. Hatuwezi kukaa tu na kuangalia.

“Chama chetu na Serikali yetu lazima vishiriki kwa vitendo na kauli kumaliza mgogoro wa Zanzibar na ikiwezekana wahamie huko. Hili tatizo ni kubwa.”

Membe alisema katika mgogoro huo, Watanzania wa Bara wana haki ya kujua kinachozungumzwa ili kushauri kwa lengo la kudumisha Muungano.

“Kuwaacha viongozi wawili tu wanakutana kila siku kwa muda wa mwezi mzima au miezi miwili na hujui kinachoendelea si sahihi. Huwezi kujua kinachoendelea,” alisema.

“Kuna mambo makubwa yanayoendelea, lakini hawataki tu kutuambia. Msije mkadanganyika kwamba wanakutana mle, wanakunywa chai, wanaondoka halafu mnasema hakuna kinachoendelea.”

Wakati ZEC imetangaza Machi 20 kuwa tarehe ya kurudia uchaguzi, CUF imekuwa imeshasema kuurudia si suluhisho na haitakubalika, badala yake ameitaka Tume kutangaza mshindi.

Membe, ambaye alikuwa mmoja wa makada 38 wa CCM waliojitokeza kuomba ridhaa ya kugombea urais lakini akaishia kwenye tano bora, alikuwa pia na maoni yake kuhusu kurudiwa kwa uchaguzi.

“Lazima uangaliwe kwa mapana, tusiangalie kama turudie uchaguzi au tusirudie. Tusifikiri viongozi wa Zanzibar wakikutana wanaulizana swali hilo tu kwamba ‘turudie uchaguzi au tusirudie’. Hapana,” alisema Membe aliyeshiriki kutatua migogoro mbalimbali barani Afrika.

“Wenzako swali hilo ni dogo sana. Huenda wako kwenye swali kubwa. Wanaweza kuuliza swali kama ‘hivi tatizo la Zanzibar ni kitu hiki au kuna tatizo kubwa zaidi ya hapa’. Hivi mnaweza kukaa saa tatu au nne mkaulizana tu kwamba, ‘turudie, tusirudie, turudie tusirudie?’”

Wakuu wa Idara 4 za huduma za meli Tanzania wasimamishwa kazi

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano imewasimamisha kazi wakuu wa Idara wanne wa Kampuni ya huduma za Meli nchini (Marine), kwa tuhuma ya ubadhirifu wa fedha zinazokadiriwa kuwa zaidi ya shilingi Millioni mia sita, zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya ukarabati wa Meli ya Mv. Victoria, inayofanya safari zake kati ya Mwanza na Bukoba. 

Kutokana na kiasi hicho cha fedha kutafunwa Meli ya Mv. Victoria haifanyikazi tangu Desemba 2014, jambo linalokwamisha huduma ya usafiri kwa wakazi wa mikoa hiyo wakiwemo wafanyabiashara, waliokuwa wakitumia huduma ya usafiri huo kusafirisha bidhaa za mahitaji ya kibinadamu katika mikoa hiyo. 

Waliosimamishwa kazi na Wizara hiyo ni Kaimu Meneja wa Kampuni ya huduma za Meli mkoa wa Mwanza Fabian Mayenga, Mwanasheria wa Kampuni hiyo Josephat Mshumbusi, Meneja miradi wa (Marine) Alex Mchauru pamoja na Kaimu Meneja manunuzi katika Kampuni hiyo Abdallah Lumila.

Kabla ya uamuzi wa Wizara hiyo Kaimu Meneja mkuu wa Kampuni hiyo Fabian Mayenga na Mwanasheria wa (MARINE) Josephat Mshumbusi, wakazungumzia hatua walizozichukua za kulitafutia ufumbuzi tatizo la ubovu wa meli ya Mv. Victoria.

Profesa Makame Mbarawa ni Waziri mwenye dhamana katika Wizara hiyo. 

BASATA yawashauri waimbaji muziki wa Injili wajisajili

BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limezidi kutoa wito kwa Waimbaji wa muziki wa Injili kujisajili katika baraza hilo ili stahiki zao zitambulike inavyotakiwa.

Mkurugenzi wa ukuzaji Sanaa na Mtukio wa Basata, Maregesi Kwirujira Ng’oko alisema waimbaji wengi wa muziki wa Injili wa Tanzania kuzingatia hilo.

Ng’oko alisema kujisajili Basata kuna faida na fursa nyingi ambazo ni msaada ambao utasaidia kupata haki zao kupitia kazi zao.

Ng’oko alisema kwa kuwa wao ndio wasimamizi wa kazi za sanaa ni jukumu lao kuwakumbusha mara kwa mara wasanii kujisajili.

Aidha Ng’oko alisema wanatoa salamu hizo kwa wasanii pindi inapotokea mikinzano katika ufanikishaji wa kazi zao.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Abihudi Mang’era alisema wanafikiria kuongeza msukumo kwa waimbaji wa muziki wa Injili kuhusu kujisajili Basata katika baadhi ya matukio.

Mang’era alisema wanafikiria kutoa elimu ya kujisajili Basata katika matamasha yao ama kusaka namna ya kufanikisha utambuzi wa waimbaji katika baraza hilo.

Mtanzania yapewa siku 3 kuomba radhi kwa ilichokichapisha
[audio] Cosmoo Mnyamwezi - Karanga (Duro rmx)

IMG-20160116-WA0000