Taarifa ya habari ChannelTEN, 29.01.2016Mahakama yamfutia kesi mtuhumiwa wa kupokea fedha za akaunti ya Tegeta Escrow


Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imemwachia huru aliyekuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Phillip Saliboko ambaye alikuwa anatuhumiwa kwa kosa la kupokea rushwa.

Job: Chief of Party - Youth Entrepreneurship Program - Tanzania

Organization: Catholic Relief Services
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 26 Feb 2016

Job: Head of Finance and Operations

Organization: ADD international
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 08 Feb 2016

Job: Change Management Lead-Tanzania

Organization: Program for Appropriate Technology in Health
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 15 Feb 2016

Job: Program Manager II - Director of Finance

Organization: Catholic Relief Services
Country: United Republic of Tanzania
Closing date: 26 Feb 2016

Employment opportunities at the Ardhi UniversityKielelezo: Mwongozo wa mavazi kwa watumishi wa ummaBaadhi ya makosa ya uhujumu uchumi, adhabu kwa mtuhumiwa na aliyeshiriki kufichaSerikali inaendelea kusimamia urejeshaji wa mali zilizopatikana kwa njia ya kihalifu kupitia mpango wa kupambana na uhalifu ulioanzishwa mwaka 2012 kwa kuwashtaki na kuwataifishia mali zao pindi upelelezi ukikamilika na kubainika mhalifu ana makosa hayo.

Baadhi ya watuhumiwa kadhaa wamepelewa mahakamani na kufungwa, ikiwemo mali zao kutaifishwa na kuwa mali ya Serikali. Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini ( DPP) Biswalo Mganga wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika leo kwenye ofiisi za Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam, ambapo alisema kuwa hatua hizo zimechukuliwa mara baada ya upelelezi wa makosa ya kuhujumu uchumi kukamilika na kumbaini mhusika.

Aidha Mganga aliongeza kwamba mhusika hushitakiwa na mali zake kutaifishwa kulingana na kosa lake, pia suala hili litamgusa kila mtu, wakiwemo watumishi wa umma.

“Mhalifu wa kuhujumu uchumi wa nchi ikiwemo usafirishaji wa nyara za Serikali, uuzaji wa madawa ya kulevya na kujipatia mali kwa njia ya rushwa watatumikia adhabu ya kulipa faini, kufungwa jela na kutaifishiwa mali zake pindi atapobainika na makosa hayo” alisema Mganga.

Alisema kufuatia mkakati huo, Jeshi la Polisi limekamilisha upelelezi wa kesi 23 ambazo ziliwasilishwa kwa DPP na kati ya hizo tatu (3) zimetolewa uamuzi na nyingine ishirini (20) ziko katika hatua ya maombi ya kupata amri ya mahakama ili ziweze kuziwa au kutaifishwa.

Alizitaja baadhi ya kesi za dawa za kulevya ambazo zimefikia ukomo na kutolewa uamuzi Januari 27, mwaka huu. Mkoani Kilimanjaro kesi mojawapo ni Josephine Waizela, ambaye ni raia wa Kenya aliyetiwa hatiani kwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya Cocaine zenye uzito wa kilogram tatu zikiwa na thamani ya Sh. Milioni 162 na kufungwa kifungo cha maisha.

Kesi nyingine ni namba 46 ya mwaka 2014 kutoka pia mkoani Kilimanjaro ambayo ilihusisha watu watatu, mmoja kati yao ambaye ni Hamis Mbwana alitiwa hatiani kwa kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroin zenye uzito wa gramu 3,191.11 na thamani ya shilingi milioni 143/=. Watuhumiwa wengine wawili katika kesi hiyo waliachiwa huru.

Mganga alizitaja baadhi ya kesi nyingine za uhujumu uchumi ni namba 6 ya mwaka 2015, ilisikilizwa mkoani Mbeya ambayo iliwahusisha raia wanne kutoka nchini China waliotiwa hatiani kwa kosa la kukutwa meno ya vifaru 11. Raia hao ni Song Lei , Xiao Shaodan, Chen Jianlin na HU Liang, ambao wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 na kulipa faini ya Sh. Milioni 9,288 kwa kila mmoja.

Kesi nyingine ya uhujumu uchumi namba 3 ya mwaka 2016 iliyomhusisha raia wa Tanzania Amani Rashid Ngaza aliyetiwa hatiani kwa kosa la kukutwa na meno ya tembo nane iliyosikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Katavi, wilaya ya Mpanda. Mtuhumiwa huyo amefungwa kifungo cha miaka 30 na kullipa faini ya Sh. bilioni 1.2.

Katika mkutano huo, Mkurugenzi Maganga alibainisha baadhi ya mali zilizotaifishwa kutoka kwa wananchi kuwa ni magari matano aina ya Toyota Rv 4 mbili ,Suzuki, Toyota Surf , Hiace pamoja na nyumba kutoka kwa washtakiwa mbalimbali wa makosa ya kuhujumu uchumi.

Aidha, Mganga alitoa rai kwa wananchi kutoa ushirikiano bila uwoga katika kufichua mali za mafisadi ili sheria ichukue mkondo wake pamoja na kuwataka wananchi wasijihusishe kwa njia yoyote ile ili kuficha umiliki wa mali ya mtu mwingine aliyoipata kiharamu kwa nia ya kuficha uhalifu wake kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria.

“Kwa mujibu wa Sheria aliyeshiriki kuficha mali ya mtu mwingine inayohusiana na uhalifu kwa njia yoyote ile pia anaweza kushitakiwa kama aliyetenda kosa la ufisadi,” alisema.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi Kamishna Diwani Athumani alisema kuwa atakayekamatwa na kosa la wizi au mali ya haramu atatumikia adhabu na mali zake kutaifishwa.

“Mhalifu akibainika na mshataka ya wizi au kujipatia mali kwa njia ya haramu atatumikia adhabu na kutaifishiwa mali zake kama vile magari, nyumba, boti, viwanja na fedha taslimu” alisema Kamishna Athumani.

Aidha, Kamishna Athumani aliongeza kuwa uzoefu wao unawaonyesha kwamba wahalifu wanatumia majina ya wake zao, waume zao, watoto wao na wakati mwingine kutumia majina ya watu ambao hawapo ili kuendelea kufaidika na mali walizozipata kwa niia za uhalifu.

“Hakuna mhalifu atakayepona katika mapambano haya pia uhalifu haulipi na hauna nafasi nchini” alisistiza Kamishina Athuman. Mbali na hayo, Mkurugenzi wa upelelezi Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini (TAKUKURU) Alex Mfungo pia alisema kuwa wameanzisha kitengo cha kutaifisha mali zilizopatikana kwa njia ya uhalifu ikiwemo rushwa.

Tangu mwaka 1990, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitambua utaifishaji wa mali zilizopatikana kwa njia ya kihalifu kama kipaumbele katika mfumo wa haki jinai wa kupigana na uhalifu. Haisadii sana katika jitihada za kupambana na uhalifu ikiwa mhalifu atapata adhabu ama ya kutozwa faini au kwenda jela ikiwa ataachiwa uhuru na kupewa fursa ya kutumia fedha au mali iliyopatikana kwa uhalifu huo.

Zaidi, fedha zilizoibwa na wanasiasa wala rushwa pamoja na wahalifu wengine, zinahitaji kutaifishwa na kuelekezwa katika maeneo muhimu yenye mahitaji. Sheria ya Utaifishaji wa Mali Haramu ilipitishwa na Bunge mwaka 1991 ili kuendana na muelekeo wa Kimataifa pamoja na mikataba ya Kimataifa ambayo imeridhiwa na nchi yetu.  • Taarifa ya NA MAGRETH KINABO na ALLY DAUD wa Idara ya Habari, MAELEZO

Katavi: Amwua askari aliyeongoza genge la wezi kumpora

Askari polisi wilayani hapa, Nobart Chacha (25) ameuawa kwa kupigwa risasi akituhumiwa kupora mali za mfanyabiashara wa madini kwa kutumia silaha za jadi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alisema jana kuwa askari huyo aliuawa kwa kupigwa risasi kifuani na mgongoni.

Diwani wa Kata ya Machimboni, Raphael Kalinga alisema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana katika Kijiji cha Ibindi kilichopo Kata ya Machimboni wilayani Mlele.

Alisema askari huyo akiwa na wenzake walifika kijijini hapo kwa lengo la kumpora mfanyabiashara huyo wa madini ambaye pia anamiliki mashine za kusaga nafaka.

Kalinga alisema askari huyo na watuhumiwa wengine walivunja mlango wa mbele wa nyumba ya mfanyabiashara huyo wakati amelala chumbani.

“Baadaye waliingia ndani, walimwamuru mfanyabiashara huyo kukaa kimya, lakini hakutii agizo na badala yake alichukua bunduki yake aina ya short gun na kumpiga askari huyo kifuani na mgongoni,” alisema.

Alisema baada ya kuona askari huyo amepigwa risasi, watuhumiwa wenzake walimchukua na kwenda kumtupa kwenye kichaka kilicho umbali wa mita 200 kutoka kwenye eneo la tukio na kisha kutoweka.

Alisema wakazi wa kijiji hicho ndiyo waliomtambua askari huyo baada ya kufuatilia michirizi ya damu na kuukuta mwili wake wake ukiwa kichakani na kutoa taarifa polisi. Alisema polisi walifika kwenye eneo hilo baada ya muda mfupi na kumtambua askari huyo.

Taarifa ya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Mwanza, Katavi - Mtweve, Chagonja

Update/Taarifa Mpya Januari 30, 2016


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Dkt. Mahadhi Juma Maalim kuwa Balozi wa Tanzania Ikulu jijini Dar es Salaam leo Januari 30, 2016


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Luteni Jenerali Venance Salvatory Mabeyo kuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ Ikulu jijini Dar es Salaam leo Januari 30, 2016


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Kamishna wa Polisi Clodwig Mathew Mtweve kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ikulu jijini Dar es Salaam leo Januari 30, 2016


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimuapisha Kamishna wa Polisi Paul Amani Moses Chagonja kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Ikulu jijini Dar es Salaam leo Januari 30, 2016


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na viongozi wa Jeshi la Wananchi na Jeshi la Polisi katika picha ya pamoja baada ya kuapishwa Mnadimu Mkuu wa TPDF, Balozi wa Tanzania Kuwait na Katibu Tawala wa Mikoa ya Katavi na Mwanza Ikulu jijini Dar es Salaam leo Januari 30, 2016
Paul Chagonja
Paul Chagonja
Chlodwig Mtweve
Chlodwig Mtweve

Kesi za uchaguzi: Mahakama yafuta kesi ya CCM dhidi ya CHADEMA Tarime Vijijini

Kulia ni Mwl. Chacha Heche ambaye ni Katibu wa CHADEMA Mkoani Mara akiongea na wanahabari nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza.

Na, George Binagi.

MAHAKA kuu Kanda ya Mwanza jana imeitupilia mbali kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Novemba 25 mwaka jana, katika Jimbo la Tarime Vijijini Mkoani Mara, iliyofunguliwa na aliekuwa mgombea ubunge katika jimbo hilo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Christopher Ryoba Kangoye.

Katika kesi hiyo, wajibu maombi walikuwa ni Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini Mhe. John Heche (CHADEMA), Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambapo mtoa maombi alikuwa akiiomba mahakama kutengua matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2015 katika Jimbo hilo kwa kuwa haukuwa huru na haki.

Baada ya Mahakama hiyo kupitia kwa Jaji Lameck Mlacha kusikiliza utetezi wa pande zote, iliamua kuifuta kesi hiyo ambayo ilikuwa ni nambari nne ya mwaka 2015 kutokana na hoja za mleta maombi kuwa na kasoro mbalimbali ikiwemo kutoainisha majina ya waliokuwa wakilalamikiwa kuvuruga uchaguzi Jimboni humo.

Wakili wa mleta maombi Costantine Mutalemwa pamoja na Wakili wa mjibu maombi Paul Kipeja aliekuwa akisaidiana na Wakili Tundu Lisu katika kesi hiyo, wameelezea kuridhika na maamuzi ya mahakama hiyo.

Naye Mwl. Chacha Heche ambaye ni Katibu wa CHADEMA Mkoani Mara ameelezea kuwa na imani na mahakama kutokana na maamuzi iliyoyatoa katika kesi hiyo pamoja na kesi nyingine zilizowahi kuamuliwa mahakamani hapo na kuongeza kuwa sasa kazi imebaki moja kwa Mhe. Heche ambayo ni kuwatumikia wakazi wa Jimbo la Tarime Vijijini.

Kwa upande wake Mrimi Zabloni ambaye ni Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, ameelezea furaha kwa wananchi wa jimbo hilo huku akiwasihi kuweka imani na mahakama hapa nchini katika kutoa maamuzi ya kesi mbalimbali.

Wananchi wengi mahakamani hapo kutoka Jimboni Tarime Vijijini walikuwa ni wafuasi wa CHADEMA na wameonesha kuyapokea maamuzi ya mahakama hiyo kwa furaha kubwa na kwamba wao waliamua ushindi wa Heche tangu Oktoba 25 mwaka jana kwenye daftari la kupigia kura.

Kesi hiyo ilisikilizwa Januari 19, 2016 mwaka huu na kuahirishwa hadi juzi kwa ajili ya kutolewa maamuzi, ambayo yalitolewa jana Januari 28, 2016.


Mrimi Zabloni (Katikati) ambae ni Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini akiongea na wanahabari


Wakili wa mjibu maombi Paul Kipeja akihojiwa na wanahabari


Wakili wa mleta maombi Costantine Mutalemwa akihojiwa na wanahabari


Mwl.Chacha Heche ambae ni Katibu wa Chadema Mkoani Mara na wafuasi wengine wa Chadema wakifurahia baada ya maamuzi ya Mahakama


Mahakamani kabla ya mashauri kutolewa


Mahakamani kabla ya mashauri kutolewa


Mahakamani kabla ya mashauri kutolewa.

Tangazo la TRA la kusitisha kwa muda kupokea maombi ya ajira


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilitoa tangazo la nafasi za kazi katika magazeti mbalimbali ambapo waombaji wanatakiwa kuwasilisha maombi kupitia tovuti ya TRA.

Kutokana na maombi ya nafasi za kazi kuingiliana na shughuli za kulipa kodi mwisho wa mwezi kupitia tovuti, TRA inasitisha kwa muda upokeaji wa maombi ya kazi kupitia tovuti hadi Jumanne tarehe mbili Februari 2016 ili kuruhusu ulipaji wa kodi uendelee bila usumbufu.

Pia TRA imeongeza muda wa kupokea maombi hadi tarehe 17 Februari 2016. Waombaji wote wa nafasi za kazi zilizotangazwa wanaombwa kutuma maombi yao kuanzia Jumanne tarehe mbili Februari 2016.

Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza kutokana na mabadiliko haya. 
 
Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na:

Kituo cha Huduma kwa Wateja
08000780078, 0800750075, 0713800333

Limetolewa na:
Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi
TRA-Makao Makuu

Wilaya 19 ambazo bado zina idadi kubwa ya wagonjwa wa ukoma Tanzania

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Watoto, na Wazee Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Mjini Dodoma katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya ukoma duniani. Kushoto ni Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma, Dkt Beatrice Mutayoba.

Tanzania inaungana na nchi nyingine Duniani itaazimisha siku ya Ukoma Duniani itakayoadhimishwa tarehe 29 Januari 2016 kwa kutoa elimu juu ya kujikinga na kupambana na ukoma Tanzania na kuifanya Tanzania iweze kuondokana na maambukizi mapya ya ukoma.

Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Watoto, na Wazee Mhe.Ummy Mwalimu akitoa tamko la Wizara hiyo leo Mjini Dodoma katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukoma Duniani ikiwa ni harakati za serikali kupambana na ugonjwa huu kwa kutoa elimu kwa umma wa watanzania.

Mhe.Ummy Mwalimu amesema siku hii itawapa fura ya kutathimini mwelekeo wa jitihada za nchi na zile za kimataifa katika kupambana na ugonjwa huu ambao umekuwa ukiogopwa sana katika jamii yetu toka enzi na enzi hasa kutokana na ukweli kwamba unasababisha ulemavu wa kuduma.
“Kwa mujibu wa takwimuza mwaka 2014, jumla ya wagonjwa 2,134 wa ukoma waligunduliwa ambapo wagonjwa 271 kati ya hao ambao ni sawa na asilimia 13 walikuwa na ulemavu na pia bado kuna Wilaya 17 za Tanzania bara na 2 za Tanzania Visiwani zilizogunduliwa idadi kubwa ya wagonjwa wa ukoma.”
“Nizitaje wilaya hizi ambazo zimekuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wa ukoma kwa Tanzania bara ni Liwale, Ruangwa, Lindi Mjini, Lindi Vijini, Masasi Vijijini, Newala, Nanyumbu, Namtumbo, Tunduru na Nkasi. Nyingine ni Mkinga, Muheza, Korogwe, Musoma, Musoma Vijijini, Chato, Shinyanga Manispaa na Rufiji na kwa Tanzania Visiwani ni Mkoa wa Mjini Magharibi na katika wilaya za Kati na Kusini.” 
Aidha amesema kuwa Tanzania katika kuadhimisha siku hii Serikali inayashukuru mashirika mbalimbali ya ndani na nje ya nchi kwa michango yao katika kuimarisha mapambano dhidi ya ugonjwa wa ukoma hapa Tanzania na hivyo kuhakikisha tunakuwa na Tanzania isiyo na maambukizi mapya ya ukoma.

Tanzania ni miongoni mwa nchi 17 Duniani ambazo bado zina viwango vya juu vya ugonjwa wa ukoma na kwa zaidi ya miaka 62, siku ya ukoma Duniani imekuwa ikiadhimishwa ulimwenguni kote kila Jumapili ya mwisho wa mwezi wa Januari.Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma Dkt Beatrice Mutayoba akitoa ufafanuzi juu ya Ugonjwa wa ukoma na kwa Tanzania Elimu zaidi itatolewa ili kupambana na ugonjwa huu


Mratibu wa Ukoma toka Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Watoto, na Wazee Dkt Deus Kamara akifanua jambo kuhusu maadhimisho ya Siku ya Ukoma Duniani


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto, na Wazee Mhe. Ummy Mwalimu akiangalia picha zikionesha wagonjwa wa Ukoma kulia ni Mratibu wa Ukoma toka Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Watoto, na Wazee Dkt Deus Kamara akiafanua jambo kuhusu maadhimisho ya Siku ya Ukoma Duniani.

Picha zote na Raymond Mushumbusi - MAELEZO

Ukaguzi wa eneo lililoharibiwa kwa mvua Morogoro - Dodoma

Mafundi wakiendelea na ujenzi wa kingo za barabara zilizo athiriwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika mikoa ya Iringa na Dodoma na kusababisha uharibifu wa barabara katika eneo la Kibaigwa mkoani Dodoma.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemwagiza Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mkoa wa Dodoma Eng. Leonard Chimagu kuhakikisha ukarabati wa barabara katika eneo la Kibaigwa unaanza Jumapili.

Profesa Mbarawa ameyasema hayo alipokuwa akikagua athari za uharibifu wa barabara zilizosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika mikoa ya Iringa – Dodoma na kusababisha mafuriko yanayoharibu kingo za barabara.

“Hakikisheni Jumapili kazi ya ujenzi hapa inaanza na ikamilike kwa muda mfupi ili kutoathiri huduma ya usafiri katika barabara hiyo kutokana na umuhimu wake”, alisema Prof. Mbarawa.

Waziri Mbarawa amewataka TANROADS washirikiane na Kikosi cha Usalama Barabarani kudhibiti magari yanayoegeshwa katika maeneo yasiyo rasmi na hivyo kusababisha ajali na uharibifu wa barabara hususani katika maeneo ya Dumila mkoani Morogoro na Kibaigwa mkoani Dodoma.

Mapema Waziri Mbarawa alikagua ujenzi wa kingo za barabara unaoendelea katika eneo la Dumila mkoani Morogoro ambapo amemuagiza Meneja wa TANROADS mkoa wa Morogoro Eng. Dorothy Ntenga kuhakikisha ujenzi huo wa kudhibiti barabara na daraja la Dumila unakamilika kabla ya Februari 15 ili kukabiliana na mafuriko wakati wa mvua za masika zinazokaribia kuanza.

“Chimbeni mchanga kwenye mto ili kuwezesha maji kupita kwa urahisi na kuondoa tishio la mafuriko yanayo athiri daraja hilo wakati wa mvua za masika”, alisisitiza Waziri Mbarawa. Naye Meneja wa TANROADS Mkoa wa Morogoro, Eng. Dorothy Ntenga amesema ili kudhibiti mafuriko katika eneo la Dumila juhudi zinaendelea kupunguza mchanga na hivyo kuwezesha kupita maji kwa urahisi.

Profesa Mbarawa alikuwa katika ziara ya kukagua athari za mafuriko katika barabara ya Morogoro-Dodoma ambapo maeneo ya Dumila na Kibaigwa yameathirika zaidi.


Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Dodoma Eng. Leornad Chimagu (kulia),akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu athari za mafuriko katika kingo za barabara ya Gairo-Dodoma eneo la Kibaigwa mkoani Dodoma.

Muonekano wa Daraja la Dumila mkoani Morogoro lilivyo sasa kufuatia mvua zinazonyesha katika mikoa ya Iringa na Dodoma na kusababisha mafuriko yanayoelekea katika Mto Mkondoa.Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), akitoa maelekezo kwa Meneja wa TANROADS mkoa wa Dodoma Eng. Leornad Chimagu kuhusu ujenzi wa kingo za barabara hiyo kabla hazija athiri huduma za usafirishaji.

Gari likipita sehemu iliyoathirika zaidi katika eneo la Kibaigwa barabara kuu ya Gairo-Dodoma.

Magari yaliyoegeshwa katika kingo za barabara yanavyochangia uharibifu wa barabara na kusababisha ajali, hili ni eneo la Kibaigwa mkoani Dododma.Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Morogoro Eng. Dorothy Ntenga akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa namna maji yanavyopiga kingo za daraja la Dumila wakati Waziri huyo akikagua ujenzi wa kingo mpya zinazojengwa kudhibiti mafuriko hayo.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.