Maoni: Shule za vipaji maalumu zifutwe!

Mwanafalsafa maarufu wa Ugiriki; Plato, alisema watu hutofautiana uwezo wao kiakili, na kwa hatua hiyo akawagawa watu katika makundi matatu.

Alisema wapo wenye akili nyingi, aliodai kuwa ndiyo viongozi wa kufanya uamuzi kwa niaba ya wengine. Wapo wenye akili ya kati na kundi la tatu ni wenye akili kiasi.

Huenda mtazamo wa Plato ukawa sawa au si sawa, lakini ni kweli kwamba wanadamu hatufanani kufikiri.

Mfano mzuri ni wachezaji wa mpira, wapo wengi, lakini mara kwa mara tunashuhudia mchezaji mmoja akipewa tuzo ya uchezaji bora wa dunia. Hii ina maana yeye ana kitu cha kipekee na cha ziada. Huu ni ushahidi kuwa binadamu tunatofatiana.

Serikali kwa kutambua kuwa huenda wapo wanafunzi wenye uelewa mkubwa kuliko wengine, kwa nia njema iliona vyema kuwapo na shule maalumu za vipaji, ambazo zilianzishwa rasmi ili wanafunzi wakihitimu darasa la saba wajiunge na shule maalumu kwa kidato cha kwanza mpaka cha nne. Vivyo hivyo kwa kidato cha tano mpaka sita.

Ni bahati mbaya tu kwamba hatuna chuo kikuu kinachobeba wahitimu wa shule maalumu. Vyuo vikuu vyetu vinabeba watu wote bila ubaguzi, na hii nadhani ni ili ujuzi na maarifa viwe shirikishi kwa ngazi ya elimu ya juu.

Kasoro

Tangu kuanzishwa kwa shule hizi maalumu, kumekuwa na matatizo mengi katika kukidhi lengo la Serikali

Ni kweli miaka ya mwanzoni ya kuanzishwa shule hizi, zilivuma na ufaulu wake ulikuwa na tija kwa Taifa, na hata mtoto kusoma katika shule hizi ilikuwa fahari ya pekee kwake na familia.

Ni kweli pia mhitimu katika shule hizi alikuwa ana tofauti ya wazi kimtazamo na wengine. Kwa hili nakiri kuwa shule hizi zilikuwa na ubora wa elimu, lakini kwa hali livyo sasa, nashawishika kuungana na wengi wanaosema kuwa shule hizi maalumu zimekuwa na ombwe la uongozi na hivyo zimepwaya.

Mwanafunzi anapochaguliwa katika shule za vipaji maalumu ina maana ya wazi kuwa amepata ufaulu mkubwa pengine kuliko wengine.

Hali hii inatakiwa iwiane na uwezo wake wa nje kiakili vikifungamanishwa na nidhamu. Ni fedheha kubwa kwa shule hizi kuona zikiwa na ufaulu wa chini ya viwango.

Kwa mfano, kwa miaka saba kutoka 2008 mpaka 2014, shule hizi zilishakufa na kupoteza sifa stahiki japo bado hazijazikwa rasmi,

Hapa natoa takwimu za nafasi za shule hizo kitaifa kwa mwaka 2014.

Kilakala nafasi ya 96, Msalato (71), Shule ya wavulana Tabora (93), Shule ya Wasichana Tabora (295), Mzumbe (56), Kibaha (87) na Ilboru (35).

Jambo la kusikitisha kuna miaka mingi tu pia shule hizi zimefaulisha kwa daraja sifuri.

Mwaka huohuo ( 2014) katika orodha ya shule tisa za mwanzo zilizofanya vyema, hakukuwa na shule hata moja yenye jina la vipaji maalumu.

Orodha ya shule bora mwaka huo na nafasi kwenye mabano ilikuwa (1). Kaizirege (2). Mwanza Alliance (3). Marian Boys (4). St. Francis Girls (5). Abbey (6). Feza Girls (7). Bethel sabs Girls (8). Marian Girls (9). Feza Boys.

Aidha, hakukuwa na hata hata mwanafunzi mmoja wa vipaji maalumu aliyethubutu kuingia katika kundi la wanafunzi 10 bora kitaifa. Yafuatayo ni majina ya wanafunzi waliofanya vema kitaifa (1) Nyakaho Marungu kutoka Baobab, (2)Elton Sadock Jacob kutoka Feza Boys (3) Samwel M Adam kutoka Marian Boys, (4) Fainess John Mwakisimba kutoka St Francis Girls (5) Mugisha Reynold Lukambuzi kutoka Bendel Memorial (6) Paul W Jijimya kutoka Marian Boys (7) Angel Lundgreen Mcharo kutoka St Francis Girls (8). Atuganile Cairo Jimmy kutoka Canossa (9) Jenifa Lundgreen Mcharo kutoka St Francis Girls (10) Mahmoud Dadi Bakili kutoka Feza Boys.

Huu ni uthibitisho kuwa shule hizi zimepwaya. Serikali itumie kila iwezavyo kuzifuta katika dira ya shule maalumu, ili kwenda na uhalisia kwani kweli utatuweka huru kama taifa linalonuia kusonga mbele.

Nini tatizo?

Ni dhahiri kinachoathiri maendeleo ya shule hizi ni kuwapo kwa ombwe la viongozi kuanzia ngazi ya shule, wilaya, mkoa hadi Taifa. Kama uongozi hauoni haja ya kubuni mikakati thabiti na inayotekelezeka, hawataki kujiendeleza kimaarifa na kuwasikiliza wadau wengine, lengo la shule hizi litapotea na mwishowe zitafifia katika ramani ya ushindani wa kielimu.

Upo uzoefu wa viongozi wa baadhi ya shule hizi waliokosa busara na mbinu bora za uongozi. Hawa ni wakuu wa shule wanaoongozwa na jazba, chuki na maarifa madogo katika kutoa maamuzi. Ni viongozi wasiokubali kuwasikiliza walimu kama wadau muhimu katika maendeleo ya shule hizi.

Kinachotakiwa sasa ni busara tu ya ama kuzifuta katika mpango wa awali wa vipaji maalumu na kuzifanya za kawaida, au Serikali isuke upya mfumo wake wa shule hizi, huku wakuu wa shule hao wakitakiwa kueleza (kama itabidi) ni kwa nini wameshindwa kuzisimamia shule hizo ili kutekeleza lengo kuu la Serikali.

Frank Chalamila
0717-707187

Job: Health Management Information Systems Advisor

Organization: Management Sciences for Health
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 29 Feb 2016

Picha kutoka Bungeni: Mkutano XI, Kikao cha Januari 26, 2016


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa hoja ya kutaka Bunge lijadili Hotuba ya Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli aliyoitoa wakati alipofungua Bunge la Kumi na Moja Novemba 20, 2015. 

Spika wa Bunge Job Ndugai (kulia) akimwapisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa , bungeni mjini Dodoma Januari 26, 2016.Spika wa Bunge Job Ndugai (kulia) akimwapisha Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Philip Mpango, bungeni mjini Dodoma Januari 26, 2016.


Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Dkt. Abdallah Possi akijibu maswali Bungeni Mjini Dodoma Januari 26, 2016.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama akijibu swali Bungeni Mjini Dodoma Januari 26, 2016.


Wabunge wakisikiliza hoja mbalimbali bungeni mjini Dodoma Januari 26, 2016.


Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde akijibu maswali Bungeni Mjini Dodoma Januari 26, 2016.


Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula akijibu maswali Bungeni mjini Dodoma Januari 26, 2016.


Mbunge wa Mvomero, Murad Sadiq akichangia bungeni mjini Dodoma Januari 26, 2016.
 • Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Avuliwa madaraka kwa kuruhusu michango shuleni

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. George Simbachawene amemvua madaraka Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Dodoma, Bw. Augustino Kalinga kufuatia kuruhusu ofisi yake kuwachangisha wazazi michango ambayo serikali imezuia katika kutoa elimu ya msingi bila malipo.

Mhe. Simbachawene alifikia uamuzi huo jana mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua zilizochukuliwa na serikali baada ya kugundua kuwa manispaa ya Dodoma imesambaza barua kwa walimu wakuu wa shule za msingi ambazo zimeagiza kuwatoza wazazi michango ya maji, umeme na mlinzi ambayo imekatazwa na serikali.

Alisema kuwa Bw. Kalinga amevuliwa madaraka yake baada ya kubainika kuwa ameshindwa kuwasimamia watumishi walio chini yake hadi kusababisha kuandika barua na kusambaza kwa walimu wakuu wa shule za msingi katika manispaa ya Dodoma ambayo inatofautiana na maelezo ya serikali yaliyopo kwenye mwongozo.

Mbali na Kapinga, Waziri Simbachawene pia alimsimamisha Ofisa elimu vifaa na takwimu-wa msingi katika Manispaa hiyo, Josephine Akimu kwa kudharau maelekezo ya kiongozi wake na kusaini barua kwa niaba ya mkurugenzi huku akitumia jina la Ofisa Elimu, Scola Kapinga ambaye pia amepewa onyo kali.

Sababu za kuwavua madaraka watumishi hao ni kutokana na kuandika barua yenye kumbukumbu HMD/ED/50/2/VOL 11/61 ya Januari 17, mwaka huu iliyosambazwa kwa walimu wakuu wote wakitakiwa kuchangisha michango katika shule za msingi wakati Serikali ilishazuia.

Barua hiyo ilikuwa na maelekezo ya kuwataka walimu wakuu kuchangisha michango ya maji, mlinzi na umeme, jambo ambalo lilimfanya waziri kufanya safari ya kushtukiza Shule ya Msingi Dodoma Makulu, na kujionea michango hiyo lakini akabaini kulikuwa na barua za maelekezo kutoka ofisi ya mkurugenzi.

“Ieleweke kuwa uchangiaji ulioelekezwa katika barua ya mkurugenzi ni kinyume na maelekezo ya Rais John Magufuli, sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 ibara ya 3.1.5 na ilani ya Uchaguzi ya CCM ibara ya 52 (a) ya mwaka 2015 ya kutoa elimu bure bila ya malipo,” alisema Simbachawene.

Alisema maelekezo ya maofisa hao ni kinyume na mwongozo namba DB.297/507/01/39 wa Desemba 28, 2015 uliotolewa na ofisi ya Tamisemi kwa makatibu Tawala wa mikoa, wakurugenzi wa majiji, manispaa na halmashauri zote kuhusu matumizi ya fedha za ruzuku ya uendeshaji wa shule za msingi za Serikali katika kutekeleza kaulimbiu ya elimu bure.

Atundika maiti ya mwanaye mtini baada ya kumchapa hadi mauti

Mtoto wa miaka 11, Nchambi Tungu, ameuawa kikatili na mama yake mzazi kwa kuchapwa fimbo kisha kumfunga kamba shingoni na kumning’iniza kwenye tawi la mwembe ili ionekane kuwa amejinyonga mwenyewe.

Inaelezwa kuwa mama wa mtoto huyo, Sado Roketi (26) mkazi wa kitongoji cha Mnyakasi, kijijini Ikuba, wilayani Mlele, mkoa wa Katavi alimuua mwanawe huyo baada ya kukataa kumfulia nguo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, jana alithibitisha kutokea kwa kifo hicho.

Alisema tukio hilo ni la Januari 23, mwaka huu saa moja jioni katika Kitongoji cha Mnyakasi. Alisema siku ya tukio mtuhumiwa alimpatia mwanawe huyo nguo amfulie lakini mtoto huyo alikataa kuzifua akaendelea kucheza na wenzake.

“Ndipo mama huyo kwa hasira alipoamua kuchukua fimbo na kuanza kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia kifo, aliubeba mwili na kuutundika kwenye matawi ya mti wa mwembe baada ya kumfunga kamba shingoni na kumwacha akining`inia ili ionekane alijinyonga mwenyewe,” alieleza Kidavashari.

Alisema mtuhumiwa anashikiliwa na Polisi na atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Taarifa ya habari ChannelTEN, 26.01.2016
Video ya ziara ya Rais Magufuli mkoani Arusha na kufunga mazoezi ya kijeshi


Uamuzi wa mahakama kuhusu kesi ya "bomoa bomoa"


Majina ya Watanzania wanaotakiwa kuchukua pasipoti zao Ubalozini Afrika Kusini

HIGH COMMISSION OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

Telephone: 012- 342 4371/93        
             [email protected]
Website: www.tanzania.org.za
Fax:  012 – 430 4383


822 GEORGE AVENUE,
           P.O. BOX 56572, 
             ARCADIA 0007,  
                         PRETORIA  
                                        

In reply please Quote
Ref. No: TZPRC/1.10/2                                                           26 Januari, 2016

YAH: PASIPOTI AMBAZO HAZIJACHUKULIWA UBALOZINI

            Tunapenda kuwataarifu watanzania ambao maweorodheshwa hapo chini kufika ubalozini PRETORIA kuchukua pasipoti,

1.                 Mkama Leonida Biseko
2.                 Mkama Deborah Biseko
3.                 Mkama Augustine Biseko
4.                 Mhumbira Jason Salvador- DHL
5.                 Kitundu Edmond Jackson
6.                 Mkama Biseko Augustine
7.                 Morris Charles Komba
8.                 Selewa Joyfrey Jacob
9.                 Said Hangaiko Kitwana
10.            Goronya Yahaya Khamis
11.            Mwalimu Yaaaub Yusuph Mohamed
12.            Mwakasaka Happy Emmanuel
13.            Sheikh Kamrudin Huseinudin
14.            Abdalah Foleni Hilali
15.            Dhoka Mansukh Babu Daya
16.            Itatiro Henry Deodatus
17.            Bakari Hussein Hassani
18.            Khamis Amiri Kassim
19.            Samba DR. Saamo Salum
20.            Mrema Regina Jared
21.            Mbwana Mkuna Seleman Salehe
22.            Nivadia Raphael John
23.            Ndumae Sylvester Robert
24.            Oisso Edmun Alfred
25.            Mchinya Mohamed Abasi
26.            Nandumba Floriaan Alanus
27.            Mosha Pamela Mkunde
28.            Mapango Loveness Persis
29.            Juma Fikiri Iddy
30.            Kiomone Mota Bwangu
31.            Hassan Halifa Mohamedi
32.            Ngereza Murtadhwa Mussa
33.            Tuguta Mussa Emmanuel
34.            Mwigani Florence James
35.            Majaliwa Rashidi Kamangale
36.            Sadick Salum Mponda
37.            Monji Romanus Gallus
38.            Monji Michael Enock
39.            Mnzava Haikaeli
40.            Swango Ramadhani Halfan
41.            Humbo Kevin Oswald
42.            Shova Hamis Maulid
43.            Mwamweta Florence Kusirie
44.            Mzingi Shenjama Suleiman
45.            Suba hatibu Hamisi
46.            Josiah Loraine Rachard Hillary
47.            Jagani John David
48.            Sengi Ramadhani Ammar
49.            Nyathi Hudson Fredrick Kamenya
50.            Malulu Asteria Gabriel
51.            Haucha Ramadhani Buguza
52.            Mbaruk Khadija Suleiman
53.            Josiah Dr. Richard Hillary Alasai
54.            Kanyange Gift Michael
55.            Kusamila Pius Peter
56.            Humbo Oswald Jeckonia
57.            Omar Hawa Abdulkadir
58.            Mdee Ladislaus Kakore
59.            Mroso Odilo Joseph
60.            Mohamed Miraji Hassan
61.            Mboya Adelphiner Zawadiel
62.            Mbingu Bwigane Kanakangondya
63.            Kamgisha Deus Archard
64.            Setebe Reagan Edwin
65.            Humbo Ndilimwave Oswald
66.            Ole –Meiludie Asante – Eli Yohane.
67.            Suleman Kaizafa Rishard
68.            Kaizafa R. Suleman
69.            Hannah Josephiner Mboya
70.            Godwin Ainamensa Mchau
71.            Mohammed Ali Kibao
72.            Happiness Kissa Mwakalindile

 NA UBALOZI WA TANZANIA PRETORIA

Job opening at PCI Tanzania


JOB TITLE:

MFFAPP Manager

REPORTS TO:

Country Director

DIRECT REPORTS:

MFFAPP Community Mobilizers (5)

Position Grade

A Program - Senior

DEPARTMENT:

Program

GENERAL POSITION SUMMARY:


Project Concern International (PCI), in partnership with Bunda, Butiama and Musoma District Councils, is implementing a field trial of Novel Sorghum Based Fortified Blended Foods for Infants and Young Children in the Mara region, led by Kansas State University (KSU) and funded by the United States Department of Agriculture’s (USDA) McGovern Dole Program under the Micronutrient Fortified Food Aid Pilot Program (MFFAPP). The study aims to determine the nutritional efficacy and consumer acceptance of new fortified-blended food products in children under five in Bunda District over a five-month period (February – July, 2016).
 
The MFFAPP Manager is responsible for managing the field trial activities at the community and district level through an integrated approach and focused on achieving the research objectives. S/he will take a lead role in the planning, training, screening, product distribution, monitoring and reporting activities.  S/he is expected to maintain effective working relationships with other PCI staff working on the project, key government partners, beneficiaries and health facilities under the MFFAPP. The MFFAPP Manager will receive support from the Health Coordinator especially in the orientation period and start-up period.

OBJECTIVE OF THE POSITION:

Oversee the development of tools to create awareness among the communities through participatory and community-centered approaches in order to recruit study participants and maintain high levels of support and understanding of the project in the community. To manage and coordinate the implementation of the research study activities at the health facility and community level; to design and implement training, monitoring and research activities; facilitate collective problem solving; promote quality assurance; strengthen linkages and information exchange between program staff, stakeholders and study participants. To represent the MFFAPP program in key stakeholder meetings and to ensure ongoing collaboration and transparency with the district.

POSITION REQUIREMENTS:


Education:
·         Master degree or equivalent, MD, Master of Public Health/Nutrition/social sciences or other related field, RN, or RD desirable. Experience in research.

Experience:
 • 5 years’ experience in managing or coordinating community health research studies, particularly nutrition studies  
 • Technical ability in designing or adapting public health and nutrition related research and skills in training facilitation, training of trainers, monitoring field trial compliance to data collection protocols, and ensuring the integrity of the data.
 •  Demonstrated experience interacting with government officials and community-based stakeholders; Excellent project management skills; Strong computer skills (MS Word, Excel, and PowerPoint); Working knowledge of monitoring and evaluation procedures and processes.
 • Excellent English skills (verbal and written);
 
KEY AREAS OF RESPONSIBILITY:
 
 1. To coordinate implementation of activities in the preparation for and implementation of the field trial
 2. Advise and provide updates to researchers from KSU on methods and procedures used for recruitment, screening, community sensitization, trainings, monitoring, and data collection for the field trial
 3. Coordinate the execution of activities and sub-activities according to detailed implementation plan, in coordination with other program units and staff, and within budget parameters
 4. Monitor and ensure staff compliance to study protocols
 5. Monitor implementation, oversee data collection, analyze relevant data to inform strategy, approach and implementation
 6. Provide ongoing technical support and supportive supervision
 7. Reporting and documentation
 8. Maintain current technical knowledge and best practices
 9. Manage relationships and represent PCI with key external stakeholders within technical area
 
PROFESSIONAL SKILLS:
 
 • Works Efficiently & Effectively/Commitment to Quality
 • Builds Relationships/Teamwork 
 • Judgment
 • Demonstrates Adaptability 
 • Problem Solving
 • Creativity and Technical Skills 
 • Manages Strategically
 • Fosters Teamwork / Leadership
 • Manages Execution
 • Coaches and Develops MFFAPP CMs
 • Equal Opportunity
APPLICATION:

Send all necessary inquiries & application documents to [email protected]

Mlowola aeleza TAKUKURU ilikofikia kuhusu Lake Oil, EGMA, RAHCO na mabehewa ya TRL

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna Valentino Mlowola akizungumza na wanahabari leo

Na Dotto Mwaibale

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU), imetoa onyo kwa taasisi nyeti nne hapa nchini ikiwemo wanaohusika na matumizi ya fedha za umma kufuata sheria, taratibu na kanuni.

Pia, TAKUKURU inashughulikia kukamilisha kesi kubwa 36, zinazowahusu watumishi wenye ushawishi na hadhi kubwa hapa nchini ambapo kati ya hizo, zipo zilizokamilika na kupelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashitaka.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, Valentino Mlowola alisema kumekuwepo na malalamiko mengi kwa wananchi kuwajulisha matendo ya rushwa na ufisadi yanayoendelea hapa nchini.

Alisema kutokana na hali ya wananchi kuona nia ya serikali ya Awamu ya Tano katika kushughulikia matatizo ya rushwa na ufisadi hapa nchini, ametoa ovyo: "Natoa onyo kwa maofisa wa umma ambao wamefanya rushwa na ufisadi kuwa ni sehemu ya kazi zao na miradi ya kuwaingizia kipato, wajitafakari kabla hawajaamua kujihusisha na vitendo vya rushwa,"alisema.

Alisema hawatasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa watumishi watakaojiingiza katika kulihujumu taifa na wananchi kwani wananchi wana kiu ya kupata maendeleo na maisha bora na kuwataka watambue wananchi wa jana si wa leo kwani wamedhamiria kuunga mkono juhudi za serikali yao.

Mlowola alitoa ovyo kwa maofisa maduhuli na watekelezaji wa jukumu la kukusanya kodi za wananchi kwa kutomuonea mtu haya kwa atakayejihusisha na ubadirifu wa fedha na mali ya umma.

"Wakusanye kodi halali ya serikali kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni zinazowaongoza kukusanya kodi. Tutachukua hatua stahiki pale kutakapokuwa na ukiukwaji wa sheria, taratibu na kanuni zilizopo," alisema.

Pia, Mlowola alitoa ovyo kwa watakaohusika kwenye matumizi ya fedha za umma kwamba wafuate sheria, taratibu na kanuni zinazowaongoza kwani taasisi hiyo haitawavumilia watakaokiuka fedha za serikali isiyo halali.

Mbali na hilo, pia Kaimu huo alitoa onyo kwa watumishi wa umma wenye jukumu la kuhudumia mahitaji ya umma kwa kutojihusisha na rushwa kwa kutekeleza majukumu yao katika muda uliotakiwa, weledi na uaminifu.

Alisema taasisi hiyo haipo kwa lengo la maslahi ya watu wabadhilifu wa mali ya umma kwani uchunguzi wa kesi ya kuisababishia hasara serikali shilingi bilioni 8.5 (kutokana na ukwepaji wa kodi wa kampuni ya Mafuta ya Lake Oil kwa kufanya udanganyifu kuuza mafuta ndani ya nchi mafuta ya petroli lita 17,461,111.58 kwa kudanganya zilisafirishwa), umefikia hatua nzuri.

"TAKUKURU imekamilisha shauri la hili na mtuhumiwa wamepewa miezi miwili kurejesha mikononi fedha zote na kuwarudisha mahakamani endapo watashindwa kurejesha kiasi hicho,"alisema.

Alisema mbali na shauri hilo, wapo kwenye hatua nzuri ya kukamilisha uchunguzi wa kesi ya hati fungani ya malipo yaliyolipwa na kampuni ya Enterprise Growth Markert Advisor (EGMA), kiasi cha dola 6,000,000 kwa lengo la kuisaidai Tanzania kupata mkopo wa dola 600,000,000.

"TAKUKURUimebaini fedha hizo dola 6,000,000 zilitakatishwa na watumishi wa umma wasio waaminifu wakishirikiana na baadhi kutoka sekta binafsi huku wakijua fedha hizo wamezipata kwa njia haramu," alisema.

Akizungumzia hatua aliyochukua rais, Dk. John Magufuli kwa kutengua uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO, Mhandisi Benhadard Tito kwa tuhuma zinazomkabili tayaari wanachunguza shirika hilo la reli.

Alisema kulikuwepo na ukiukwaji wa kuwapata wazabuni kwenye ujenzi wa reli ya kisasa ya kimataifa (Standard Gauge) unaosimamiwa na Shirika la Hodhi la Reli Nchini (RAHCO), wanamekamatwa ikiwemo raia wa Kenya aliyekuwa kwenye mchakato huo, Kanji Muhando.

Kaimu huyo alisema shauri la kesi ya mabehewa ya kokoto 25 ya shirika la reili nchini (TRL), ya kukiuka sheria ya manunuzi ya umma Na. 21/2004 pamoja na kanuni zake kutoka kampuni ya Hindustha Engineering and Industries Limited limekamilika.

"Uchunguzi umekamilika na tumeshapeleka kwa mkurugenzi wa mashitaka kuomba kibali cha kuwafikisha watuhumiwa waliobainika kujihusisha na matendo ya rushwa na ukiukwaji wa sheria, taratibu na kanuni za ununuzi wa umma mahakamani,"alisema.

Alisema rais alijipa kazi ya kutumbua majipu hivyo aliwasihi watumishi wa taasisi hiyo kutumikia wananchi kwa eledi huku akibainisha tayari wanatekeleza azma na dhamira ya rais ya kupambana na rushwa.

Akitolea ufafanuzi swala la kumsubiri rais kutumbua majipu ndio taasisi hiyo ifanye ufafanuzi, Mlowola alisema taasisi hiyo imejipanga vilivyo tangu Novemba 20 mwaka jana wakati rais alipohutubia bungeni alipoonesha dhamira ya na nia ya dhati ya kupambana na rushwa na ufisadi bila kumuonea mtu haya.

"Nitoe rai kwa wananchi kutoa taarifa ili tuweze kujua kabla hatujapigwa, tukiweza kuisaidia serikali kuokoa fedha kabla hatujapigwa zitasaidia wananchi kutoa elimu bure, upatikanaji wa dawa na mishahara mizuri,"alisema.

Alisema tayari wameshaanza kuchunguza madai ya aliyekuwa mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), kwani tayari wapo hata viongozi wakubwa.

"Siwezi kusema kuwa kulikuwa na ulegevu, na hatua zimechukuliwa nchini imefikisha mhakamani mawaziri ila nchi ipo kwenye ufagio mpya hivyo tumeweka nguvu zaidi na hali zaidi,"alisema.

Akizungumzia maofisa takukuru waliofukuzwa kazi a rais baada ya kukiuka maagizo ya rais ya kupata kibali cha kusafiri nje, alisema maofisa hao walikwenda kwenye mkutano wa taaisis za kupambana na rushwa uliofanyika Congo-Kinshasa.

Baadhi ya wakurugenzi wa Taasisi hiyo wakiwa katika mkutano huo
 • Imeandaliwa na mtandao wa www.habarizajamii.com - simu namba 0712-727062NesiWangu show w/ Rev. Kennedy on "ObamaCare" registration before Jan 31st deadlineThe Affordable Care Act (ACA) or OBAMA CARE is a United States federal statute signed into law by President Barack Obama on March 23, 2010.

The ACA was enacted to increase the quality and affordability of health insurance, lower the uninsured rate by expanding public and private insurance coverage, and reduce the costs of healthcare for individuals and the government.

This message is brought to you by HELP AFRICA, which is an organization that targets African Communities in abroad and at home.

We urge you to register so you can access quality health services health services, avoid penalties and strengthen the health of our communities.

Tamko la vyama visivyo na Wabunge kuhusu mjadala wa akaunti ya Tegeta Escrow/IPTL

UMOJA WA MAKATIBU WAKUU WA VYAMA VISIVYO NA WABUNGE


MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI KUZUNGUMUZIA NIA YA KUTAKA KURUDISHA MJADALA WA AKAUTI YA TEGETA ESCROW/IPTL BUNGENI.


Mahali: White Mark Hotel 

Tarehe: 25 Januari 2016

Ndugu wanahabari,

Awali ya yote, tunachukua nafasi hii kuwatakia wote heri ya Mwaka Mpya 2016, na kuwatakieni kila la kheri katika majukumu yenu ya kila siku!

Umoja wetu wa makatibu wakuu wa vyama visivyo na uwakilishi bungeni, tumewaiteni hapa leo hii ili tuweze kuzungumzia masuala mbali mbali yanayohusu mjadala uliyoibuliwa na baadhi ya wabunge kutaka kurejesha hoja ya akaunti ya Tegeta Escrow na kampuni ya kufua umeme ya IPTL bungeni ilihali ikizungumuziwa kama kipaumbele cha bunge, tofauti na mtazamo wetu juu ya masuala muhimu likiwemo la sintofahamu ya kisiasa Zanzibar na katiba mpya.

1. Sakata la Tegeta Escrow/IPTL

Ndugu waandishi wa habari, tumeona ni vyema tuanze na hili kwa sababu sisi tunaona ni jambo jepesi ambalo halistahili kutuchukulia muda mrefu au hata bunge kuliwekea umuhimu na kulipa kipaumbele kama inavyodaiwa na baadhi ya wabunge ambao wanataka kuwaaminisha wananchi kuwa hili suala ni muhimu.

Tumesoma katika baadhi ya vyombo vya habari tamko lililotolewa na IPTL, likitahadharisha dhidi ya dhamira hiyo, huku wakitoa ufafanuzi wa kisheria na wakionyesha mgongano wa kimaslahi na hatua zilizowahi kuchukuliwa kwa baadhi ya wabunge hao, jambo ambalo linadhihirisha kuwa hoja hii iko kimaslahi zaidi ya watu binafsi na si kwa maslahi ya umma.

Sisi tunaamini kwamba serikali hii ya Mheshimiwa Rais Magufuli, imejipambanua kuwa ni serikali ambayo inataka kufanya kazi ambazo zitakuwa na tija kwa taifa na si malumbano ambayo yanaonekana kupata msukumo wa kisiasa kutoka kwa watu wanaoonekana kuwa na mgongano wa kimaslai katika kutengeneza mijadala isiyo na tija kwa faida zao.

Suala la Escrow hatuoni kama ni ajenda mpya ambayo inaweza ikaleta msukumo wa kuonekana kuwa ni jambo la kipaumbele na badala yake, tunaona ni mijadala ambayo inataka kufifisha na kupunguza kasi ya utendaji wa Rais wetu kwa kigezo cha kuteua watu waliotajwa katika sakata la Escrow kwenye bunge lililopita.

Tunaamini kwamba serikali iliyopita ya awamu ya nne iliweza kupokea mapendekezo ya Bunge lililopita na kuyafanyia kazi ambapo tuliona baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali wakiachia ngazi na wengine kuhojiwa kwenye vyombo mbali mbali vyenye mamlaka husika.

Tunasikitishwa na kushangazwa kwa baadhi ya wabunge wetu kulipigia kelele suala la IPTL huku wakikalia kimya suala la kampuni ya kufua umeme ya Songas ambayo pia inasemekana ufisadi wake ni mkubwa kuliko ufisadi wowote uliowahi kuibuliwa hapa nchini. Na inasemekana kwamba kampuni hii ya Songas inalipwa takriban Dola za Kimarekani milioni tisa na point (takribani TZS.19,440,000,000/=) kama malipo ya capacity charge kila mwezi, ilihali umiliki wa kampuni ya Songas ukiwa ni kitendawili kwa kutokujulikana kwa mwekezaji wa kampuni hiyo pamoja na wanahisa wengine ambao inasemekana ni Tanesco na TPDC.

Je, iweje kama wabia ni Tanesco na TPDC, waweze kujilipa capacity charge kubwa kiasi hicho ilihali wao ni sehemu ya serikali, huku wananchi wa kipato cha chini wakiendelea kuumia kwa gharama kubwa za umeme?

Kwa mantiki hiyo, hatuoni kama hili suala la Escrow ni muhimu kwa sasa kuliko hali ya kisiasa Zanzibar na mchakato wa kupata katiba mpya.

Tungeshauri wabunge wetu kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao pasipo kuliingiza bunge katika mgogoro wa kikatiba kama tulivyoshuhudia katika bunge la 10, ambapo spika wa bunge, mwanasheria wa serikali na baadhi ya wabunge walishtakiwa kwa kujadili na kutoa maazimio katika suala la Tegeta Escrow, baada ya zuio la mahakama.

Kwa sasa, tunajua kuwa kuna baadhi ya wabunge kama Mheshimiwa Zitto Kabwe, ambao bado wanakesi mahakamani, huku wao wakiendelea kulitaka bunge liendelee kujadili tena suala hili. Sasa swali tunalojiuliza ni kwamba, bunge linatakiwa lijadili suala hili la ESCROW lililoko mahakamani kwa maslahi ya nani?

2. Hali ya Kisiasa Zanzibar

Ndugu waandishi wa habari, mtakumbuka kwamba mnamo tarehe 25 Disemba 2015 nchi yetu ilikuwa kwenye kipindi cha uchanguzi mkuu uliohusisha pande zote mbili, Tanzania bara na Tanzania visiwani (Zanzibar) kwa uchaguzi wa madiwani, wabunge na maraisi, ambapo katika sintofahamu hiyo, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha alijitokeza hadharani na kutangaza kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi Zanzibar na kusema kwamba uchaguzi utarudiwa baada ya siku 90 kulingana na jinsi Tume hiyo itakavyoona inafaa.

Sisi makatibu wakuu wa vyama visivyo na waakilishi bungeni, kama wadau muhimu wa siasa, tunatoa msimamo wetu kwamba tumesikitishwa na kushangazwa kwa vyama vya CUF na CCM kuliteka suala la mgogoro wa kisiasa Zanzibar na kuufanya ni mgogoro wa vyama viwili pekee ambavyo vimekuwa na mazungumuzo ya muda mrefu kuhusu kutafuta muafaka wa mgogoro huo pasipo kushirikisha vyama vingine vilivyoshiriki uchaguzi huo vipatavyo 12 katika nafasi mbali mbali zikiwemo na za urais wakati vyama vyote vina haki sawa. Hivyo, kwetu sisi tunaona huo ni ubaguzi wa kisiasa wa wazi wazi.

Tunatamka kwamba, kurudiwa kwa uchaguzi wa Zanzibar, kama ilivyotangazwa hivi karibuni na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) si haki ya kidemokrasia kwani mwendelezo wote wa mazungumzo kati ya CUF na CCM yamekuwa ni ya siri takriban vikao 10 ambavyo wananchi pamoja na viongozi wengine wa kisiasa wa vyama vilivyoshiriki uchaguzi huo visiwani Zanzibar hawajui ni nini kilichokuwa kinajadiliwa kwa vyama viwili pekee kwa kipindi hicho chote ilihali Zanzibar si ya CCM wala CUF pekee.

Haya ni baadhi ya mambo muhimu ambayo wabumbe wetu na Bunge kwa ujumla, wanapaswa kuyapa kipaumbele katika mkutano wao wa bunge la 11 linaloanza vikao vyake tarehe 26 mwezi huu, badala ya kung’ang’ana na masuala ya IPTL yasiyo na tija wala maslahi kwa umma.

Mwisho, tunampongeza Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kwa kasi nzuri ya utendaji wake wenye maamuzi yasiyo shaka katika kushughulikia ubadhirifu na wabadhirifu wa mali za umma katika kuhakikisha tunatengeneza Tanzania mpya. Tunasema katika hili, tutaweka tofauti zetu za kisiasa pembeni katika masuala ya msingi na kumpa ushirikiano kwa namna itakavyohitajika.

Asanteni kwa kutusikiliza.

Imetolewa na ummoja wa makatibu wakuu wa vyama visivyo na wawakilishi bungenu.

Imesomwa na Katibu wa umoja huo Renatus Muabi (ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Kijamii -CCK)

Vyama ni:-


NRA

AFP

SAU

CCK

CHAUSTA

DEMOKRASIA MAKINI

ADC

UPDP

AFP

TLP

UDP

TADEA

JAHAZI ASILIA

CHAUMA

Kanusho kuhusu habari iliyochapishwa gazetini: Polisi "waisoma" namba


Tanga: Mtoto achoma nyumba baada ya kuambiwa akalale

WATOTO wa kiume wenye umri wa miaka sita na saba (majina tunayahifadhi) wamechoma moto nyumba yao yenye thamani ya zaidi ya shilingi million 300 kwa kutumia kibiriti hali iliyosababisha kuteketea yote, baada ya magodoro katika chumba chao kushika moto ikiwemo vifaa vya magari matairi vilivyokuwemo ndani ya chumba hicho.

Akizungumza na Majira mfanyakazi wa ndani Semeni Masele 20 alisema aliona chumba cha watoto kikiwa kinawaka moto na moshi mkubwa ambapo alilazimika kuwatoa nje akiwemo Bibi kikingwe mwenye umri wa zaidi ya miaka 100 kisha kuwahifadhi kwa majirani zao na kulazimika kukimbilia faya kuomba msaada.

Semeni alisema baada ya kuona hali tete aliwapigia simu askari wa zimamoto lakini alipoona namba haipokelewi alilazimika kukondi pikipiki na kwenda fanya kuomba msaada kwa lengo la kuokoa mali zilizokuwepo ndani.

Tukio hilo la kusikitisha limetokea juzi majira ya saa 14:30 kijiji cha Mikanjuni Tarafa ya Ngamiani kati kata ya Mabawa wilayani Tanga ambapo Tanesco na askari wa kikosi cha zimamoto walifanikiwa kufika katika eneo la tukio na kuzibiti moto huo usizingile nyumba za majirani ambapo nyumba hiyo iliteketeza vyumba vinne kati ya vyumba saba.

Uchunguzi wa awali uliofanywa na gazeti la MAJIRA katika eneo la tukio ulibaini kuwa watoto hao walikuwa wawili, mmoja alikuwa na miaka sita na mwingine saba, baada ya chakula cha mchana waliambiwa na dada yao, Semeni walale, lakini cha kushangaza mtoto huyo alikuta boksi la vibiriti vyenje njiti ndani na kuwasha kisha kuchoma boksi hilo, hali iliyosababisha matairi ya gari yaliyokuwa ndani kuteketea kwa moto na kusababisha moshi mkubwa.

Kwa upande wake wakazi wa Mikanjuni walipongeza hatua ya Tanesco kufika kwa wakati kuzima umeme licha ya kuwa miundombinu ya nyumba ilikwa imekushika moto lakini jitihada zilionekana ambapokikosi cha zimamoto kilifanikiwa kuzibiti moto huo mkubwa ambao ungeweza kuteketeza nyumba za mtaa mzima katika eneo hilo.

“Sisi wananchi wa mkoa wa Tanga hatutambui namba ya kikosi cha uwokoaji cha zimamoto pindi majanga yanapotokea hivyo tunaomba kuelimishwa kwa kutangaza namba zao ili tuweze kunusuru mali wakai wa majanga” walisema baadhi ya wananchi katika tukio hilo.

Akizungumzia tukio kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Mihayo Msikhela alisema tukio hilo limetokea juzi majira ya saa nane mchana baada ya watoto hao kutakiwa kwenda kulala na dada yao ambaye ni mfanyakazi wa ndani ambapo mtoto wa kiume alichukuwa kibiriti na kuchoma box kisha moto huo kuteketeza magodoro ikiwemo viashiria vya vimiminika.

Hata hivyo kamanda Msikhela aliwataka wananchi kuacha tabia ya kuweka vitu vya hatari ndani ya vyumba vya kulala watoto ili kunusuru madhara kama hayo yasitokee.

“Ninawaomba wananchi wa mkoa wa Tanga kuwa makini wakati wa kuwalea watoto kuondoa dhana ndani ya vyumba vyao vya kulala ili kunusuru madhara pamoja na majanga yasitokee kutokana watoto ni watu wa kujaribu pindi anapoona kitu anataka kukitumia bila kuchukuwa tahadhari yeyote.”

Taarifa ya UDA kuhusu takwimu zake na kanusho la habari ya kufilisika


Mwanza walalamika: Elimu bure inawabagua wanafunzi wa Elimu ya Watu WazimaWazazi na Walezi wa Wanafunzi wanaosoma kitengo cha elimu ya Watu Wazima katika Shule ya Sekondari Pasiansi iliyopo Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza, wameiomba Serikali kuondoa ada kwa wanafunzi hao ili nao waweze kunufaika na mpango wa elimu bure nchini.

Wazazi hao wametoa ombi hilo hii leo baada ya kumalizika kwa kikao baina yao na uongozi wa Shule hiyo pamoja na Kitengo cha Elimu ya Watu Wazima Mkoani Mwanza, sanjari na viongozi wengine akiwemo diwani wa Kata ya Pasiansi pamoja na Afisa elimu Sekondani katika Manispaa ya Ilemela.

Malalamiko yao yanafafanua kwamba, hawakuambiwa tangu awali kuwa watoto wao wanasoma elimu ya Watu Wazima, malalamiko ambayo hata hiyo yamekanushwa na Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Joseph Bangirana.

Awali wazazi hao walisema kuwa hawako tayari kulipa ada kwa ajili ya watoto wao wanaosoma katika shule hiyo, jambo lililomlazimu Malimi Joram ambae ni Mkufunzi Msaidizi kutoka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Mkoani Mwanza kueleza bayana kwamba, wanafunzi wa Elimu ya Watu Wazima hawanufaiki na mpango wa elimu bure nchini kwa kuwa Serikali haitoi ruzuku kwa ajili yao.

Ufafanuzi huo ukaungwa mkono na Mwalimu Juma Kasandiko ambae ni Afisa Elimu Sekondari katika Manispaa ya Ilemela.

Wakati ufafanuzi huo ukitolewa, mmoja wa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo ya Pasiansi akasisitiza suala la wao kuondolewa ada ili nao wanufaike na mpango wa elimu bure.

Kitengo cha Elimu ya Watu Wazima katika shule ya Sekondari Pasiansi, kilianzishwa Mwaka 2014 na kuanza kupokea wanafunzi waliomaliza darasa la Saba waliokuwa na ufaulu wa chini ya Wastani wa pinti 100 kwa lengo la kuwapa fursa ya kupata elimu ya Sekondari ambapo mbali na michango mingine, wanafunzi hao wanalipa ada ya Shilingi Laki Moja na Elimu Hamsini kwa mwaka.
Mmoja wa Wazazi akiwasilisha malalamiko yake juu ya suala la elimu bure kuwabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima


Mmoja wa Wazazi akiwasilisha malalamiko yake juu ya suala la elimu bure kuwabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima


Wanalalamikia suala la elimu bure kuwabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima
 • Kutoka Pasiansi Sekondari Jijini Mwanza, Mimi ni Mzee wa Karanga fotoooooooo, GB Pazzo wa Binagi Media Group

Mzumbe - UNIDO: Call for applications for internship in SMEs