Maelezo ya Waziri Nnauye nje ya Bunge baada ya "mtafaruku" 27.01.2016

Tuhuma za uonevu kwa wafanyakazi na ukwepaji kodi Leopard Tours


Kampuni ya Utalii ya Leopard Tours inayotajwa kuwa kubwa kuliko kampuni yoyote kwenye tasnia hiyo hapa nchini, inakabiliwa na tuhuma za ukwepaji kodi.

Pamoja na ukwepaji kodi kupitia mishahara ya waajiriwa, nyaraka zinaonesha kuwa Leopard Tour yenye makao yake jijini Arusha, imekuwa ikiwaachisha kazi wafanyakazi bila kufuata taratibu za kisheria.

Pigo la karibuni kabisa liliwakumba madereva 45 ambao ni sehemu ya madereva zaidi ya 280 walioajiriwa katika kampuni hiyo inayoendeshwa na Zuher Fazal.

Aidha, wafanyakazi wengine walifukuzwa kazi wiki iliyopita kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kutoa siri za kampuni kwa Naibu Waziri, kwa waandishi wa habari na kwenye mitandao ya kijamii. Miongoni mwa waliofukuzwa ni wafanyakazi wa mapokezi.

Uchunguzi uliofanywa na JAMHURI umebaini kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ajira, Kazi na Vijana, Anthony Mavunde, katika ziara yake ya ghafla katika kampuni hiyo mapema mwezi huu, alipewa taarifa nyingi za upotoshaji.

Kati ya taarifa hizo ni zile zilizohusu mishahara ya watumishi ambako msemaji wa Leopard Tours, Joel Mmbaga, alimweleza Naibu Waziri Mavunde kwamba mishahara ya watumishi wa kampuni hiyo ni kati ya Sh 150,000 na Sh 300,000 kwa mwezi.

Uchunguzi wa kina uliofanywa na JAMHURI umebaini kuwa kuna tofauti kubwa kwenye mikataba ya ajira; na hati ya malipo kwa wafanyakazi wa Leopard Tours. Kilichoandikwa kwenye mikataba si kile kinacholipwa na kuoneshwa kwenye hati ya malipo ya wafanyakazi ya kila mwezi.

“Nadhani Fazal anadhani kuwa hii Serikali ni sawa na zile zilizopita, Leopard Tours imesema kuwa inawalipa mishahara wafanyakazi wake kati ya Sh 150,000 na Sh 300,000. Hii siyo kweli kabisa, tunaweza kuthibitisha hilo kwa sababu sisi guides tunalipwa kati ya dola 500 (Sh milioni 1.09) na dola 1,000 (Sh milioni 2.18) kwa mwezi,” amesema mmoja wa wafanyakazi wa Leopard Tours.

Chanzo cha habari kinasema ujanja huo unatumiwa na Leopard Tours kama njia ya kukwepa kodi na pia kuwapunja wafanyakazi kwenye michango yao inayopaswa kupelekwa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii. Kisheria, mtumishi anayelipwa chini ya Sh 170,000 kwa mwezi, kodi yake serikalini ni sifuri. Kwa maana hiyo, wafanyakazi wa Leopard Tours kwa kuonesha kuwa wanalipwa Sh 150,000 hii ina maana baada ya makato ya NSSF ya Sh 15,000 wanabakiwa na Sh 135,000.

Amekuwa akiwasainisha karatasi za Sh 150,000 na huku akiwalipa kati ya dola 500 na dola 1,000 za Marekani. Kisha hata hizo alizowasainisha alikuwa hapeleki NSSF. Ndiyo maana ukifuatilia wale madereva zaidi ya 40 aliowafukuza mwaka 2014 na ambao walikwishafanya kazi Leopard Tours kwa miaka 20 wengi walioenda NSSF walikuta kuna kati ya Sh 600,000 na Sh 1,000,000 tu.

“Tulipoenda NSSF tuliambiwa kuwa ‘jamani tajiri yenu ni mkorofi sana hakuna wa kushindana naye shukuruni Mungu hata kwa hicho kidogo mlichopata’. Haya ni maneno ya mtu wa Serikali. Anajua namna wakubwa wa Serikali walivyowekwa mfukoni,” kinasema chanzo chetu.

Wakati wa ziara yake, Mavunde aliambiwa Mhasibu Mkuu, Mmbaga analipwa Sh 500,000 lakini imebainika kuwa kama dereva analipwa dola kati ya 500 na dola 1,000; Mmbaga anacholipwa ni kikubwa zaidi. Kuna madai kwamba Mmbaga analipwa dola 4,000 za Marekani (zaidi ya Sh milioni 8) kwa mwezi.

“Tumefanya kazi zaidi ya miaka 10 Leopard Tours na hakuna asiyejua mshahara wa Mmbaga, maana wote mshahara tunauchukulia sehemu moja kwenye dirisha maalumu na unasaini, kwa hiyo tunajuana vizuri mishahara yetu. Huo ndiyo ukweli na si kama alivyomdanganya waziri kwamba analipwa Sh 500,000,” amesema mmoja wa wafanyakazi aliyeomba jina lake lihifadhiwe.

Ukweli kuhusu wanacholipwa madereva wa Leopard Tours umebainishwa kwenye kesi ambayo baadhi ya madereva walimfungulia Leopard Tours katika Idara ya Kazi- kesi ya Honesty Kessy na wenzake 2 dhidi ya Leopard Tours: CMA/ARS/ARB/44/2015; kesi ya Hashimu na Humud Magoma dhidi ya Leopard Tours -CMA/ARS/ARB/76/2015; na kesi nyingine na 78 ya mwaka 2015.

Katika kesi hizo, Mahakama iliitisha mikataba halisi ya kazi ya wafanyakazi wa Leopard Tours na ikabainika kuwa wanalipwa kuanzia dola 500 kwa mwezi.

Akitoa maelezo kwa Mavunde, Mmbaga alimweleza kuwa Leopard Tours haina Meneja Rasilimali Watu (HR); hali iliyomshitua Naibu Waziri huyo.

Hata hivyo, katika kesi ya Honesty Kessy na wenzake 2 dhidi ya Leopard Tours CMA/ARS/ARB/44/2015, kwenye kiapo Mmbaga alijitambulisha kuwa ndiye HR wa kampuni ya Leopard.

Aidha, kwenye barua ya Zitta Lumato, aneyadai mishahara yake tangu Desemba, 2014, Mmbaga amejitambulisha kama HR wa Leopard Tours.

Wageni wanafichwa?

Kuna taarifa kuwa siku ambayo Naibu Waziri alizuru Leopard Tours, baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo, raia wa kigeni walifichwa kwa kuwa hawana vibali vya kufanya kazi nchini. Miongoni mwa watumishi hao ni mwanamke raia wa Malawi ambaye JAMHURI inalihifadhi jina lake kwa sasa.

Mwanamke mwingine raia wa Senegal, naye anatajwa kuwapo kwenye kampuni hiyo, akiwa anaishi na kufanya kazi zinazotajwa kuwa zingeweza kufanywa na Watanzania.

“Amepewa nyumba ya kuishi hapo hapo Leopard Tours ghorofani ambako anaishi na familia yake na watoto ambao kampuni ya Leopard Tours inawalipia shule ya St. Constantine, Arusha,” kimesema chanzo chetu.

Taarifa zilizopatikana wiki iliyopita zilisema mwanamke huyo ameonesha nia ya kuacha kazi.

“Kuna Meneja Karakana. Huyu ni Mshelisheli, amepangishiwa nyumba Njiro. Kuna walinzi wa karakana raia wa Nepal. Kazi yao ni kufungua geti tu na kufunga ila wanalipwa vizuri, wamepewa nyumba bure hapo hapo karakana. Hatuna hakika kama hawa watu wana vibali vya kufanya kazi nchini. Lakini unaweza kujiuliza, sheria gani inaweza kuruhusu mgeni aajiriwe kwa kazi za ulinzi wa karakana! Kwa namna mambo yalivyo sasa katika Serikali hii ya Awamu ya Tano, hawa walinzi wanaweza kutoroshwa,” kimesema chanzo chetu.

Kesi ya madereva 45


Madereva 42 wa Leopard Tours waliachishwa kazi mwaka jana, tuhuma kuu dhidi yao ikiwa kwamba waliwasilisha ofisini stakabadhi zilizoghushiwa kuonesha waliwapeleka watalii katika eneo la Olduvai Gorge.

Kwa upande wao, madereva waliozungumza na JAMHURI wanakanusha vikali madai hayo wakisema waliwapeleka watalii sehemu hiyo, na hakuna malalamiko kutoka kwao kuwa hawakufikishwa huko.

“Ofisini walisema hatuwapeleki watalii Olduval Gorge na badala yake tunaghushi stakabadhi. Hili ni jambo la kushangaza kwa sababu kabla ya kuanza safari sisi na wageni hupewa ratiba ya safari na vituo vyote.

“Kama humpeleki mgeni sehemu iliyoandikwa kwenye ratiba ataandika malalamiko ofisini. Waulizeni wapi kuna hayo malalamiko? Hayapo,” anasema mmoja wa madereva waliofukuzwa.

Dereva huyo anaungwa mkono na wenzake (majina tunayahifadhi kwa sasa) wanaosema uamuzi wa Leopard Tours kuwafukuza ulitokana na kudorora kwa biashara ya utalii duniani, na kwa maana hiyo wakaona wapunguze idadi ya wafanyakazi.

“Hakuna stakabadhi za kughushi, walichofanya ni kupunguza wafanyakazi kutokana na kudorora kwa utalii. Wakaona watupunguze sisi lakini ili tusilipwe stahiki zetu, basi waseme tumeghushi stakabadhi,” kimesema chanzo chetu.

Kwa sasa JAMHURI inahifadhi baadhi ya nyaraka zinazohusu madai hayo kwa kuwa suala hilo kwenye ngazi ya uamuzi ya vyombo vya sheria.

Madereva waliotimuliwa kwa mbinu hiyo ni:

1: Anthony Milinga

2: Godwin Makundi

3: Jurgen John

4: Lawrence Mosha

5: Micky Molobere

6: Mosses Anderson

7: Noeli Elifuraha

8: Oswald Fabian

9: Ramadhan Kanyenga

10: Sabastian Edward

11: Saleh Rashid

12: Salum Said

13: Samson Kisamo

14: Simon Matei

15: Wilbard Azaria

16: Yahaya Muruma

17: Ciryl P. Cyril

18: Emmanuel Urio

19: Gilbert Munisi

20: Joseph Sirikwa

21: Joseph Sarwat

22: James Ringo

23: John Boris

24: Munir Said

25: Mosses Charles

26: Maxi Mbise

27: Nuru Mangula

28: Onesmo Peter

29: Peter Shampula

30: Rodrick Ndemfoo

31: Victor Mkulia

32: Vicent Fares

33: Tuhery Mawala

34: Charles Minja

35: Frank Mollel

36: Hashim Abdulrahman

37: Humud Magoma

38: Honesi Kessy

39: Didmus Joseph

40: Samuel Simon

41: Silva Justine

42: Saad Zuber

43: Iddi Abdul

44: Juma Sumbi

45: Joseph Ngwenya

Aidha, imebainika kuwa uongozi wa Leopard Tours ulimnyang’anya leseni yake ya udereva dereva Salva Justine pamoja na vyeti halisi vya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) tangu mwaka 2014. Hadi wiki iliyopita, Justine alikuwa hajarejeshewa vitu hivyo, hali iliyomfanya akose kuomba kazi sehemu nyingine.

Naibu Waziri Mavunde anena
Mavunde amezungumza na JAMHURI kuhusu ziara yake katika Leopard Tours na sehemu nyingine mbalimbali mkoani Arusha.

“Lengo ni kuhakikisha tunatekeleza matakwa ya kisheria kwa kuhakikisha waajiri wote wanatekeleza sheria za kazi na za ajira kwa wageni.

“Nilipita maeneo tofauti – viwandani, ofisi za ujenzi, sehemu mbalimbali na nikamalizia Leopard Tours. Ilikuwa ziara ya kushitukiza, na kwa kweli niseme hatukupata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wafanyakazi.

“Nilibaini mambo mengi, lakini kubwa ni tofauti kubwa sana ya kile wanacholipwa wafanyakazi mwisho wa mwezi na kinachoandikwa kwenye ‘payroll’. Nilibaini kuwa Serikali inapoteza mapato mengi sana. NSSF wanapata hasara.

“Nikaagiza TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania), Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wafanye ukaguzi wabaini kwa nini mishahara inayolipwa ni tofauti kabisa na iliyoandikwa kwenye mikataba,” amesema Mavunde.

Alipoambiwa na JAMHURI kwamba wapo wafanyakazi na waliowahi kufanya kazi Leopard Tours ambao wako tayari kuisaidia Serikali, Mavunde alisema: “Nawakaribisha kabisa. Naomba waziwasilishe moja kwa moja kwangu, au kwa kupitia utaratibu maalumu nitakaowapa.

“Naomba walete taarifa maana katika hali ya kawaida huwezi kukubali kuwa dereva amzidi mshahara mhasibu.”

Naibu Waziri akaongeza: “Sitaki kuwalaumu waandishi wa habari, lakini nadhani wanapaswa kuandika mambo makubwa yanayoibuka wakati za ziara hizi. Kuna mambo makubwa sana.”

Msemaji wa Leopard Tours azungumza


Msemaji wa Leopard Tours, Mmbaga, alipotafutwa na JAMHURI mwishoni mwa wiki hakuwa tayari kuulizwa maswali.

“Kwa sasa tunavyoongea mimi niko barabarani, nilikuwa ofisini kweli tangu saa mbili, lakini sasa napiga mwendo naelekea Usa River. Niko mwendo kweli kweli,” alisema.

Alipoombwa apigiwe simu baadaye akishafika huko anakoenda, alijibu: “Hapana, ninachoenda kufanya huko siwezi kwenda na kula na watu kwenye vishughuli vidogo vidogo vya kifamilia, siyo muda mwafaka. Nitafute kesho asubuhi…sasa hivi nakimbia maana ndugu zangu wamenialika wanataka tukae pamoja, sasa nimechelewa.”

Kwa upande wake, mmiliki wa Leopard Tours, Fazal, alipotafutwa naye alikataa kuzungumza na mwandishi wa JAMHURI.

Alisema: “Leo Jumapili, naomba nipumzike tafadhali. Kwa saa moja nimepata masimu ya waandishi wa habari mpaka nimechoka sasa hivi, naomba tafadhali. Mmbaga ndiye msemaji, na leo ni Jumapili sote hatupo kazini. Mmbaga ndiye mzungumzaji wa kampuni, siyo mimi. Naomba Mmbaga azungumze tafadhali.”

Tuhuma za ukwepaji kodi za Serikali na uonevu dhidi ya wafanyakazi zimeendelea kuibuliwa dhidi ya kampuni ya utalii nchini ya Leopard Tours yenye makao yake jijini Arusha.

Kampuni hiyo inatajwa kuwa ni nambari wani kwa ukubwa na usafirishaji wageni katika hifadhi na mapori mbalimbali nchini. Inakisiwa kuwa na Land Cruiser zaidi ya 280.

Nyaraka ambazo Gazeti la JAMHURI zimelipata zinaonyesha kuwapo kwa ukwepaji kodi uliokithiri kupitia mianya kadhaa, lakini mwanya mkubwa usiotiliwa shaka ni wa udanganyifu kwenye mishahara ya wafanyakazi.

Uchunguzi uliofanywa na JAMHURI umebaini kuwa katika benki moja ambayo kwa sasa jina lake tunalihifadhi kwa sababu za kitaaluma, Leopard Tours wamekuwa wakiingiza mishahara ambayo kiwango chake kinatofautiana mno na kile kinachosainiwa na kupokewa na waajiriwa dirishani.

Imebainika kuwapo kwa wafanyakazi wanaolipwa hadi dola 1,000 (Sh milioni 2.2) kwa mwezi, lakini hawakatwi chochote kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii, na pia hawakatwi kodi.

Kwa mfano, mmoja waliokuwa wafanyakazi mwenye jina la Kivuyo, katika bank statement inaonyesha kuwa Leopard Tours wanamwingizia Sh 600,000 kama mshahara wake kwa mwezi, lakini kwenye nyaraka za ofisini kwa Fazal, mshahara wake anaosaini ni Sh 150,000.

Kiasi hicho kinakatwa Sh 15,000 kwa ajili ya NSSF na yeye anabakiwa na Sh 135,000. Kwa mbinu hiyo, Leopard Tours wamekuwa hawalipi kodi serikalini ya P.A.Y.E kwa kuwa kiwango cha chini kilichoidhinishwa kisheria kukatwa kodi ni Sh 170,000.

Mtumishi mwingine, Salum Said Mohamed, kuna habari kuwa alilazimishwa kuandika barua ya kuacha kazi wakati huo akiwa analipwa Sh 600,000 kwa mwezi.

Kama ilivyo kwa Kivuyo, naye alifanyiwa ‘mchezo’ kama huo. Aliajiriwa mwaka 2008, lakini nyaraka zinaonyesha kuwa fedha zake za NSSF zilianza kuwekwa mwaka 2011. Ushahidi mwingine wa kuthibitisha madai hayo ya ukwepaji kodi yako kwa mtumishi mwingine, Oswald Kimolo. Kwa jumla wafanyakazi wote, wakiwamo madereva wanaofikia 300, mtindo wa malipo na ukwepaji kodi ni huo huo.

“Suala la Leopard Tours kuhusu kodi liko wazi, sisi hapa TRA hatuwezi kulishughulikia kwa sababu mtandao wa wake ni mkubwa sana hapa Arusha, labda kama inawezekana waje wakaguzi kutoka Dar es Salaam,” kimesema chanzo chetu ndani ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) jijini Arusha.

Madai ya unyanyasaji

Watumishi wanalalamika kunyanyaswa na uongozi wa Leopard Toures kwa masuala mbalimbali. Ufuatao ni baadhi ya ushuhuda walioutoa kwa JAMHURI walipohojiwa.

Pancha

“Ni jambo la kawaida kwa gari kupata pancha, ila katika kampuni ya Leopard ikitokea pancha ni lazima dereva atalipishwa tairi jipya kwa kukatwa katika mshahara wake gharama ya kununua tairi jipya.

“Cha ajabu ni kwamba hata ukilipishwa tairi jipya, lile la zamani ambalo unaambiwa umeliharibu hupewi, wanalichukua wao na kwenda kwa dealer aliyewauzia kudai walipwe jipya.

“Huu ni unyanyasaji, na bado ukidai risiti ya ulichokatwa au kulipia hupewi,” anasema mmoja wa madereva.

Vioo vya gari

“Kutokana na field yetu huwa tunapita barabara mbaya, mfano ukipishana na gari lingine porini kwa bahati mbaya hilo gari likarusha jiwe na kukuvunjia kioo ni lazima utalipishwa kioo kipya- utake usitake. Fazal atamwamrisha Mhasibu Mkuu, Joel Mmbaga, akukate kwenye mshahara. Shock absorber, spring vikivunjika dereva analipa,” amedai dereva mwingine.

Ajali

Dereva mwingine anasema: “Kitu cha ajabu na cha kusikitisha ambacho kinatuuma ni pale inako imetokea ajali barabarani- iwe umesababisha dereva au gari jingine limekugonga wewe, ni lazima utalipishwa gharama zote za kulitengeneza hilo gari bila kujali kama hilo gari lina bima, ndiyo maana magari ya Leopard mengi yana bima ndogo maana wanajua kuwa litakalotokea dereva atalipa. Akikataa atawekwa rumande au kufukuzwa.

“Wapo madereva wenzetu waliofanyiwa haya, na ushahidi upo, lakini tunamwonyesha nani ambaye ataweza kusimamia haki na kututetea sisi madereva?

“Kwa mfano dereva anayeitwa Frank Mollel aligongwa gari lake. Baada ya kupimwa ajali alipelekwa polisi, ingawaje yeye ndiye aliyegongwa; ila yeye ndiye aliyewekwa rumande kwa amri ya Fazal.

“Kesi ilipelekwa mahakamani akapigwa faini na kesi ikaisha ila cha ajabu huyu dereva aliporudi kazini alikutana na invoice ya kutengenezea gari. Akatakiwa alipe. Ushahidi upo.

“Kuna dereva mwingine anayeitwa Mzee Lyimo, alipata ajali Musoma kwa kugongwa na basi nyuma na wageni wakafa, ila alitakiwa alilipe hilo gari na akafukuzwa kazi.

“Silva Justine akiwa safarini mbugani na wageni aliugua ghafla usiku saa 6, ikabidi atumie gari analoliendesha la kampuni ili aende kutafuta matibabu hospitali ya karibu na Serena (Manyara) - umbali kaka kilometa 3 kwenda na kurudi.

“Aliporudi ofisini aliadhibiwa kwa ‘kosa’ la kutumia chombo cha kampuni kwa matumizi yake, na alikatwa kwenye mshahara wake dola 150 kwa sababu analipwa kwa dola za Marekani,” kimesema chanzo chetu.

Viambatanisho vya madai na malipo ya fedha hizo, JAMHURI inavyo.

Chanzo chetu kimeongeza: “Wako madereva wengine wamepoteza kazi kutokana na ajali na kutokukubali kulipia hizo gharama na wapo madereva wengine ambao wanaendelea na adhabu.”

Mafao kwa wazee

Uchunguzi ulifanywa na JAMHURI umebaini kuwa baadhi ya watumishi, hasa madereva waliostaafu au kufukuzwa kazi; ama wamekuwa wakikosa mafao yao kwenye mifuko ya kijamii, au wanaambulia kiasi kidogo mno.

Imebainika kuwa mmoja wa madereva aliyefanya kazi kwa karibu miongo miwili (miaka 20), Lucas Kivuyo alipowenda NSSF aliambulia Sh 800,000 tu.

Polisi watuhumiwa

Kuna madai kutoka kwa wafanyakazi kwamba Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, haliwezi kuchukua hatua zozote dhidi ya wamiliki na viongozi wa Leopard Tours kila wanapopelekewa malalamiko.

Baadhi ya wafanyakazi wamesema tofauti na ilivyozoeleka, Leopard Tours wakiwahitaji polisi, badala ya kuwafuata, polisi ndiyo huitwa kwenda kupewa ‘maelekezo’.

“Hapa ofisini polisi kuanzia wa vyeo vya chini hadi vya juu kabisa mkoa wanaitwa, na wanakuja hapa. Inasikitisha kuona polisi wakifika wanadiriki hata kumpigia saluti (jina linatajwa). Kama kuna wafanyakazi au mfanyakazi anayeonekana ‘mjuaji’, polisi wanaamuriwa wamkamate, na wao wanatii bila tatizo.

“Kuna magari mengi ya Jeshi la Polisi na ya maofisa wa polisi yanayofanyiwa matengenezo kwenye karakana ya Leopard Tours. Ni nadra sana gari la Leopard Tours kukamatwa barabarani, anayethubutu kulikamata atakiona cha moto,” kimesema chanzo chetu.

Majina ya polisi wanaotajwa tajwa kwenye sakata hili ni ya Faustine na Njau. Maelezo zaidi, pamoja na majina yao ya pili vitachapishwa kwenye JAMHURI matoleo yajayo baada ya kuzungumza nao.

Msemaji wa Leopard Tours, Mmbaga, ametafutwa lakini hakuwa tayari kupokea simu.

Mapema mwezi huu, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ajira, Kazi na Vijana, Anthony Mavunde, katika ziara yake ya ghafla katika kampuni hiyo alipewa taarifa nyingi zinazoelezwa kwa zilikuwa za kumpotosha.

Kati ya taarifa hizo ni zile zilizohusu mishahara ya watumishi ambako Msemaji wa Leopard Tours, Mmbaga, alisema mishahara ya watumushi wa kampuni hiyo ni kati ya Sh 150,000 na Sh 300,000 kwa mwezi.

Uchunguzi wa kina uliofanywa na JAMHURI umebaini kuwa kuna tofauti kubwa kwenye mikataba ya ajira; na hati ya malipo kwa wafanyakazi wa Leopard Tours. Kilichoandikwa kwenye mikataba si kile kinacholipwa na kuonyeshwa kwenye hati ya malipo ya wafanyakazi ya kila mwezi.

“Nadhani Fazal anadhani kuwa hii serikali ni sawa na zile zilizopita Leopard Tours imesema kuwa inawalipa mishahara wafanyakazi wake kati ya Sh 150,000 na Sh 300,000. Hii siyo kweli kabisa tunaweza kuthibitisha hilo kwa sababu sisi guides tunalipwa kati ya dola 500 (Sh milioni 1.09) na dola 1,000 (Sh milioni 2.18) kwa mwezi,” amesema mmoja wa wafanyakazi wa Leopard Tours.

Pia uchunguzi umebaini kuwapo kwa idadi kadhaa ya raia wa kigeni katika kampuni hiyo wanaofanya kazi zikiwamo za kufungua malango na ulinzi; ambazo zingefanywa na Watanzania.

UDA-RT kuanza kuuza hisa mwezi Machi

Robert Kisena
Robert Kisena
MWENYEKITI wa Kampuni ya Simon Group, Robert Kisena, amesema UDA-RT imewekeza zaidi ya Sh bilioni 90 na kuanzia Machi mwaka huu kuna mpango wa kuanza kuuza hisa kwenye Soko la Hisa.

Pamoja na hali hiyo kampuni hiyo imeweka wazi wamiliki halali wa UDA wanaotambulika kwa mujibu wa sheria.

Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Karimjee Dar es Salaam jana kuhusu tuhuma kwamba Kampuni ya Simon Group ilipata upendeleo kununua Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA), pamoja na kutoa ufafanuzi wa wanahisa halali kwa mujibu wa sheria.

Alisema hivi sasa kampuni hiyo imejikita katika kuhakikisha Mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi, unaanza kwa wakati sambamba na uuzaji wa hisa.

Kisena alisema kuna mpango wa kuuza asilimia 70 ya hisa zake kwenye soko la hisa.
“Tunatarajia kupata Sh bilioni 600 ambazo zitatumika kujenga maegesho ya magari ambayo yatakuwa na huduma nyingine kama maduka na kadhalika,” 
alisema Kisena. Alisema wamiliki wa mabasi 138 ya dalalala wameshalipwa fidia ya Sh bilioni mbili ambako kila basi limelipiwa Sh milioni nne na katika fedha hizo Sh milioni moja zitabaki kama hisa.

Akizungumzia suala la umiliki wahisa wa familia ya Rais Kikwete katika UDA, alisema ni vema washindani wake wa biashara wamwache Rais mstaafu Jakaya Kikwete apumzike kwa kuwa hahusiki katika biashara zake.

Kisena alisema kuna watu wanataka kumchafua yeye katika biashara huku akiwataka wasimhusishe Rais Kikwete, badala yake wamshambulie yeye bila kuhusisha wala kuumiza watu wengine ambao hawana uhusiano na biashara zake.
“Kama kuna watu wana ugomvi wa siasa na Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, washambuliane wao kwa wao huko huko, wasitumie kampuni yangu kama jukwaa la mashambulio hayo.
“Mimi niliacha siasa tangu mwaka 2010… nilipongombea nikashindwa nimebaki kuwa mwanachama hai na mwaminifu kwa CCM,” 
alisema na kuongeza:
“Kampuni hii tumeipa jina la marehemu baba yangu, Mzee Simo.
Tangu imeanzishwa imekuwa kampuni ya familia, wamiliki wake ni mimi, mdogo wangu William Simon, mpwa wangu Kulwa Simon, ndugu yangu Ngalula Saguda, mke wangu na watoto wangu, imekuwa hivyo tangu ianzishwe na haijabadilishwa”.
Akizungumzia ununuzi wa hisa katika za UDA, alisema alinunua hisa zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya kuuzwa (allotted shares) kwa Sh bilioni saba mwaka 2011.

Alisema baadaye mwaka 2013 alinunua hisa za Halmashuri ya Jiji la Dar es Salaam ambazo zilikuwa ni asilimia 24 ya hisa zote za UDA, kwa Sh bilioni 5.8.

Imekanushwa! Taarifa inayodai Rais Magufuli atahudhuria kumbukumbu ya vifo vya wakina Odinga


Kumekuwepo na habari za uongo na potofu katika mtandao wa jamii wa www.kenya-today.com kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli atazuru Kenya kuhudhuria kumbukumbu ya marehemu Mhe. Jaramongi Odinda na Fidel Odinga Jumamosi hii.

Inasikitisha kuona kwamba mwandishi wa Kenya anachukua nafasi ya Mwanahabari wa Rais wa Tanzania kwa kuwa na ratiba ya Mhe. Rais wa Tanzania kuliko Watanzania wenyewe.

Haijulikani ni nini has nia ya mtandao huo, lakini ukweli ni kwamba ratiba hiyo ni batili na ya uongo uliotukuka. Hawa watani wetu wa jadi wana lao jambo!

Wapuuzeni. Taarifa hiyo si ya kweli.

  • Tumeshirikishwa na Muhidin Issa Michuzi

Taarifa ya habari ChannelTEN, 27.01.2016Tanzanian Immigration Services introduced Business Visa and Pass

The Immigration Services Department has introduced Business Visa and Business Pass after abolishing the Carrying On Temporary Assignment Pass (CTA) following a number of shortcomings.

The spokesperson of the Department, Deputy Commissioner Abbas Irovya, said in a statement to the press in Dar es Salaam that the Business Visa and Business Pass would not be issued to foreigners who are entering the country for employment purpose.

“Those who are entering the country with such purpose will be required first to apply for the work permit to the Department of Labour before landing the job,” said the deputy commissioner.

Mr Irovya pointed out that the 90-day Business Visa would be issued to foreigners who come from the country whose citizens require entry visa and that the period would not be extended after the visa expiry.

“The Business Pass which lasts for 90 days will be issued to foreigners who come from the country whose citizens require visa while entering the country,” he observed.

Mr Irovya said the Immigration Department has started to issue Business Visa at USD 250 and the Business Pass at USD 200 since January 15 this year.

He pointed out further the Business Visa and Business Pass would be issued under the permit of Commissioner General of Immigration through the Immigration Services Headquarters, the Office of Immigration Commissioner in Zanzibar, Entry Points and Tanzania Missions abroad.

As for CTA, the Deputy Commissioner said the government was working on shortcomings in issuing of the CTA, saying the government has already amended Visa Regulations to improve the CTI issuing.

Mr Irovya said the government started to review the 1997 Immigration Regulations with the purpose to solve challenges facing the CTA issuing, saying the Minister for Foreign Affairs has already signed the amendment of the regulations to improve the CTA issuing.

“The Home Affairs Minister has already signed the new regulations ready to be published in the government gazette,” he said.
  • via The Daily News
Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Naibu Kamishna Abbas Irovya, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu kuanza kutoa hati za Business Visa na Business Pass kwa ajili ya wageni wanaoingia nchini kwa shughuli za muda mfupi. Wa pili kulia ni Mrakibu Mwandamizi wa idara hiyo, Philou Kyetema. (Picha na Kassim Mbarouk - www.bayana.blogspot.com)

IDARA ya Uhamiaji inapenda kuwataarifu Wananchi na Wadau wote wa huduma za uhamiaji kama ifuatavyo;

1. Idara ya Uhamiaji hapo awali ilikuwa ikitoa hati iliyojulikana kama “Carrying On Temporary Assignment Pass” maarufu kama CTA,ili kuwawezesha Raia wa kigeni wanaoingia nchini kwa shughuli za muda mfupi kufanya shughuli zao. Utoaji wa CTA ulisitishwa tarehe 16 Desemba 2015, baada ya kubainika changamoto za kiutendaji ikiwemo ukiukwaji wa Taratibu za Utoaji wa Hati hiyo na hata matumizi yake.

2. Baada ya kusitishwa utoaji wa CTA, zilijitokeza changamoto mbali mbali ambazo kwa kiasi zilisababisha usumbufu kwaRaia wa kigeni ambao waliingia au walikuwa wanataka kuingia nchini kwa shughuli za muda mfupi “Short Term Business Activities”.

3. Idara ya Uhamiaji inapenda kuwafahamisha Wananchi na Wadau wa huduma za uhamiaji kuwa, tokea mwezi Machi 2015 ilikwishaanza mchakato wa kurekebisha Kanuni za Uhamiaji za mwaka 1997, kwa lengo la kufanyiakazi changamoto zilizojitokeza katika utoaji wa CTA. Tayari marekebisho ya Kanuni hizo yamekwishasainiwa na Mhe. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na taratibu za kuzitangaza katika Gazeti la Serikali zinaendelea ikiwemo kupitisha Kanuni zinazosimamia utoaji wa Visa (Visa Regulations).

4. Kwa taarifa hii, Idara ya Uhamiaji inapenda kuwafahamisha wananchi na wadau wa huduma za Uhamiaji na Raia wa kigeni wanaotakakuingia nchini kwa shughuli za muda mfupi kuwa Mhe. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mamlaka aliyonayo kupitia kifungu cha 33 cha Sheria ya Uhamiaji Na. 7 ya mwaka 1995 (Sura ya 54 Rejeo la 2002) ameidhinisha Idara ya Uhamiaji kuanza kutoa Business Visa kwa ada ya dola za Kimarekani mia mbili na hamsini (USD 250), na Business Pass kwa ada ya Dola za Kimarekani mia mbili (USD 200), kuanzia tarehe 15 Januari, 2016 wakati utaratibu wa kurasimisha utoaji wa hati hizi katika Kanuni unaendelea.

5. Hati hizi “Business Visa na Business Pass” zitatolewa kwa idhini ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji kupitia mamlaka zifuatazo;

i. Ofisi ya Uhamiaji Makao Makuu
ii. Ofisi ya Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar
iii. Vituo vya Uhamiaji vya kuingilia nchini “Entry Points”
iv. Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nje ya nchi (Tanzania Missions Abroad).

6. “Business Visa” itatolewa kwa wa siku tisini (90), kwa raia wa kigeni wanaotoka katika nchi ambazo raia wake wanahitaji Visa kuingia nchini na haitaongezwa muda.

7. “Business Pass” itatolewa kwa muda wa siku tisini (90), kwa raia wa kigeni wanaotoka katika nchi ambazo raia wake hawahitaji Visa kuingia nchini na haitaongezwa muda.

8. “Business Visa na Business Pass” hazitatolewa kwa raia wa kigeni wanaokuja nchini kwa madhumuni ya kupata ajira, kwani wageni wa aina hiiyo wanapaswa kabla ya kuajiriwa kuomba kibali cha Kazi kutoka Idara ya Kazi.

26 Januari, 2016.

IMETOLEWA NA
KITENGO CHA UHUSIANO
MAKAO MAKUU YA IDARA YA UHAMIAJI

Taarifa ya Polisi Arusha kuhusu habari ya gazetini: “Waendesha bodaboda Arusha waandamana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha SACP Liberatus Sabas amekanusha habari iliyoandikwa na gazeti la Jambo Leo la Januari 27, 2016 lenye kichwa cha habari “Waendesha bodaboda Arusha waandamana.”

Akiongea kwa njia ya simu Kamanda Sabas alisema hakukuwa na maandamano yoyote ya bodaboda jijini Arusha zaidi ya vijana wachache waendesha bodaboda waliojikusanya kwa Mkuu wa Mkoa.

Kamanda Sabas amesema kuwa, wapo katika operesheni ya waendesha bodaboda ambao wamekuwa wakivunja sheria za barabarani mara kwa mara. Operesheni hiyo ni ya nchi nzima na wameianza Januari 14, 2016.

“Mpaka sasa tumekusanya sh. mil. 21,330,000 ambazo zimetokana na makosa mbalimbali yanayofanywa na waendesha bodaboda wawapo barabarani, makosa hayo ni kutovaa kofia ngumu, kutokuwa na leseni ya udereva, kubeba abiria zaidi ya mmoja, kutokuwa na kadi za pikipiki na kadi za bima,” alisema Kamanda Sabas.

Kamanda Salas amesema kuwa wasingeweza kukusanya kiasi hicho cha pesa kwa kipindi hicho kifupi kama askari polisi wangekuwa wakichukua pesa hizo kwa maslahi yao wenyewe, ila wamekuwa wakiziingiza katika vitabu vya Polisi.

Aidha Kamanda Salas amesema hakuna dereva wa bodaboda anayedaiwa cheti cha udereva bali wametakiwa kuonyesha leseni zao za udereva kwani ndizo zinazothibitisha kwamba wamepitia vyuo vya udereva.

Kamanda Salas amewataka madereva wa bodaboda ambao bado hawajapitia vyuo vya udereva wakajifunze udereva ndipo waendeshe bodaboda na amewaambia kuwa ili wasikamatwe na askari polisi basi wasivunje sheria za barabarani.

  • Lilian Lundo – Maelezo.

Picha kutoka Bungeni: Mkutano XI, Kikao cha Januari 27, 2016


Waziri Mkuu, Kassim Majalliwa akiteta na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama Buneni mjini Dodoma Januari 27, 2016.


Spika wa Bunge, Job Ndugai (kulia) akimwapisha Waziri wa Elimu , Sayansi, Tekinolojia na Mafunzo ya Ufundi Joyce Ndarichako, bungeni mjini Dodoma Januari 27, 2016.


Waziri wa Habari,Utamaduni, Wasanii,na Michezo Nape Nnauye akitoa kauli Bungeni mjini Dodoma Januari 27, 2016.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, Bungeni mjini Dodoma January 27, 2016.


Mwenyekiti wa Bunge, Mtemi Andrew Chenge akiongoza kikao cha Bunge mjini Dodoma Januari 27, 2016.


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na wabunge kwenye jengo la Utawala la Bunge mjini Dodoma Januari 27, 2016. Kutoka kushoto ni Ruth Mollel wa Viti Maalu Chadema, Hawa Mwinga wa Viti Maalum Cahdema na Ali Saleh wa Malindi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Chenge achaguliwa kuwa mmoja wa Wenyeviti wa Bunge

Mwenyekiti wa Bunge, Mtemi Andrew Chenge akiongoza kikao cha Bunge mjini Dodoma Januari 27, 2016. (picha: Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, ambaye aligombea uspika mwaka 2010 akisema anataka kutibu majeraha yaliyoliumiza Bunge, Taifa na CCM kutokana na kashfa mbalimbali, amechaguliwa kuwa mmoja wa wenyeviti watatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.

Chenge, ambaye alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kabla ya kuingia bungeni na kuteuliwa kuwa waziri aliouachia wakati kashfa ya ununuzi wa rada ilipopambamoto, ataongoza Bunge kwa nafasi ya mwenyekiti akiwa na Dk Mary Mwanjelwa na Najma Murtaza, ambao walikuwa wagombea pekee wa nafasi hizo.

Hata hivyo, ilibidi Spika Job Ndugai amuokoe kwa kuzima swali lililohusu kashfa ya uchotwaji wa Sh306 bilioni kutoka akaunti ya Tegeta Escrow lililoulizwa na mbunge kutoka Chadema, Latifa Chande.

Chenge alitajwa kwenye kashfa ya ununuzi wa rada baada ya taasisi ya Uingereza inayoshughulikia makosa makubwa ya jinai, kubaini kuwa alikuwa na dola 1 milioni kwenye akaunti yake iliyokuwa mjini Jersey, fedha zilizohusishwa na ununuzi wa rada hiyo ambayo bei yake ilikuzwa.

Kashfa hiyo ilimfanya Chenge alazimike kujiuzulu nafasi ya Waziri wa Miundombinu mwaka 2008, lakini Novemba, 2010 Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ilimsafisha na siku chache baadaye akagombea tena ubunge na kushinda.

Wakati huo aligombea uspika akisema: “Nagombea kiti cha uspika nikiamini kwamba ninao uwezo wa kutibu majeraha makubwa yaliyoumiza Bunge na Taifa, wananchi na chama changu kwa sababu tu ya kuwa kiongozi aliye tayari kujitafutia na kujitwalia umaarufu au ushujaa binafsi kwa njia ya kuwahujumu, kuwaumiza na kuwachafua wengine kwa kutengeneza tuhuma na kashfa za kila namna. Tiba ya uongozi wa aina hii ni kuchagua kiongozi bora wa Bunge.”

Hakueleza kuwa aliyekuwa akimtuhumu ni Samuel Sitta, spika wa Bunge la Tisa ambalo liliboresha kanuni na kuruhusu mijadala moto, hasa ya kashfa dhidi ya viongozi wa Serikali na kusababisha mawaziri kujiuzulu.

Mwaka juzi alijikuta kwenye kashfa ya Tegeta Escrow baada ya kubainika kuwa aliingiziwa Sh1.6 bilioni na mmoja wa wamiliki wa IPTL na kusababisha apelekwe kwenye Baraza la Maadili la Viongozi wa Umma, ambako alijaribu kulizuia lisimhoji kwa kuomba ufafanuzi Mahakama Kuu, lakini aligonga mwamba na kurejeshwa kuhojiwa.

Kashfa hiyo ilimfanya avuliwe uenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Bunge, lakini alirejea tena bungeni baada ya uchaguzi wa mwaka jana.

Jana, Chenge ambaye aliwahi kujiita “nyoka wa makengeza” wakati wa kashfa ya Escrow, pamoja na wenzake wawili walikuwa wagombea pekee wa nafasi hiyo ya mwenyekiti ambayo hushikwa na watu watatu wanaomsaidia Spika kuendesha chombo hicho cha kutunga sheria.

Mara baada ya Dk Mwanjelwa kumaliza kujieleza mbele ya wabunge na kuulizwa maswali, Chenge alifuatia na alianza kubanwa swali la Mbunge wa Ndanda (Chadema), Cecil Mwambe.

“Katika Bunge lililopita CCM na wabunge walikuwajibisha kwa kashfa ya Escrow na sasa hivi unaomba kuwa mwenyekiti, siku ukiwa unaliongoza Bunge hili na hoja ya hiyo ikarudi bungeni je Utatenda haki katika kulisimamia Bunge? “ alihoji Mwabe.

Huku akicheka, Ndugai alisema hilo siyo swali jambo ambalo liliwafanya wabunge kupinga, huku wengine wakicheka. Hata hivyo alimruhusu Chenge kujibu.

“Bunge linaongozwa na kanuni na pale ambapo inakuja hoja bungeni au katika kamati zetu na inaonekana kuna masilahi fulani au inakuhusu mwenyewe, ni busara tukazingatia kanuni,” alisema Chenge.

“Ni vyema nafasi (ya mwenyekiti) ikashikwa na mwingine ili shughuli za Bunge zisiwe na makandokando yoyote. Ningeweza kusema zaidi ya hapo ila naomba niishie hapo.”

  • via MWANANCHI

Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge, jana alipata wakati mgumu Bungeni mjini hapa, baada ya wabunge wa upinzani, kumbana kwa maswali juu ya kashfa ya Tegeta Escrow, iliyoibuliwa wakati wa Bunge la 10.

Chenge alikutwa na masahibu hayo wakati wa kujieleza na baadaye kuulizwa maswali alipokuwa akiomba kura kwa ajili ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa bunge. Mwanasheria huyo mkongwe alipendekezwa na Kamati ya Uongozi wa Bunge kuwania nafasi hiyo.

Baada ya kujieleza ili kushawishi wabunge wamchegue katika nafasi hiyo, ulifika wakati wa maswali ambapo wapinzani walimuuliza kuhusu kashfa ya Tegeta Escrow.

Hatua hiyo ilisaababisha kuchafuka kwa hali ya hewa ndani ya bunge baada ya kuibuka zomeazomea kati ya wabunge wa CCM waliokuwa wakipinga baadhi ya maswali ya wale wa upinzani walioonekana kumkamia Chenge.

Bunge lililopita baada ya kujadili ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kuhusu miamala iliyofanyika kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow, iliyokuwa imefunguliwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), lilipitisha maazimio manane likiwamo la kuwajibishwa viongozi wa serikali na wale wa Kamati za Bunge walioonekana kuhusika katika kashfa hiyo.

Viongozi wa kamati ambao Bunge liliazimia wawajibishwe ni pamoja na Chenge, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti. Wengine ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Katiba, Sheria na Utawala, William Ngeleja, na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Victor Mwambalaswa.

Katika kashfa ya Escrow, Chenge alidaiwa kupokea Sh. bilioni 1.6 kutoka kwa james Rugemalira, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya VIP Engineering and Marketing Limited, iliyokuwa na asilimia 30 kwenye Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), inayodaiwa kuuzwa kinyemela kwa Kampuni ya Pan African Power (PAP).

Jana, hali ya hewa bungeni ilianza kuchafuka pale Chenge alipomaliza kujieleza kwa wabunge na Spika Job Ndugai kuruhusu aulizwe maswali, hatua iliyofanya wabunge wengi wa upinzani kusimama kutaka kupewa nafasi huku wale wa CCM wakiwa wameketi.

Mbunge wa kwanza aliyepata nafasi ya kuulizwa swali ni wa Ndanda (CHADEMA), Cecil Mwambi, ambaye alimtaka Chenge kujibu suala la Escrow likirudi bungeni, kama ataweza kulisimamia ilhali aliwajibishwa na Bunge kwa sababu ya kashfa hiyo.

Akijibu swali hilo, Chenge alisema Bunge linaendeshwa kwa kanuni ambazo baadhi yake zinasema kama kuna suala linajadiliwa na una masilahi nalo, ni vyema ukakaa pembeni na kuacha lijadiliwe.

“Linapokuwa suala ambalo una maslahi nalo, ni bora ukakaa pembeni ili uendeshwaji wa shughuli za Bunge usiwe na makandokando, ningeweza kuendelea kuzungumza sana, lakini ngoja niishie hapa,” alisema Chenge.

Baada ya swali hilo, Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Latifah Chande, alikoleza moto kwenye hoja ya Escrow alipomwuliza Chenge kama haoni kuwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Bunge ilhali alikuwa kwenye kashfa hiyo ambayo ilijadiliwa na wananchi walio wengi, kutashusha hadhi ya chombo hicho cha kutunga sheria.

“Huoni kwamba wananchi watakosa imani na Bunge hili litakalokuwa likiongozwa na mtu kama wewe?” alihoji Latifah.

Swali hilo lilionekana kuwasha moto zaidi bungeni huku wale wa CCM wakianza kupiga kelele kwa kudai kwamba hilo si swali.

Spika Ndugai aliyekuwa akiongoza kikao hicho cha asubuhi, hakutoa nafasi kwa Chenge kujibu swali hilo na badala yake akamruhusu Mbunge wa Mtwara Vijijini (CCM), Hawa Ghasia, kuuliza swali lingine.

“Ratiba inaonyesha baadaye kutakuwa na mjadala wa kuchangia hotuba ya rais na wakati alivyokuja kuhutubia hapa kuna watu walitoka nje ya Bunge. Je, ukiwa mwenyekiti utawaruhusu kuchangia hotuba hiyo?” aliuliza Hawa.

Swali hilo lilionekana kuwakera wabunge wa upinzani ambao walianza kumzomea mbunge huyo huku wengine wakisema “ndiyo maana uliachwa (kwenye uteuzi wa mawaziri),… umekosa sifa.”

Swali hilo lilijibiwa na Ndugai aliyesema kila mbunge atakuwa na haki ya kuchangia kwenye hotuba hiyo ya Rais.

Wengine waliopendekezwa na Kamati ya Uongozi kuwania nafasi hiyo ni, Mary Mwanjelwa na Najima Murtaza Giga.

Mbali na uenyekiti wa Bunge, Chenge pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo.

Kwa kuwa wenyeviti wa Bunge wanaotakiwa ni watatu na waliopendekezwa kushika nafasi hiyo ni idadi hiyo hiyo, wabunge hawakupiga kura na badala yake, baada ya kujieleza na kuulizwa maswali, spika alihoji Bunge zima juu ya wanaokubali kuwa wabunge hao washike nafasi hizo.

Wenyeviti wa Bunge pamoja na mambo mengine, huongoza vikao vya Bunge pale spika na naibu wake wanapokuwa hawapo bungeni na wakishachaguliwa hushika nafasi hiyo kwa miaka miwili na nusu.

Hali ya Zanzibar
Wabunge wa upinzani waliopata nafasi ya kuchangia hotuba ya Rais John Magufuli, pamoja na mambo mengine, walizungumzia hali ya kisiasa Zanzibar wakisema ni vyema ikashughulikiwa mapema.

Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea (CUF), alisema kitendo cha Rais Magufuli kwenye hotuba yake ya ufunguzi wa Bunge kusema suala la Zanzibar linashughulikiwa na CCM na CUF, kinaonyesha kwamba anajitoa kwenye mgogoro huo.

Alisema maelezo hayo ya Rais juu ya Zanzibar yaliyo ukurasa wa 10 wa hotuba yake, yanaaonyesha kwamba anataka kulikwepa suala hilo.

“Jambo kama hili utaliachaje kwa Serikali ya Zanzibar? Sehemu moja ya Muungano ikiingiwa na machafuko kwingine hakutakuwa salama,” alisema.

Naye Mbunge wa Mbozi (Chadema), Paschal Haonga, aliitaka serikali kutangaza mapema mshindi pindi uchaguzi unapofanyika kwa kuwa mara nyingi hali ya kuchelewesha matokeo huleta machafuko.

Alisema anashangaa Rais Magufuli kusema uchaguzi ulikuwa huru na ulitawaliwa na amani wakati kuna sehemu watu wamekimbia makazi yao kwa sababu ya uchaguzi na mpaka sasa hali ya Zanzibar haieleweki.

Mbunge mwingine aliyezungumzi hali ya Zanzibar ni Suleiman Sadick wa Mvomero (CCM), ambaye alisema ni vyema Rais Magufuli akaachwa aendelee na mambo mengine huku Wazanzibari wakijiandaa na uchaguzi wa marudio.

“Uchaguzi wa Zanzibar ni wa kisheria na umefutwa kwa sababu ya mizengwe iliyokuwapo. Tusubiri Machi 20 uchaguzi wa marudio ufanyike. Sisi tuwaombee Wazanzibari uchaguzi mwema,” alisema.


Mbali na mambo mengine, Mbunge wa Temeke, Mtolea, alipokuwa akichangia alisema Rais Magufuli badala ya kusema tu ataanzisha Mahakama ya Mafisadi, ajikite kuhakikisha kesi za watuhumiwa wa wauaji wa albino zinaendeshwa haraka na waliohukumiwa kunyongwa wanyongwe.

Alisema Rais ndiye mwenye mamlaka ya kuruhusu watu hao kunyongwa na hatia hiyo itasaidia kupunguza vitendo hivyo vya mauaji.

  • via NIPASHE

Ombi la Diwani wa kata ya Mkuzi, Tanga kwa Mustafa Sabodo

Mimi ni Diwani wa kata ya mkuzi ([email protected]) wilayani muheza mkoani Tanga, katika kata yetu tunashida sana ya maji. 
Wakinamama wanatembea umbali mrefu kutafuta maji nawanaondoka kuanzia saa kumi na moja alfajiri na kurudi nyumbani saa nne au tano asubuhi na ndoo moja tu ya maji, na pengine maji hayo si salama kwani visima vyenyewe ni vya kiasili vipo wazi.

Hivyo basi mzee Sabodo kwa imani yako naomba kwa niaba ya wananchi wa kata ya Mkuzi Halmashauri ya wilaya ya Muheza, tunaomba msaada huo wa kuchimbiwa visima, ili wananchi wa Kata hiyo ya Mkuzi tuondokewe na adha hiyo.
Imeawasilishwa hapa kupitia ukurasa wa 'contact'.

Tangazo: Nyaraka (vitambulisho, kadi) za Edda Mushi zimeokotwa


Picha ya msichana huyo kwenye moja ya vitambulisho vyake.


Mkoba wa mtu anayesadikika kuwa ni wa binti anayetambulika kwa jina la Edda J Mushi (pichani), umeokotwa maeneo ya Kota za Jeshi, Mtaa wa Nzasa, Mwenge jijijni Dar ambapo ndani yake kuna kadi ya benki ya CRDB na NMB, Kitambulisho cha kupigia kura, Kitambulisho cha NHIF huku kukiwa na kipochi kidogo.

Yeyote anayemfahamu binti huyu anaombwa ampe taarifa au apige simu kwenda namba 0683214128.

Kilichotokea baada ya kauli ya serikali ya kusitisha matangazo ya TBC "live" ya vikao vya Bunge

Mtafaruku umeibuka muda mfupi uliopita katika mkutano wa Bunge uliokuwa unaendelea mjini Dodoma.

Taarifa kutoka kwa waandishi wa habari waliokuwa ndani ya Bunge hilo zimeeleza kuwa polisi walilazimika kuingia ndani kuwatoa nje wabunge wa upinzani kufuatia maigizo ya mwenyekiti wa kikao hicho, Andrew Chenge, baada ya kukaudi amri ya kutoka nje.

Taarifa hizo zimeeleza kuwa awali, wabunge wa upinzani walipinga kuendelea kwa mjadala wa Bunge wakitaka kauli ya Waziri wa Habari, Utamaduni, sanaa na michezo, Nape Nnauye kuhusu TBC kutorusha ‘Live’ matangazo ya Bunge ijadiliwe kwanza.

Mwenyekiti wa Bunge alieleza kuwa huo haukuwa muda wa mjadala huo na kutaka Bunge liendelee na ratiba yake.

Hata hivyo, wabunge wanne pekee wa Upinzani ndio waliokuwa wametakiwa kutoka nje ya Bunge, lakini wabunge wote wa Ukawa waliwatetea na kuanza kuimba nyimbo mbalimbali. Hivyo, Mwenyekiti aliamuru wote watoke nje ili wabunge wengine waendelee kujadili hotuba ya Rais.

Mwandishi wa East Africa Radio aliyekuwa ndani ya Bunge alieleza kuwa Mwenyekiti wa Bunge aliondoka kwenye kiti chake wakati vurugu hizo zikiendelea na waandishi wa habari waliagizwa kutoka nje.

Wakati wa kiako cha asubuhi Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge amelazimika kuahirisha kikao cha Bunge mara mbili leo asubuhi baada ya wabunge wa upinzani kupinga hoja ya serikali ya kutorusha moja kwa moja shughuli zote za Bunge hicho kupitia TBC.

Vuta nikuvute hiyo ilitokana na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, kutoa kauli ya serikali kuwa TBC itapunguza muda wa kurusha matangazo ya moja kwa moja ya Bunge ili kupunguza gharama za uendeshaji wa kituo hicho cha luninga cha umma.

Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo) akiungwa mkono na wabunge wenzake kutoka kambi ya upinzani, alipinga hoja hiyo ya serikali na kumtaka Chenge asitishe mjadala wa hotuba ya Rais John Magufuli hadi hoja hiyo ya serikali itakapojadiliwa.

Zitto alisema TBC ni mali ya umma na inaendeshwa kwa kodi za wananchi ambao wana haki kuhabarishwa bila kuangalia gharama zinazotajwa na serikali kwani kituo hicho hakiendeshwi kibiashara.

Huku Chenge akijitahidi kumtuliza ili ratiba ya Bunge iendelee kama ilivyopangwa, Zitto aliungwa mkono na Halima Mdee, Mbunge wa Kawe (CHADEMA) hali iliyomfanya mwenyekiti huyo aliyechaguliwa jana kusema ataagiza Kamati ya Uongozi kujadili mara moja.

Kana kwamba hiyo haitoshi, wabunge wa upinzani walimjia juu Chenge kutaka Bunge lisiendelee kujadili hotuba ya Dk Magufuli iliyorushwa ‘live’ mwishoni mwa mwaka jana, mara baada ya kuapishwa kuwa rais wa nchi.

Baada ya malumbano yaliyoambatana na kurushina vijembe baina ya wabunge wa kambi ya upinzani na wale wa chama tawala, CCM, Chenge alisitisha kikao cha Bunge kwa saa moja kutafakari hoja hiyo.

Hata hivyo Chenge aliyesitisha kikao cha bunge kupisha Kamati ya Uongozi kukutana na kutoa mrejesho baada ya saa moja alilazimika kuahirisha tena Bunge hadi jioni.Polisi wakiwa wameimarisha ulinzi ndani ya Ukumbi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya wabunge wa upinzani kupinga hatua ya Serikali ya kupunguza matangazo ya moja kwa moja kutoka bungeni.


Hali ilivyokuwa ndani ya ukumbi wa Bunge.


Wabunge wakiwa wamesimama kupinga hatua ya Serikali kupunguza matangazo ya moja kwa moja ya kutoka Bungeni.

Kongamano lajadili mpango wa maendeleo wa Sekta ya Elimu 2017 - 2021

Salum Mnjagila akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano la kujadili ESDP. Kushoto ni Zulmira Rodrigues
Salum Mnjagila akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano la kujadili ESDP. Kushoto ni Zulmira Rodrigues

Na Rabi Hume wa Modewjiblog

Katika kuhakikisha elimu ya Tanzania inakua yenye ubora zaidi, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limepanga kuisaidia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi kuandaa Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP), mpango ambao umelenga kusaidia serikali ya Tanzania kutengeneza maudhui na mikakati ya kuendeleza elimu kwa upande wa Tanzania bara.

Akizungumzia mpango huo katika kongamano la siku mbili la kutambua vipaumbele vinavyotakiwa katika kuandaa mpango huo wa elimu, kwa niaba ya Kamishna wa Elimu wa Wizara ya Elimu, Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima na Elimu iliyo nje ya Mfumo rasmi kutoka Wizara ya Elimu, Salum Mnjagila alisema mpango huo unatarajiwa kufanya kazi kwa kipindi cha miaka mitano kwa kuanzia mwaka 2017 – 2021 ili kuona ni jinsi gani utabadili elimu ya Tanzania.

Alisema kupitia kongamano hilo wanataraji kuchagua baadhi ya vipaumbele ambavyo wataona vinaumuhimu zaidi kuanza navyo kwa miaka mitano ya kwanza kwa mpango huo na baadae wataanza utekelezaji wa vipaumbele ambavyo vitakuwa vimepewa kipaumbele na washiriki wa kongamano hilo.

“Tupo hapa kufanya tathimini ya vipaumbele ambavyo vimeletwa mbele yetu ili tufanyie uchambuzi na tuone ni vipaumbele vipi tutaviweka kwenye mpango wa miaka mitano katika kuboresha sekta ya elimu nchini,” alisema Mnjagila.

Nae Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara ya Elimu, Makuru Petro ambaye ameshiriki kufanya uchambuzi wa elimu ya Tanzania kwa kushirikiana na wataalamu kutoka UNESCO alisema katika kuchambua elimu ya Tanzania wamegundua kuwa elimu imekuwa ikishuka na hilo linatokana na kuongezeka kwa wanafunzi wanaosajiliwa kuanza shule huku kukiwa hakuna maboresho ambayo yanafanyika ili kuboresha elimu hiyo.

Alisema baada ya uchambuzi kufanyika wanafanya tathmini ili kupata matokeo ambayo watajadili kwa pamoja kwa kushirikisha wadau mbalimbali kutoka mashirika ya kiserikali na yasiyo ya serikali ili kupitisha vipaumbele ambavyo vitafanyiwa kazi kati ya vipaumbele ambavyo wao waliwasilisha kwa washiriki hao.

“Elimu ya Tanzania hali sio nzuri tumefanya uchambuzi hata mashuleni hakuna hali nzuri mfano hata Geita tumekuta darasa moja linatumiwa na wanafunzi 80 hadi 100 na hilo ni tatizo na baada ya kuchambua changamoto na kuzifanyia tathmini tunazileta hapa ili tuchague vipaumbele vya kuanza kuvifanyia kazi,” alisema Petro.

Nalo Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kupitia kwa Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa shirika hilo nchini, Zulmira Rodrigues alisema lengo la kuweka mpango huo ni kuboresha elimu ya Tanzania kwa kuifanya kuwa bora na iliyo na usawa kwa makundi yote ya jamii kwa matokeo mazuri ya baadae.

Alisema kuna mambo ambayo yanatakiwa kupewa vipaumbele ikiwepo ni pamoja na ubora wa elimu, fursa za elimu kwa makundi yote katika jamii na kujenga uwezo kwa watendaji ambao wanatoa hiyo elimu kama ni walimu basi wawe wanapewa mafunzo kuendana na wakati uliopo ili kuwa na kitu kipya ambacho kinahitajika kwa wanafunzi kwa wakati huo.Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusiana na kongamano hilo la siku mbili linalofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NACTE jijini Dar es Salaam.


Mkuu wa kitengo cha Ushirikiano wa Kiufundi kutoka Makao Makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini Ufaransa, Anton De Grauwe akiwasilisha vipengele mbalimbali vinavyotakiwa kujadiliwa na washiriki wa kongamano hilo katika kuandaa Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP) kwa mwaka 2017 - 2021.


Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akiwasilisha mambo mbalimbali muhimu yanayotakiwa kuzingatiwa kwenye Ajenda 2030 ya elimu na mpango wa utekelezaji katika kongamano la kujadili Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP).


Ofisa Mipango ya Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Jennifer Kotta (kushoto) akiteta jambo na Maofisa wenzake kutoka UNESCO, Faith Shayo (katikati) na Leonard Kisenha (kulia) wakati kongamano la kujadili Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP) kwa mwaka 2017 - 2021 likendelea.


Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara ya Elimu, Bw. Makuru Petro ambaye akishiriki kufanya uchambuzi wa elimu ya Tanzania kwa kushirikiana na wataalamu kutoka UNESCO kwenye kongamano hilo.


Mshauri wa Taasisi ya kimataifa ya mipango ya elimu (IIEP)/UNESCO, Barnaby Rooke akielekeza vipaumbele kwenye bajeti ya sekta ya elimu ambayo inahitaji maboresho makubwa ili kuleta mabadiliko kwenye sekta elimu nchini.


Moja ya 'Papers' zilizowasilisha kwa washiriki.


Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Elimu, Clifford Tandari akishiriki kwenye kongamano la kujadili Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP) kwa mwaka 2017 - 2021 linalofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za NACTE jijini Dar es Salaam.


Mwenyekiti wa Mtandao wa Redio za Jamii nchini (COMNETA), Joseph Sekiku akitoa maoni kuhusiana na udhaifu wa mipango ya sekta elimu nchini ambayo haitekelezeki wakati wa kongamano la kujadili Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP).


Bi. Helena Reutersward, kutoka Ubalozi wa Sweden kitengo cha Elimu akitoa maoni wakati wa kongamano la kujadili Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP) nchini linaloendelea katika ukumbi wa mikutano NACTE jijini Dar es Salaam.


Pichani juu na chini ni wajumbe walioshiriki kongamano hilo kutoka taasisi mbalimbali za serikali, Wizara ya Elimu, Taasisi za Elimu na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).


  • Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog

Tony Elumelu Found., UBA and USA-DOC partner to enable entrepreneurship in Africa


U.S Secretary of Commerce, Penny Pritzker; Select Tony Elumelu Foundation Entrepreneurs; Kehinde Yinusa, Evans George, Nosakhare Oyegun, Belema Alagun and Founder Tony Elumelu Foundation, Mr. Tony Elumelu during the panel and roundtable discussion between members of the U.S. Presidential Advisory Council on Doing Business in Africa (PACDBIA) and a diverse community of entrepreneurs hosted by Tony Elumelu Foundation and UBA Plc in Lagos yesterday.


The Tony Elumelu Foundation and United Bank for Africa Plc (UBA) partnered with the United States Department of Commerce to host a panel and roundtable discussion between members of the U.S. Presidential Council on Doing Business in Africa (PCDBIA)and a diverse community of African entrepreneurs.

The 11 person U.S. delegation, along with representatives of several U.S. government trade and investment-focused agencies, was led by the Honourable Penny Pritzker – U.S. Secretary of Commerce. The Council visited Lagos as part of a fact-finding mission to help inform their upcoming report to President Obama on how to strengthen commercial engagement between the U.S. and Africa, which will result in mutually-beneficial growth.

The event – titled “Unleashing Africa’s Entrepreneurs: Strengthening the Entrepreneurial Ecosystem to Empower the Next Generation of Africa’s Business Leaders” – brought together American business leaders and Nigerian entrepreneurs to discuss challenges, solutions and innovations in the current African business environment. The event was designed to allow representatives of the U.S. Government to participate in direct and substantive discussions with Africa’s emerging business leaders – an opportunity to engage in a dialogue that has the potential to influence U.S. foreign policy for Africa.

"President Obama believes, as I do, that the American private sector, working in partnership with the African business community, and African entrepreneurs can help address many of the continent’s most pressing challenges, including creating jobs and opportunity for young people across the continent," said U.S. Secretary of Commerce Penny Pritzker. "I am proud to lead our Administration’s effort to support and empower aspiring entrepreneurs, both in the United States and across the globe."

UBA Chairman Tony O. Elumelu, through his eponymous Foundation, hosted the delegation, and expressed gratitude for the collaborative approach the Council and U.S. Commerce Department are taking in engaging local entrepreneurs as part of their deliberations.

“Too often, well-meaning foreign policy-makers develop strategies to help Africans without actually engaging us,” he said. “In order to effectively help or support people, we should ask them what kind of help they want. So, I thank you for doing that with African businesses.”

For the U.S. Government, this trip begins the Road to GES 2016 – the Global Entrepreneurship Summit; an annual gathering of entrepreneurs at all stages of business development, designed to demonstrate the U.S. Government’s commitment to fostering entrepreneurship around the world.

Expressly designed to address the needs of and provide opportunities for the next generation of African entrepreneurs, the entrepreneurs in attendance included SMEs supported by UBA Plc, UNCTAD’s EMPRETEC Nigeria Foundation and those selected for the Tony Elumelu Entrepreneurship Programme (TEEP) – a 10-year, $100 million commitment by the Tony Elumelu Foundation to empower the next generation of Africa’s entrepreneurs with businesses that have the potential to generate income and jobs for their nations.

The Tony Elumelu Entrepreneurs in attendance were selected from the Agriculture, Media & Entertainment, ICT, Transport, Healthcare and Financial Services sectors. Their startups reflect the potential that entrepreneurship holds for spurring Africa's transformation; already, they have begun creating jobs in their local communities and generating tax revenues for governments earning them recognition in both local and international media.