Taarifa ya habari ChannelTEN, 28.01.2016Two Tanzanians featured in CNN's "12 of Africa's brightest young entrepreneurs" under 23

George Mtemahanji is working to solve Tanzania's rural energy shortages through his startup SunSweet Solar. The company imports solar photovoltaic products from Europe and builds affordable small-scale power plants for homes and businesses.
Sirjeff Dennis hopes to tackle malnourishment and poverty in rural Tanzania through poultry and vegetable farming. His company, Jefren Agrifriend Solutions, rears and sells day-old chicks to communities for meat and egg production.

Read the article at CNN.com

Mfanyakazi aiburuza Access Bank mahakamani kwa uonevu, manyanyaso

TAASISI ya Fedha ya Access Bank yenye anwani 95068, inatarajiwa kufikishwa mahakama ya usuluhishi Dar es Salaam kujibu tuhuma mbalimbali dhidi ya mfanyakazi wake.

Nyaraka ambazo Mwanahalisionline limefanikiwa kuziona mahakamani zinaonyesha CMA/DSM/KIN/R.638/15 ikiutaka uongozi wa benki hiyo kufika mbele ya tume ya usuluhishi ili kwenda kujitetea.

Taarifa hizi zinakuja ikiwa kuna nyaraka zingine zinazoonyesha kuwa benki hiyo imetuhumiwa kwa kuwanyanyasa wafanyakazi wake.

Imearifiwa kuwa hali ya manyanyaso na uonevu imezidi kuwa hatarishi na ya kutisha kwa wafanyakazi wa kawaida katika Benki ya Access hadi kufikia kusitishwa kwa huduma ya mikopo kwa wafanyakazi.

Hali hiyo imeelezwa kuwa imetokana na maamuzi ya ghafla yaliyotolewa na Mkurugenzi wa wa Access Bank Roland Coulon akielekeza kusitishwa huduma hiyo kwa wafanyakazi hata wale ambao maombi yao yalishakubaliwa au yapo kwenye hatua za mwisho.

MwanaHALISI Online limefanikiwa kuona nyaraka zilizosambazwa kwa wafanyakazi nchi nzima ikisema sababu zilizotajwa kusitisha huduma hiyo ni pamoja na benki kudai kupata hasara na pia kuwa nje ya uwiano unaotakiwa na Benki Kuu.

Waraka huo ulielekeza kuwa huduma ya mikopo kwa wafanyakazi itarudishwa pale tu wenye hisa za kampuni hiyo watakapotoa kiasi kingine cha fedha ili kuendeshea benki.

Wafanyakazi wa benk hiyo wanaendelea kuulalamikia uongozi wa benk hiyo kwa kurudisha kwa kiasi kidogo huduma hiyo kwa maelezo kuwa huduma hii itarudi kikamilifu ifikapo February 2016.

“Tunaomba kwa kupitia waraka huu Benki ielewe nia yetu safi na ya dhati ya kuihitaji huduma hii kama benki nyingine zinavyowapatia wafanyakazi wake, ni aibu tunapata shida, tunanyanyasika na kuaibika mitaani wakati mwajiri wetu anao uwezo wa kutusaidia na hataki tukope sehemu nyingine kwa dhamana yake.”

Uongozi wa Benki hiyo ulipoulizwa kuhusu tuhuma hizi na kwamba wanapaswa kufika mahakama ya usuluhishi kesho umedai kuwa hadi sasa hawana taarifa.

Kauli ya CHADEMA: Serikali ya Awamu ya Tano ina dalili za kidikteta

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani). Kulia ni Afisa Habari wa chama hicho, Tumaini Makene

SERIKALI YA AWAMU YA 5 YAONYESHA DALILI ZA KUTAKA KUENDESHA NCHI KIDIKTETA


Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA Salum Maalim amelaani vikali kitendo cha serikali kutaka kutoonyeshwa kwa matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya bunge kwa sababu ya gharama, akiongea na waandishi wa habari leo Alhamisi 28/01/2016 katika ofisi za CHADEMA makao makuu Kinondoni Dar es salaam, alilaani kitendo hicho na kusema ni kuwanyima wananchi haki yao ya msingi ya kupata habari na kwamba serikali ya awamu ya tano inataka kuendesha nchi kidikteta na kutaka kuficha maovu yake.

Kutokana na kile kilichotokea ndani ya bunge la Jamuhuri la muungano wa Tanzania siku ya Jumatatno 27 Januari 2016, na matukio mengine ambayo yameendelea kufanywa na serikali ya awamu ya tano inadhihirishasha ni vitendo vya udikteta. Serikali ilianza kwa kupiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa na wakiwa Lindi Waziri mkuu na Katibu wa, Itikadi na uenezi CCM ambaye pia ni waziri wa habari, michezo, wasanii na utamaduni Mhe. Nape Nnauye alisema, Kaimu Katibu Mkuu Salum Mwalimu akanukuu alichokisema Mhe. Nape “Waachwe walioshindwa wafanye kazi yao, hakuna mikutano ya hadhara kwa vyama vyote”.

Baadae likafuata tamko la jeshi la polisi likikazia, kauli hiyo ya serikali, baaada ya hapo, tukaoana bungeni namna ambavyo kamati za bunge zilivyoundwa, ukiangalia umuhimu na unyeti wa kamati zenyewe na shughuli za kamati hizo katika kutimiza shughuli za bunge na kuisimamia serikali, kamati zimeundwa katika namna ambayo unaona kabisa ya kwamba serikali hii haitaki changamaoto, haitaki kusimamiwa, haitaki kuonekana upande wake mwingine.

Wiki moja baadae serikali inakuja kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya bunge, achilia kwamba sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 inaeleza wazi kabisa chama cha siasa kitaendesha shughuli zake kwa mikutano ya hadhara na maandamano, lakini wao wakasema hapana, kauli ya walioshindwa waachwe wafanye kazi zao hii ina maana kwamba wengine wote hamna thamani ondekeni uwafanye wanavyotaka, wakakiuka sheria hatijulikani mamlaka hayo wameyatoa wapi?.
Kamati za bunge zilivyotenegenezwa unajua kabisa kuna mtu alipaswa kuwa pale, huyu alipaswa kuwa hapa kwa uzoefu wake au kutokana na uwezo wake lakini haikuwa hivyo, badala yake tunashuhudia vituko vya hali juu katika uundwaji wa kamati hizo, baada ya wiki tunaoana tena katiba ikivunjwa, kule wakati wanapiga marufuku mikutano walisema nchi bado ipo katika joto la uchaguzi.

Leo wanavunja katiba ya kimsingi kabisa inayowapa watu haki kupata taarifa kwa kisingizio cha gharama, wakitoa mfano wa mabunge mengine, hii ni wazi kwamba serikali ya awamu ya tano inataka kuendesha nchi kidikteta na inataka kuficha maovu yao.
Huwezi kupiga marufuku mikutano ya hadhara, mtu muovu huwa anajijua anajitafutia kinga, huwezi kuzuia bunge, hawataki watu wawasikilize nje katika mikutano, na hilo kimsingi wakati haujafika hatukuwa tayari na operesheni , opersheni za CHADEMA bado zinaandaliwa zitafanyika tu, hayupo mwenye mamlaka juu ya sheria, wengine wameuliza kwanini CHADEMA hawafanyi mikutano lakini ni kwa sababu muda bado ila tupo kwenye mikakati ya kuanza ziara kwa sababu tunaruhusiwa na katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Hatuwezi kukubali kuzuiliwa kufanya shughuli zetu kwa kauli zisizo namashiko, mikutano ipo program zinaandaliwa.

Leo wanaminya bunge, ni dalili za Udikteta, dalili za hofu , serikali imejawa na hofu, na wanajua hawana kitu ni mbwembwe tu, zisizokuwa na mashiko, leo imekuwa ni fasheni unasikia huyu kamfukuza huyu huyu kamfukuza yule, hakuna hata mmoja aliyetoka akatuambia amefanya hiki, amefanya hiki, kufukuza fukuza watu ni dalili za udikteta pia, kwa sababu udikteta maana yake ni kinyume cha utawala wa sheria kwa maana ya utawala bora, na usio zingatia misingi ya sheria na katiba, sasa tunaona jinsi sheria zinavyovunjwa, katiba inavyovunjwa, hakuna tafsiri nyingine, kwamba kama hutaki kuzinagatia sheria, kanuni na taratibu maana yake wewe ni dikteta.

Tunapinga sababu zilizotolewa na Mhe. Nape, hazina mashiko, amezungumza sababu za gharama, ni gharama zipi? Akizungumza Salum Mwalimu alisema “ eti 4.2 bilioni, sijui, labda katika utawala ule ule wa kiserikali, mimi nimekuwa mwandishi wa habari, nanimefanya kazi kwenye TV, kila nikichambua, 4.2 bilioni kwa ajili ya kurusha bunge muda ambao sio prime time? Yani kila nikipitia rates za televisheni zote sioni hiyo 4.2 bilioni inapatikanaje, Nape aje atuchambulie, asiishie kutaja figures za jumla, aje atuambie amekokotoaje hiyo 4.2 bilioni ya TBC kurusha vipindi vya bunge, bunge linakaa mara ngapi kwa mwaka? Leo tuangalie vipindi vya TBC, with very due respect, wala sina sababu ya kuwasema vibaya TBC, vipindi vinavyorushwa majira ya saa 3 mpaka saa 7 ni vipindi vya aina gani? Na sio kwa TBC tu…Televisheni zote” alisema MSalum Mwalimu.

Akiendelea kuongea Kaimu Katibu Mkuu CHADEMA Salum Mwalimu aliongeza “Mimi nimeafanya kazi kwenye TV muda wa saa 3 mpaka saa 7, utakuta muziki, utakuta marudio ya tamthilia, utakuta sijui burudani, ndio muda huo vipindi vya bunge vinaporushwa, Nape aje atuambie ni kitu gani cha msingi kinachorushwa kwenye TV yeyote hapa nchini ikiwemo TBC muda huo? Na kama ni cha msingi inakuwa ni marudio, sijaona kipindi cha msingi kwa mara ya kwanza kimerushwa saa 4 asubuhi, saa 5 asubuhi, saa 6 mchana na saa 7 mchana sijaona, kwa sababu muda ule sio prime time” aliongeza.

Mhe. Nape aliulizwa na waandishi wa habari serikali si imetenga fedha? Mhe. Nape akajibu kwamba kweli fedha zimetengwa lakini hazitoki, lakini hapo uzembe ni wa nani? Huwezi kuwahukumu wananchi kwa uzembe wa serikali, kwamba wanatennga bajeti lakini fedha hazitoki. Lakini hao hao ndio wanatamba, tumeokoa hiki, tumeokoa kile, makusanyo yameongezeka kama makusanyo yameongezeka wangeenda kupitia bajeti.

Kwa hiyo alichokizungumza Mhe. Nape hakina uhalisia na kama Mhe. Nape anataka tumuamini atukokotolee hizo gharama, hakuna televisheni inayoonyesha mambo mazito ya msingi yanayowaweka watu pamoja kuyaangalia saa 4 usiku, ndo maana hakuna televisheni inayoonyesha taarifa ya habari saa 4 usiku. Hata mtu ukijiuliza saa 4 usiku unakuwa wapi? Unafanya nini? Unajiandaa na nini? Walio wengi kama hawako njiani wamechelewa kutoka makazini, basi washafika nyumbani, washaangalia habari saa 2 na vipindi vingine hadi saa 3 kisha unakwenda kulala tayari kupambana na siku inayofuata.

Kijiji gani, wakulima gani ambao Mhe. Nape anasema watakaa wasubiri bunge? Umeme wenyewe ni wa solar, Tv zenyewe ni kushirikiana watu wanakusanyika wanaangalia, baada ya hapo TV zinazimwa watu wanakwenda kulala, hakuna mtu anayekaa mpaka saa 5 usiku kuangali tamthilia hakuna. Serikali inadanganya umma inaona watu wote wajinga.

Utafiti gani alioufanya Mhe. Nape unasema saa 4 usiku ndiyo kuna watazamaji wengi ? na ukitaka kujua muda wa usiku saa 4 sio prime time kama ilivyo asubuhi huwezi ukakuta movies au tamthilia, unakuta tamthilia kwa sababu tamthilia sio za kila mtu anatazama.Jana amefanya PRESS saa 3 usiku kwanini asingefanya saa 4, kwa kile alichokisema ilibidi PRESS yake afanye saa 4 usiku, lakini alijua saa 4 usiku sio muda watu wengi wanatazama TV.

Mhe. Nape alisema kunatafiti za mabunge mbalimbali lakini hizo nchi zina channels maalum kwa ajili ya bunge muda wote, lakini kwanini uige nchi nyingine kwa kuficha maovu yako, kwanini asituambie Uingereza kuna uhuru mkubwa wa vyombo vya habari, vyombo vya habari havifungiwi hovyo? Tuige na hilo.

Kwanini asituambie kuna nchi kama Kenya na Congo matokeo ya Urais yanaweza kupingwa mahakamani ? na wao wakaiga tukayapinga matokeo ya Urais mahakamani , kwanini wasiige kwenye nchi za wenzetu kuna uwajibikaji na utawala bora? Nchi hii ukiona jambo linaigwa nje ujue linamaslahi yao.

Lakini na sisi tutakuwa wa kuiga mpaka lini? Kwanini sisi siku moja tusiwe mfano, kwamba Tanzania bunge linaonyeshwa moja kwa moja ili wengine waige, zinakuja whatsapp, face book, twitter, instagram zote hizi zinaletwa ili kupashana habari kwa urahisi zaidi, lakini unataka urudishe watu enzi hizo, haiwezekani kabisa, mambo yamebadilika.

Vyombo vinavyoshughulika na sekta ya habari kikiwemo MOAT, MCT e.t.c kuliangalia hili ili kuhakikisha haki ya watu kupata taarifa haiguswi, watafute ni jinsi haki ya kupata habari haiguswi, bunge lionyeshwe au taifal ipate TV maalum irushe matangazo,hatuwezi kulirudisha taifa nyuma.


Sababu za gharama, watu hawatafanya kazi haipo, haiwezekani mtu aache kazi yake aangalie TV, kwa ofisi gani za serikali saa 10 jioni ndio kazi zinachanganya? Au waziondoe TV ili wenye majukumu wafanye kazi, waacche uongo, kama sababu ni fedha waseme wadau wapo, bunge halionyeshwi siku 365 na siku nzima asubuhi mpaka jioni.

  • Hawataki serikali ya Rais Magufuli ishughulikiwe kuna maovu mengi ndani ya muda mfupi,wasitake kuficha maovu hayo, MOAT,MCT na wengine watazame hili wahakikishe haki ya wananchi kupata taarifa haiguswi.Imenukuliwa kutoka kwenye ukurasa wa CHADEMA wa Facebook

Watumishi wa TRA 7 kati ya 8 waliotuhumiwa kutoroka wamekamatwa

Wafanyakazi saba kati ya wanane wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) waliotuhumiwa kuhusika kutorosha makontena 11,019 na magari 2,019 kutoka bandarini ambao walitoroka, wamepatikana na tayari wanaendelea kuhojiwa na polisi juu ya tuhuma hizo.

Watumishi hao ni kati ya watuhumiwa 15 wa TPA waliotangazwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kuwa wameshiriki kuondosha makontena na magari hayo kutoka katika bandari kavu saba bila kulipa ushuru wa Bandari.

Meneja Mawasiliano wa TPA, Janet Ruzangi alisema jana kuwa mfanyakazi mmoja kati ya hao wanane, hajapatikana; na anaendelea kusakwa na polisi ili afikishwe kwenye vyombo vya sheria.

“Wote walishapatikana kasoro mtumishi mmoja, Happygod Naftali, ambaye huyu alishaacha kazi siku nyingi baada ya viongozi kuanza kufuatilia suala hilo; lakini bado polisi wanaendelea kumsaka,” alisema Ruzangi.

Mkuu wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alithibitisha watuhumiwa hao, kukamatwa na kwamba bado wanaendelea kuhojiwa kuhusu tuhuma hizo.

“Ni kwamba tunaendelea na upelelezi wetu,” alisema Sirro licha ya kuwa hakutaka kutaja idadi ya wafanyakazi wa TPA ambao wamepatikana.“Kwa kweli idadi nitaitoa siku nitakapozungumza na waandishi wa habari wiki hii,” alifafanua.

Watumishi waliokuwa wanasakwa na polisi waliopatikana kwa mujibu wa Ruzangi ni Aron Lusingu, Amani Kazumari, John Mushi, Valentine Sangawe, Bonasweet Kimaina, Zainab Bwijo na Nathan Edward.

Watumishi hao wanaungana na watumishi wengine saba John Elisante, Leticia Masaro, Christina Temu, Merina Chawala, Adnan Ally, Masoud Seleman na Benadeta Sangawe waliokamatwa na kuhojiwa kuhusu sakata hilo. Watumishi hao saba, kwa mujibu wa Sirro, tayari walishapelekwa mahakamani.

“Ukiacha wale saba ambao tumeshawafikisha mahakamani, hawa wengine bado tuko nao tunaendelea kufanya upelelezi,” alieleza.

Wafanyakazi hao wanatuhumiwa kuhusika kutorosha makontena 11,884 na magari 2,019 ambayo yalitoroshwa kutoka katika Bandari Kavu (ICD) saba bila kulipiwa ushuru wa bandari na hivyo kuipotezea Serikali mapato ya Sh bilioni 48.55.


Kuhusu mawakala 280 waliopewa siku saba wawe wamewasilisha maelezo yao makao makuu ya TPA namna ya walivyohusika kulipia makontena hayo, Ruzangi alisema mamlaka yake inajipanga kutoa taarifa kamili juu ya suala hilo.


“Tunaendelea kuandaa taarifa ya kilichotokea na kilichobainika kuhusu mawakala hao, tutatoa taarifa hivi karibuni,” alisema Meneja Mawasiliano huyo.

Bank of Tanzania issues license to Hakika Microfinance Bank Limited

PUBLIC NOTICE

This is to inform the general public that Bank of Tanzania (BOT) has issued a banking license to a new Microfinance Bank namely Hakika Microfinance Bank Limited. The license allows the company to carry out banking business as a Microfinance bank operating in Tanzania. The bank's head office is located at Arusha Consultants House No. 12, Col. Middleton Road, Arusha.

Bank of Tanzania,
28th January 2016.

Kauli ya WM Majaliwa kuhusu kurushwa vikao vya Bunge kupitia TBCWaziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kwamba matangazo ya bunge hayatarushwa yote live kama serikali ilivyosema jana na tayari hatua hiyo imekwisha kuanza.

Majaliwa ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la papo kwa papo la Mbunge wa Hai ambaye pia ni msemaji wa kambi ya upinzani Bungeni Freeman Mbowe aliyetaka kujua kwanini serikali imefanya maamuzi ya kuzuia wananchi wasione matangazo ya Bunge moja kwa moja.

Akijibu swali hilo Waziri Mkuu amesema kwamba uamuzi wa kutoonyeshwa kwa matangazo ya moja kwa moja uliombwa na chombo cha umma chenyewe kwamba hakina uwezo kujiendesha na uamuzi wao huo umeungwa mkono na serikali.
''Maamuzi ya chombo hiki yameungwa mkono na serikali na Waziri Nape Nnauye amefanya kipindi maalum kuhusiana na jambo hilo na wananchi wameelewa vizuri na wameiunga mkono serikali kwamba matangazo yatarekodiwa na yatarushwa kama kipindi maalum usiku.'' 
Aidha chombo cha umma kitakuwa kinarusha matangazo ya moja kwa moja kwa muda wa maswali na majibu kwa serikali na baada ya hapo matangazo yatarekodiwa na kurushwa katika kipindi kiitwacho leo katika Bunge.Tamko la ACT-Wazalendo: Tusimruhusu Rais Magufuli kusimika utawala wa kidikteta


JANA limetokea tukio la aibu katika nchi yetu pale serikali ilipofanya jaribio la hatari la kuzuia wananchi kuona na kusikia kinachoendelea bungeni.

Kitendo cha serikali ya CCM kuzuia kuonyeshwa moja kwa moja vipindi vya bunge katika televisheni ya taifa ni cha kijima na sisi chama cha ACT-Wazalendo tunakilaani kwa nguvu zetu zote.

Tunakitafsiri kitendo hiki cha serikali kama mwendelezo wa hatua na juhudi za Rais Magufuli za kuminya demokrasia na kusimika utawala wa kiimla.

Tunawasihi wananchi kusimama imara na kuzipinga jitihada zozote ovu za kuminya demokrasia nchini.

Tunawapongeza wabunge wazalendo wa upinzani kwa kusimama pamoja na kupinga nia ovu ya serikali ya kuua demokrasia katika nchi yetu.

Tunawatia shime wabunge wote wazalendo kuendelea kupigania maslahi mapana ya taifa letu.

ACT-Wazalendo! Taifa kwanza leo na kesho!

Samson Mwigamba,
KATIBU MKUU.

Taarifa ya uteuzi wa Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, amemteua Ndugu Julian Banzi RAPHAEL, kuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.

Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue imeeleza kuwa uteuzi huo umeanzia tarehe 26 Januari, 2016.

Kabla ya uteuzi huu Ndugu Julian Banzi RAPHAEL alikuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Biashara na Viwanda, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Ndugu Julian Banzi RAPHAEL anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Juma RELI ambaye muda wake umemalizika tarehe 12 Julai, 2015.

Gerson P. Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU,
DAR ES SALAAM.

28/01/2016

Athari za mvua jijini Dar es Salaam leo 28.02.2016


Vijana wakiwa wamekaa nje baada ya nyumba wanazoishi kujaa maji maeneo ya Jangwani jijini Dar es Salaam kufuatia mvua zilizonyesha leo.


Kituo cha daladala za kwenda Gongolamboto cha Suwata Kariakoo kikiwa kimejaa maji hivyo kuleta adha kwa watumiaji kufuatia mvuo hizo.


Dimbwi la maji likiwa mbele ya jengo la Yanga.


Daraja la Jangwani na Kituo cha mabasi ya mwendokasi kikiwa kizingirwa na maji.


Magari yakipita kwenye dimbwi la maji barabara ya mtaa wa Lindi Ilala.


Moja ya vibanda wanavyoishi wananchi waliobomolewa eneo la Kinondoni Mkwajuni maji yakipita katikati yake jambo ambalo ni hatari kwa watu wanaoishi ndani humo.


Nyumba ikiwa imezingirwa na maji eneo la Mchikichini Ilala kufuatia mvua hiyo iliyonyesha leo


Vijana wakiuangalia Uwanja wa Klabu ya Yanga ulivyojaa maji.

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habarizajamii.com - simu namba 0712-727062)Jibu la WM Majaliwa kuhusu mkanganyiko wa Elimu Bure


Inasikitisha! Morogoro: Gari linalazimishwa kuvuka maji, watoto wamezama, Mzungu/Mhindi anajitahidi kuwaokoa


Job: Director of Finance and Administration, Tanzania

Organization: Management Systems International
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 27 Feb 2016

Wabunge waondoka ukumbini katika kikao cha Bunge 28.01.2016Hali ya kutokuelewana iliendelea tena leo ndani ya Bnge baada ya wabunge wote wa upinzani kususia vikao na kutoka kwenye ukumbi mara baada ya Wabunge kuanza kuchangia hotuba ya Rais Magufuli.

Baada ya kipindi cha Maswali na Majibu ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu, yalifuata matangazo na kisha wabunge walipewa fursa ya kuchangia hotuba ya Rais, ndipo wabunge kadhaa wa upinzani (UKAWA) akiwemo mbunge wa Ubungo (CHADEMA), Saed Kubenea kuomba muongozo wa Naibu Spika.

Naibu Spika alikataa wito wa kutolewa miongozo hiyo na kutaja jina la Mbunge kwa ajili ya kuchangia kujadili Hotuba ya Rais. Hali hiyo iliwakera wabunge wa upinzani waliodai kuwa wamezibwa midomo na ndipo walipoamua kutoka nje ya ukumbi wa bunge.

Wabunge wa CCM waliaendelea kujadili Hotuba ya Rais.Azimio la CUF kuhusu tangazo la ZEC la uchaguzi wa marudio Zanzibar


AZIMIO LA BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA KUHUSU TANGAZO LA MWENYEKITI WA TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR LA KUITISHA UCHAGUZI WA MARUDIO ZANZIBAR


Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la THE CIVIC UNITED FRONT (CUF – Chama Cha Wananchi), likiwa ndiyo chombo cha juu cha maamuzi katika Chama baada ya Mkutano Mkuu wa Taifa, limefanya kikao cha dharura leo, tarehe 28 Januari, 2016, katika Ofisi Kuu ya CUF, mjini Dar es Salaam. Kikao hicho kilikuwa na ajenda moja tu, ambayo ni kufanya maamuzi kuhusiana na tangazo la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar la kuitisha uchaguzi wa marudio.

Baada ya kujadili kwa kina tamko hilo la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salum Jecha, la kuitisha uchaguzi wa marudio tarehe 20 Machi, 2016 na mwenendo mzima wa hali ya kisiasa Zanzibar tokea alipotoa tamko lake batili la tarehe 28 Oktoba, 2015 kudai kwamba amefuta uchaguzi mkuu wa Zanzibar wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na matokeo yake, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limefikia maazimio yafuatayo:

1. KWAMBA Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar umeshafanyika tarehe 25 Oktoba, 2015, ambapo kwa upande wa uchaguzi wa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani ulikwisha kamilika na washindi wote kupewa shahada za kuwathibitisha na kuwatambua kama washindi halali. Kwa upande wa uchaguzi wa Rais wa Zanzibar, matokeo yalikwisha bandikwa nje ya vituo vya majumuisho vya majimbo yote 54. Kilichokuwa kinaendelea baada ya hapo ni kuhakiki matokeo hayo kutoka majimboni na kazi hiyo ilikwishakamilika kwa majimbo 40 na katika hayo, matokeo ya uchaguzi wa Rais kwa majimbo 31 yalikwishatangazwa kabla ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jecha Salum Jecha, kutangaza isivyo halali kwamba ameufuta uchaguzi huo.


2. KWAMBA Chama Cha Wananchi (CUF) hakitoshiriki katika uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika tarehe 20 Machi, 2016 kwa sababu uchaguzi huo si halali kwani uchaguzi halali ulishafanyika.

3. KWAMBA linatoa wito kwa Wazanzibari wote wanaoipenda nchi yao na ambao wanaamini katika utawala wa sheria, demokrasia na kuheshimu Katiba na Sheria za nchi yetu kutoshiriki katika uchaguzi huo usio halali wa marudio.

4. KWAMBA sababu kuu ya Baraza Kuu kufikia maamuzi haya ni kutokana na matamko yote mawili ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salum Jecha, kutokuwa halali na kwenda kinyume na Katiba ya Zanzibar na Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar Nam. 11 ya 1984. Hakuna kifungu chochote cha Katiba ya Zanzibar au Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar kinachotoa uwezo kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar na hata kwa Tume yenyewe kufuta uchaguzi au kuitisha uchaguzi wa marudio.

5. KWAMBA linazipongeza na limetiwa moyo sana na taasisi na jumuiya zote za kimataifa na kikanda zikiwa ni pamoja na Jumuiya ya Madola (The Commonwealth), Umoja wa Ulaya (European Union), Umoja wa Afrika (African Union), Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na nchi za Marekani na Uingereza kwa msimamo wao wa kuungana na Wazanzibari na kutetea haki yao ya kidemokrasia na maamuzi halali waliyoyafanya katika uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na kutaka mchakato wa uchaguzi huo ukamilishwe na matokeo yake kutangazwa.

6. KWAMBA linazipongeza na kutiwa moyo pia na taasisi za hapa nchini zikiwemo taasisi na jumuiya za kidini, taasisi za haki za binadamu, vyombo huru vya habari, vyama vyengine vya siasa na Wazanzibari na Watanzania wote wanaopenda amani na demokrasia kwa msimamo wao wa kutetea maamuzi ya Wazanzibari waliyoyafanya katika uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na kuendelea kusisitiza haja ya kuheshimu na kufuata Katiba na Sheria za nchi yetu na pia haja na umuhimu wa kutunza amani ya nchi yetu kwa kutaka haki itendeke. Baraza Kuu linazihakikishia taasisi na jumuiya hizo zote na pia kuwahakikishia Wazanzibari na Watanzania wote kwamba CUF itaendelea kusimama kidete katika kulinda na kutetea Katiba na Sheria za nchi yetu na pia kutetea maamuzi ya Wazanzibari waliyoyafanya tarehe 25 Oktoba, 2015.

7. KWAMBA limesikitishwa na kushangazwa na kitendo cha Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, kuandika barua na kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kutaka vyama vya siasa vishiriki uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika tarehe 20 Machi, 2016 bila ya kujali kwamba uchaguzi huo ni haramu na unakiuka matakwa ya Katiba ya Zanzibar na Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar Nam. 11 ya 1984. Baraza Kuu halikutarajia mtu mwenye hadhi ya Ujaji kufanya kazi ya kutumikia maslahi ya watawala ambao wameamua kuvunja Katiba na Sheria za nchi yetu na kukanyanga misingi ya haki na demokrasia huku akishindwa kukemea uhuni mkubwa uliofanywa wa kubaka demokrasia na haki za watu.

8. KWAMBA limesikitishwa na kitendo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk. John Pombe Magufuli, kukwepa dhamana na wajibu wake kama Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu kwa kuiacha njiani kazi aliyoianza ya kutafuta ufumbuzi wa mkwamo wa uchaguzi Zanzibar. Baraza Kuu linamtaka Rais Magufuli kujitathmini na kujiuliza anajiweka vipi na kutoa taswira gani mbele ya macho ya Watanzania na jumuiya ya kimataifa kutokana na kutosimamia ahadi yake aliyoitoa mbele ya Watanzania wakati akilizindua Bunge jipya kwamba atafanya kazi na vyama vya CUF na CCM ili kuupatia ufumbuzi mkwamo huu.

9. KWAMBA linalaani matumizi ya nguvu kubwa ya vyombo vya ulinzi na usalama vya Jamhuri ya Muungano na Vikosi vya SMZ dhidi ya wananchi wasio na hatia na ambao wamekuwa watulivu licha ya vitendo vingi vya uchokozi wa makusudi na hata mashambulizi ya hujuma dhidi yao yanayofanywa na makundi ya vijana wa CCM waliowekwa katika makambi kadhaa kisiwani Unguja.

10. KWAMBA linaitaka jumuiya ya kimataifa na hasa taasisi zinazosimamia haki za binadamu na zinazopambana na makosa ya jinai kimataifa ikiwemo Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (International Criminal Court – ICC) kufanya uchunguzi wa kauli na matendo ya uhalifu, uvunjwaji mkubwa wa haki za binadamu na ubaguzi ambao umekuwa ukifanywa dhidi ya wananchi wa Zanzibar na kuchukua hatua dhidi ya watu walio nyuma ya maamuzi na utekelezaji wa matukio hayo.

11. KWAMBA linawapongeza wananchi wa Zanzibar kwa kuonesha ukomavu wa hali ya juu na kuwa watulivu licha ya machungu makubwa waliyoyapitia na wanayoendelea kuyapitia tokea pale maamuzi yao yalipopinduliwa na CCM kwa kumtumia Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salum Jecha. Baraza Kuu linatoa wito kwa Wazanzibari wote kuungana pamoja chini ya chama chao cha CUF walichokipa ridhaa halali kupitia uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 kutetea maamuzi yao waliyoyafanya kupitia sanduku la kura kwa njia za amani. Baraza Kuu linawasisitiza tena Wazanzibari kwamba waendelee kutunza amani ya nchi yetu na kutambua kwamba kutunza amani si udhaifu bali ni jambo linaloipa nguvu jumuiya ya kimataifa kufuatilia haki za kidemokrasia za wananchi wa Zanzibar.

12. Baraza Kuu la Uongozi la Taifa linawatahadharisha CCM na watawala wasiowajali na kuwaheshimu wananchi kwamba zama za utawala wa mabavu usioheshimu Katiba na Sheria za nchi hazina nafasi tena katika dunia ya leo. Baraza Kuu lina imani kwamba HAKI ITASHINDA.

LIMETOLEWA NA:

BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA
THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF – Chama Cha Wananchi)
DAR ES SALAAM

28 JANUARI, 2016Call for applications: 2016 Fellowship Programme - Dag Hammarskjold Fund for Journalists

APPLICATIONS INVITED FOR DAG HAMMARSKJÖLD JOURNALISM FELLOWSHIPS


United Nations, New York. The Dag Hammarskjöld Fund for Journalists is now accepting applications from professional journalists from developing countries for its 2016 fellowship program. The application deadline is March 18, 2016.

The fellowships are available to radio, television, print and web journalists, age 25 to 35, from developing countries who are interested in coming to New York to report on international affairs during the 71st session of the United Nations General Assembly. The fellowships will begin in early September and extend to late November and will include the cost of travel and accommodations in New York, as well as a per diem allowance.

The fellowship program is open to journalists who are native to one of the developing countries in Africa, Asia, and Latin America/the Caribbean and are currently working for media organizations. Applicants must demonstrate an interest in and commitment to international affairs and to conveying a better understanding of the United Nations to their readers and audiences. They must also have approval from their media organizations to spend up to three months in New York to report from the United Nations.

In an effort to rotate recipient countries, the Fund will not consider journalist applications for 2016 from nations selected in 2015: Brazil, India, Ghana, and Kenya. Journalists from these countries may apply in 2017.

Journalists are selected each year after a review of all applications. The journalists who are awarded fellowships are given the incomparable opportunity to observe international diplomatic deliberations at the United Nations, to make professional contacts that will serve them for years to come, to interact with seasoned journalists from around the world, and to gain a broader perspective and understanding of matters of global concern. Many past fellows have risen to prominence in their professional and countries. The program is not intended to provide basic skills training to journalists; all participants are media professionals.

Information about the Fund, including fellowship eligibility criteria, documentation requirements, and the application process can be found on the Fund’s web site at www.unjournalismfellowship.org.

Questions can be directed by email to [email protected]

Kongamano la UNESCO na Wizara ya Elimu lamalizika kwa kupata vipaumbele vya ESDP

Zulmira Rodrigues akisisitiza jambo
Na Rabi Hume, Modewjiblog

Kongamano lililoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi limemalizika jana jijini Dar es Salaam baada ya kupitisha vipaumbele ambavyo vitatumika katika Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP) kwa miaka mitano kuanzia 2017 – 2021.

Akizungumza na Mo Dewji Blog, Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Elimu, Clifford Tandari alisema kupitia kongamano hilo wamethibitisha vipaumbele ambavyo vitatumika ili kuifanya elimu ya Tanzania kuwa bora na yenye manufaa kwa miaka ya mbeleni.

Alisema kupitia kongamano hilo wamethibitisha ili kuwapo na elimu bora nchini kunahitajika kuwa na walimu wenye sifa na ubora unaohitajika, mashuleni kutumika vitabu vya ziada na kiada, kuimarisha huduma ya ukaguzi mashuleni, watoto wote wenye umri wa kwenda shule wapelekwe shuleni na kuwajengea uwezo wa stadi za kazi wahitimu ili hata wanapomaliza masomo waweze kujiajiri.

“Tumethibitisha yale maeneo muhimu ya sekta ya elimu ambayo tumegundua kwamba ili tuweze kusonga mbele lazima tuimarishe ubora wa elimu yetu kama ni walimu wasome vizuri wawe na ubora, tuwe na vitabu wanafunzi wapate maarifa kutoka kwenye vitabu, kudhibiti ubora wa elimu na watoto waende shule kwa shule za msingi, sekondari, vyuo vya ufundi na elimu ya juu,” alisema Tandari.

Aidha Tandari alieleza kuwa awali walikuwa wakishindwa kuwa na mipango ya aina hiyo kutokana na kutokuwepo kwa fedha lakini kwa sasa wataweza kugharamia mpango huo wa elimu kutokana na serikali kuwa tayari kusimamia mpango huo wa kuboresha elimu ya serikali.

Aliongeza kuwa wao kama Wizara ya Elimu wanaamini kuwa mfumo wa elimu kwa sasa utakwenda vizuri kutokana na kasi aliyonayo rais wa awamu ya tano, Dkt. John Pombe Magufuli ambaye ameamua kutoa elimu bure kwa wanafunzi wa shule za msingi hadi sekondari na kutokana na kasi yake ya utendaji kazi wanataraji utafanyika kama jinsi unavyopangwa.

Naye Mkuu wa Ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikiaa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues alisema kuwa kongamano hilo limekuwa zuri kutokana na makubaliano ambayo washiriki wameyafikia katika kusaidia elimu ya Tanzania kukua kwa kipindi cha miaka mitano ijayo na hiyo ni hatua ya awali ambayo wameanza nayo na hadi kufikia mwezi Mei watakuwa wameshakamilisha hatua zote zikiwepo bajeti na jinsi utekelezaji huo utakavyofanyika.

Awali Zulmira alieleza kuwa UNESCO ndiyo shirika la Umoja wa Mataifa ambalo linasimamia elimu na wao ndiyo wameandaa mpango huo wa ESDP na wataendelea kusaidia kukua kwa elimu nchini na hiyo ni moja kati ya kazi wanazozifanya katika kusaidia ukuaji wa elimu na kuifanya kuwa bora katika nchi mbalimbali ambazo shirika hilo wanafanya kazi.Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Elimu, Clifford Tandari akiwaelezea washiriki wa kongamano hilo (hawapo pichani) kuhusu Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP) ambao utafanyiwa kazi kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2017 – 2021.Mkuu wa Ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikiaa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akielezea jambo katika kongamano la kujadili vipaumbele vya Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP).Mmoja wa washiriki wa kongamano hilo akizugumza kuhusu Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP), Katikati ni Mkuu wa Ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikiaa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues na kushoto ni Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Elimu, Clifford Tandari.Mmoja wa wanakikundi akiwaelezea wanakikundi wenzake kuhusu kipaumbele ambacho walikuwa wamechaguliwa kukijadili na baadae kuwasilisha mbele ya washiriki wote jinsi kipaumbele hicho kitakavyotumika pamoja na faida zake.Mkuu wa kitengo cha Ushirikiano wa Kiufundi kutoka Makao Makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kutoka Ufaransa, Anton De Grauwe akimuelekeza jambo mwana kikundi mwenzake wakati wa kongamano la kujadili vipaumbele vitakavyotumika katika Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP).Baadhi ya wanakikundi wakiwa makini kufuatilia kila jambo ambalo linaendelea katika kongamano hilo la siku mbili ili kupata vipaumbele ambavyo vitatumika katika Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP).Picha ya pamoja.