[video] Mavazi ya binti yazua utata katika ofisi za umma


[video] "Hatunaye" kichekesho cha Katarina na HD


Benki ya Walimu yakana kutangaza nafasi za kazi


Uongozi wa Benki ya Walimu Tanzania (MCB) umekanusha vikali taarifa iliyotolewa katika mtandao wa ZOOM Tanzania na mitandao mingine ya kijamii ikidai kuwa benki hiyo iko katika mchakato wa kujaza nafasi 120 za ajira.

Taarifa hiyo iliyoanza kutolewa Ijumaa tarehe 22, 2016 inadai kuwa MCB imetafuta wataalamu washauri katika sekta ya benki wanaojulikana kama Quality Service Consultants kusimamia swala zima la ajira hizo na mafunzo katika muda wa miezi sita.

Imesema kuwa baada ya hapo, wale watakaofaulu wataajiriwa na benki hiyo na kuendelea na mafunzo kwa vitendo chini ya uangalizi wa wataalamu.

Pia taarifa hiyo iliyotolewa na mtu aliyejiita Christopher Mwakingwe ilidai kuwa benki hiyo inatafuta wazoefu na wenye bidii ambao wako tayari kufanyakazi katika mazingira shindani na kwenye matawi ya benki hiyo yanayoanzishwa nchini pote.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Afisa Mkuu Mtendaji wa benki hiyo, Bw. Ronald Manongi alisema taarifa hiyo ni ya uongo na yenye lengo la kupotosha umma.

“Benki haijawahi kutoa tangazo kama hilo wala kutafuta mtaalam mshauri kufanya kazi hiyo kwa niaba yetu,” alisema Bw. Manongi.

Alitoa tahadhari kwa wananchi kutoomba kazi hizo kwani hazipo.

“Tunaitaka kampuni hiyo kukanusha taarifa hiyo kupitia mitandao waliyotumia ndani ya siku tatu kuanzia leo na kueleza chanzo cha taarifa hizo au wachukuliwe hatua za kisheria na benki,” alisema Bw. Manongi.

Benki hiyo pia imeitaka Quality Service Consultants kueleza ni mara ngapi wameshatoa taarifa kama hiyo siku za nyuma na watu wengine wanaoshirikiana nao kuchapisha taarifa za uongo zenye nia ya kupotosha umma.

Call for nomination: Grant Application for a 2016 World of Children Award

Thank you for your interest in submitting a Nomination Grant Application for a 2016 World of Children Award. Please sign in orcreate an account.

**Please Note: The deadline for submitting a Nomination for a 2016 Awards is Friday, April 1, 2016 at 11:59pm EDT **

WHAT TO EXPECT:

The Nominations process consists of a few simple steps including:

1) Nomination Grant Application
After creating an account, you will be taken to the Nomination Grant Application, which consists of two separate forms:
 • The About the Nominator  form asks for some basic information about you, the Nominator.
 • The Nomination Form consists of all the questions you need to answer in order to Nominate someone for an Award. When you have completed these two forms, you will submit them for review.
2) Review
After your Nomination is submitted, our rigerous review process begins. If we need more information about your Nominee, we will contact you by email.

3) Announcement
We announce our newest class of Honorees each year around September. All other Nominees are notified of their status by this time.

This year, Awards will be given in the following categories:
 • Education Award
 • Health Award
 • Humanitarian Award
 • Protection Award
 • Youth Award

IMPORTANT INFORMATION:

 • Frequently Asked Questions
 • Requirements
 • Awards Program Timeline
 • You will NOT be able to edit your Nomination Grant Application after it has officially been submitted and the Nomination process is closed. However, you may continue to log into and out of your Nomination form as many times as needed, making sure to save your work until you are ready to submit your final application.
 • We can only accept Nominations written in English at this time.

HOW TO PREPARE:

To make the process as easy as possible, it's helpful to review the types of questions you will be asked. The links below provide helpful resources to learn how to prepare for your Nomination and how to submit a Nomination:

**Please Note: The deadline for submitting a Nomination for a 2016 Awards is Friday, April 1, 2016 at 11:59pm EDT **

TCRA notice: Vacancy at ITU in Geneva

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
TANZANIA COMMUNICATIONS REGULATORY AUTHORITY
ISO 9001:2008 CERTIFIED


PUBLIC NOTICE

VACANCY AT THE INTERNATIONAL TELECOMMUNICATIONS UNION (ITU) IN GENEVA

The Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA), is quasi-independent Government body established under the Tanzania Communications Regulatory Act No.12 of 2003 to regulate communications and broadcasting sectors in Tanzania, on behalf of International Telecommunications Union ( ITU) a world-wide organization which brings government and industry together to coordinate the establishment and operation of global telecommunication network and services hereby invites applications from suitably qualified Tanzanians to fill the following post available at the ITU Headquarters in Geneva- Switzerland:-

1.     FUNCTIONS: Head, Least Developed Countries Division 
        POST NUMBER:       TD43/P5/585
        Deadline for application submission to TCRA:    4th March, 2016
        Vacancy Notice No. 2P-2016/BDT-PKM/EXTERNAL/P5
        Duty Station: Geneva, SWITZERLAND

Details on duties, responsibilities and qualifications may be accessed on the ITU’s website: http:www.itu.int/employment/Recruitment/index.html

Email:     [email protected]: Website www.itu.int
Applicants for this post are advised to state their nationality, quote the vacancy notice number and address applications with completed ITU Personal History form (PHF) to the undersigned so as to reach him not later than 04th March 2016 respectively. The post applied for should be clearly marked on top of the envelope.

Deadline for application submissions to TCRA:  04th March 2016

Applications from women are encouraged.

ITU is an equal opportunity employer
Applications should be addressed to:

Director General,
Tanzania Communications Regulatory Authority,
Mawasiliano Towers
20 Sam Nujoma Road
P.O. Box 474,
14414, DAR ES SALAAM

Maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni linalotarajiwa kuanza kazi Machi

Mwonekano wa Ofisi za Daraja la Kigamboni zitakazotumiwa na wasimamizi wa daraja hilo linalotarajiwa kuanza kazi rasmi mwezi Machi mwaka huu.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano sehemu ya Ujenzi Eng. Joseph Nyamhanga amesema daraja la Kigamboni litaanza kutumika kuanzia Machi mwaka huu.

Akizungumza mara baada ya kukagua hatua za ujenzi wa daraja hilo Eng. Nyamhanga amemtaka msimamizi wa ujenzi huo kuhakikisha hatua ya ujenzi iliyobaki inakamilika katikati ya mwezi februari na kuanza kazi mwanzoni mwa mwezi Machi.

“Hakikisheni Machi mosi magari yaanze kupita rasmi kwenye daraja hili na hivyo kufungua ukurasa mpya kwa wakazi wa Kigamboni ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na msongamano katika eneo la Magogoni”, amesema Eng. Nyamhanga.

Eng. Nyamhanga amesisitiza kuwa Serikali inaangalia uwezekano wa kuunganisha daraja la Kigamboni na barabara ya Charambe, Mlandizi hadi Chalinze ili kupunguza msongamano wa magari katikati ya Jiji.

Amemtaka meneja wa mradi wa ujenzi wa daraja hilo toka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eng. John Msemo kuhakikisha anatafuta Wakala makini atakayesimamia na kuendesha mradi huo.

Daraja la Kigamboni lenye urefu wa mita 680, unasimamiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano linatarajiwa kuishi zaidi ya miaka 100 na kuwa na uwezo wa kupitisha mizigo ya tani 56 zinazokubalika katika nchi za jumuiya ya madola.


Lango la kuingilia daraja la Kigamboni linavyoonekana, pembeni ni ofisi za huduma mbalimbali zitakazokuwa zinatolewa darajani hapo.


Sehemu ya juu ya daraja la Kigamboni, likiwa katika hatua za mwisho za ujenzi wake.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO

Waziri Ndalichako ataja sababu za kuondoka NECTA tofauti na yanayosemwaWaziri wa Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako, amesema mfumo wa wastani wa alama za mtihani (GPA) haukuwa sabababu ya yeye kuondoka katika nafasi ya Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA).

Prof, Ndalichako alisema hayo wiki iliyopita wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari kutokana na uvumi uliozagaa mitaani ikiwemo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa alijiuzulu nafasi hiyo kutokana na kushinikizwa kuukubali mfumo huo.

Alisema aliondoka NECTA baada ya kufanya kazi katika baraza hilo kwa miaka tisa, hivyo muda huo aliona unatosha kwa yeye kuliongoza baraza hilo la mitihani nchini.
“GPA haikuniondoa NECTA kama ambavyo nimekuwa nikisikia maneno mitaani kuwa niliondoka ili kupisha mfumo huu wa GPA kuanza kutumiwa na baraza hili la mitihani nchini,”
Prof. Ndalichako alisema kuondoka kwake kulisukumwa na kazi kubwa alizokuwa amezifanya katika baraza hilo, pamoja na kuweka mifumo mbalimbali ya kisasa katika usajili na mambo mengine ya kitaalamu ambayo hayakuwapo kabla yake.
“Nimefika pale NECTA nikakuta kuna baadhi ya watendaji wanadai hawaejenda likizo kwa zaidi ya miaka mitatu, hii yote ilikuwa ni kutoka na mifumo iliyokuwa ikitumika ambayo kwa kiasi kikubwa ilikuwa kwenye vichwa vya watu hivyo wao kama hawatakuwapo basi kazi nyingine hazifanyiki…nikamua kuanzisha mifumo ya kisasa na kuacha kutegemea vichwa vya watu,” 
Prof. Ndalichako alisema sababu nyingine iliyomuondoa NECTA ni kutaka kujiendeleza kielimu kutoka alipokuwa wakati huo na kupanda katika ngazi nyingine, kwani kama angeendelea kubaki asingeweza kujiendeleza.
“Nilitoka Necta nikarudi Chuo Kikuu cha Dar es Salaamu ili kujiendeleza na hivi sasa mimi ni profesa lakini nilipokuwa Necta nilikuwa dokta, hivyo hayo maeneno yanayozagaa kuwa mimi nilikimbia GPA si ya kweli hata kidogo na mfumo huo ulianzishwa mimi nikiwa sipo pale,” 

High Level workshop: Identification of Education Priorities for 5-year Education Sector Development Plan

UNESCO Dar es Salaam Office in collaboration with the Ministry of Education, Science and Technology (MoEST), cordially invites the media to the opening of a High Level workshop for the Identification of Education Priorities for Development of the 5 Year Education Sector Development Plan (ESDP) on Tuesday 26th January 2016, to be held at the National Council for Technical Education (NACTE) at 0800 am.  

The workshop aims to identify education priorities required for formulation of outcomes, strategies and outputs of the education sector for the next 5 years .The meeting will be chaired by the Commissioner of Education, Professor Eustella Bhalalusesa and will bring together Senior government officials from MoEST and Education Institutes, the President’s Office Regional Administration and Local Government (PO-RALG), Development Partners and Civil Society Organizations representatives as well as members of the Academia. The UNESCO team, will be led by the International Institute for Education Planning (IIEP) and further  composed by experts from the UNESCO Institute of Lifelong Learning (UIL), the Education and TVET Units of the HQs and the Dar es Salaam Office.


EVENT:           WORKSHOP FOR IDENTIFICATION OF EDUCATION PRIORITIES FOR 
                           5 YEAR EDUCATION DEVPT PLAN   
                         
DATE:             26 JANUARY, 2016

TIME:              0800 AM

VENUE:          NATIONAL COUNCIL FOR TECHNICAL EDUCATION (NACTE), ITV                                  ROAD, MIKOCHENI


Mkuu wa Kitengo: Sheria imepunguza 60% makosa ya kimtandao

SHERIA za Makosa ya Mtandao na Miamala ya Kielektroniki ya Mwaka 2015, imesaidia kupunguza makosa ya mtandao kwa asilimia 60 tangu kuanza kutumika Septemba mosi, mwaka jana.

Hatua hiyo imetokana na wananchi kuanza kuelewa matumizi bora ya mitandao na kuwezesha matumizi ya mtandao kutumika kwa jinsi ilivyokusudiwa .

Hayo yalisemwa jana katika kikao cha kujadili sheria hiyo kwa wafanyakazi na walimu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kilichofunguliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Mawasiliano, Profesa Faustine Kamuzora.

Akizungumza katika kikao hicho, Mkuu wa Kitengo cha Sheria katika wizara hiyo Kitengo cha Mawasiliano, Veronika Sudayi alisema kati ya makosa yaliyokuwa yameshamiri na sasa kupungua kwa kiasi kikubwa baada ya kuanza kutumika sheria hiyo ni picha za ngono mitandaoni, makosa ya udhalilishaji watoto na watu wazima.

Sudayi alisema kuna makosa ambayo bado yanaendelea kwa kasi mitandaoni yanayohitaji kuchukuliwa hatua stahili ikiwemo elimu kwa umma ambayo ni uchochezi na taarifa za uongo unaofanywa na kundi kubwa la vijana.

Agizo: Offer Letter waziwasilishe Halmashauri sasa hadi Machi 30 wapewe Hati za kumiliki ardhi

SERIKALI imewataka wamiliki wa ardhi ambao mpaka sasa wanamiliki kwa barua za Toleo (Letter of Offer) kuziwasilisha katika Halmashauri zao kuanzia sasa hadi Machi 30 mwaka huu ili waweze kuandaliwa Hati za kumiliki Ardhi.

Hatua hiyo inatokana na azma ya serikali kuwa wamiliki wote wa ardhi nchini waliopewa umiliki na serikali wanakuwa na hati za kumiliki ardhi.

Taarifa iliyotolewa na Kaimu Kamishna wa Ardhi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mary Makondo alisema barua hizo zinapaswa kuwasilishwa katika halmashauri ili uandaaji wa Hati za kumiliki Ardhi uweze kufanyika.

Alisema wamiliki wote wenye barua badala ya hati za kumiliki ardhi wanatakiwa kuwasilisha barua zao katika halmashauri kuanzia juzi hadi Machi 30 mwaka huu.
“kila Halmashauri ya Jiji, Manispaa, Miji au wilaya nchini itawatambua wanaomiliki ardhi kwa barua hizo ili waandaliwe hati na uhakiki wa barua hizo utafanyika ili kuondoa uwezekano wa kutoa katika maeneo yasiyotakiwa,”
alisisitiza.
 • Taarifa hii imenukuliwa kutoka kwenye gazeti la serikali, HabariLeo

Waziri Lukuvi awapa Manispaa siku 30 kubomoa ghorofa iliyopo Indira Gandhi

Sehemu ya jengo ambayo inaonekana imepasuka. (Picha: Emmanuel Massaka)

WAZIRI wa Nyumba, Ardhi na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amewaagiza watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na Shirika la Nyumba la Taifa kubomoa jengo refu lilojengwa chini ya kiwango lililopo katika mtaa wa Indira Ghandhi ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa.

Lukuvi ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam kabla ya kuelekea kwenye ziara fupi katika Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani ambapo nako pia amebaini matatizo mbalimbali katika sekta ya Ardhi.

“Miezi sita iliyopita Rais Mstaafu alikuja hapa akaagiza jengo hili libomolewe na nyie mkajiridhisha kweli lafaa kubomolewa sasa inakuwaje mpaka leo linaendelea kuwepo? Naagiza mfanye haraka jengo hili ndani ya mwezi mmoja taratibu za ubomoaji ziwe zimeanza ili kulinusuru taifa kuingia katika janga jingine.”alisema Waziri Lukuvi.

Akiwa bagamoyo waziri Lukuvi alibaini katika Wilaya ya Bagamoyo upotevu wa viwanja vya wanachi ambavyo walitakiwa kupewa katika eneo la ukuni ambapo vimetoweka

Mara baada ya kupata taaarifa hiyo mmoja wa wakaazi wa bagamoyo ambaye alitoa malalamiko juu ya viwanja hivyo mbele ya mkutano wa hadhara na kutaja kuwa Halmashauri ilichukua kiasi cha pesa kuanzia laki sita kwa kila mtu mwaka 2005 na kuahaidi kuwapatia viwanja lakini mpaka leo hawajapewa.

Mara baada ya kupata taarifa hiyo waziri Lukuvi aliwagiza watendaji wa wilaya hiyo ndani ya miezi sita wawe wamewapatia wakazi hao viwanja hivyo.


 • Taarifa hii ya agizo la Waziri imepatikana kupitia blogu ya Michuzi

Habari inayohusiana na jengo hilo kama ilivyochapishwa kwenye gazeti la serikali, HabariLeo Agosti 20, 2015 inasomeka hivi...

ACHOMOA KUBOMOA JENGO PACHA


UBOMOAJI wa jengo pacha lenye ghorofa 16, lililopo mtaa wa Indira Ghandi Dar es Salaam, imeshindikana.

Imeelezwa kuwa mkandarasi aliyepewa kazi hiyo amebadili msimamo wake dakika za mwisho kwa madai kuwa, kazi ya kubomoa ni ngumu na yenye madhara kwa majengo yaliyo jirani.

Hayo yamebainishwa jana Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mngurumi wakati akizungumzia hatua zilizofikiwa wa ubomoaji wa jengo hilo, kufuatia kubainika kuwa limekiuka sheria za mipango miji.

Mngurumi alisema mmiliki wa jengo hilo baada ya kupewa taarifa ya kulibomoa alikimbilia mahakamani, na kwamba kesi hivi sasa imesikilizwa na imeisha na maamuzi ni kwamba jengo hilo linapaswa kubomolewa.

Alisema Manispaa ya Ilala ilitangaza zabuni kwa ajili ya kumpata mkandarasi atakayeweza kubomoa jengo hilo, na kwamba katika zabuni hiyo, alijitokeza mkandarasi mmoja kampuni ya kichina ya CRJ, ambapo ilikubali kazi hiyo, ila ilijitoa dakika za mwisho.

Aliongeza, wao hawawezi kulibomoa kwa kuwa hawana ujuzi wa kazi hiyo na kwamba kinachofanyika hivi sasa ni Manispaa hiyo inazungumza na Bodi ya Wakandarasi Nchini (CRB), kuangalia kama wanaweza kumpata mkandarasi mwenye sifa na uwezo wa kufanya kazi hiyo ya ubomoaji.

Kubomolewa kwa jengo hilo, kunatokana na kuporomoka kwa jengo lililokuwa jirani na hilo ambalo lilisababisha vifo vya watu 36, na kujeruhi wengine 18, tukio lililotokea Machi 29 mwaka 2013.

Hata hivyo, sababu za kuporomoka kwake zilitokana na kujengwa chini ya kiwango lakini pia ukiukwaji wa sheria kwa kuongeza idadi ya ghorofa kutoka ghorofa nane zilizoidhinishwa kisheria hadi ghorofa kumi na tano.

Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, inatoa maelekezo kwa mwekezaji yeyote anayetakiwa kufanya ujenzi wa mradi wowote ambao ni zaidi ya ghorofa tano, lazima aombe kibali cha tathimini ya mazingira katika ofisi hiyo.

Mara baada ya tukio hilo, la Machi 29, Aprili 5 mwaka 2013, aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka aliyeambatana na wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira walitembelea eneo hilo na kutoa siku 30 kwa mmiliki wa jengo hilo, Ally Raza kulibomoa baada ya kubainika kujengwa chini ya kiwango na sehemu isiyo zingatia mipango miji.

Kulingana na sheria ya Ardhi namba 4 ya mwaka 1999, kifungu cha 44 na 45 na pia kanuni za ardhi za 2001 inaelekeza mhusika aliyekiuka masharti ya uendelezaji anapaswa kupewa ilani ya kubomoa na akiendelea kukaidi amri analipa faini ya asilimia mbili.

Hata hivyo, mmiliki huyo alikaidi na kukimbilia mahakamani kufungua kesi ya kupinga kubomolewa kwake, kesi ambayo imeisha na hukumu yake ni jengo hilo linapaswa kubomolewa.

Kesi za uchaguzi: Mahakama yafuta kesi ya CHADEMA Mbarali dhidi ya CCM

Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya imeiondoa kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Jimbo la Mbarali kwa maelezo kuwa mwombaji kupitia mawakili wake, hakuwasilisha vielelezo vya msingi katika kesi hiyo.

Aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Mbarali, Liberatus Mwang’ombe (CHADEMA) alifungua kesi hiyo akiiomba mahakama hiyo kutengua matokeo yaliyompa ushindi Mbunge Haroon Pirmohamed wa CCM kwenye uchaguzi uliofanyika nchini Oktoba 25, mwaka jana.

Jaji wa Mahakama hiyo, Atuganile Ngwala alitoa uamuzi huo jana na kusema mwombaji kupitia kwa mawakili wake, Benjamin Mwakagamba na Adrian Mhina, hakuambatanisha vielelezo muhimu katika kesi hiyo, ikiwamo hati ya fomu ya matokeo ya ubunge ambayo ndiyo msingi wa kesi.

Hata hivyo, Mwang’ombe kupitia kwa wakili wake, Mhina alisema hawakuridhishwa na uamuzi uliotolewa mahakamani hapo wa kuiondoa kesi hiyo, hivyo wanakusudia kukataa rufaa.

Taarifa ya Ikulu: Rais atengua maamuzi, asimamisha kazi, arejesha Mabalozi nyumbani

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akizungmza katika mkutano na waandishi wa habari, Ikulu Dar es Salaam leo

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telegrams : "CABINET"
DAR ES SALAAM
Telephone : 2116898, 2116900/6
Fax : 2113425/2116914/2117272
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD
11400 DAR ES SALAAM.


1.0 Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)

1.1 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ametengua uteuzi wa Bwana Dickson E. MAIMU, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kuanzia leo, tarehe 25 Januari, 2016.

1.2 Aidha, baada ya utenguzi huo, Bwana Dickson E. MAIMU amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi, pamoja na wafuatao:

1.2.1 Bwana Joseph MAKANI, Mkurugenzi wa TEHAMA

1.2.2. Bi Rahel MAPANDE, Afisa Ugavi Mkuu

1.2.3 Bi Sabrina NYONI, Mkurugenzi wa Sheria

1.2.4 Bwana George NTALIMA, Afisa usafirishaji

1.3 Taarifa zilizomfikia Rais zinaonesha kuwa NIDA hadi sasa imetumia Sh.179.6 bilioni. Kiasi hiki ni kikubwa na Rais angependa ufanyike uchunguzi na ukaguzi jinsi fedha hizi zilivyotumika, maana Rais amekuwa akipokea malalamiko ya wananchi kuhusiana na kasi ndogo ya utoaji wa Vitambulisho vya Taifa.

1.4 Hivyo, Rais ameelekeza Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) wafanye ukaguzi maalum wa manunuzi yote yaliyofanywa na NIDA.

1.5 Rais pia ameelekeza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali afanye ukaguzi maalum wa hesabu za NIDA, ikiwemo ukaguzi wa “value for money” baada ya kuthibitisha idadi halisi ya vitambulisho vilivyotolewa hadi sasa.

1.6 Rais vile vile ameelekeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ifanye uchunguzi kujiridhisha kama kulikuwa na vitendo vya rushwa au la.

2.0 Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa

2.1 Aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenye Serikali ya Awamu ya Nne, Mhe. Mahadhi Juma MAALIM ameteuliwa kuwa Balozi wa kwanza wa Tanzania nchini Kuwait, kufuatia uamuzi wa Serikali kufungua Ofisi ya Ubalozi katika nchi hiyo rafiki.

2.2 Rais ameagiza Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kianda na Kimataifa kuwarejesha nyumbani mara moja Mabalozi wawili ambao mikataba yao imeisha. Leo hii Mabalozi hao wanatakiwa kukabidhi kazi kwa Afisa Mkuu au Mwandamizi aliye chini yao. Mabalozi hao ni:

2.2.1 Bi Batilda Salha BURIANI, aliyeko Tokyo, Japan

2. 2.2 Dkt. James Alex MSEKELA, aliyeko Rome, Italia.

2.3 Rais amemrejesha nyumbani Balozi wa Tanzania aliyeko London, Uingereza, Bwana Peter Allan KALLAGHE. Anarejea Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa atakapopangiwa kazi nyingine.

2.4 Kwa maana hiyo, vituo vya Ubalozi vifuatavyo viko wazi:

2.4.1 London, kufuatia kurejea nchini kwa Balozi Peter A. KALLAGHE

2.4.2 Brussels, kufuatia aliyekuwa Balozi, Dkt. Deodorous KAMALA kuchaguliwa kuwa Mbunge.

2.4.3 Rome, Italia, kufuatia kuisha kwa mkataba wa Dkt. James Alex MSEKELA.

2.4.4 Tokyo, Japan, kufuatia kuisha kwa mkataba wa Bibi Batilda BURIANI

2.4.5 Kuala Lumpar, Malaysia, kufuatia aliyekuwa Balozi, Dkt. Aziz Ponary MLIMA, kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa.

2.4.6 Brasilia, Brazil, kufuatia kustaafu kwa aliyekuwa Balozi, Bwana Francis MALAMBUGI.

3.0 Tawala za Mikoa

3.1 Rais ametengua uteuzi wa Eng. Madeni Juma KIPANDE kabla hajathibitishwa kwenye cheo cha Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi kutokana na utendaji kazi usioridhisha.

4.0 Utumishi wa Umma

3.2 Nachukua nafasi hii kuwahimiza viongozi wote katika Utumishi wa Umma, na watumishi wote wa umma, kubadilika kwa dhati kwenye utendaji wao na uadilifu wao.

3.3 Napenda kusisitiza kuwa Rais na sisi tunaomsaidia hatuoni raha kuchukua hatua dhidi ya viongozi na watumishi wengine. Tungependa kila mtu mwenyewe ajirekebishe na kutomfikisha Rais mahali ambapo inabidi amchukulie hatua. Mambo yafuatayo ni muhimu:

4.2.1 Kila kiongozi na kila mamlaka ya nidhamu isipate kigugumizi kusimamia utendaji na maadili ya kazi.

4.2.2 Kila kiongozi na kila mamlaka ya nidhamu asipate kigugumizi kuchukua hatua za nidhamu, lakini afanye hivyo kwa kuzingatia kwa ukamilifu sheria, kanuni na taratibu katika Utumishi wa Umma.

4.2.3 Lazima uongozi na watumishi wa umma wawahudumie wananchi kwa haki, weledi, uadilifu na heshima. Kwa sababu hiyo:

a) Kila ofisi ya Serikali iwe na dawati la kusikiliza shida za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

b) Kwenye kila Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya wajenge uwezo wa kushughulikia shida za wananchi kwa ukamilifu na kwa wakati. Kwa muundo wa Serikali yetu hakuna sababu kwa mwananchi kufunga safari mpaka Ikulu Dar es Salaam kwa kuamini kuwa ni Rais tu anayeweza kumaliza matatizo yake, maana wawakilishi wa Rais wako kila pembe ya nchi yetu. Ikibidi wananchi wafike Ikulu ina maana hao wawakilishi wa Rais hawakutimiza wajibu wao.

c) Kuanzia sasa watumishi wote wa umma wavae majina yao ili iwe rahisi kwa mwananchi kumtambua anayemhudumia na hivyo kumsifu mtumishi wa umma anayewahudumia kwa weledi, uaminifu na kwa wakati, na kumtolea taarifa yule anayefanya mambo ya hovyo.

d) Kila ofisi ya Serikali iwe na utaratibu wa kupokea maoni ya wananchi kuhusu huduma inayotolewa kwenye ofisi hizo, na kushughulikia haraka maeneo yote ambayo wananchi wataonesha kutoridhika na huduma. 

Balozi Ombeni Y. Sefue

KATIBU MKUU KIONGOZI
IKULU,
DAR ES SALAAM.

25 Januari, 2016


Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akizungmza katika mkutano na waandishi wa habari, Ikulu Dar es Salaam leo

Kesi za uchaguzi: Ester Bulaya amwangusha Stephen Wasira mahakamani

Ester Bulaya

Mahakama Kuu, Kanda ya Mwanza imetupilia mbali kesi ya uchaguzi ya kupinga ubunge wa Bunda mjini uliompa ushindi Ester Bulaya, kutokana na walioleta maombi kutokuwa na vigezo vya kisheria vya kufungua kesi.

Baada ya Mahakama kutupilia mbali kesi hiyo, Mbunge huyo wa Bunda Mjini Ester Bulaya kupitia kwenye ukurasa wake wa Facebook ameandika:
Nilimshinda Wasira kwa wananchi, na leo nimemshinda kisheria, Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza imetupilia mbali kesi ya Uchaguzi dhidi yangu, iliyofunguliwa na wapambe wa wasira. Mungu husimama na watu waliowema. Nakutumaini mungu wangu na wewe ndiye mlinzi wangu.Asante sana Wananchi wangu wa Bunda Mjini mliokwenda Mwanza kusikiliza Hukumu. Mbunge wenu nipo dodoma tayari kwa kuanza vikao vya Bunge Kesho.

Serikali yasimamisha kazi watumishi kadhaa NEMC

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA MAKAMU WA RAIS


TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUIMARISHA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA BARAZA LA TAIFA LA HIFADHI NA USIMAMIZI WA MAZINGIRA-NEMC

Katika kikao kilichoitishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba (Mb), tarehe 24 Januari 2016, mjini Dodoma kuhusu kuimarisha utendaji ndani ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira-NEMC maamuzi yaliyofikiwa ni kama ifuatavyo:

1. Kuhusu suala la kiwanda cha kusindika minofu ya punda Mkoani Dodoma, imegundulika kulikuwa na ukiukwaji mkubwa, wa makusudi na wa wazi wa miiko ya kazi kwa watumishi wa NEMC walioshughulika na kiwanda hicho. Hivyo, Mhe. Makamba ameagiza watumishi wa NEMC wafuatao wasimamishwe kazi mara moja:

a. Dkt. Eladius Makene -Afisa Mazingira Mwandamizi,
b. Wakili Heche Suguta Manchare - Mwanasheria Daraja la II
c. Mhandisi Boniface Benedict Kyaruzi, Afisa Mazingira

Hatua nyingine za kinidhamu na kisheria zitafuatia.

2. Vile vile, imebainika kwamba usimamizi wa watumishi wa NEMC siyo makini na thabiti na kusababisha malalamiko mengi kuhusu utendaji wa Baraza. Hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Mhandisi Bonaventura Baya apewe barua ya onyo kali la mwisho kwa udhaifu katika usimamizi wa watumishi wa Baraza.

3. NEMC kama chombo muhimu nchini kilichopewa jukumu la kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira inatarajiwa kazi zake zifanyike kwa ufanisi wa kiwango cha juu kulingana na majukumu yaliyoko kwa mujibu wa Sheria. Hivyo, kwa mapungufu yanayojitokeza Mhe. Makamba, ndani ya wiki moja ataunda jopo la wataalamu wasiozidi watano ili kutathmini utendaji wa NEMC na changamoto mbali mbali katika usimamizi wa hifadhi ya mazingira na kuishauri Serikali ipasavyo.

4. Ili kuimarisha ufanisi na udhibiti wa utendaji wa NEMC, ndani ya wiki moja litatolewa Tangazo litakalokuwa na mambo yafuatayo: Anwani ya barua pepe (email), Nukushi (fax), Namba ya simu, Namba ya Whatsapp ili mtu yeyote mwenye malalamiko au aliyewahi kuombwa rushwa ama chochote na watumishi wa NEMC ambacho ni kinyume na maadili ya kazi yao atoe taarifa mara moja ili uchunguzi ufanyike na hatua zichukuliwe.

5. Kutokana na mapungufu yanayojitokeza katika utekelezaji wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira, ndani ya wiki moja, NEMC ipitie upya orodha ya wataalamu na taasisi elekezi zilizosajiliwa na kufuta wataalamu na taasisi zote ambazo zimekuwa zikikiuka maadili ya kazi zao likiwemo suala la kuwasilisha taarifa zilizo chini ya viwango, kuchelewesha kazi za wateja wao na kutowasiliana na wateja wao kuhusu hatua za utekelezaji wa maombi yao.

6. Ndani ya wiki tatu uitishwe mkutano wa dharura wa Bodi ya NEMC kujadili na kufanya maamuzi juu ya changamoto za utendaji katika Baraza.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
08.01.2016

Taarifa ya uteuzi wa George Sambali kuwa kaimu Mkurugenzi Mkuu TAA

George Sambali
George Sambali

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Profesa Makame Mbarawa amemteua aliyekuwa Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Mhandisi George Sambali kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kufuatia kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Mhandisi Suleiman S. Suleiman.

Mhandisi Suleiman alifariki dunia tarehe 18 Januari, 2016 wakati akipelekwa katika hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam baada ya kuishiwa nguvu ghafla akiwa katika mazoezi ya kuogelea katika eneo la Feri, jijini Dar es Salaam.

Akitangaza uteuzi huo kwa niaba ya Waziri Mbarawa mbele ya Menejimenti ya TAA Jumatano tarehe 20 Januari, 2016 katika Ofisi za Makao Makuu ya Mamlaka hiyo kwa niaba ya Mh. Waziri, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuliho, alisema uteuzi wa Mhandisi Sambali umeanza rasmi tarehe 20 Januari, 2016.

Mhandisi George Sambali alizaliwa mwaka 1965, mkoani Tabora na ana shahada ya Uzamili ya Sayansi Uhandisi Uchukuzi na Barabara (MSc. Transportation (Transport & Road) Engineering, aliyoipata mwaka 1999- 2001 nchini Uholanzi.

Mhandisi Sambali alihitimu shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Uhandisi Ujenzi (BSc.Civil Engineering) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka 1995 .

Mhandisi Sambali pia amepata mafunzo na kozi mbalimbali za masuala ya anga kutoka katika vyuo vya hapa nchini na nje ya nchi, ikiwemo Stashahada ya Uongozi wa Viwanja vya Ndege (Certificate in Airport Executive Leadership) mwaka 2014 huko Montreal, Canada.

Pia mwaka 2015 alitunukiwa Stashahada ya Wataalamu wa Kimataifa wa Viwanja vya ndege (Post-Graduate Diploma in International Airports Professionals (AIP) chini ya AMPAP nchini Canada.Mhandisi Sambali aliajiriwa na TAA mwaka 2001 kama Meneja Mipango, Usanifu na Uthamini (Manager Design, Planning and Evaluation) na mwaka 2012 aliteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uhandisi na Ufundi.

Mwaka 2013, Mhandisi Sambali aliteuliwa kuwa Mshauri Maalum wa Mkurugenzi Mkuu kabla ya mwishoni mwa mwaka jana kuteuliwa tena kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).

Mhandisi Sambali ni mwanachama kwenye vyama mbalimbali vya kitaaluma kikiwemo cha Wataalamu wa Kimataifa wa Viwanja vya Ndege chini ya Baraza la Viwanja vya Ndege Duniani (ACI) na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO).

Pia Mhandisi Sambali ni Mjumbe wa Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET); Mjumbe katika Jukwaa la Kimataifa la Uendeshaji wa Uchukuzi Vijijini (IFRTD); na Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB).

IMETOLEWA NA KITENGO CHA SHERIA NA UHUSIANO –TAA Januari 25, 2016

Wauzaji bidhaa kiholela sokoni Buguruni wapigwa marufukuNa Jacquiline Mrisho MAELEZO

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala yapiga marufuku uuzwaji holela wa bidhaa katika soko la Buguruni unaochafua mazingira ya soko na kuhatarisha afya za walaji.

Hayo yamesemwa leo na Afisa Habari wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala David Langa wakati akifafanua kuhusu kero ya wauzaji holela wanaopanga bidhaa chini katika soko la Buguruni.

“Bidhaa zinazopangwa chini katika soko la Buguruni sio rasmi na hakuna utaratibu unaoruhusu wauzaji kufanya biashara hiyo, hivyo natoa tahadhari kwa wale wote wenye tabia hiyo kuwa ni marufuku kufanya biashara ya kupanga bidhaa chini na sio kwa soko la Buguruni tu ila katika masoko yote yaliyopo katika manispaa yetu” Alisema Langa

Afisa langa amesema kuwa wapo maaskari wanaolinda na kuthibiti uuzwaji holela wa bidhaa katika soko hilo ila wauzaji wamekuwa wakifanya mchezo wa kuwavizia maaskari pindi wanapoondoka ndipo wanapanga bidhaa zao.

Ameongeza kuwa suala hili limekuwa sugu katika masoko mengi na njia ya kukabiliana na changamoto hii ni kuongeza askari wengi watakaokaa muda wote ili waweze kukabiliana na wauzaji holela.

Aidha Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa kushirikiana na Maafisa Afya inafatilia kwa karibu masoko yote ili kufatilia kama wauzaji wanazingatia kanuni za afya kwa kuweka mazingira safi ili kuokoa afya za walaji.

Uchafu wa mazingira katika masoko ya Jiji la Dar es Salaam umekithiri na imekuwa ni tatizo sugu lakini Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imejipanga kupambana nalo ili kuondoa uwezekano wa kutokea kwa magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu.

Bidhaa chini ya kiwango na zilizoisha muda kutoka Marekani, China zateketezwa na TBSNa Charity James

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS), limeteketeza bidhaa zenye ubora hafifu na zilizokwisha muda wake zenye thamani ya shilingi milioni 20 kutoka nchini Marekani na China.

Akizungumza wakati wa uteketezaji wa bidhaa hizo Dar es Salaam jana, Ofisa habari wa TBS, Roida Andusamile alizitaja bidhaa hizo kuwa ni dawa za meno, nepi (diapers), sabuni za kuogea na wipes.

Alisema miongoni mwa bidhaa hizo zilikuwa ni kwa ajili ya kutoa msaada katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime mkoani Mara huku nyingine zikiingizwa kwaajili ya biashara.

"Kazi ya kuteketeza bidhaa zenye ubora hafifu ni endelevu lengo letu ni kuhakikisha tunaepusha madhara kwa watumiaji ambao wanashindwa kutambua bidhaa hafifu," alisema.

Alisema bidhaa zote zinazoingia nchini ziwe za biashara au misaada ni lazima zipimwe kwa lengo la kuondoa changamoto ya kuwauzia au kugawa zikiwa ni hafifu au kuisha muda wake.

Kwa upande wake, Ofisa Mdhibiti Ubora wa TBS, Salome Emmanuel alitoa mwito kwa wafanyabiashara kuhakikisha wanaingiza bidhaa zenye ubora na kuongeza kuwa wafanyabiashara ndiyo walinzi tosha wa kuhakikisha bidhaa hafifu haziingizwi nchini, hivyo ni vyema wakafuata sheria kukwepa matatizo.Katapila likizikanyagakanyaga kwa lengo la kuziharibu bidhaa mbalimbali zikiwemo pampasi na dawa za meno zilizopitwa na wakati na zingine zisizo na ubora katika Dampo la Pugu Kinyamwezi, Dar es Salaam. Bidhaa hizo zenye thamani ya sh. mil. 20, kutoka Marekani na China zilikamatwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), katika Bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni. 
 • Tumeshirikishwa taarifa na Richard Mawikenda

Chama cha karate Kilimanjaro chaiomba serikali itupie jicho karatekaVero Ignatus - Moshi Kilimanjaro.

Chama cha Karate Mkoa wa Kilimanjaro wanaiomba serikali kutupia macho kwenye mchezo huo kwani imekuwa ikiwasahau ukizingatia mchezo huo ni michezo kama ulivyo mingine na kwamba mchezo huo umekuwa ukifundishwa pia katika majeshi mbalimbali hapa nchini. Hayo yamesemwa nakapteni wa timu na katibu msaidizi wa chama cha Katrate mkoa wa Kilimanjaro bwana Wembo Hamisi katika viwanja vya mazowezi mkoani hapo na amekusema kuwa wamekuwa wakikwama mara wanapohitajika kwenye mechi za kirafiki,ndani na nje ya nchi kwasababu hawana sapoti kutoka serikalini na wafadhili.

Aidha amesema kuwa Karate ni mchezo ambao mtu yeyote anaweza kuucheza na akatengeneza afya ya mwili,na mchezo huo ni wa kawaida kama ilivyo michezo mingine kama mpira wa miguu amewataka watu wote kujitokeza kwa wingi kujiunga katika mchezo huo wa Karate kwa sifa kuu ya karate ni nidhamu. Sambamba na hayo bwana Wembo amesema kuwa katika mchezo huo wapo wanawake na ameiomba jamii waondokane na ile dhana potofu kwamba mwanamke akicheza mchezo huo wa Karate hawezi kupata mtoto na kufanya shughuli nyingine za kijamii amesema huo ni upotoshaji kwani mwanamke anao uwezo wa kupata mtoto kama walivyo wengine na anatengeneza afaya nzuri kabisa.

Aidha amesesema kuwa mchezo huo wa Karate kwa historia umeanzishwa miaka mingi kwa mkoa wa Kilimanjaro chama cha karate kina takribani miaka saba sasa tangia kuanzishwa kwa chama hicho,na baadae wakaunda shirikisho la Karate nchini Tanzania ambapo inajumuisha michezo yote ya karate ,ambapo januari 30 watakuwa na tamasha la Karate la kuwatambulisha wachezaji wa timu litakalofanyika mkoani hapo katika ukumbi wa shule ya msingi Mwenge.

Katibu huyo ameinisha ratiba yao ndani ya miezi sita ambapo watafanya matamasha mbalimbali ikwemo februari 13/2016 watafanya tamasha wilayani Same katika ukumbi wa kimweli same mjini, machi 24-26, mashindano ya mchezo wa GOJUKAI KARATE ya Afrika Mashariki, Kampala Uganda , aprili 30 mashindano ya GOJUKAI Karate ya wazi ya kuuenzi mlima Kilimanjaro ambapo watashiriki watoto wenye umri wa kati na watu wazima yatafanyika Moshi, Mwisho ni Tamasha la shukrani litakalofanyika mei 16 hapo hapo Moshi Kilimanjaro. Kwa mkoa wa Kilimanjaro mchezo wa karate unaochezwa unajulikana kama Gojukai Stayle, ambayo ilianzishwa kutoka nchini Japan,na chama katika mkoa huo kinaundwa na vilabu mbalimbali ambavyo klabu mama ni Ralway club, Pasua Club, Mwenge Club, Ccp Club,Rau Club,na vilabu vingine vinaundwa na wanafunzi mbalimbali ambapo kila club ina zaidi ya wanafunzi 20-30.hivyo wanawaomba ,Taasisi mbalimbali ,wafanyabiashara,makampuni mbalimbali hata watu binafsi kujitokeza kuudhamini mchezo huo wa Karate.

Washindi wa Bongo Style wapatikana


WASHIRIKI wa shindano la Bongo Style linaloratibiwa na asasi isiyo ya kiserikali ya FASDO, Jocktan Cosmas Maluli (25) na Daniel Msirikale (24) wameibuka kidedea kwa kujinyakulia tuzo za shindano hilo katika fainali iliyofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar.
Shindano hilo lililoanzishwa mtandaoni mwezi Septemba mwaka 2015, lilijumuisha washiriki wapatao mia tatu wenye vipaji vya upigaji picha na ubunifu wa mitindo huku washiriki kumi pekee wakiingia kwenye fainali baada ya michujo mbalimbali kabla ya washiriki hao wawili wakishinda tuzo hizo.

Washiriki hao walishinda kutokana na kura za majaji waliobobea katika fani hizo ambapo kwa upande wa picha majaji hao walikuwa ni: Sameer Kermalli, Hanif Abdulrasul, Idd John na Angela Kilusungu huku kwenye ubunifu wa mavazi majaji hao wakiwa ni: Martin Kadinda, Rio Paul, Zamda George na Comfort Badaru.

Jocktan Maluli ambaye ameshinda katika kipengele cha Best Fashion Designer 2015 na Daniel Msirikale aliyeshinda katika kipengele cha Best Photographer 2015, wote pamoja wamepokea kitita cha dola 500 kila mmoja huku wakipata nafasi ya kwenda nchini Ubelgiji kwa ajili ya kuonesha ubunifu wao katika maonesho ya Africa Firm Festival Belgium kuonesha kazi zao pamoja na washiriki 18 walioshiriki shindano hilo, yatakayofanyika hivi karibuni nchini humo.

Aidha washindi wa vipengele vingine ni: Shahbaaz Yusuf aliyeshinda kipengele cha Best Personality of the Year 2015, Winfrida Touwa aliyeshinda katika kipengele cha Peoples Choice Award for Fashion Designers na Rasheed Rasheed aliyeshinda kipengele cha Peoples Choice Awards for Photograph.

Fainali hizo zilizohudhuriwa na wageni waalikwa na wadau mbalimbali wa kazi za sanaa na kupambwa na burudani mbalimbali kama vile nyimbo za asili, muziki na maonesho ya mavazi na kazi za sanaa kutoka kwa washiriki hao.


Mshindi wa kipengele cha The Best Photographer, Daniel Msirikale (mwenye miwani) akipokea tuzo yake.

Mlezi wa FASDO, Reuben Nabora akitoa salamu kutoka kwa mwasisi wa FASDO, Lilian Nabora aliyeko Ubelgiji.


Mratibu wa FASDO nchini, Joyce Msigwa akitoa muhtasari wa shindano la Bongo Style.


Mshereheshaji, Mario Mpingirwa akifafanua jambo.


Mtumbuizaji wa ngoma za asili akionesha uwezo wake wa kuchezea nyoka.


Baadhi ya viongozi wa wa FASDO wakifuatilia shindano hilo.


Majaji wa ubunifu mitindo wakitathmini kazi za washiriki wao.


Majaji wa upande wa wapiga picha wakitazama kazi za washiriki wao.


Mshindi wa ubunifu mitindo, Jocktan Maluli akiwa katika picha ya pamoja na wanamitindo wanaoonesha mavazi yake.


Wanamitindo wakionesha mavazi yaliyobuniwa na washiriki.


Washiriki wa ubunifu wa mitindo wakitambulishwa mbele za watazamaji.


Mkurugenzi Mtendaji wa Entango, Emma Kawawa akitoa salamu zake na kuendesha harambee kwa ajili ya FASDO.


Mkurugenzi Mtendaji wa FASDO, Chande akizungumza jambo.


Mwenyekiti wa FASDO, Stanley Kamana akiongea jambo.


Mshindi wa kipengele cha Best Personality of The Year, Shahbaaz S. Yusuf akipokea tuzo kutoka kwa mlezi wa FASDO, Reuben Nabora.


Mshindi wa Peoples Choice Awards for Fashion Designer, Winfrida Touwa akipokea tuzo yake.Mshindi wa Peoples Choice Awards for Photograph, Rasheed Hamis akipokea tuzo.


Msanii Alvin Dullah 'DY' akitumbuiza baadhi ya nyimbo zake.
Baadhi ya washiriki wakichukua vyeti vya ushiriki wa shindano hilo.


Baadhi ya watu wakijifotoa.


Baadhi ya wadau wakiongozwa na Mzee Nabora wakizitazama picha za washiriki.


Mshindi wa Ubunifu mitindo Jocktan Cosmas Maluli A.k.a Makeke (aliyeshika cheti) akiwa katika picha ya pamoja na waratibu wa shindano hilo kuanzia kushoto ni Zamda George, Comfort Badaru, Martin Kadinda, Reuben Nabora na Stanley Kamana.


Umati wa watu waliohudhuria fainali hizo wakifutatilia shindano hilo kwa umakini. (picha: na Fredy Njeje)

Mo Dewji Foundation yazindua shindano la kukuza mitaji kwa vijana wajasiriamaliNa Modewjiblog team

Mwenyekiti wa Taasisi wa MO Dewji, Mohammed Dewji kwa kushirikiana na kampuni ya Darecha Limited leo (jumatatu) wamezindua shindano la Mo Mjasiriamali lenye lengo la kusaidia kukuza ujasiriamali miongoni mwa vijana.

Shindano ya Mo Mjasiriamali litatoa fursa ya ukuzaji wa mitaji, ulezi wa wajasiriamali na mitandao ya biashara kuongeza mwanga, ujasiri na kuzalisha wajasiriamali Tanzania.

“Mimi kama Mjasiriamali kijana na mzaliwa wa Singida vijijini, sikufikiria hata mara moja kama leo ningekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa moja ya makampuni yaliyofanikiwa sana katika nchi yetu na hata barani Afrika.” Inasema taarifa Mkurugenzi Mtendaji huyo wa MeTL kwa vyombo vya habari mwishoni mwa wiki.

Aidha alisema Afrika ni moja ya bara linalokua kwa haraka na lenye ukuaji imara wa uchumi na amini vijana wa Tanzania wana nafasi kubwa ya kutumia fursa hizo ili kujiletea uchumi endelevu.

Lakini pamoja na ukweli huo changamoto kama za ukosefu wa mitaji, ukuzaji ujasiriamali na mitandao ya biashara zimekatisha tamaa vijana wengi kukuza kwa mafanikio makampuni yao hapa Tanzania na hivyo kupunguza kasi ya ukuaji wa uchumi kwa watu wa kipato cha kati.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Benki ya maendeleo ya Afrika (ADB), watu wenye kipato cha kati katika bara la Afrika wataongezeka na kufikia watu bilioni 1.1 ifikapo mwaka 2060.

Watu wa kipato cha kati ndio wanaochagiza ukuaji wa uchumi kutokana na mahitaji yao na pia ari ya ujasirimali.

Pamoja na ukweli huo kunachangamoto nyingi zinawakabili watu hao wa kipato cha kati. Mathalani nchini Tanzania changamoto kubwa kwa vijana wajasirimali ni gharama za kutafuta mtaji kwa kazi hizo.

“Kuna haja kubwa ya kuhakikisha kwamba vijana hawa wanaondolewa tatizo la ujasirimali ili waweze kusukuma mbele uchumi wa Tanzania.” inafafanua taarifa hiyo.

Aidha kwa kuwa Tanzania inaelezwa kuwa ni nchi ya 19 katika bara la Afrika kuhusiana na fursa na ujasirimali ipo haja ya kusaidia ili kuiondoa katika nafasi hiyo. Taarifa ya nafasi ya Tanzania imo katika ripoti yake ya mwaka 2014 ya Africa Prosperity Report.

Taarifa ilifafanua zaidi kwamba kutokana na haja hiyo Taasisi ya Mo Dewji na Darecha Limited wameungana pamoja na kuanzisha shindano la Mo Entrepreneurs ili kutambua na kuuenzi mchango wa wajasirimali chipukizi na kufanikisha ndoto zao.

Ili kufanikisha nia ya kuwa na wajasiriamali wengi, shindano hilo linatarajiwa kuwa daraja kwenda kwa Mkurugenzi Mtendaji, Mohammed Dewji (MeTL Group na Mwenyekiti wa Mo Dewji Foundation) ambapo vijana ambao wanaonekana wana kitu cha kufanya, lakini hawana msaada watashiriki kwa lengo la kupata msaada katika mfumo wa mtaji, mtandao na usimamizi wa ukuaji wa shughuli wanayofanya au kutaka kuifanya ili kuianzisha na kuikuza.

Mambo hayo yatatekelezwa katika mfumo wa shindano litakalogusa wajasiriamali ambao wana ari na nia ya dhati ya kuendeleza shughuli walizofikiria na kuzianzisha kwa lengo la kuinua uchumi wao binafsi na wa taifa.

Washindi watatu watakaotangazwa Aprili mwaka huu watapatiwa mtaji wa kuanzia au kuendeleza, pia watapatiwa maarifa ya kuendeleza shughuli zao na kuanzishwa mtandao wa kibiashara na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa MeTL Group na mwenyekiti wa Mo Dewji Foundation, Mohammed Dewji.

Wakati akipewa tuzo ya Forbes ya mwaka 2015, Mohammed Dewji aliitoa kwa heshima ya vijana akiwatakia kila la heri waking’aa, kuvunja nira ya woga, kukabili changamoto na kuendelea katika ujasiriamali kwa lengo la kufanya dunia yetu mahali bora pa kuishi.

Kwa habari zaidi tembelea: modewjifoundation.org/mo-entrepreneurs-competition